Pongezi Rais Magufuli: Barabara za Wilaya ya Rungwe sasa kuendelea kuwekwa lami

masopakyindi

Platinum Member
Jul 5, 2011
17,853
13,137
Baada ya kilio cha muda mrefu, hatimaye Awamu ya Tano imesikia kilio cha wananchi wa wilaya ya Rungwe.
Barabara ya Katumba-Mbambo-Tukuyu.

Mzunguko wa barabara hii utakuwa mkombozi kwa maisha ya mkulima na wanachi kwa sehemu kubwa sana wilaya ya Rungwe.

Asante Rais Magufuli juhudi zako zitaonekana katika uchaguzi wa 2020.
 
Attachments

  • 20190102_082901.jpg
    20190102_082901.jpg
    240.5 KB · Views: 59
Sifa pia ziwaendee wanaCCM na Watanzania wengi waliompigia kura ili akaisimamie Ilani ya Uchaguzi ya CCM.

Watanzania wengi hawahitaji mambo makubwa.

Watanzania wengi wanachotaka ni barabara nzuri, Maji safi na salama, huduma ya afya, elimu na uboreshaji wa kilimo na biashara.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Magufuli apewe pongezi sana.
Barabara hii imeahidiwa toka enzi ya Mwinyi, Mkaoa na Kikwete.
Wote walipiga kampeni kuomba urais wakiahidi kuijenga kwa kiwango cha lami.

Magufuli kafanya kweli, hongera sana maana vijana wstapata ajira za ujenzi, na barabara zikikamilika maendeleo yatapaa.
 
Kumsikia Trump kuhusu nini?

2020 John Walker out
Anafanya kile anachojisikia na anaona ni bora kwa watu wake.
Magufuli kajitanabaisha kufanya yale yanayowsendeleza wananchi wa Rungwe~barabara za lami.
Sasa wewe njanga unacholalamikia nini wananchi walengwa tukimpongeza.
Mbaya zaidi wasema ni upumbavu.

Kweli watu mmekalia misumari, ila hamjioni.
 
Baada ya kilio cha muda mrefu, hatimaye Awamu ya Tano imesikia kilio cha wananchi wa wilaya ya Rungwe.
Barabara ya Katumba-Mbambo-Tukuyu.

Mzunguko wa barabara hii utakuwa mkombozi kwa maisha ya mkulima na wanachi kwa sehemu kubwa sana wilaya ya Rungwe.

Asante Rais Magufuli juhudi zako zitaonekana katika uchaguzi wa 2020.
Kila awamu ya Urais barabara hujengwa nadhani Rungwe sasa ni zamu yao,sioni ajabu.
Kwa kodi zetu Nyerere alijenga,Mwinyi alijenga,Mkapa alijenga,Kikwete alijenga,Magufuli anajenga,akija mwingine atajenga.
Ya kijijini kwetu nayo itajengwa zamu yetu imefika.
Nia ya serikali yeyote duniani, ni kujenga barabara zote nchini hata za vijijini.
Ujenzi wa miundombinu ndio kazi za serikali.
Baba kumpeleka mtoto shule ni jukumu lake sio hisani inayohitaji kusifiwa.
 
Maendeleo kwa wananchi yanapogeuka kuwa fadhila ya viongozi ni upumbavu wa hali ya juu sana

2020 John Walker out
Hii komenti yako ni fupi sana kimaandishi,lakini ni ndefu na ya maana sana kiuhalisia,nakubali kabisa kuwa wewe ni Great Thinker.
Sisi watanzania ni watu wajinga kabisa ukiondoa watu wachache sana wewe na mimi tumo.viongozi wanaosifiwa wangekua wanatoa hela mifukono mwao ningesifu.
 
Magufuli apewe pongezi sana.
Barabara hii imeahidiwa toka enzi ya Mwinyi, Mkaoa na Kikwete.
Wote walipiga kampeni kuomba urais wakiahidi kuijenga kwa kiwango cha lami.

Magufuli kafanya kweli, hongera sana maana vijana wstapata ajira za ujenzi, na barabara zikikamilika maendeleo yatapaa.
Huyu Kijana toka Chatto Ni zawadi Maalum aliyotuachia Jk

Magu Piga kazi utakumbukwa ukishastaafu Kwa Kuwa ndio Tabia yetu sio wakati ukiwa Madarakani
 
Hii komenti yako ni fupi sana kimaandishi,lakini ni ndefu na ya maana sana kiuhalisia,nakubali kabisa kuwa wewe ni Great Thinker.
Sisi watanzania ni watu wajinga kabisa ukiondoa watu wachache sana wewe na mimi tumo.viongozi wanaosifiwa wangekua wanatoa hela mifukono mwao ningesifu.
Great thinker unayefika kwenu kwa punda, hongera na endelea ku think!
 
Great thinker unayefika kwenu kwa punda, hongera na endelea ku think!
Kwani wewe umeanza lini kufika kwenu kwa basi?,na wewe si umeanza leo? na mimi itafika tu zamu yangu,huyuhuyu Magufuli atanijengea, zamu yangu ikifika.
Kuna watu walianza zamani sana kufika kwa mabasi makwao,tangu 2006 wakati Magufuli akiwa waziri.nyinyi sasa ni zamu yenu na zamu yetu inakuja.
 
Back
Top Bottom