Pongezi na ushauri wangu kwa mhe. Rais jakaya kikwete. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pongezi na ushauri wangu kwa mhe. Rais jakaya kikwete.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ASK, Mar 24, 2011.

 1. A

  ASK Member

  #1
  Mar 24, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimekuwa nikifuatilia ziara za Rais wangu Mhe. Jakaya Kikwete katika wizara mbalimbali. Kwa dhati nampongeza kwa kufanya ziara hizo kwa kuwa si kuwa zinawakumbusha wajibu wao watendaji wa wizara hizo lakini pia zinawaweka katika mazingira ya kufanya kazi kwa ufanisi hasa wakikumbuka kwamba kuna siku watatakiwa kutoa maelezo kwa kile walichokifanya katika kipindi fulani na utekelezaji wa maagizo yake kwa ziara yake ya mwisho. Kwa hili Mhe. Rais nakupongeza sana.
  Pamoja na pongezi zangu kwako naomba nitoe angalizo/ushauri kuwa ziara hizo zitakuwa na ufanisi/mafanikio kama zitakuwa za mara kwa mara walau mara mbili kwa mwaka au kila mwaka kwa maana ya mara moja kwa mwaka. Kwa kufanya hivyo wazi kuwa utakuwa unapata mrejesho wa ziara yako ya mwaka ulipita au ya mwisho na utekelezaji wa maagizo yako. Nafahamu kuwa kila unachoagiza/ unachoshauri/unachoomba vyoye ni maagizo na watakupa mrejesho lakini hautakuwa bayana kwa umma kama ulivyoagiza na hivyo umma hautaweza kufahamu kama uliyoagiza katika ziara ya mwisho yalitekelezwa.
  Nakumbuka ulipoingia madarakani katika awamu yako ya kwanza ulifanya ziara kama hiyo lakini sikumbuki kusikia ukifanya ziara kama hiyo tena katika kipindi hicho tena.

  Kwa pamoja tumaweza.
   
 2. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #2
  Mar 24, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  hiyo ni kaz ya pinda.

  wala ucpoteze mda wako kumpongeaza. labda kama unajipendekeza.
   
 3. d

  dotto JF-Expert Member

  #3
  Mar 24, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  HAlafu baada ya ziara za MaWizara Umeme utakuwa historia TAnzania................. Acha upofu. Ziara Mawizarani maanake Pinda usingizi!!?/
   
Loading...