hp4510
JF-Expert Member
- Jan 16, 2012
- 6,451
- 6,325
Wanabodi,
Naendelea kusisitiza kwenye mazuri, tupongeze, kwenye mabaya tukosoe,kwenye maovu tulaani, kwenye mapungufu tushauri na kutoa mapendekezo.
Leo nilikuwa napitia ripoti ya Benki ya Dunia(WB) kuhusu hatua ambazo zimechukuliwa na nchi mbalimbali kupunguza umasikini uliotopea, I was surprised kukuta Tanzania ndio nchi ya kwanza inayoongoza duniani kwa kupiga hatua kubwa zaidi kuondoa umasikini uliotopea, hivyo japo data ni miaka iliyopita, lakini ripoti ni mwaka huu!, hapa tunajadili ripoti ya 2019 na sio data ni za lini, hivyo Rais Magufuli na serikali yake ya Awamu ya Tano, wanastahili pongezi za dhati kwa kufanya maajabu makubwa kabisa katika vita dhidi ya umasikini uliotopea kwa kupiga hatua kubwa zaidi kupunguza idadi ya familia zilizokuwa zinaishi chini ya kipato cha dola moja kwa siku.
Ripoti hiyo ni hii
View attachment 1304778Year in Review: 2019 in 14 Charts
These charts highlight some remarkable achievements and the serious challenges that remain as we head into 2020.t.newsletterext.worldbank.org
Hata Hivyo, Ripoti ambayo ni ya mwaka huu 2019 imeonyesha data za Tanzania kuongoza kwa kupungunguza umasikini uliotopea, zilikusanywa katika kipindi cha miaka 10 tangu 2000 hadi 2011 ila haikusema in details, Tanzania imefanya nini katika kupunguza umasikini huo, naomba tuisome ripoti hii kwa kanuni ya "the end justify the means, kwasababu kwa sasa Tanzania ni Tanzania ya Magufuli, na Tanzania ndio inayoongoza kwa kupunguza umasikini, regardless ni kipindi cha nani umasikini huo ulipungua, as long as ripoti ndio imetoka sasa na Tanzania tunaongoza, then ni haki na halali kabisa pongezi hizi ziende kwa Magufuli na awamu yake ya tano, ila pia kwa vile najua kuna kazi nzuri inayofanywa na TASAF, kwenye ule mpango wa kunusuru kaya masikini, huku MKURABITA, ukirasimisha rasilimali na biashara za wanyonge, na hatua nyingine mbalimbali zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya tano katika kupunguza umasikini na kuinua kipato.
Wajameni, taarifa hii ni kwa mujibu wa datas za kuaminini za WB, maana humu jf kumezuka mtindo wa kubeza tuu kila kizuri kinachofanywa na awamu hii. Kwa vile mimi sio mchumi, hata ule ukuaji wa uchumi wa taifa wa zaidi ya asilimia 7% kwa mwaka, ulikuwa unanitatiza kwa sababu nikiangalia hali halisi huku mitaani mambo yanakuwa ni magumu sana, na kujiuliza huo ukuaji wa uchumi wa zaidi asilimia 7% unamfaidia nani, ni mpaka mchumi wetu Number 1 aliponifafanulia ndipo nikaelewa.
Hivyo hata bandiko hili, kama familia yako sii miongoni mwa kaya zinazoishi kwa kipato cha chini ya dola 1 kwa siku, unaweza usielewe kuwa Rais Magufuli na awamu yake ya tano, wanafanya mambo makubwa mazuri ya kuleta maendeleo kwa taifa letu.
Hongera rana rais Magufuli na kikosi kazi chako cha awamu ya 5, inawezekana kabisa sisi Watanzania, tusione, lakini kama World Bank wameona, dunia imeona, wasioona sasa wataonyeshwa.
Na kwa vile mwaka ujao ni mwaka wa uchaguzi mkuu, kuna wanasiasa ambao watapanda jukwaani na kujinadi kuwamkituchagua tutafanya hiki na hiki na hiki, lakini kuna wengine, watapanda jukwaani sio tuu kusema, bali kuonyesha walichofanya, hivyo naomba kuwaandaa watu kisaikolojia, usije kufika muda huo, watu ambao hawana chochote cha kuonyesha kuwa wamefanya, watakatakiwa kupanda kilingeni na watu wenye good track records za waliyoyafanya, kisha wasio na kitu wakaamua kuweka tena mpira kwapani, nashauri tuu, lets save time, money and resources, kama Watanzania tunachotaka ni maendeleo, na maendeleo hayo yanapatikana, yanaonekanika, then kwa nini tusiwaache tuu tuendelee tuu bila kufanya ....
naomba nisimalizie watu wasije kuniparura bure humu.
Maendeleo haya mazuri ya vita dhidi ya umasikini pia yamezungumzwa kwenye ripoti hii ya UNDP
Ripoti: Kiwango cha umasikini kinapungua kwa kasi
Dodoma. Poverty in Tanzania has decreased from 64 per cent in 2015 to 47.4 per cent in 2017, according to the 2017 Tanzania Human Development (THDR). The government in collaboration with the Economic and Social Research Foundation and UNDP yesterday unveiled the HDR in a ceremony officiated by...www.jamiiforums.com
Nawatakia maandalizi mema ya kuingia 2020!.
Paskali
Report zikisema mambo mabaya inakuwa ni mabeberu hawana nia njema na sisi ila report za hao hao zikisema mambo mema tunaungana nao na kujivunia uwepo wao 😂