Pongezi Rais Magufuli na Awamu Yake ya Tano, Wafanya Maajabu Vita Dhidi ya Umasikini, Tanzania Yaongoza Dunia Kupunguza Umasikini Uliotopea-WB.

Wanabodi,
Naendelea kusisitiza kwenye mazuri, tupongeze, kwenye mabaya tukosoe,kwenye maovu tulaani, kwenye mapungufu tushauri na kutoa mapendekezo.

Leo nilikuwa napitia ripoti ya Benki ya Dunia(WB) kuhusu hatua ambazo zimechukuliwa na nchi mbalimbali kupunguza umasikini uliotopea, I was surprised kukuta Tanzania ndio nchi ya kwanza inayoongoza duniani kwa kupiga hatua kubwa zaidi kuondoa umasikini uliotopea, hivyo japo data ni miaka iliyopita, lakini ripoti ni mwaka huu!, hapa tunajadili ripoti ya 2019 na sio data ni za lini, hivyo Rais Magufuli na serikali yake ya Awamu ya Tano, wanastahili pongezi za dhati kwa kufanya maajabu makubwa kabisa katika vita dhidi ya umasikini uliotopea kwa kupiga hatua kubwa zaidi kupunguza idadi ya familia zilizokuwa zinaishi chini ya kipato cha dola moja kwa siku.

Ripoti hiyo ni hii
View attachment 1304778

Hata Hivyo, Ripoti ambayo ni ya mwaka huu 2019 imeonyesha data za Tanzania kuongoza kwa kupungunguza umasikini uliotopea, zilikusanywa katika kipindi cha miaka 10 tangu 2000 hadi 2011 ila haikusema in details, Tanzania imefanya nini katika kupunguza umasikini huo, naomba tuisome ripoti hii kwa kanuni ya "the end justify the means, kwasababu kwa sasa Tanzania ni Tanzania ya Magufuli, na Tanzania ndio inayoongoza kwa kupunguza umasikini, regardless ni kipindi cha nani umasikini huo ulipungua, as long as ripoti ndio imetoka sasa na Tanzania tunaongoza, then ni haki na halali kabisa pongezi hizi ziende kwa Magufuli na awamu yake ya tano, ila pia kwa vile najua kuna kazi nzuri inayofanywa na TASAF, kwenye ule mpango wa kunusuru kaya masikini, huku MKURABITA, ukirasimisha rasilimali na biashara za wanyonge, na hatua nyingine mbalimbali zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya tano katika kupunguza umasikini na kuinua kipato.

Wajameni, taarifa hii ni kwa mujibu wa datas za kuaminini za WB, maana humu jf kumezuka mtindo wa kubeza tuu kila kizuri kinachofanywa na awamu hii. Kwa vile mimi sio mchumi, hata ule ukuaji wa uchumi wa taifa wa zaidi ya asilimia 7% kwa mwaka, ulikuwa unanitatiza kwa sababu nikiangalia hali halisi huku mitaani mambo yanakuwa ni magumu sana, na kujiuliza huo ukuaji wa uchumi wa zaidi asilimia 7% unamfaidia nani, ni mpaka mchumi wetu Number 1 aliponifafanulia ndipo nikaelewa.

Hivyo hata bandiko hili, kama familia yako sii miongoni mwa kaya zinazoishi kwa kipato cha chini ya dola 1 kwa siku, unaweza usielewe kuwa Rais Magufuli na awamu yake ya tano, wanafanya mambo makubwa mazuri ya kuleta maendeleo kwa taifa letu.

Hongera rana rais Magufuli na kikosi kazi chako cha awamu ya 5, inawezekana kabisa sisi Watanzania, tusione, lakini kama World Bank wameona, dunia imeona, wasioona sasa wataonyeshwa.

Na kwa vile mwaka ujao ni mwaka wa uchaguzi mkuu, kuna wanasiasa ambao watapanda jukwaani na kujinadi kuwamkituchagua tutafanya hiki na hiki na hiki, lakini kuna wengine, watapanda jukwaani sio tuu kusema, bali kuonyesha walichofanya, hivyo naomba kuwaandaa watu kisaikolojia, usije kufika muda huo, watu ambao hawana chochote cha kuonyesha kuwa wamefanya, watakatakiwa kupanda kilingeni na watu wenye good track records za waliyoyafanya, kisha wasio na kitu wakaamua kuweka tena mpira kwapani, nashauri tuu, lets save time, money and resources, kama Watanzania tunachotaka ni maendeleo, na maendeleo hayo yanapatikana, yanaonekanika, then kwa nini tusiwaache tuu tuendelee tuu bila kufanya ....
naomba nisimalizie watu wasije kuniparura bure humu.

Maendeleo haya mazuri ya vita dhidi ya umasikini pia yamezungumzwa kwenye ripoti hii ya UNDP

Nawatakia maandalizi mema ya kuingia 2020!.
Paskali

Report zikisema mambo mabaya inakuwa ni mabeberu hawana nia njema na sisi ila report za hao hao zikisema mambo mema tunaungana nao na kujivunia uwepo wao 😂
 
Rais Magufuli anapopewaga Salaam za pongezi kwa Uhuru na Jamhuri, huwa anapongezewa nini?. Kwani Uhuru kaleta yeye?. Hapa hatuzungumzii data collected lini, inazungumziwa ni ripoti ya mwaka huu.
Pongezi ni kwa Magufuli na awamu yake.
P
Tuna mpongeza rais wa JMT katika kumbukumbu ya miaka 58 ya Uhuru.

Ama

TBC inampongeza rais wa JMT kwa kupata uhuru.

Hongera rais Magufuli kwa miaka 58 ya uhuru..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sema ww jamaa unajuhudi sana .sijui kwanini hupatagi teuzi .au nyota huna.
Hili Lijamaa linazeeka vibaya.
Unazeeka vibaya ww .
Mkuu Adudala Kovu, nikijipima hoja zangu za sasa nikilinganisha na nilipokuwa Kijana, na yale maswali yangu ya kiti moto type, kiukweli nazeeka vizuri, maana ningeendelea vile, saa hizi ingekuwa ni kitambo usawa wa kiroba if I was lucky if not I would have disappeared into thin air kama Azory Gwanda na Ben Saanane.
P
 
Hua anapewa pongezi za kuleta Uhuru au za kuadhimisha siku ya Uhuru ? Pongezi za kuleta uhuru hua anapewa baba wa taifa yy anapewa za kuazimisha tu siku ya uhuru ,Mbona mfano wako unapingana na uhalisia , kumbe wakati mwingine hua huhusishi ubongo kwenye kufikiri
Rais Magufuli anapopewaga Salaam za pongezi kwa Uhuru na Jamhuri, huwa anapongezewa nini?. Kwani Uhuru kaleta yeye?. Hapa hatuzungumzii data collected lini, inazungumziwa ni ripoti ya mwaka huu.
Pongezi ni kwa Magufuli na awamu yake.
P

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanabodi,
Naendelea kusisitiza kwenye mazuri, tupongeze, kwenye mabaya tukosoe,kwenye maovu tulaani, kwenye mapungufu tushauri na kutoa mapendekezo.

Leo nilikuwa napitia ripoti ya Benki ya Dunia(WB) kuhusu hatua ambazo zimechukuliwa na nchi mbalimbali kupunguza umasikini uliotopea, I was surprised kukuta Tanzania ndio nchi ya kwanza inayoongoza duniani kwa kupiga hatua kubwa zaidi kuondoa umasikini uliotopea, hivyo japo data ni miaka iliyopita, lakini ripoti ni mwaka huu!, hapa tunajadili ripoti ya 2019 na sio data ni za lini, hivyo Rais Magufuli na serikali yake ya Awamu ya Tano, wanastahili pongezi za dhati kwa kufanya maajabu makubwa kabisa katika vita dhidi ya umasikini uliotopea kwa kupiga hatua kubwa zaidi kupunguza idadi ya familia zilizokuwa zinaishi chini ya kipato cha dola moja kwa siku.

Ripoti hiyo ni hii
View attachment 1304778

Hata Hivyo, Ripoti ambayo ni ya mwaka huu 2019 imeonyesha data za Tanzania kuongoza kwa kupungunguza umasikini uliotopea, zilikusanywa katika kipindi cha miaka 10 tangu 2000 hadi 2011 ila haikusema in details, Tanzania imefanya nini katika kupunguza umasikini huo, naomba tuisome ripoti hii kwa kanuni ya "the end justify the means, kwasababu kwa sasa Tanzania ni Tanzania ya Magufuli, na Tanzania ndio inayoongoza kwa kupunguza umasikini, regardless ni kipindi cha nani umasikini huo ulipungua, as long as ripoti ndio imetoka sasa na Tanzania tunaongoza, then ni haki na halali kabisa pongezi hizi ziende kwa Magufuli na awamu yake ya tano, ila pia kwa vile najua kuna kazi nzuri inayofanywa na TASAF, kwenye ule mpango wa kunusuru kaya masikini, huku MKURABITA, ukirasimisha rasilimali na biashara za wanyonge, na hatua nyingine mbalimbali zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya tano katika kupunguza umasikini na kuinua kipato.

Wajameni, taarifa hii ni kwa mujibu wa datas za kuaminini za WB, maana humu jf kumezuka mtindo wa kubeza tuu kila kizuri kinachofanywa na awamu hii. Kwa vile mimi sio mchumi, hata ule ukuaji wa uchumi wa taifa wa zaidi ya asilimia 7% kwa mwaka, ulikuwa unanitatiza kwa sababu nikiangalia hali halisi huku mitaani mambo yanakuwa ni magumu sana, na kujiuliza huo ukuaji wa uchumi wa zaidi asilimia 7% unamfaidia nani, ni mpaka mchumi wetu Number 1 aliponifafanulia ndipo nikaelewa.

Hivyo hata bandiko hili, kama familia yako sii miongoni mwa kaya zinazoishi kwa kipato cha chini ya dola 1 kwa siku, unaweza usielewe kuwa Rais Magufuli na awamu yake ya tano, wanafanya mambo makubwa mazuri ya kuleta maendeleo kwa taifa letu.

Hongera rana rais Magufuli na kikosi kazi chako cha awamu ya 5, inawezekana kabisa sisi Watanzania, tusione, lakini kama World Bank wameona, dunia imeona, wasioona sasa wataonyeshwa.

Na kwa vile mwaka ujao ni mwaka wa uchaguzi mkuu, kuna wanasiasa ambao watapanda jukwaani na kujinadi kuwamkituchagua tutafanya hiki na hiki na hiki, lakini kuna wengine, watapanda jukwaani sio tuu kusema, bali kuonyesha walichofanya, hivyo naomba kuwaandaa watu kisaikolojia, usije kufika muda huo, watu ambao hawana chochote cha kuonyesha kuwa wamefanya, watakatakiwa kupanda kilingeni na watu wenye good track records za waliyoyafanya, kisha wasio na kitu wakaamua kuweka tena mpira kwapani, nashauri tuu, lets save time, money and resources, kama Watanzania tunachotaka ni maendeleo, na maendeleo hayo yanapatikana, yanaonekanika, then kwa nini tusiwaache tuu tuendelee tuu bila kufanya ....
naomba nisimalizie watu wasije kuniparura bure humu.

Maendeleo haya mazuri ya vita dhidi ya umasikini pia yamezungumzwa kwenye ripoti hii ya UNDP

Nawatakia maandalizi mema ya kuingia 2020!.
Paskali
Hivi Paschali huwa unakosa vitu vya kuandika hapa jukwaani ?, yaani wewe kazi yako ni kusifia tu hili liserikali ?, mbona kuna mambo mengi sana ya msingi ya kuandika ili kuwajulisha wananchi ambayo kimsingi yana maslahi kwao ??, kwa mfano Ukosefu wa Madawa kaktika hospitali za serikali ?!, au wanafunzi zaidi ya 140,000 ambao watashindwa kujiunga na kidato cha kwanza hapo mwezi january kwa kukosa madarasa katika shule za sekondari za serikali ?!, cha kushangaza kabisa hiyo ripoti inasema taarifa ya kuanzia mwaka 2000 mapaka 2011, lakini wewe unatuambia pongezi kwa serikali ya awamu ya 5 ya magufuli !!
Ukichukuliwa hatua za kisheria kwa kutoa ripoti tata utalaumu ?, ukiitwa Bungeni kwenda kuhojiwa na kamati ya bunge ya nidhamu utalalamika umeonewa, unajua kwamba ni kosa kuzungumzia takwimu ilhali wewe sio mtumishi wa idara ya takwimu, jifunze kuandika mambo tofauti na ngonjera hizi, unatuchafua roho sana wengine, wakati wa Utawala wa awamu ya kwanza ya Mwalim Julius Kambarage Nyerere hakukuwa na waimba ngojera kama tunaoshuhudia sasa hivi, sijui shida ni nini ?!!, hata Mzee Kikwete aliwahi kuwakaripia wapambe waliokuwa wanajifanya kumsifia sifia.
 
Mkuu Adudala Kovu, nikijipima hoja zangu za sasa nikilinganisha na nilipokuwa Kijana, na yale maswali yangu ya kiti moto type, kiukweli nazeeka vizuri, maana ningeendelea vile, saa hizi ingekuwa ni kitambo usawa wa kiroba if I was lucky if not I would have disappeared into thin air kama Azory Gwanda na Ben Saanane.
P
Kwa hiyo Paschali umeacha kuandika hoja za msingi kwa sababu unaogopa kupotezwa !?, kwa hiyo umeacha kuandika ulichokuwa unaamini, ?!, sikutaraji kwa umri wako huo unaweza kuwa bado muoga hivyo, bora ungekaa kimya ujifanye shujaa, kwa sababu mwanaume huwa hajitangazii uoga, lakini pia (nikiamini wewe ni mkristo) hata Biblia imeandika "Waoga wote hawatweza kuuona Ufalme wa Mungu"
 
Report zikisema mambo mabaya inakuwa ni mabeberu hawana nia njema na sisi ila report za hao hao zikisema mambo mema tunaungana nao na kujivunia uwepo wao 😂
Mkuu umenena kweli, hao hao WB wakisema serikali inakiuka Haki za Binadamu anakuja kabudi hapa na kusema hawa mabeberu wasituingiie eti hii ni nchi huru, na Pasco hushangilia, leo WB wame
 
Kwa hiyo Paschali umeacha kuandika hoja za msingi kwa sababu unaogopa kupotezwa !?, kwa hiyo umeacha kuandika ulichokuwa unaamini, ?!, sikutaraji kwa umri wako huo unaweza kuwa bado muoga hivyo, bora ungekaa kimya ujifanye shujaa, kwa sababu mwanaume huwa hajitangazii uoga, lakini pia (nikiamini wewe ni mkristo) hata Biblia imeandika "Waoga wote hawatweza kuuona Ufalme wa Mungu"
Ni uzee ndio unanijia ki hivi, more mature, more conscious, more reasonable, more considerate and doing more responsible journalism.

Hilo la Ufalme wa Mungu, tunaokolewa kwa neema tuu na sio kwa matendo. Uoga ni matendo, kama neema ipo, ipo tuu, tutakutana mbinguni na nikikukuta nitakukumbusha.
P
 
Pascal Mayalla Walioko mitaani na wananchi ndo wanajua wenyewe kama umasikini ume wapungukia au umezidi.
Graduates ndio wanajua kama kazi zipo bwerere unachagua.
Na walioko kazini wanajua kama mshahara unakidhi mahitaji.
Na hata Wakuu wa nchi wanajua pia kuwa mazingira waloweka biashara zinakua na kodi itaongezeka . Naamini wanajua ukweli
Mfano mimi nilikua na biashara turnover yangu kabla ya 2015 ilikua 3.5 bilion kwa mwaka
Si haba.
Mkuu Bopwe, hii report ni ripoti ya kundi la watu wale wanaoishi kwenye Lindi la umasikini uliotopea wa kipato cha chini ya dola 1 kwa siku. Wewe wa 3.5 B pa wewe ni tajiri kwa sababu hiyo turn over yako kwa miaka yote kumi ya Magufuli, take home yake haifiki hata nusu ya hiyo, hivyo wewe sii mwenzetu kabisa. Walengwa hapa ni wale wanufaika wa TASAF kupitia ule mpango wa kunusuru kaya masikini.
P
 
Mkuu Adudala Kovu, nikijipima hoja zangu za sasa nikilinganisha na nilipokuwa Kijana, na yale maswali yangu ya kiti moto type, kiukweli nazeeka vizuri, maana ningeendelea vile, saa hizi ingekuwa ni kitambo usawa wa kiroba if I was lucky if not I would have disappeared into thin air kama Azory Gwanda na Ben Saanane.
P
Hapo umekuwa Mkweli! Hata kuna clip moja ya Prof Safari amekusifia kwa swali lile ulilomuuliza Mkuu. Nami nimekuwa nikikuheshimu kwa swali hilo. Ila sasa umekengeuka (labda kama unaandika kinyume cha ukweli wako- maana na hiyo ni aina nzuri ya uandishi katika awamu hii ya mauaji ya wana habari) kwa kuunga juhudi mauaji, uvunjifu wa katiba, utekaji etc
 
Ni uzee ndio unanijia ki hivi, more mature, more conscious, more reasonable, more considerate and doing more responsible journalism.

Hilo la Ufalme wa Mungu, tunaokolewa kwa neema tuu na sio kwa matendo. Uoga ni matendo, kama neema ipo, ipo tuu, tutakutana mbinguni na nikikukuta nitakukumbusha.
P
Askofu Niwemugizi alisema kweli, watu ambao wangetarajiwa ku fight for this nation Humar rights (below 60 years old) ndio hao wanakuwa waoga, wale waliochoka (above 60 years Old) ndio wanahangaika kutafuta kupigania Uhuru wa mtu mmoja mmoja), ni aibu kwa Paschali
 
Validity ya ripoti ni date of publication na sio data zilikuwa collected lini??!!...kweli???!...unachoweza kuipongeza serikali (kama kweli kipo cha kupongeza) ni kwa kuwezesha ripoti kutolewa. Lakini hata hivyo sio wao walioitoa, kwahiyo kwa kifupi hapo hakuna cha kupongeza.

Sent using Jamii Forums mobile app
Five years ago, ulipata safari ya Ghana kuhudhuria African Public Service Day, akukutana na kente ya ukweli ukamnunulia mkeo zawadi ya gauni zuri la kente. Alipolijaribu, halikumfiti hivyo hakulivaa kwa sababu alikuwa ana breastfed again excessive weight, sasa ame trim gauni limemfit, amelivaa this Christmastime, kila anayemuona anamsifia alivyopendeza na alivyotokelezea, na kila baada ya kuaifiwa kuwa kapendeza, anaulizwa umelinunua wapi na mimi nikanunue, si unajua tena mambo ya wanawake, akiona mwenzake kapendeza na yeye lazima atataka kupendeza kivile!. Hapo hapo mkeo huwaambia nililetewa na mr wangu toka safari, hivyo wewe hawawezi kukuuliza ulinunua wapi bali unapewa tuu pongezi za kumpendezesha mkeo Christmas hii, wewe kazi yako ni kusema tuu asante. Jee pongezi unazopewa wewe leo kwa kumpendezesha mkeo kwa kumnunulia gauni zuri la Christmas, utazikataa kwa kusema no sikulinunua leo nilinunua 5 years ago?.

Ripoti ya Tanzania kuongoza ni ripoti ya mwaka huu. Hata kama data ni za 2011, data hizo ndio zimetupa ushindi leo, na ni ushindi wa jumla tumeongoza dunia nzima leo na sio huo mwaka 2011. Pongezi za ripoti hiyo zinashuka kwa Magufuli kwa jinsi ile ile unavyosifiwa leo kwa kumpendezesha mkeo kwa kente kali ya five years before.

P
 
Hapo umekuwa Mkweli! Hata kuna clip moja ya Prof Safari amekusifia kwa swali lile ulilomuuliza Mkuu. Nami nimekuwa nikikuheshimu kwa swali hilo. Ila sasa umekengeuka (labda kama unaandika kinyume cha ukweli wako- maana na hiyo ni aina nzuri ya uandishi katika awamu hii ya mauaji ya wana habari) kwa kuunga juhudi mauaji, uvunjifu wa katiba, utekaji etc
Naomba nitafutie hiyo clip ya Prof. Safari, ni mwalimu wangu pale UDSM, hata Prof. Shivji, Prof. Kabudi, Prof. Juma, Prof. Mchome, Dr. Mwakyembe, Dr. Tulia etc.
P
 
Five years ago, ulipata safari ya Ghana kuhudhuria African Public Service Day, akukutana na kente ya ukweli ukamnunulia mkeo zawadi ya gauni zuri la kente. Alipolijaribu, halikumfiti hivyo hakulivaa kwa sababu alikuwa ana breastfed again excessive weight, sasa ame trim gauni limemfit, amelivaa this Christmastime, kila anayemuona anamsifia alivyopendeza na alivyotokelezea, na kila baada ya kuaifiwa kuwa kapendeza, anaulizwa umelinunua wapi na mimi nikanunue, si unajua tena mambo ya wanawake, akiona mwenzake kapendeza na yeye lazima atataka kupendeza kivile!. Hapo hapo mkeo huwaambia nililetewa na mr wangu toka safari, hivyo wewe hawawezi kukuuliza ulinunua wapi bali unapewa tuu pongezi za kumpendezesha mkeo Christmas hii, wewe kazi yako ni kusema tuu asante. Jee pongezi unazopewa wewe leo kwa kumpendezesha mkeo kwa kumnunulia gauni zuri la Christmas, utazikataa kwa kusema no sikulinunua leo nilinunua 5 years ago?.

Ripoti ya Tanzania kuongoza ni ripoti ya mwaka huu. Hata kama data ni za 2011, data hizo ndio zimetupa ushindi leo, na ni ushindi wa jumla tumeongoza dunia nzima leo na sio huo mwaka 2011. Pongezi za ripoti hiyo zinashuka kwa Magufuli kwa jinsi ile ile unavyosifiwa leo kwa kumpendezesha mkeo kwa kente kali ya five years before.

P
Huu mfano ni wa ki zwazwa, huyo Bwana alinunua yeye hiyo nguo hata kama ingekuwa imepita miaka 100 bado angestahili kupongezwa kwa sababu huyu mkewe hakuwa na mme mwingine before, mafanikio uliyoyasema yamefanywa na seikali iliyokuwa kwenye Power kati ya mwaka 2000 mpaka 2011, sielewi ni kitu gani unalazimisha hapa, wapo wanaostahili waliofanya hizo jitihada, hata kama wangekuwa wamekufa tungewapongeza tu na sio huyu mtekaji wa watu
 
Naomba nitafutie hiyo clip ya Prof. Safari, ni mwalimu wangu pale UDSM, hata Prof. Shivji, Prof. Kabudi, Prof. Juma, Prof. Mchome, Dr. Mwakyembe, Dr. Tulia etc.
P
Hata mimi hiyo Clip niliiona, ulikuwa mtu wa maana kweli, sasa sijui huenda yale hayakuwa yanatoka kwenye kichwa chako !!, huyu sio Paschali niliyemhusudu, Prof Assad anashangaa sana, kuna mambo mengi saana ya muhimu hayasemwi hapa nchini
 
22 Reactions
Reply
Back
Top Bottom