uchumi2018
JF-Expert Member
- Mar 4, 2018
- 1,420
- 1,950
Habari zenu wadau.
Nimeona mimi kama mfanyakazi ninayeguswa na sheria na taratibu za mifuko ya hifadhi ya jamii nitoe pongezi kwa wabunge hawa Halima Mdee na Ester Bulaya kwa hoja zao bungeni kutetea wastaafu ambao ndio wachangiaji na wanufaika wa mifuko hii.
Ni mara nyingi tumesikia wabunge wengi wakitetea wakulima,wafanyabiashara wafugaji n.k lakini si mara nyingi kusikia mfanyakazi akitajwa pamoja na kwamba naye anahusika kuwachagua.
Ni ukweli usiopingika kwamba mfanyakazi ndo mtu pekee anayelipa kodi kwa uaminifu bila hata kuhusishwa kujadili namna gani akatwe kodi,Cha ajabu na kusikitisha ni pale ambapo hata baada ya kulipa kodi kwa uaminifu,bado fedha aliyokatwa ili imsaidie akistaafu inapangiwa mipango mingine tofauti na malengo yake na wakati wa kustaafu anakutana na danadana.Jambo hili limeleta usumbufu mkubwa kwa wastaafu na hata kupelekea vifo vya mapema kwa wahusika.
Pamoja na utetezi huo uliotolewa na wabunge hawa,naomba pia tuongelee mafao yanayotolewa, iwe kwa kuwahi au kwa kuchelewa.
Nichukulie mfano mfuko wa NSSF ambao unahudumia sekta binafsi, mstaafu hupewa asilimia ishirini na tano (25%) ya fedha yake yote aliyokusanya muda wake wote wa utumishi.
Kiasi hiki ni kidogo sana ukilinganisha na kiwango kinachotolewa na mifuko mingine. Pia mantiki ya kutoa kiasi hiki kwa mstaafu mwenye miaka 60 ukilinganisha na matarajio umri wa kuishi wa mtanzania(life expectance).
Ni muhimu mifuko yote ikawa na kiwango kimoja maana wote tunaishi taifa moja lenye matumizi/mahitaji yanayofanana,
Nawapongeza waheshimiwa wabunge hawa kwa kuliona hili na naomba wabunge wengine waige mfano huo.
Pamoja na kwamba wao mafao yao wanapata moja kwa moja lakini ni vyema kujua kuwa wapo watanzania wenzenu mnao wawakilisha,ndugu zenu na hata watoto wenu ambao au wameajiriwa au wataajiriwa baadaye.
Asanteni saaana.