PONGEZI RPC MTWARA NA KIKOSI CHAKO.

Mpalakugenda

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
2,138
1,391
Eid mubarak ndugu zangu,
Leo nimebahatika kuwepo mkoani Mtwara katika sherehe hizi za kumalizika kwa mwezi mtukufu wa ramadhani.
Mtwara ni moja ya mikoa ambayo inaidadi kubwa ya waamini wa kiislamu. Hivyo siku kama ya leo tarajia kuona mishe nyingi sana,sehemu za starehe pamoja na beach. Hivyo leo mtwara ni kuchele.
Pamoja na msongamano huo jeshi la polisi limefanya kazi kubwa sana ya kuwepo kila sehemu na kuhakikisha taratibu mbali mbali zinazingatiwa kwa usalama wa kila raia.
Bila shaka leo polisi wote hawakuwa na mapumziko ili kusaidia kuimarisha usalama. Hata utendaji wao unaonekana ni askari wanaojitoa kwa dhati kutimiza wajibu wao.
Hii inaashiria ni namna gani mama huyu RPC~NEEMA MWANGA anavyounganisha timu yake.
Hongera sana mama. Wewe pamoja na mkuu wa mkoa mama Halima Dendegu mnautendea vyema mkoa wa Mtwara.

Bila shaka huko pia mikoani mlipo hali ya utulivu imetawala.
 
Back
Top Bottom