Pongezi Rais Magufuli na Awamu Yake ya Tano, Wafanya Maajabu Vita Dhidi ya Umasikini, Tanzania Yaongoza Dunia Kupunguza Umasikini Uliotopea-WB.

You are wrong my bro!! Pongezi ziende kwa wale waliokuwa hicho kipindi. Mkuu unapotosha kwa makusudi. Taifa linawategemea wasomi kama ninyi, ila mnatuangusha, hata habari mnazotoa ni za kupotosha badala ya ukweli. Ni kwa nini usingetafuta ripoti currently ili ku-validate unachosema mkuu?!
Mkuu Msnajo, kiukweli umeuliza swali la msingi sana, ambalo jibu lake linanisaidia sana kuwaelimisha hawa vichwa maji tunaobishana nao humu kuhusu ripoti hii. World Bank ni moja ya taasisi zinazoongoza kwa kufanya tafiti, tafiti hii ya kupunguza umasikini imetumia sampling za 2000-2015, halafu ripoti imetolewa 2019. Kitendo cha kuniuliza "Ni kwa nini usingetafuta ripoti currently ili ku-validate unachosema mkuu?!", ni uthibitisho na wewe pia ni mmoja wa hawa hawa vilaza wa humu ambao mkiwekewa link hamsomi, nimeweka link, ripoti hii ni ya mwaka huu!, hivyo kuulizia the current report ni ukilaza tuu wa wewe kutosoma kuwa hii repoti ni ya Dec, 2019, hivyo ni very current!. Swali labda lingekuwa kwanini utumie data za 2011 kutoa report ya 2019, hili sasa sio langu, ni la WB.
P
 
Mkuu Masiya, Ripoti hii ni Ripoti ya 2019!. Jambo lolote jema au baya, siku linapotangazwa, pongezi au lawama zinakwenda kwa utawala uliopo madarakani kipindi ripoti inatolewa.

Mfano sisi tumepata uhuru mwaka 1961. Tanzania ni mwanachama wa EAC nyenye nchi 5. Ukifanywa Research ya Nchi za EAC zilizoongoza kwa hukumu ya kunyonga ndani ya miaka 50, Nyerere alinyonga watu wawili, Mwamwindi na yule mhindi aliyemua mkewe ili alipwe bima. Mwinyi alinyonga kadhaa idadi haikutangazwa, Mkapa hakunyonga, Kikwete hakunyonga, Magufuli hakunyonga na wala hatanyonga. Lakini kutokana na walionyongwa kipindi cha Mwinyi, ripoti ikitoka mwaka huu 2019, na kuonyesha Tanzania ndio nchi iliyoongoza Afrika Mashariki kwa kunyonga ndani ya kipindi cha miaka 50 iliyopita, ni nani atalaumiwa?. Ni rais wa sasa wa Tanzania, hata kama katika kipindi chake hajanyonga hata mtu mmoja!. Unadhani Magufuli atasoma ripoti na kusema msinilaumu mimi, mlaumuni Mwinyi ndiye aliyenyonga, mimi sijanyonga!.

Ripoti ni ya mwaka huu inaonyesha Tanzania ndio inaongoza dunia kwa kupunguza umasikini, maadam ripoti ni ya mwaka huu, then pongezi kwa ushindi huu ni kwa serikali iliyopo madarakani kwa sasa.
Hongera Magufuli.
P
Na tutaandika kichwa cha habari;
PONGEZI RAIS MAGUFULI, AWAMU YA TANO IMENYONGA WATU WENGI!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Msnajo, kiukweli umeuliza swali la msingi sana, ambalo jibu lake linanisaidia sana kuwaelimisha hawa vichwa maji tunaobishana nao humu kuhusu ripoti hii. World Bank ni moja ya taasisi zinazoongoza kwa kufanya tafiti, tafiti hii ya kupunguza umasikini imetumia sampling za 2000-2015, halafu ripoti imetolewa 2019. Kitendo cha kuniuliza "Ni kwa nini usingetafuta ripoti currently ili ku-validate unachosema mkuu?!", ni uthibitisho na wewe pia ni mmoja wa hawa hawa vilaza wa humu ambao mkiwekewa link hamsomi, nimeweka link, ripoti hii ni ya mwaka huu!, hivyo kuulizia the current report ni ukilaza tuu wa wewe kutosoma kuwa hii repoti ni ya Dec, 2019, hivyo ni very current!. Swali labda lingekuwa kwanini utumie data za 2011 kutoa report ya 2019, hili sasa sio langu, ni la WB.
P

Bado sana kaka, kwa ukilaza wangu hakukupi uhalali wa wewe kutumia information za mwaka 2011 kusifia 2019. Tafiti ni tafiti, na ripoti ni ripoti. Kuna mengi yametokea toka hicho kipindi mpaka leo! Ulipaswa kujiongeza kidogo tu, hata WB ni watu, sio miungu kwamba wapo perfect bro!! Na kuna uwezekano toka huo muda hakuna utafiti uliofanyika, na ndio maana wakatumia hizo data za zamani, so wewe ungejiuliza hicho kipindi hadi leo kuna uhalali wa kusifia awamu ya tano na sio ya tatu na ya nne?! Kwa nini hukuziona awamu zilizo katika kipindi husika?! Kwa mfano nikuulize swali, hali iliyopo leo ni sawa na ilivyokuwa 2011 kijamii, kiuchimi na kisiasa? Ukijibu hapa nitajua nawe sio kilaza. Unataka kuniambia data za mwaka 1970 tukizi publish leo utasema ni recent information?
 
Kwa mfano nikuulize swali, hali iliyopo leo ni sawa na ilivyokuwa 2011 kijamii, kiuchimi na kisiasa? Ukijibu hapa nitajua nawe sio kilaza. Unataka kuniambia data za mwaka 1970 tukizi publish leo utasema ni recent information?
Kwa vile sijafanya research, hivyo hapa naomba niite tuu kilaza.
Mwaka kesho ikizinduliwa Ripoti ya Miaka 50 ya Maonyesho Japan, Banda la Tanzania Limetia Fora, Pongezi zitakwenda kwa rais Magufuli, ila ukisoma hilo banda la Tanzania lilitia fora lini, lilitia fora mwaka 1970 wakati Tanzania ilipeleka kikosi cha wasanii 100 nchini Japan kushiriki Maonyesho Japan, Banda la Tanzania ndio liliongoza kwa ukubwa, wingi wa wasanii, na kuongoza kwa kivutio, bendi mbili za muziki, Afro 70 na Moro Jazz, Ikampeleka Mzee Morisi na ngoma zake 10, Ikampeleka Mzee Mayagilo na Bendi ya Polisi, ikampeleka Mzee Mwinamila na ngoma za asili na kujuisha wasanii wa fani zote. Toka mwaka huo 1970 mpaka leo hakuna nchi iliyovunja rekodi ya Tanzania, katika maadhimisho ya miaka 50 ya maonyesho Japan, mwakani 2020, pongezi zitakwenda kwa Magufuli kwasababu ni ripoti ya 2020 na the current regime ni ya Magufuli.
P
 
Watanzania tujifunze kusoma ni ripoti ya lini!. Ripoti hii ni Ripoti ya mwaka 2019 regardless data zilikuwa collected lini, validity ya ripoti yoyote ni the date of publication of the report na sio dates of data collection, hivyo as of now, Tanzania ndio inaongoza kwa kupunguza umasikini uliotopea kwa mwaka huu 2019!.
P
Mtani Pascal usitufanye mazuzu,kwa ripoti hiyo , jina mh.Magufuli linakuja je kwenye uzi hata kama ripoti ni ya 2019.Hizo pongezi mwaka 2020 au mwingine wowote taarifaa zikija kinyume utamlaumu nani huyo huyo mheshimiwa au?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
054CECA8-C6EA-48BE-B9B7-095043C7B5A2.jpeg

PHD holder akinywa kikombe kwa babu
 
Mkuu Msnajo, kiukweli umeuliza swali la msingi sana, ambalo jibu lake linanisaidia sana kuwaelimisha hawa vichwa maji tunaobishana nao humu kuhusu ripoti hii. World Bank ni moja ya taasisi zinazoongoza kwa kufanya tafiti, tafiti hii ya kupunguza umasikini imetumia sampling za 2000-2015, halafu ripoti imetolewa 2019. Kitendo cha kuniuliza "Ni kwa nini usingetafuta ripoti currently ili ku-validate unachosema mkuu?!", ni uthibitisho na wewe pia ni mmoja wa hawa hawa vilaza wa humu ambao mkiwekewa link hamsomi, nimeweka link, ripoti hii ni ya mwaka huu!, hivyo kuulizia the current report ni ukilaza tuu wa wewe kutosoma kuwa hii repoti ni ya Dec, 2019, hivyo ni very current!. Swali labda lingekuwa kwanini utumie data za 2011 kutoa report ya 2019, hili sasa sio langu, ni la WB.
P
Paskali hivi ukipima ukimwi 2015 result ni negative, halafu ukaja yaleta hayo majibu yako 2019 bado yatakuwa valid?
Kwenye andiko lako wewe mwenyewe umeandika "I was surprised kukuta Tanzania ndio nchi ya kwanza inayoongoza duniani kwa kupiga hatua kubwa zaidi kuondoa umasikini uliotopea, hivyo japo data ni miaka iliyopita, lakini ripoti ni mwaka huu!", yaani hata wewe umeshangazwa na hiyo ripoti kwa kuwa unajua hali halisi.
Average of total extreme poverty percentage points change over the circa year 2000-15 (start year - end year). Hata kama repoti ya 2019 lakini data ni za zamani. Hata kwenye ripoti bado wanaeleza "In some of the countries in Sub-Saharan Africa (e.g. Democratic Republic of Congo, Tanzania, Burkina Faso), extreme poverty rates, even after rapid reduction, remain above 40%. Kwa hiyo bado tuna kazi kubwa ya kuondoa umaskini uliyotopea. Tunampongeza Mh. raisi kwa kuichukua nchi ikiwa umaskini uliyotopea umepungua. Kuna mambo mengi ambayo ameyaanzisha ni mazuri ambayo huenda yakakamilika baada kumaliza muda wake, hivyo raisi ajaye anaweza kupewa hongera kwa hayo mambo.
 
Aliyesema Tanzania tunaongoza duniani katika kupunguza umasikini sio mimi wala sio Magufuli, ni Bank ya Dunia, na hawa taarifa zao ni data oriented, numbers don't lie. Sio bla bla ni ripoti ya utafiti wa kina uliofanywa na watafiti wa ukweli.
P
Awamu hii itaturudisha nyuma tena vibaya sana.
 
Mkuu ulichoelewa hebu tuwekee hapa ili wot tuelewe!!
jamaa huwa anaenda kinyume na anachomaanisha.......


msome kwa umakini utaelewa, hapa alichotaka kuonesha ni kwamba awamu hii inarudisha umaskini nchini badala ya kuzidi kupunguza.........


hujiulizi kwanini anasisitiza kwamba taarifa ni za 00-11? hujiulizi kwann anasema hawajaweka details?.... halafu anamalizia kwa kusema hizi takwimu zitatumika kwenye kampeni 2020.......


huyu jamaa ni kama alivyo masudi kipanya, ukikurupuka huwezi kumwelewa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mgeni anapokuja nyumbani, akala akashiba, anamshukuru mwenyeji. Hata house girl wa Kitanga, akipika mahanjumati kama samaki wa nazi wa kupaka kwenye familia ya Wachagga, mgeni akila na kufurahia chakula pongezi ni kwa mama mwenye nyumba wa Kichagga na sio house girl wa Kitanga.

Hata tulipokaribishwa Ikulu, ile ni nyumba yetu, wafanyakazi tunawalipa sisi, chakula tunanunua sisi, wapishi tunawalipa sisi, bado tukila tukashiba, tunamshukuru mwenyeji wetu.

Any credits kwa Tanzania ya sasa, pongezi ni kwa the current regime.
P
For him to get such credit from me personally he would have to wait until the analysis of his regime is given after his retirement. Half of what he is doing in economics is right but the other half especial in the human right, good governance and rule of law i don't agree with him. To vouch if his economic theories and doing have any impact to the whole community he will have to wait. Right now the credit should go to our greatest diplomatic man after Nyerere. He had his flaws but he did something to the whole community whether some of the people got a bigger part of the pie and some didn't at all but all of us had a little share of the pie.
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la pongezi kwa Rais Magufuli na awamu yake ya tano.

Naomba kuanza na angalizo,
Kuna watu wana allergy na pongezi zozote kwa rais Magufuli na awamu yake ya 5, hivyo akifanya jema lolote au akipongezwa kwa zuri lolote, wao wanakasirika. Kwa vile bado tuko kwenye festival season, kama wewe ni mtu wa kundi hili, nakuomba uishie hapa ili tusiharibiane festivals seasons zetu.

Naendelea kusisitiza kwenye mazuri, tupongeze, kwenye mabaya tukosoe,kwenye maovu tulaani, kwenye mapungufu tushauri na kutoa mapendekezo.

Leo nilikuwa napitia ripoti ya Benki ya Dunia(WB) kuhusu hatua ambazo zimechukuliwa na nchi mbalimbali kupunguza umasikini uliotopea, I was surprised kukuta Tanzania ndio nchi ya kwanza inayoongoza duniani kwa kupiga hatua kubwa zaidi kuondoa umasikini uliotopea, hivyo japo data ni miaka iliyopita, lakini ripoti ni mwaka huu!, hapa tunajadili ripoti ya 2019 na sio data ni za lini, hivyo Rais Magufuli na serikali yake ya Awamu ya Tano, wanastahili pongezi za dhati kwa kufanya maajabu makubwa kabisa katika vita dhidi ya umasikini uliotopea kwa kupiga hatua kubwa zaidi kupunguza idadi ya familia zilizokuwa zinaishi chini ya kipato cha dola moja kwa siku.

Ripoti hiyo ni hii
View attachment 1304778

Hata Hivyo, Ripoti ambayo ni ya mwaka huu 2019 imeonyesha data za Tanzania kuongoza kwa kupungunguza umasikini uliotopea, zilikusanywa katika kipindi cha miaka 10 tangu 2000 hadi 2011 ila haikusema in details, Tanzania imefanya nini katika kupunguza umasikini huo, naomba tuisome ripoti hii kwa kanuni ya "the end justify the means, kwasababu kwa sasa Tanzania ni Tanzania ya Magufuli, na Tanzania ndio inayoongoza kwa kupunguza umasikini, regardless ni kipindi cha nani umasikini huo ulipungua, as long as ripoti ndio imetoka sasa na Tanzania tunaongoza, then ni haki na halali kabisa pongezi hizi ziende kwa Magufuli na awamu yake ya tano, ila pia kwa vile najua kuna kazi nzuri inayofanywa na TASAF, kwenye ule mpango wa kunusuru kaya masikini, huku MKURABITA, ukirasimisha rasilimali na biashara za wanyonge, na hatua nyingine mbalimbali zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya tano katika kupunguza umasikini na kuinua kipato.

Wajameni, taarifa hii ni kwa mujibu wa datas za kuaminini za WB, maana humu jf kumezuka mtindo wa kubeza tuu kila kizuri kinachofanywa na awamu hii. Kwa vile mimi sio mchumi, hata ule ukuaji wa uchumi wa taifa wa zaidi ya asilimia 7% kwa mwaka, ulikuwa unanitatiza kwa sababu nikiangalia hali halisi huku mitaani mambo yanakuwa ni magumu sana, na kujiuliza huo ukuaji wa uchumi wa zaidi asilimia 7% unamfaidia nani, ni mpaka mchumi wetu Number 1 aliponifafanulia ndipo nikaelewa.

Hivyo hata bandiko hili, kama familia yako sii miongoni mwa kaya zinazoishi kwa kipato cha chini ya dola 1 kwa siku, unaweza usielewe kuwa Rais Magufuli na awamu yake ya tano, wanafanya mambo makubwa mazuri ya kuleta maendeleo kwa taifa letu.

Hongera rana rais Magufuli na kikosi kazi chako cha awamu ya 5, inawezekana kabisa sisi Watanzania, tusione, lakini kama World Bank wameona, dunia imeona, wasioona sasa wataonyeshwa.

Na kwa vile mwaka ujao ni mwaka wa uchaguzi mkuu, kuna wanasiasa ambao watapanda jukwaani na kujinadi kuwamkituchagua tutafanya hiki na hiki na hiki, lakini kuna wengine, watapanda jukwaani sio tuu kusema, bali kuonyesha walichofanya, hivyo naomba kuwaandaa watu kisaikolojia, usije kufika muda huo, watu ambao hawana chochote cha kuonyesha kuwa wamefanya, watakatakiwa kupanda kilingeni na watu wenye good track records za waliyoyafanya, kisha wasio na kitu wakaamua kuweka tena mpira kwapani, nashauri tuu, lets save time, money and resources, kama Watanzania tunachotaka ni maendeleo, na maendeleo hayo yanapatikana, yanaonekanika, then kwa nini tusiwaache tuu tuendelee tuu bila kufanya ....

Paskali
Update 17/02/20
Shuhudieni live jinsi Awamu ya Tano inavyoondoa umasikini



P

Kiukweli kabisa, nilitaka kusema, Magufuli akipewa kipindi cha pili, ataumaliza kabisa umasikini, naomba kurekebisha, nikisema akipewa ni kama nimeonyesha kuna possibility asipewe, wakati hali halisi ni JPM, ameishashinda zamani, kinachotafutwa sasa ni kura nyingi tuu za kutosha!. Hapo alipo tayari anayo over 80% victory, tunahangaikia ipande hadi 90%, na wiki ya lala salama, tufike over 95%.
Kwa maendeleo ya Tanzania,
Chagua Magufuli,
Chagua CCM,
na kwa jimbo langu la KAWE, Twende na GwajiBoy!.
P
 
Kiukweli kabisa, nilitaka kusema, Magufuli akipewa kipindi cha pili, ataumaliza kabisa umasikini, naomba kurekebisha, nikisema akipewa ni kama nimeonyesha kuna possibility asipewe, wakati hali halisi ni JPM, ameishashinda zamani, kinachotafutwa sasa ni kura nyingi tuu za kutosha!. Hapo alipo tayari anayo over 80% victory, tunahangaikia ipande hadi 90%, na wiki ya lala salama, tufike over 95%.
Kwa maendeleo ya Tanzania,
Chagua Magufuli,
Chagua CCM,
na kwa jimbo langu la KAWE, Twende na GwajiBoy!.
P
Acha kujiaminisha uongo . Izo takwimu feki unazitoa wapi.
 
Back
Top Bottom