Pongezi Mhe. Spika Kuliongoza Vyema Bunge Letu, ila Sio Busara Kutumia Bunge Kujibu Trivia Issues za Mitandaoni, Zina Downplay Hoja Rasmi za Msingi!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
36,284
2,000
Wanabodi,

Naendelea kusisitiza kwenye mazuri tupongeze, kwenye mabaya tukosea na kwenye mapungufu tushauri, katika uendeshaji wa Bunge la safari hii, kiukweli wa dhati ya moyo wangu, safari hii Mhe. Spika anajitahidi sana kuliendesha vyema Bunge letu kiasi cha kustahili pongezi

Hivyo hili ni bandiko la pongezi kwa Spika wetu, Mhe. Job Yustino Ndugai jinsi anavyoliendesha Bunge hili kwa weledi sana. hivyo, nampa hongera Mhe. Spika kuliongoza Bunge letu vyema, hata hivyo, naomba kutoa angalizo muhimu la kihabari, sio busara sana, kulitumia Bunge letu kujibu hoja za muflslis na trivia Issues zinazoibuliwa kwenye mitandao ya kijamii. Baadhi ya hoja zinazojibiwa zina outwasha or ku downplay hoja rasmi za muhimu na za msingi!.

Hoja za mitandaoni zijibiwe mitandaoni na hoja rasmi za Bungeni ndizo zijibiwe Bungeni. Kufuatia sasa dunia inamilikiwa na mitandao ya kijamii, natoa wito kwa viongozi wetu wote, wawe na hangle zao za mitandao ya kijamii kama ilivyo kwa rais Magufuli, na baadhi ya mawaziri, Bunge pia liwe na Twitter account, Facebook account, Instagram account na YouTube channel yake, kisha kila kiongozi awe na social media accounts zake, ziwe manned na wasaidizi wao, mtu yoyote akiibua issue yoyote kwenye mitandao ya kijamii, ajibiwe huko huku, sio mtu aibuke kwenye mitandao ya kijamii kutuhumu, halafu anajibiwa rasmi Bungeni.

Mimi niliwahi kuitwa kuhojiwa na Kamati ya Bunge kwa tuhuma za kulidhalilisha Bunge, kufuatia makala yangu fulani niliyo iandika humu jf. Malala iliandikwa mtandaoni tarehe 7 September, 2017 Wabunge Wetu wa Ajabu!, Wanaachaje Bunge Lijipendekeze Kwa Serikali!, Wanajua Wajibu Wao?. Check 'n' Balance Itoke Wapi? - JamiiForums makala hii ilipokuwa mtandaoni, haikua issue, na baada ya kudumu humu jf zaidi ya miezi 6, ndipo gazeti la Raia Mwema likaichapisha gazetini,
1731124_RM.jpg

ndiko kukapelekea mimi kuitwa kuhojiwa na kamati ya Bunge tarehe 12/04/2018 ndipo nikaitwa Bungeni. Spika aagiza mwandishi Pascal Mayalla na Wahariri wa gazeti la Raia Mwema wahojiwe kwa kulidhalilisha Bunge - JamiiForums

Leo wakati Waziri Mkuu amekamilisha hotuba yake kuhitimisha bajeti yake, Waziri Mkuu amesema mambo makubwa mazuri na ya msingi sana kuhusu taifa letu na vita vya janga la Corona. Baada ya Waziri Mkuu kuhitimisha hotuba hiyo rasmi, katika kuahirisha Bunge, Mhe Spika akachomekea taarifa ya Tundu Lissu kutoka kwenye mitandao ya kijamii kwa kutumia muda wa zaidi ya dakika 10 kumzungumzia Tundu Lissu.
Kufuatia umuhimu wa hotuba ya Waziri Mkuu kuhitimisha bajeti yake, Mhe. Spika, hakupaswa kuchomekea kujimjibu Tundu Lissu kwa hoja alizoziibua mitandaoni. Hoja za mitandaoni zijibiwe mitandaoni zisijibiwe Bungeni, zina downplay umuhimu wa hotuba rasmi za kiserikali na sometimes zina outwash hotuba rasmi na muhimu za Bungeni kwa kujadili trivial issues zilizoibuliwa mitandaoni ambazo hazina maana yoyote or umuhimu wowote compared.

Vyombo vya habari vinaandika habari kutokana na uzito wa kihabari hivyo habari ya Spika kumjibu Tundu Lissu inaweza kupewa uzito na baadhi ya vyombo vya habari kuliko hata habari muhimu ya Waziri Mkuu.

Moja ya matumizi mazuri ya mitandaoni ya kijamii kama huu mitandao wetu wa JF, ni kuisaidia jamii, ikiwemo kuisaidia serikali yetu na pia kuwasaidia viongozi wetu, hivyo kufuatia mimi kuwa ni mwanahabari na Mhe Spika sio mwanahabari bali ni mtoa habari, baada ya hotuba muhimu kama ile ya Waziri Mkuu Bungeni, Mhe. Spika hakupaswa kutoa habari za yale makorokocho ya Lissu Bungeni.

Hili la kuwashauri viongozi wetu waongee nini, sisi jf tumeshauri sana na kiukweli tumesaidia sana viongozi wetu, serikali yetu na taifa letu.

Ushauri huu unatolewa very honestly kwa nia njema ya kusaidia without any malice aforethougts.

Namaliza kwa kumpongeza Spika kwa Kazi Nzuri, na Kumpongeza Waziri Mkuu kwa Hotuba Nzuri, na kuipongeza serikali yetu kwa hatua zote inazochukua kupambana na Corona

Nawatakia Jumatatu Jioni Njema.
Paskali
Rejea

Mada mbalimbali za mwandishi huyu kuhusu uendeshaji wa Bunge Letu

Je, Wajua Bunge linaweza kuvunjwa Siku 7 Zijazo?. lisipopokea ripoti ya CAG, Bunge linavunjwa kwa mujibu wa Katiba - JamiiForums

Vurugu za jana Bungeni: Chanzo ni Mhe. Job Ndugai!- Ni Dikteta Hatari Kuliko Spika Anne Makinda!. - JamiiForums

Wito: Wabunge Badilini Kanuni Kuondoa Udikteta wa Spika/N.Spika! - JamiiForums

Je, wajua kikatiba, CAG ana hadhi ya Jaji Mkuu?. Je, wajua ripoti ya CAG ni Zaidi ya Bill?. Je, wajua kwenye ripoti ya GAG, CAG ni zaidi ya Rais ? - JamiiForums

Mhe. Tundu Lissu, Please Acha Kumsulubu Spika Wetu!, Unammaliza Kabisa Hadi Ameshindwa Kazi!. - JamiiForums

Je, kukosekana kwa baadhi ya wabunge makini, machachari bungeni, kumepunguza ari na msisimko wa vikao vya bunge?. - JamiiForums

CHADEMA Wameliharibu Sana Bunge Letu! Hadi Mawaziri Wetu!, Kama Vipi Kifutwe Kabisa Tujue Moja?!. - JamiiForums

Nani Zaidi Kati ya Bunge na Mahakama?!. The Doctrine of "Separation of Powers" Nothing, Just a Myth! - JamiiForums

Je, Wajua Bunge linaweza kutoa azimio batili? CAG yuko kikatiba. Je, Bunge lina uwezo kutopokea ripoti ya CAG? - JamiiForums

Wabunge Wetu wa Ajabu!, Wanaachaje Bunge Lijipendekeze Kwa Serikali!, Wanajua Wajibu Wao?. Check 'n' Balance Itoke Wapi? - JamiiForums

Wapinzani msione aibu kushirikiana na CCM kwenye hoja zenye maslahi ya Taifa! Bashe ni mzalendo, aungwe mkono na wote! - JamiiForums

Vicky Kamata Anastahili Pongezi!, Asimama Kidete Kupinga Uonevu, Ubabe na Double Standards za Zungu! - JamiiForums

Kwa Hili! Hongera Sana Chadema, Hongera Mhe. Mbowe!, Sasa Muwege Mnasikilizaga Ushauri!. - JamiiForums

Waziri Mkuu anapotoa majibu mapesi kwa maswali mazito!: Ni uwezo or just saving faces?!.. - JamiiForums

Napendekeza Bunge Lianzishe Maswali Kwa Spika, Ili Maswali Kwa Waziri Mkuu Yabaki - JamiiForums
 
Trust None

JF-Expert Member
Feb 12, 2018
867
1,000
Wanabodi,

Hili ni bandiko la pongezi kwa Spika wetu, Mhe. Job Yustino Ndugai jinsi anavyoliendesha Bunge hili kwa weledi sana. hivyo, nampa hongera Mhe. Spika kuliongoza Bunge lete vyema, hata hivyo, sio busara sana, kulitumia Bunge letu kujibu hoja za muflslis na trivia Issues zinazoibuliwa kwenye mitandao ya kijamii. Baadhi ya hoja zinazojibiwa zina outwasha or ku downplay hoja rasmi za muhimu na za msingi!.

Hoja za mitandaoni zijibiwe mitandaoni na hoja rasmi za Bungeni ndizo zijibiwe Bungeni. Kufuatia sasa dunia inamilikiwa na mitandao ya kijamii, natoa wito kwa viongozi wetu wote, wawe na hangle zao za mitandao ya kijamii kama ilivyo kwa rais Magufuli, na baadhi ya mawaziri, Bunge pia liwe na Twitter account, Facebook account, Instagram account na YouTube channel yake, kisha kila kiongozi awe na social media accounts zake, ziwe manned na wasaidizi wao, mtu yoyote akiibua issue yoyote kwenye mitandao ya kijamii, ajibiwe huko huku, sio mtu aibuke kwenye mitandao ya kijamii kutuhumu, halafu anajibiwa rasmi Bungeni.

Mimi niliwahi kuitwa kuhojiwa na Kamati ya Bunge kwa tuhuma za kulidhalilisha Bunge, kufuatia makala yangu fulani niliyo iandika humu jf.

Kuitwa kule Bungeni, kulifuatia makala hiyo ya JF kuchapishwa kwenye gazeti la Raia Mwema. Makala ile ilikaa mwezi mzima humu jf bila kuleta kelele zozote, hadi ilipochapishwa gazetini, ndipo ikawa issue.

Leo wakati Waziri Mkuu amekamilisha hotuba yake kuhitimisha bajeti yake, Waziri Mkuu amesema mambo makubwa mazuri na ya msingi sana kuhusu taifa letu na vita vya janga la Corona.

Baada ya Waziri Mkuu kuhitimisha hotuba hiyo rasmi, katika kuahirisha Bunge, Mhe Spika akachomekea taarifa ya Tundu Lissu kutoka kwenye mitandao ya kijamii.

Kufuatia umuhimu wa hotuba ya Waziri Mkuu kuhitimisha bajeti yake, Mhe. Spika, hakupaswa kuchomekea kujimjibu Tundu Lissu kwa hoja alizoziibua mitandaoni. Hoja za mitandaoni zijibiwe mitandaoni zisijibiwe Bungeni, zina downplay umuhimu wa hotuba rasmi za kiserikali na sometimes zina outwash hotuba rasmi na muhimu za Bungeni kwa kujadili trivial issues zilizoibuliwa mitandaoni ambazo hazina maana yoyote or umuhimu wowote compared.

Vyombo vya habari vinaandika habari kutokana na uzito wa kihabari hivyo habari ya Spika kumjibu Tundu Lissu inaweza kupewa uzito na baadhi ya vyombo vya habari kuliko hata habari muhimu ya Waziri Mkuu.

Moja ya matumizi mazuri ya mitandaoni ya kijamii kama huu mitandao wetu wa JF, ni kuisaidia jamii, ikiwemo kuisaidia serikali yetu na pia kuwasaidia viongozi wetu, hivyo kufuatia mimi kuwa ni mwanahabari na Mhe Spika sio mwanahabari bali ni mtoa habari, baada ya hotuba muhimu kama ile ya Waziri Mkuu Bungeni, Mhe. Spika hakupaswa kutoa habari za yale makorokocho ya Lissu Bungeni.

Hili la kuwashauri viongozi wetu waongee nini, sisi jf tumeshauri sana na kiukweli tumesaidia sana viongozi wetu, serikali yetu na taifa letu.

Ushauri huu unatolewa very honestly kwa nia njema ya kusaidia without any malice aforethougts.

Namaliza kwa kumpongeza Spika kwa Kazi Nzuri, na Kumpongeza Waziri Mkuu kwa Hotuba Nzuri, na kuipongeza serikali yetu kwa hatua zote inazochukua kupambana na Corona

Nawatakia Jumatatu Jioni Njema.
Paskali
Nasikia una mpango wa kugombea jimbo mojawapo hapo Dar kupitia CCM

KILA LA KHELI
 
USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
3,615
2,000
Hii kasumba hata serkalini ipo sana. Hoja za mitandaoni zijibiwe kule kule mitandaoni

Kuna siku niliwahi kuondoka jambo kwenye group la whtssup la kazini kesho yake baada ya kikao cha kazi jamaa Mmoja akajakuniuliza kuhusu Yale maoni yangu nilimjibu kama Pasco kwamba ungeniuliza kule kule kwenye group maana nikikuona upo online

Nimeipenda hii yustino alifanyie kazi

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mnyakatari

JF-Expert Member
Oct 25, 2010
1,820
2,000
Mkuu pasco we ni kati ya great thinker wachache waliobaki humu JF..inabidi tumuite Huyo Jobu Ndugai kwenye kamati ya haki,maadili na madaraka ya JF atueleze kwanini anafanya kinachoonekana ni makosa ya wazi katika kutekeleza wajibu alioapa kuutumikia ipasavyo.
 
Tumpara Dudu

JF-Expert Member
Nov 15, 2016
591
500
Nakuonea huruma umemaliza bure mb zako kupost utumbo. Hivi kweli bunge hili la 11 chni ya huyu spika linaongozwa kwa weledi? Kaz ya bunge ni kuisimamia serikali,kutunga sheria na kuidhinisha bajeti ya serikali. Serikali inatumia pesa hazina bila ya ridhaa ya bunge af bunge linashindwa kuihoji CAG anawasisitiza kuihoj serikal juu ya hilo spika anatangaza bifu na CAG af unasema analiongoza bunge kwa weled? Bora hela uliyonunulia hilo bando ungenunua sanitizer tunawe mikono kujikinga na corona asee
 
nguruka wa kig0ma

JF-Expert Member
Jan 16, 2020
707
1,000
Pascal sikuhumu bali nakwambia ukweli kuwa, unapoandika uwe unamwogopa Mungu.
Kwa mtindo huu unaofanya nina mashaka hutouona ufalme wa Mungu, maana mara nyingi kwenye mabadiko yako nakuona una tenda dhambi ya unafiki.
Uhalisia wa ninachokisema kipo kwenye hili bandiko.
1. Umetangulia kupongeza kuanzia kwenye utangulizi wa bandiko lako.
2. Ukakosoa
3. Umeshauri.
Kitendo cha kupongeza kwanza kinapooza nguvu ya ukosoaji
Muhusika hatatafakari kosa bali atatafakari na mema.

Peleka upanga ukatao kuwili ufanyekazi yake.
Panapostahili kushauri, shauri
Panapostahili kukemea kemea
Panapostahili kushauri, shauri.

UNAFIKI NI DHAMBI MBAYA SANA pascal
 
mtingi1

JF-Expert Member
Mar 21, 2020
582
500
Napenda uandishi wako brother.
Wanabodi,

Naendelea kusisitiza kwenye mazuri tupongeze, kwenye mabaya tukosea na kwenye mapungufu tushauri, katika uendeshaji wa Bunge la safari hii, kiukweli wa dhati ya moyo wangu, safari hii Mhe. Spika anajitahidi sana kuliendesha vyema Bunge letu kiasi cha kustahili pongezi

Hivyo hili ni bandiko la pongezi kwa Spika wetu, Mhe. Job Yustino Ndugai jinsi anavyoliendesha Bunge hili kwa weledi sana. hivyo, nampa hongera Mhe. Spika kuliongoza Bunge letu vyema, hata hivyo, naomba kutoa angalizo muhimu la kihabari, sio busara sana, kulitumia Bunge letu kujibu hoja za muflslis na trivia Issues zinazoibuliwa kwenye mitandao ya kijamii. Baadhi ya hoja zinazojibiwa zina outwasha or ku downplay hoja rasmi za muhimu na za msingi!.

Hoja za mitandaoni zijibiwe mitandaoni na hoja rasmi za Bungeni ndizo zijibiwe Bungeni. Kufuatia sasa dunia inamilikiwa na mitandao ya kijamii, natoa wito kwa viongozi wetu wote, wawe na hangle zao za mitandao ya kijamii kama ilivyo kwa rais Magufuli, na baadhi ya mawaziri, Bunge pia liwe na Twitter account, Facebook account, Instagram account na YouTube channel yake, kisha kila kiongozi awe na social media accounts zake, ziwe manned na wasaidizi wao, mtu yoyote akiibua issue yoyote kwenye mitandao ya kijamii, ajibiwe huko huku, sio mtu aibuke kwenye mitandao ya kijamii kutuhumu, halafu anajibiwa rasmi Bungeni.

Mimi niliwahi kuitwa kuhojiwa na Kamati ya Bunge kwa tuhuma za kulidhalilisha Bunge, kufuatia makala yangu fulani niliyo iandika humu jf.

Kuitwa kule Bungeni, kulifuatia makala hiyo ya JF kuchapishwa kwenye gazeti la Raia Mwema. Makala ile ilikaa mwezi mzima humu jf bila kuleta kelele zozote, hadi ilipochapishwa gazetini, ndipo ikawa issue.

Leo wakati Waziri Mkuu amekamilisha hotuba yake kuhitimisha bajeti yake, Waziri Mkuu amesema mambo makubwa mazuri na ya msingi sana kuhusu taifa letu na vita vya janga la Corona.

Baada ya Waziri Mkuu kuhitimisha hotuba hiyo rasmi, katika kuahirisha Bunge, Mhe Spika akachomekea taarifa ya Tundu Lissu kutoka kwenye mitandao ya kijamii.

Kufuatia umuhimu wa hotuba ya Waziri Mkuu kuhitimisha bajeti yake, Mhe. Spika, hakupaswa kuchomekea kujimjibu Tundu Lissu kwa hoja alizoziibua mitandaoni. Hoja za mitandaoni zijibiwe mitandaoni zisijibiwe Bungeni, zina downplay umuhimu wa hotuba rasmi za kiserikali na sometimes zina outwash hotuba rasmi na muhimu za Bungeni kwa kujadili trivial issues zilizoibuliwa mitandaoni ambazo hazina maana yoyote or umuhimu wowote compared.

Vyombo vya habari vinaandika habari kutokana na uzito wa kihabari hivyo habari ya Spika kumjibu Tundu Lissu inaweza kupewa uzito na baadhi ya vyombo vya habari kuliko hata habari muhimu ya Waziri Mkuu.

Moja ya matumizi mazuri ya mitandaoni ya kijamii kama huu mitandao wetu wa JF, ni kuisaidia jamii, ikiwemo kuisaidia serikali yetu na pia kuwasaidia viongozi wetu, hivyo kufuatia mimi kuwa ni mwanahabari na Mhe Spika sio mwanahabari bali ni mtoa habari, baada ya hotuba muhimu kama ile ya Waziri Mkuu Bungeni, Mhe. Spika hakupaswa kutoa habari za yale makorokocho ya Lissu Bungeni.

Hili la kuwashauri viongozi wetu waongee nini, sisi jf tumeshauri sana na kiukweli tumesaidia sana viongozi wetu, serikali yetu na taifa letu.

Ushauri huu unatolewa very honestly kwa nia njema ya kusaidia without any malice aforethougts.

Namaliza kwa kumpongeza Spika kwa Kazi Nzuri, na Kumpongeza Waziri Mkuu kwa Hotuba Nzuri, na kuipongeza serikali yetu kwa hatua zote inazochukua kupambana na Corona

Nawatakia Jumatatu Jioni Njema.
Paskali
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom