Kwa mara ya kwanza leo nimepita barabara ya KIA -Mirerani na kwa macho yangu nimejionea uzuri na uimara wa barabara ya lami iliyozinduliwa na Mh. Rais hivi karibuni. Kwa wanaofahamu barabara hiyo kabla ya kuwekwa lami, watakubaliana na mimi kwamba kazi kubwa imefanywa na Serikali ya JPM katika kuimarisha miundombinu ya bara bara kutoka KIA hadi Mirerani. Nimebahatika pia kufika kwenye ukuta unaozunguka migodi ya Tanzanite One na kujionea kazi kubwa iliyofanywa na Serikali. Hongera sana Mh. Rais na Serikali yako.