Uchaguzi 2020 Pongezi nyingi kwa kamati ya ushindi Chadema, hakika nyie ni wataalam wa siasa

PAZIA 3

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
1,074
1,855
Napenda kuipongeza kamati ya ushindi Chadema kwa mkakati mzuri wa kuifanya Chadema kushinda uchaguzi huu, Mambo haya mmeyafanya kisayansi zaidi na kuibomoa kabisa ccm kiasi Cha kukosa Cha kuzungumza mbele ya watu, badala yake unaona mgombea wa ccm anasimama anasema, " Chadema wametumwa na mabeberu" bila kujibu hoja za wapinzani, mfano, utekaji watu, udhalilishaji wanawake, maisha magumu, uwazi wa raslimali taifa, misallocation ya pesa za vuja jasho la nchi hii, na mambo mengine mengi.

Niipongeze kamati iliyomteua kampeni meneja Wa T. Lisu, analitawala jukwaa vyema, niwapongeze walioiongoza tume kuwapa ratiba nzuri ya maeneo ya kufanyia kampeni, mmeanza na POTENTIAL ZONES na mmepata kuungwa mkono kwa asilimia kubwa, niwapongeze pia kwa kutokutumia picha nyingi za mgombea uraisi, maana picha hazizungumzi, na wananchi siyo wajinga, wanajua picha huwa ni danganya Toto, hongereni kwa kuandaa wasanii tulivu wasio maarufu lakini wameleta amshaamsha hata watu kucheza kwa furaha wakati mgombea uraisi akiwa anaingia jukwaani, mnastahiri NISHANI baada ya ushindi mkubwa mwezi October, 28.

MUNGU ANAJAMBO LAKE KUIONDOA CORONA TANZANIA
 
EiyVY6gXYAUtAkI.jpeg

NI YEYE
 
Duh....aisee....nimeamini kweli kuwa Kuna watu hutumwa na mabeberu...ushindi gani unazungumzia?!
 
Nakumbuka kisa cha bwana mmoja bausa hivi alikuwa akitoka kwenye kichaka huku akiwa anasonya na kuongea peke yake kibabe na kwa sauti ya chini akisema "wamenifi** lakini kwa mbinde sana!".Baada ya oct 28 CCM nao watakuwa wakisema maneno yanayofanana na haya kwamba "wametushinda lakini kwa mbinde sana"
 
Yaliyotokea Mwanza jana mchana na usiku huu yanasema mengi sana kuhusu ccm kama mmeyasoma. Ccm inakufa hivyo.
Duh....aisee....nimeamini kweli kuwa Kuna watu hutumwa na mabeberu...ushindi gani unazungumzia?!
Kampeni zimekaa ki-spy zaidi . Hakuja longo longo ni actions tu.

Kumbe hawa jamaa miaka mitano walikuwa na kampeni za chini kwa chini. Huo umati hauwesi kuwa umeamshwa n Lissu peke yake.
 
Hata mimi nawapa pongezi mshindani wao wa karibu ACT tayari wamempiga chini maana hata kampeni kaishia mkoa mmoja tu.. acha wahangaike na lipumba kwa sasa..
 
Chadema ndio chuo pekee cha kupika wanasiasa kitegemewacho na hata ccm.
Ina hazina mpya ya vijana vichwa hata ccm ikiwanunua wote haiwezi wamaliza
Hiyo ndiyo Siri ya Ushindi,Watanzania waelewa hujiunga na Upinzani kwa sababu ya Hoja za Wananchi.CCM Mpya inategemea nguvu za vyombo vya Dola na Tume.

Hivi,kwa jinsi CHADEMA ilivyoweka wagombea wenye Sifa Bora za Uongozi nchi nzima,halafu ndiyo wanaoongoza kukatwa wagombea wao kwa kukosea kujaza fomu?Baadhi ya Majimbo wamekoseshwa mgombea hata moja?Vilaza wa CCM wote wakapita?Hizi fomu za wagombea zinakuwaje ngumu(Complex) had I kuwashinda wasomi kuzijaza?

Wenye akili wanafahamu sababu, hata Tume na Wasimamizi wanafahamu kuwa hii ni mbinu ya CCM kutawala bila ridhaa ya Wananchi. Kwa nini kama hakuna mgombea mwingine aliyekidhi vigezo,zisipigwe kura za Ndiyo/Hapana kwa hao waliokidhi vigezo?Ni aibu,hata Waziri Mkuu mnampitisha bila kupingwa?Ndiyo Demokrasia hiyo?
 
Team ya kampeni ya Chadema iko vizuri sana. Wamejiandaa kweli kweli na wanamuongoza vizuri sana mgombea wao. Watanzania pia tunajua cha kufanya hapo October 28. Ni kuweka historia kuu kwa kumstaafisha magufuli na CCM.

Hongereni Chadema na sifa na utukufu zimrudie Mungu
 
Lazima kife. Kama unakabidhiwa chama kikiwa na Viongozi waandamizi, halafu wewe unawapangua kwa 90% na kuwaleta wakwako ambao hawana uzoefu wa kukiendesha chama unategemea nn?

Zile nafasi za uteuzi walizokuwa wakipewa Makada Kindakindaki wewe unazitumia kama rushwa ya kuwarubuni Wapizani unategemea nn?? Imefikia hatua hata ya kuwaokota wengine majalalani na kupewa nafasi huku wafia chama kama kina Nape na January wakitishiwa na kuachwa wakipiga miayo unategemea nn?

Acha tu kijifie chenyewe kwakuwa wamekosa maarifa. Ukiangalia kwa makini Uongozi wa juu wa ccm utagundua kuwa umekosa Hekima na Busara na kujawa na Ubabe na Vitisho.
 
Hiyo ndiyo Siri ya Ushindi,Watanzania waelewa hujiunga na Upinzani kwa sababu ya Hoja za Wananchi.CCM Mpya inategemea nguvu za vyombo vya Dola na Tume.

Hivi,kwa jinsi CHADEMA ilivyoweka wagombea wenye Sifa Bora za Uongozi nchi nzima,halafu ndiyo wanaoongoza kukatwa wagombea wao kwa kukosea kujaza fomu?Baadhi ya Majimbo wamekoseshwa mgombea hata moja?Vilaza wa CCM wote wakapita?Hizi fomu za wagombea zinakuwaje ngumu(Complex) had I kuwashinda wasomi kuzijaza?

Wenye akili wanafahamu sababu, hata Tume na Wasimamizi wanafahamu kuwa hii ni mbinu ya CCM kutawala bila ridhaa ya Wananchi. Kwa nini kama hakuna mgombea mwingine aliyekidhi vigezo,zisipigwe kura za Ndiyo/Hapana kwa hao waliokidhi vigezo?Ni aibu,hata Waziri Mkuu mnampitisha bila kupingwa?Ndiyo Demokrasia hiyo?
Kuna sehemu ya kusaini...my hataki kusaini...weka picha hataki...weka wadhamini haweki...uliwahi kushitakiwa? Hajazi ...yaani fomu makosa kibao...hata tarehe hajazi...declare Mali zako hataki...Sasa kwanini watu wasikatwe?! I am just assuming...
 
Back
Top Bottom