Pongezi nyingi kwako Mheshimiwa Rais Dr. John pombe Magufuli

lunyiliko

Senior Member
Jun 10, 2011
171
79
Kwa mara ya kwanza leo nimepita barabara ya KIA -Mirerani na kwa macho yangu nimejionea uzuri na uimara wa barabara ya lami iliyozinduliwa na Mh. Rais hivi karibuni. Kwa wanaofahamu barabara hiyo kabla ya kuwekwa lami, watakubaliana na mimi kwamba kazi kubwa imefanywa na Serikali ya JPM katika kuimarisha miundombinu ya bara bara kutoka KIA hadi Mirerani. Nimebahatika pia kufika kwenye ukuta unaozunguka migodi ya Tanzanite One na kujionea kazi kubwa iliyofanywa na Serikali. Hongera sana Mh. Rais na Serikali yako.
 
Kiongozi na serikali wamechaguliwa wayafanye hayo. Hatutegemei wafanye kinyume chake. Ni kazi walioomba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa mara ya kwanza leo nimepita barabara ya KIA -Mirerani na kwa macho yangu nimejionea uzuri na uimara wa barabara ya lami iliyozinduliwa na Mh. Rais hivi karibuni. Kwa wanaofahamu barabara hiyo kabla ya kuwekwa lami, watakubaliana na mimi kwamba kazi kubwa imefanywa na Serikali ya JPM katika kuimarisha miundombinu ya bara bara kutoka KIA hadi Mirerani. Nimebahatika pia kufika kwenye ukuta unaozunguka migodi ya Tanzanite One na kujionea kazi kubwa iliyofanywa na Serikali. Hongera sana Mh. Rais na Serikali yako.
Rais anafanya kazi kubwa na nzuri yenye kushabihiana na utashi wake kama kiongozi. Katika awamu hii ya tano hakuna hela inayopotea mikononi mwa mabeberu bali kuwasaidia wananchi kwa kuimarisha miundombinu yao. Asante JPM

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo barabara ni juhudi za KIKWETE. yan ningekuona una akili kama ungemsifu yeye. Mzee jiwe ye kaja kuzindua tu kama ilivyo hospitali ya mloganzila
 
Naona tupo kwenye awamu ya kusifiana na kupongezana tu. Na kwa wale wanao onekana hawapigi makofi, hawapongezi, badala yake wanakosoa kwa namna yoyote ile basi huonekana si wazalendo, ni wasaliti, wapiga dili, wanatumiwa na mabeberu, nk. Kwani kazi ya serikali iliyopo madarakani ni nini?

Na hiyo barabara imejengwa kwa hela ya mtu ya mfukoni mwake au ni kwa hizi kodi zetu tunazotozwa kila siku? Kwa nini hii tabia imeanza na kushamili sana awamu hii kuliko awamu zote zilizopita? Mimi naamini kizuri kinajiuza chenyewe hivyo hakuna sababu ya kutumia nguvu kubwa kumtukuza mwanadamu kuliko hata Mungu tunayemwamini na kumwabudu siku zote.

Nakumbusha hii tabia ya kumsifia, kumtukuza na kumpongeza mwanadamu wakati mwingine pasipokua na sababu yenye mashiko, madhara yake mtakuja kuyaona baadae na siyo leo wala kesho. Hamjui ni kwa namna gani madaraka hulevya.
 
Kwa mara ya kwanza leo nimepita barabara ya KIA -Mirerani na kwa macho yangu nimejionea uzuri na uimara wa barabara ya lami iliyozinduliwa na Mh. Rais hivi karibuni. Kwa wanaofahamu barabara hiyo kabla ya kuwekwa lami, watakubaliana na mimi kwamba kazi kubwa imefanywa na Serikali ya JPM katika kuimarisha miundombinu ya bara bara kutoka KIA hadi Mirerani. Nimebahatika pia kufika kwenye ukuta unaozunguka migodi ya Tanzanite One na kujionea kazi kubwa iliyofanywa na Serikali. Hongera sana Mh. Rais na Serikali yako.
Huku Dar karibu kila barabara ya kuingia mitaani na kuyokea mitaa mingine na hatimaye kuingia barabara kubwa zimejengwa tayari au zinajengwa sasa si mbezi beach, kinondoni au segerea. Ni mwendo wa kuimarisha miundo mbinu.
 
Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni. Kwa kifupi Rais anafanya kazi kweli kweli. Haihitaji kuwa na cheti au diploma kuona kazi tangible kabisa zilizo na zinazoendelea kufanywa na mheshimiwa Rais JPM na serikali yake. Panapo mazuri, tuipongeze Serikali yetu kwa dhati kabisa. Its not about criticising everything. Let's appreciate where possible.JPM deserves appreciation for what he is doing for the wellbeing of our Nation.

Back
Top Bottom