Elections 2010 Pongezi polisi Arusha

kitalolo

JF-Expert Member
Dec 4, 2006
1,827
707
Kweli wanastahili pongezi kwa kuwasimamia vizuri wadai haki wa chadema walipokuwa wamekusanyika mbele ya jengo kuu la manispaa ya arusha kusubiri matokeo rasmi ya ubunge kutangazwa baada ya mama kukataa kusaini kwani eneo lote la barabara kutokea mbele ya manispaa hiyo kuelekea mnara wa saa na kuelekea kwenye ofisi za mkuu wa wilaya kupitia mbele ya ofisi za mkuu wa mkoa zilikuwa zimejaa wana mapinduzi waliokuwa tayari kwa lolote mpaka kieleweke .
jambo la kujivunia kwa polisi wetu waliweza kudhibiti amana na hakuna hata mtu mmoja aliyekanyangwa maka nilivyomsikia ripota mmoja wa radio dochi vele dw mchana wa jana akiripoti ulipoaji wa mabomu na kumwagwa ma maji washa jambo ambalo halikuwa la kweli nimepigiwa simu nyingi sana kutoka mikoani wakiniuliza hali ya arusha kutokana na uvumi ulioenezwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa hali arusha sio swari mabomu yapigwa na mengineyo. nilikuwa nje ya mji na baada ya kupokea simu nyingi na kusikia vyombo vya habari ilinilazimu kuacha shughuli zangu na kurudi mjini arusha ili niende kumchukua mtoto wangu shuleni kwana anasoma shule moja maeneo ya jimkana nikajua kama mjini kuna fujo basi pengine dereva wa basi linalowachukua wanafunzi akashawishika kuingia kwenye ushabiki hivyo kuweka hali ya watoto kwenye hatari kwani kwa jinsi nilivykuwa namjua dereva huyo alikuwa mwanachama wa chadema na na mwanangu alikuwa akiniambia wakati wa kampeni dereva alikuwa akiendesha gari kwa mkono moja na mkono mwingine alikuwa akipunga bendera ya chadema wakati akikutana na wenzake. hivyo kwa kujua kuwa ni mkereketwa nikaona nichukue tahadhari.
lakini nilipofika mjini hali iliyoikuta ilikuwa tofauti kabisa kwani niliwakuta watu waliojipanga kwa utulivu, polisi wanaoongoza magari na waliowasimamia wananchi wadai haki kwa mani magari ya polisi yaliyojipaga kwa utaratibu likiwemo gari la kurusha maji washa. kama vile kwenye nchi za wenzetu tunavyoonaga polisi wakiwaongoza waandamanaji au wagomaji au jinsi wanavyodhibiti watu wanaoleta fujo kwa utaratibu biala kuleta madhara. sikuamini kama niko tanzania au afrika mabapo tumezoea pigapiga ya polisi au kutumika kwa nguvu za ziada ambazo wakati mwingine huwa hazihitajikia, nikakumbuka maneno ya mgombea wa chadema kuwa watakaosababisha fujo sio chadema bali ni vyombo vya dola vikichochewa na chama tawala maana chadema hawana majeshi.
ila peoples power.
kilichonifurahisha zaidi na hata baada ya matokeo rasmi kutangazwa watu walishangilia kiustaarabu tofauti na nilivyosikia kwenye jimbo moja alikoshinda kapuya kwamba wanachama kadhaa wamekufa kwa kushangilia ushindi.

hapo ndipo nilipoona kuwa jeshi la polisi mkoani arusha wanastahili pongezi na pia ni sehemu ambayo jeshi la polisi kwa mikoa mingine wangeweza kujifunza kama daresalamu na mwanza ambapo tumeona kwney vyombo vya habari wakiwashambulia raia kwa nguvu za ziada kma raia hana hata jiwe kwanini kutumia zisasi kama raia hana panga kwanini kutumia virungu polisi kwajinsi tulivyowaona walikuwa mamevaa mavazi maalumu utafikiri wanakwenda vitani.
nikajifunza kuwa wakati mwingine kuna fujo zinazosababishwa na polisi.

hongera basilio matei najua watakuhamisha kwa kushindwa kulilinda jimbo lakini kwa hapo ulistahili kupelekwa daresalamu maana umehimili vishindo vya arusha basi kwa ustaharabu wa kuwaongoza polisi wako nafikiri hekima uliyotumia ilistahili kutumika daresalamu na mwanza pia na kwingineko.

najua watakuhamisha kwa kushindwa kulilinda jimbo lakini na kwaakili zao walitaka utumie nguvu ili wachakachue matokea wakati watu wanapofanya fujo hekima uliyotumia kulinda jimbo ni kubwa sana hivyo wakikuamisha kwaakili zao watakushusha cheo kwamba sio mpiganaji lakini Mungu atakulipa na kurudisha kile watakachokunyanganya kwasasa endelea kumwamini nina mengi ya kuzungumza ila naomba tu niwahesabu polisi wa arusha kama mashujaa na watu wanahitajika katika kuilinda amani ya nchi na ya dunia kwani kwa kupatika amani na utulivu wa wana arusha na watanzania kwaujumla. viongozi na polisi kama nyie ndio wanaotakiwa na dunia ya leo tunayoishuhudia ikipoteza amani kila kukicha kwaajili ya tamaa ya madaraka na ufisadi.

nitaendelea baadae
 
Hilo ni agizo toka ikulu wala si wao, wanajua kuna mahakama ya uhalifu dhidi ya binadamu kule the hague
 
Hilo ni agizo toka ikulu wala si wao, wanajua kuna mahakama ya uhalifu dhidi ya binadamu kule the hague

inamaana polisi wa dar na mwanza hawaijui hiyo mahakama au ikulu inatoa amri kwa baadhi ya maeneo kwamba maeneo amabayo raia watapigwa na kujeruiwa kwao wao sio watanmzania?
 
Back
Top Bottom