Pongezi Rais Magufuli na Awamu Yake ya Tano, Wafanya Maajabu Vita Dhidi ya Umasikini, Tanzania Yaongoza Dunia Kupunguza Umasikini Uliotopea-WB.

Mimi nafikiri ni bora ripoti ingesema "Umaskini umepungua kwa Paskali Mayalla na wanufaika wa system, kwani sisi waTz bado tunao umaskini.
Kiukweli kama hajawahi kuizunguka Tanzania haswa kule deep interiors huwezi kuujua umasikini uliotopea. Mimi mwenyewe niliushuhudia baada ya kupata tender ya TASAF kuzunguka nchi nzima kuripoti kazi ya uhaulishaji fedha kwa kaya masikini.
Katika kundi la wenye umasikini uliotopea, kipimo cha kwanza ni kuishi kwa kipato cha chini ya dola moja kwa siku. Kwenye kundi hilo, kiukweli mimi ni tajiri mkubwa. Ile kumiliki tuu smart phone ni kipimo tosha wewe sio mtu wa kundi hili.
P
 
Kiukweli kama hajawahi kuizunguka Tanzania haswa kule deep interiors huwezi kuujua umasikini uliotopea. Mimi mwenyewe niliushuhudia baada ya kupata tender ya TASAF kuzunguka nchi nzima kuripoti kazi ya uhaulishaji fedha kwa kaya masikini.
Katika kundi la wenye umasikini uliotopea, kipimo cha kwanza ni kuishi kwa kipato cha chini ya dola moja kwa siku. Kwenye kundi hilo, kiukweli mimi ni tajiri mkubwa. Ile kumiliki tuu smart phone ni kipimo tosha wewe sio mtu wa kundi hili.
P
Ndi maana nikasema wanufaika wa system, nyie mnakula hizo hela za Tasaf bila jasho, ni lazimu muwe wapiga filimbi wa serikali, Eti umasikini umepunguzwa
 
Kiukweli kama hajawahi kuizunguka Tanzania haswa kule deep interiors huwezi kuujua umasikini uliotopea. Mimi mwenyewe niliushuhudia baada ya kupata tender ya TASAF kuzunguka nchi nzima kuripoti kazi ya uhaulishaji fedha kwa kaya masikini.
Katika kundi la wenye umasikini uliotopea, kipimo cha kwanza ni kuishi kwa kipato cha chini ya dola moja kwa siku. Kwenye kundi hilo, kiukweli mimi ni tajiri mkubwa. Ile kumiliki tuu smart phone ni kipimo tosha wewe sio mtu wa kundi hili.
P
Pascal Mayalla , umeona eh! uliuliza swali la nguvu, ila siku hizi umekengeuka!
 
Ndi maana nikasema wanufaika wa system, nyie mnakula hizo hela za Tasaf bila jasho, ni lazimu muwe wapiga filimbi wa serikali, Eti umasikini umepunguzwa
Aliyesema Tanzania tunaongoza duniani katika kupunguza umasikini sio mimi wala sio Magufuli, ni Bank ya Dunia, na hawa taarifa zao ni data oriented, numbers don't lie. Sio bla bla ni ripoti ya utafiti wa kina uliofanywa na watafiti wa ukweli.
P
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la pongezi kwa Rais Magufuli na awamu yake ya tano.

Naomba kuanza na angalizo,
Kuna watu wana allergy na pongezi zozote kwa rais Magufuli na awamu yake ya 5, hivyo akifanya jema lolote au akipongezwa kwa zuri lolote, wao wanakasirika. Kwa vile bado tuko kwenye festival season, kama wewe ni mtu wa kundi hili, nakuomba uishie hapa ili tusiharibiane festivals seasons zetu.

Naendelea kusisitiza kwenye mazuri, tupongeze, kwenye mabaya tukosoe,kwenye maovu tulaani, kwenye mapungufu tushauri na kutoa mapendekezo.

Leo nilikuwa napitia ripoti ya Benki ya Dunia(WB) kuhusu hatua ambazo zimechukuliwa na nchi mbalimbali kupunguza umasikini uliotopea, I was surprised kukuta Tanzania ndio nchi ya kwanza inayoongoza duniani kwa kupiga hatua kubwa zaidi kuondoa umasikini uliotopea, hivyo japo data ni miaka iliyopita, lakini ripoti ni mwaka huu!, hapa tunajadili ripoti ya 2019 na sio data ni za lini, hivyo Rais Magufuli na serikali yake ya Awamu ya Tano, wanastahili pongezi za dhati kwa kufanya maajabu makubwa kabisa katika vita dhidi ya umasikini uliotopea kwa kupiga hatua kubwa zaidi kupunguza idadi ya familia zilizokuwa zinaishi chini ya kipato cha dola moja kwa siku.

Ripoti hiyo ni hii
View attachment 1304778

Hata Hivyo, Ripoti ambayo ni ya mwaka huu 2019 imeonyesha data za Tanzania kuongoza kwa kupungunguza umasikini uliotopea, zilikusanywa katika kipindi cha miaka 10 tangu 2000 hadi 2011 ila haikusema in details, Tanzania imefanya nini katika kupunguza umasikini huo, naomba tuisome ripoti hii kwa kanuni ya "the end justify the means, kwasababu kwa sasa Tanzania ni Tanzania ya Magufuli, na Tanzania ndio inayoongoza kwa kupunguza umasikini, regardless ni kipindi cha nani umasikini huo ulipungua, as long as ripoti ndio imetoka sasa na Tanzania tunaongoza, then ni haki na halali kabisa pongezi hizi ziende kwa Magufuli na awamu yake ya tano, ila pia kwa vile najua kuna kazi nzuri inayofanywa na TASAF, kwenye ule mpango wa kunusuru kaya masikini, huku MKURABITA, ukirasimisha rasilimali na biashara za wanyonge, na hatua nyingine mbalimbali zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya tano katika kupunguza umasikini na kuinua kipato.

Wajameni, taarifa hii ni kwa mujibu wa datas za kuaminini za WB, maana humu jf kumezuka mtindo wa kubeza tuu kila kizuri kinachofanywa na awamu hii. Kwa vile mimi sio mchumi, hata ule ukuaji wa uchumi wa taifa wa zaidi ya asilimia 7% kwa mwaka, ulikuwa unanitatiza kwa sababu nikiangalia hali halisi huku mitaani mambo yanakuwa ni magumu sana, na kujiuliza huo ukuaji wa uchumi wa zaidi asilimia 7% unamfaidia nani, ni mpaka mchumi wetu Number 1 aliponifafanulia ndipo nikaelewa.

Hivyo hata bandiko hili, kama familia yako sii miongoni mwa kaya zinazoishi kwa kipato cha chini ya dola 1 kwa siku, unaweza usielewe kuwa Rais Magufuli na awamu yake ya tano, wanafanya mambo makubwa mazuri ya kuleta maendeleo kwa taifa letu.

Hongera rana rais Magufuli na kikosi kazi chako cha awamu ya 5, inawezekana kabisa sisi Watanzania, tusione, lakini kama World Bank wameona, dunia imeona, wasioona sasa wataonyeshwa.

Na kwa vile mwaka ujao ni mwaka wa uchaguzi mkuu, kuna wanasiasa ambao watapanda jukwaani na kujinadi kuwamkituchagua tutafanya hiki na hiki na hiki, lakini kuna wengine, watapanda jukwaani sio tuu kusema, bali kuonyesha walichofanya, hivyo naomba kuwaandaa watu kisaikolojia, usije kufika muda huo, watu ambao hawana chochote cha kuonyesha kuwa wamefanya, watakatakiwa kupanda kilingeni na watu wenye good track records za waliyoyafanya, kisha wasio na kitu wakaamua kuweka tena mpira kwapani, nashauri tuu, lets save time, money and resources, kama Watanzania tunachotaka ni maendeleo, na maendeleo hayo yanapatikana, yanaonekanika, then kwa nini tusiwaache tuu tuendelee tuu bila kufanya ....
naomba nisimalizie watu wasije kuniparura bure humu.

Maendeleo haya mazuri ya vita dhidi ya umasikini pia yamezungumzwa kwenye ripoti hii ya UNDP


Nawatakia maandalizi mema ya kuingia 2020!.
Paskali

Mambo mengi anayofanya Magu bado hayajaenda kwa mtu wa kawaida na hakuna mradi mkubwa hata mmoja umekamilika. Hivyo jitihada zake zitaonekana mbele baada ya watu kuanza kutumia umeme nafuu, treni kwa mizigo, maji safi, kutibiwa kirahisi na ongezeko la elimu. Hivyo credit kwa sasa na kwa Maraisi wa nyuma
 
Mkuu P nadhani hapa hauko sahihi kabisa labda kama utabadilisha heading ya uzi wako. Heading yapaswa ianze na pongezi kwa serikali ya JMT............., alafu uendelee na kusifia poti wako kama ulivyoamua kwa hiyari yako. Ninachojua ni kuwa muda si mrefu utapata posti haswa kabla ya uchaguzi mkuu kazi utakayoifanya vizuri sana.
Kwa hili naona Mayalla ameweka pamba masikioni yaani hasikii la mtu. Na cha ajabu anakuja na mifano ya ajabu ajabu kweli. Cha kufurahisha ana amini kuwa karibu jeshi zima lililo changia hapa ni vilaza wanashindwa kuelewa kitu kidogo kama hicho. Kwa mwandishi wa habari nilitegemea angejiuliza tena na kuvuta pumzi lakini yeye hilo si hoja. Sasa naamini mapenzi yame mpofua.
Somo kwa wana JF mapenzi yanayopitiliza hupofua huu ni mfano hai na pia chuki inayopitiliza hupofua.
 
Vipaumbele na malengo kwa wakati huo (2000-2011) vilikuwa tofauti sana na wakati tulionao. Wakati huo, lengo lilikuwa kupunguza umaskini wa kipato kwa kaya maskini na leo hii malengo ni upatikanaji wa huduma mbalimbali za jamii bila kujali vipato vyao. Sasa hivi tukaamua kukusanya data kwa sample space ile ile, kwa vigezo vya kupunguza umaskini wa kipato, ripoti inaweza kutupa matokeo tofauti sana. Hivyo sifa hizo haziakisi uhalisia tulionao sasa.
 
Kwa hili naona Mayalla ameweka pamba masikioni yaani hasikii la mtu. Na cha ajabu anakuja na mifano ya ajabu ajabu kweli. Cha kufurahisha ana amini kuwa karibu jeshi zima lililo changia hapa ni vilaza wanashindwa kuelewa kitu kidogo kama hicho. Kwa mwandishi wa habari nilitegemea angejiuliza tena na kuvuta pumzi lakini yeye hilo si hoja. Sasa naamini mapenzi yame mpofua.
Somo kwa wana JF mapenzi yanayopitiliza hupofua huu ni mfano hai na pia chuki inayopitiliza hupofua.
Mkuu Masiya, kiukweli tuna vilaza wengi kuliko tunavyojidhania. Kwenye Economics data kati ya World Bank na sisi humu jf, who would be right kuhusu economic dataz?.

Nimeweka ripoti humu na kuweka ile chart, watu hamsomi the report, what does it say kuhusu Tanzania bali mnasoma tuu chart na kuishia kukomaa na data collection period.

Kati ya hawa World Bank walio collect data za 2000-2015 na kuja kutoa report 2019, na watu humu wanaosoma report ya 2019 kuilazimisha iwe ya mwaka wa data collection, nani mjinga?.

Nasisitiza kama hujui reason behind data za 2000-2015 kuja kutolewa report 2019, please don't argue.
Ushindi wowote unaotolewa kwa nchi yoyote, mwaka wa ushindi huo unapotangazwa pongezi zinakwenda kwa serikali iliyopo Madarakani wakati ushindi ulipotangazwa.
Hivyo Tanzania ndio nchi iliyoongoza duniani kwa kupunguza umasikini uliotopea kwa mujibu wa taarifa ya Benki ya Dunia ya mwaka huu 2019.
Pongezi kwa rais Magufuli wa Tanzania, na serikali yake.
P
 
maendeleo kwa mtanzania mmoja mmoja uchagizwa na juhudi za serikali katika kuimarisha na kuboresha miundombinu ya mawasiliano na usafiri, huduma mbalimbali kama maji, umeme na afya na awamu hii imejitahidi kiasi chake. huenda ripoti ijayo ikawa nzuri au mbaya



Hasara Umfika Mwenye Mabezo
 
Watanzania tujifunze kusoma ni ripoti ya lini!. Ripoti hii ni Ripoti ya mwaka 2019 regardless data zilikuwa collected lini, validity ya ripoti yoyote ni the date of publication of the report na sio dates of data collection, hivyo as of now, Tanzania ndio inaongoza kwa kupunguza umasikini uliotopea kwa mwaka huu 2019!.
P
Sijajua unatumia principal ipi Ku reason yaani data zikusanywe 2000 -2011 then to be published 2019 , halafu unasema hayo matokeo ni ya 2019 na sio 2000-2011? Yaani kwa lugha nyingine unamaanisha gesi inayo zalishwa mtwara na kusafilishwa mpka dar es salaam via pipe line, halafu uaminishe watu hii gesi inachimbwa dar na sio mtwara. Naomba uniambie unatumia ubongo gani ku-reason, na kupost katka jukwaa la ma elites kama hili .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu ngoja waje vijana wa Zitto na kigogo2014 kutoka ufipani Uone watakavyokushambulia kuwa data zimepikwa.

Nitarud baada ya masaa5 kupitia jumbe.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tuwe wakwel
Screenshot_20190913-155432.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kati ya hawa World Bank walio collect data za 2000-2015 na kuja kutoa report 2019, na watu humu wanaosoma report ya 2019 kuilazimisha iwe ya mwaka wa data collection, nani mjinga?.

Nasisitiza kama hujui reason behind data za 2000-2015 kuja kutolewa report 2019, please don't argue.
Mkuu P. mapenzi yakizidi hupofusha.
 
You very right, utafiti ni Between 2000-2015 nchi 15 zimeondoa watu milioni 800 kutoka katika umasikini uliotopea, Tanzania ndio imeongoza kwa kutoa watu wengi zaidi. Kwa vile ripoti ni ya mwaka huu, nchi kinara inayoongoza dunia kwenye ripoti hii ni Tanzania, pongezi zinakwenda kwa utawala wa Tanzania wa sasa 2019 wakati ripoti inatoka.
P

You are wrong my bro!! Pongezi ziende kwa wale waliokuwa hicho kipindi. Mkuu unapotosha kwa makusudi. Taifa linawategemea wasomi kama ninyi, ila mnatuangusha, hata habari mnazotoa ni za kupotosha badala ya ukweli. Ni kwa nini usingetafuta ripoti currently ili ku-validate unachosema mkuu?!
 
Nakusoma Pascal, unadhani Mystery amekosea kuliweka hivyo? Sisi ni binadamu kuna wakati huteleza. Tatizo la juzi sio kusifu bali ulimpa sifa asiyestahili bahati mbaya kama ujuavyo naye ana wapinzani wakutosha. Ndio maana wengine tunasema mahaba [yakizidi] hupofusha. Umesema "Tuwe wakweli, mazuri tusifu, mabaya tukosoe", nakubaliana nawe lakini kwenye ule uzi mazuri yale hayakuwa ya yule uliempa pongezi kana kwamba yeye ndiye aliye yaleta (causal attribution).
Mkuu Masiya, Ripoti hii ni Ripoti ya 2019!. Jambo lolote jema au baya, siku linapotangazwa, pongezi au lawama zinakwenda kwa utawala uliopo madarakani kipindi ripoti inatolewa.

Mfano sisi tumepata uhuru mwaka 1961. Tanzania ni mwanachama wa EAC nyenye nchi 5. Ukifanywa Research ya Nchi za EAC zilizoongoza kwa hukumu ya kunyonga ndani ya miaka 50, Nyerere alinyonga watu wawili, Mwamwindi na yule mhindi aliyemua mkewe ili alipwe bima. Mwinyi alinyonga kadhaa idadi haikutangazwa, Mkapa hakunyonga, Kikwete hakunyonga, Magufuli hakunyonga na wala hatanyonga. Lakini kutokana na walionyongwa kipindi cha Mwinyi, ripoti ikitoka mwaka huu 2019, na kuonyesha Tanzania ndio nchi iliyoongoza Afrika Mashariki kwa kunyonga ndani ya kipindi cha miaka 50 iliyopita, ni nani atalaumiwa?. Ni rais wa sasa wa Tanzania, hata kama katika kipindi chake hajanyonga hata mtu mmoja!. Unadhani Magufuli atasoma ripoti na kusema msinilaumu mimi, mlaumuni Mwinyi ndiye aliyenyonga, mimi sijanyonga!.

Ripoti ni ya mwaka huu inaonyesha Tanzania ndio inaongoza dunia kwa kupunguza umasikini, maadam ripoti ni ya mwaka huu, then pongezi kwa ushindi huu ni kwa serikali iliyopo madarakani kwa sasa.
Hongera Magufuli.
P
 
Back
Top Bottom