Uchaguzi 2020 Pongezi nyingi sana kwa Lissu, Mkewe, Uongozi wa CHADEMA na Watanzania walioshiriki kwenye kampeni za CHADEMA

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
105,167
2,000
Napenda kuchukua fursa hii kumpongeza sana Lissu kwa kampeni zake za hali ya juu na zilizokuwa na mahudhurio makubwa sana kila kona ya Nchi yetu uliyopita. Lugha zako za upendo ulizotumia na kutugusa mamilioni ya Watanzania Wazee, vijana na hata watoto. Ulikutana na vikwazo vya aina mbali mbali lakini vyote kwa ujasiri wako mkubwa ulivuka salama.

Napenda pia kutoa pongezi zangu za dhati kwa Mke wa Lissu kwa kuwa bega na bega na Mh. Lissu tangu mwanzo wa kampeni hadi mwisho wa kampeni. Hongera sana Mama na ahsante sana kwa ujasiri wako pia

Pongezi zangu pia ni kwa viongozi wote wa Chadema kwa uongozi wenu bora pamoja na matatizo mbali mbali mliyopitia tangu 2015 mengine ya kutisha sana lakini hakumkata tamaa hata kwa sekunde moja mliendelea kukipigania chama kwa uwezo wenu wote. Tunawashukuru sana ๐Ÿ™๐Ÿฝ๐Ÿ™๐Ÿฝ๐Ÿ™๐Ÿฝ

Mwisho kabisa pongezi zangu ni kwa Watanzania wa kila kona ya Nchi yetu. Upendo mkubwa sana mliouonyesha kwa Chadema kusema kweli umenishangaza sana na kunipa matumaini makubwa sana kwa Nchi yetu. Pamoja na Chadema kuzuiwa kwa miaka mitano kufanya shughuli zozote za kichama lakini upendo mliouonyesha ni kama vile Chadema ilikuwa very active kwa miaka yote mitano. Mahudhurio makubwa kwenye mikutano ya kampeni Nchi nzima michango yenu mikubwa kusaidia gharama mbali mbali za wagombea wa nafasi mbali mbali Nchini ilikuwa ni ushahidi tosha kwamba Chadema iko mioyoni mwa Watanzania hivyo juhudi za kuiua Chadema kamwe hazitafanikiwa.

Sasa masaa machache yajayo tukamilishe jambo letu kwa kishindo.

Mungu ibariki Chadema, Mungu ibariki Tanzania ๐Ÿ™๐Ÿฝ๐Ÿ™๐Ÿฝ๐Ÿ™๐Ÿฝ

๐Ÿ’ช๐Ÿพ๐Ÿ’ช๐Ÿพ๐Ÿ’ช๐Ÿพ
 
JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
21,067
2,000
Mimi nakumbuka September 7, 2017 alivyopakiwa kwenye ile ndege.

Hivi kuna yeyote siku ile aliamini miaka mitatu baadae Tundu Lissu atafunga kampeni za Cdm kama mgombea Uraisi?

Na baada ya kupona, na jinsi CCM na vyombo vyake walivyokuwa wamefura kwasababu Tundu Lissu amepona, kuna aliyeamini atarudi Tanzania chini ya utawala wa Magufuli?

Na baada ya kurejea nchini, na kupitishwa kugombea Uraisi, na kuanza kutafuta wadhamini, na mahakama kuanza kumnyatia. Kuna aliyeamini Polisi hawatamkamata na kumnyima dhamana?

Halafu siku ile ya kurudisha fomu, na jinsi alivyosubirishwa mpaka usiku mzito. Je, ni wangapi waliamini hatapitishwa na Tume?

Na hata alivyoanza kampeni ni wangapi walitegemea atamaliza salama?
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
105,167
2,000
Mkuu JokaKuu mimi nilikuwa mmoja wa wale walioamini kwamba Lissu angeenguliwa. Kilichofanya niamini kwamba angeenguliwa ni kwamba pamoja na kuwa aliwasili saa tano asubuhi na ushee katika ofisi za tume lakini wote waliokuja nyuma yake walipitishwa kabla yake nakumbuka ilibidi asubiri hadi baada ya saa 12 jioni na kukawa na hofu kubwa kwamba wasiojulikana wangeweza kumteka.
 
..Nadhani walitafuta kila sababu ya kumuengua ikashindikana.

..Sasa angalia vikwazo ambavyo kampeni yake wamepitia.

..mashambulizi toka kwa CCM, Kamati ya Amani, Igp,Nec, Msajili, Tcaa, Tcra, na wengine.

..angekuwa mtu wa kawaida angevunjika moyo na kubwaga manyanga.

..Tunashukuru kwa kampeni zake, na tunamuombea USHINDI.
 
Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
54,651
2,000
Hii damu isiyo na hatia, aliyeamuru imwagwe, itampeperusha kwa tufani Kali kuliko Tsunami, kutoka kwenye kiti chake Cha enzi Hadi sakafuni mavumbini

IMG_20201028_002359.jpg
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
105,167
2,000
Huzuni kubwa sana. Kwanini Watanzania waumizwe, watiwe vilema au kupoteza maisha yao kwa kutimiza wajibu wao kama ulivyo kwenye katiba wa kupiga kura kuchagua viongozi wanaowataka?
Hii damu isiyo na hatia, aliyeamuru imwagwe, itampeperusha kwa tufani Kali kuliko Tsunami, kutoka kwenye kiti chake Cha enzi Hadi sakafuni mavumbini

View attachment 1614194
 
Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
54,651
2,000
Huzuni kubwa sana. Kwanini Watanzania waumizwe, watiwe vilema au kupoteza maisha yao kwa kutimiza wajibu wao kama ulivyo kwenye katiba wa kupiga kura kuchagua viongozi wanaowataka?
Itamgharimu Firauni Yule yeye nanwatu wake na vizazi vyao
 
  • Love
Reactions: BAK

mshunami

JF-Expert Member
Feb 27, 2013
4,166
2,000
ALERT
Taarifa toka jimbo la Kavuu nikuwa mawakala 30 wa CHADEMA wamekamatwa na polisi waliokuwa wanajiandaa kwenda kwenye vituo..

@tanpol Sirro ndiyo maana tunataka kukupeleka ICC kwa huu upumbavu wako unaofanya na CCM

@TumeUchaguziTZ who is instructing this to be done?
Kazi ndiyo imeanza. Tusikubali. Sasa basi!
 
sifongo

JF-Expert Member
Jun 5, 2011
4,837
2,000
ALERT
๐Ÿ‘‰Taarifa toka jimbo la Kavuu nikuwa mawakala 30 wa CHADEMA wamekamatwa na polisi waliokuwa wanajiandaa kwenda kwenye vituo..

@tanpol Sirro ndiyo maana tunataka kukupeleka ICC kwa huu upumbavu wako unaofanya na CCM

@TumeUchaguziTZ who is instructing this to be done?
Halafu wanakuja Watanzania fulani wanasema CCM inakubalika, awamu hii imefanya maendeleo sana.......kama ni kweli kamata kamata ya nini.....acheni uwanja wazi watu watoe ya moyoni.
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
79,118
2,000
Mkuu JokaKuu mimi nilikuwa mmoja wa wale walioamini kwamba Lissu angeenguliwa. Kilichofanya niamini kwamba angeenguliwa ni kwamba pamoja na kuwa aliwasili saa tano asubuhi na ushee katika ofisi za tume lakini wote waliokuja nyuma yake walipitishwa kabla yake nakumbuka ilibidi asubiri hadi baada ya saa 12 jioni na kukawa na hofu kubwa kwamba wasiojulikana wangeweza kumteka.
Hivyo ndivyo walivyopanga , hata Ndugai aliropoka lakini baadaye baada ya kuona uhalali wa fomu za wadhamini wa Lissu wakatenguka , ndani ya Tume kuna mtu wangu ambaye baada ya jambo lile alininong'oneza kwamba katika fomu za Lissu hakukukutwa hata kosa moja la kusingizia , tume nzima ilishangaa!
 
1000 digits

JF-Expert Member
Oct 16, 2012
4,996
2,000
Kamuacha mtu hoi huko... sidhani kama ana hamu na wabongo!

Daah nilijua tuna gari madhubuti kumbe ni la mkaa... tripu shamba tripu nne gereji!!

Hongera Lissu!!
Wasiwasi wangu ni mitano tena ikipatikana , kuna watu watalimia meno.
Visasi vitakua vikubwa sana.

Kheri na Musiba nadhani watapewa na mabomu ya nyuklia kuwaangamiza watu . Kwenye mikutano yote hakuna neno haki lilipotamkwa hata mara moja.
Haki za binadam zitaondolewa kabisa na watu wataonekana kama panya wa Libya wakati wa Ghadhaf.

Tumuombe Mungu ashushe roh o wake mtakatifu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom