Pongezi kwenu Mdee na Bulaya kwa kuzungumzia mifuko ya Hifadhi ya Jamii Bungeni

uchumi2018

JF-Expert Member
Mar 4, 2018
906
1,000
Habari zenu wadau.

Nimeona mimi kama mfanyakazi ninayeguswa na sheria na taratibu za mifuko ya hifadhi ya jamii nitoe pongezi kwa wabunge hawa Halima Mdee na Ester Bulaya kwa hoja zao bungeni kutetea wastaafu ambao ndio wachangiaji na wanufaika wa mifuko hii.
Ni mara nyingi tumesikia wabunge wengi wakitetea wakulima,wafanyabiashara wafugaji n.k lakini si mara nyingi kusikia mfanyakazi akitajwa pamoja na kwamba naye anahusika kuwachagua.

Ni ukweli usiopingika kwamba mfanyakazi ndo mtu pekee anayelipa kodi kwa uaminifu bila hata kuhusishwa kujadili namna gani akatwe kodi,Cha ajabu na kusikitisha ni pale ambapo hata baada ya kulipa kodi kwa uaminifu,bado fedha aliyokatwa ili imsaidie akistaafu inapangiwa mipango mingine tofauti na malengo yake na wakati wa kustaafu anakutana na danadana.Jambo hili limeleta usumbufu mkubwa kwa wastaafu na hata kupelekea vifo vya mapema kwa wahusika.

Pamoja na utetezi huo uliotolewa na wabunge hawa,naomba pia tuongelee mafao yanayotolewa, iwe kwa kuwahi au kwa kuchelewa.

Nichukulie mfano mfuko wa NSSF ambao unahudumia sekta binafsi, mstaafu hupewa asilimia ishirini na tano (25%) ya fedha yake yote aliyokusanya muda wake wote wa utumishi.

Kiasi hiki ni kidogo sana ukilinganisha na kiwango kinachotolewa na mifuko mingine. Pia mantiki ya kutoa kiasi hiki kwa mstaafu mwenye miaka 60 ukilinganisha na matarajio umri wa kuishi wa mtanzania(life expectance).

Ni muhimu mifuko yote ikawa na kiwango kimoja maana wote tunaishi taifa moja lenye matumizi/mahitaji yanayofanana,

Nawapongeza waheshimiwa wabunge hawa kwa kuliona hili na naomba wabunge wengine waige mfano huo.

Pamoja na kwamba wao mafao yao wanapata moja kwa moja lakini ni vyema kujua kuwa wapo watanzania wenzenu mnao wawakilisha,ndugu zenu na hata watoto wenu ambao au wameajiriwa au wataajiriwa baadaye.

Asanteni saaana.
 
mandawa

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
294
500
Nami naunga mkono pongezi hizi kwa waheshimiwa hawa...kweli wamewakilisha wafanyakazi wengi hasa wa secta binafsi ambao hawana watetezi wa kutegemewa.

Wengi hawajui kuwa maendelea au miradi mingi ya maendeleo tunayosifia leo..yanatokana na hela za wafanyakazi kupitia mifuko...kwa maana nyingine..wakati watu wanaimba sifa za miradi..hawajui.miradi hii inafanyika kwa gharama ya kuminya haki za wafanyakazi.

Wastaafu wengi wanaumiza vichwa muda wa kustaafu unavyokaribia...hajui ataishije na asilumia 25 wakati nyumba hana..watoto bado wanasoma n.k.

Ni maombi yangu Mh.Raisi Samia..aliangalie hili kwa jicho la kipekee. Bila hivyo..umoja na amani tunayoiombea haitawezekana wakati wengi wa wafanyakazi wanalia mioyoni mwao kwa kukosa haki.
 
amaizing

JF-Expert Member
May 3, 2013
3,584
2,000
Serikali ipitie upya pia fao la kujitoa..haiwezekan mfanyakazi wa taasisi binafsi asiruhusiwe kuchukua mfao yake pindi akiacha kazi au mradi anaoufanyia kazi ukiisha eti asuburi umri wa kustaafu..hii inatuumiz Sana waajiriwa wa taasisi binafsi
Mshahara wangu, Makato yametoka katika mshara wangu na bado siruhusiwi kuchukua pesa yangu wakati kazi imeshaisha
Tena ukienda NSSF wanakujibu watakupa asilimia 35 ya pesa ulizochangiaTena hiyo utaipata baada ya miez sita..
 
Trimmer

JF-Expert Member
Apr 25, 2014
1,677
2,000
Hivi waliokaa wakatengeneza hiki kinachoitwa kikokotoo wanaamini uwepo wa Mungu kweli,,?
 
uchumi2018

JF-Expert Member
Mar 4, 2018
906
1,000
Hivi waliokaa wakatengeneza hiki kinachoitwa kikokotoo wanaamini uwepo wa Mungu kweli,,?
Mkuu si unajua miungu ni mingi,inategemea imani zao,zinawaelekeza wapi,lakini kwa Mungu aliyeumba mbingu na nchi huwezi kumwamini alafu ukatunga sheria ya kuwabinya wenzako ili wewe unufaike.
Mimi mpaka sasa mnaamini,mbali na serikali kuna watu binafsi wanaojinufaisha na fedha ya hii mifuko,mfano kujikopesha bila riba n.k
vinginevyo wasingetunga sheria za kukandamiza walengwa wa mfuko husika.
 
Odhiambo cairo

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
15,199
2,000
Ajabu ni kuwa. Katika michango ya Bulaya na Halima niliona kama Mzee Kimei anageuka kuwa "chawa" . Nilibaki simuelewi anatetea nini dhidi ya wafanyakazi wastaafu
emoji56.png
emoji3517.png
. Sijui ndiyo kufukuzia uaziri ?!
 
uchumi2018

JF-Expert Member
Mar 4, 2018
906
1,000
Serikali ipitie upya pia fao la kujitoa..haiwezekan mfanyakazi wa taasisi binafsi asiruhusiwe kuchukua mfao yake pindi akiacha kazi au mradi anaoufanyia kazi ukiisha eti asuburi umri wa kustaafu..hii inatuumiz Sana waajiriwa wa taasisi binafsi
emoji3064.png
Kweli kabisa,maana kama kazi imeisha mtu asilazimishwe kuendelea kutafuta kazi,huku fedha yake imeshikiliwa mahali fulani,anaweza kutumia fedha yake kujiajili au hata kufanya kitu kingine cha kimaendeleo.

Huwa najiuliza,hivi mbona wakulima na wafanya biashara hawahimizwi kujiunga kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii? au hawa sio watanzania?

ok,kama wapo watanzania wanafanya shughuli zao na wakizeeka wana utaratibu wao wa kujitunza,ni kwa nini linapokuja suala la mfanyakazi

huyu anaonekana hawezi kutumia fedha yake akajitunza hadi atakapotoka kwenye maisha haya?

Kweli kuna mambo mengi ya kujiuliza,naamini wahusika wanasoma wayafanyie kazi.
 
Mlenge

R I P
Oct 31, 2006
2,131
2,000
Nichukulie mfano mfuko wa NSSF ambao unahudumia sekta binafsi,
mstaafu hupewa asilimia ishirini na tano (25%) ya fedha yake yote aliyokusanya muda wake wote wa utumishi.
Kiasi anacholipwa mtu kinatokana na formula ('kikokotoo'). Kikokotoo hicho mtu hupata hela nyingi kuliko alizochangia.

Wakisema wakurudishie kile tu ulichochangia (na kafaida kidogo) ni hela kidogo kuliko za kikokotoo.

Hoja kuu ni je, hizohizo unazozilalamikia, wataweza kuendelea kuzilipa? Au wata default?
 
Mlenge

R I P
Oct 31, 2006
2,131
2,000
Huwa najiuliza,hivi mbona wakulima na wafanya biashara hawahimizwi kujiunga kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii?
Hili likifanyika litakuwa ni vema. Kila mtu alazimike kujiunga na mfuko wa hifadhi ya jamii. Au kila mtu awe na hiari ya kujiunga.
 
uchumi2018

JF-Expert Member
Mar 4, 2018
906
1,000
Kikokotoo hicho mtu hupata hela nyingi kuliko alizochangia.
Hili sijui kama umelifanyia utafiti,mimi ni miongoni mwa wanufaika wa fao la kujitoa kabla halijafutwa.

Nimechukua fedha hiyo mara mbili. Kila nilipohama kampuni niliomba fedha na kulipwa. Nilichokiona kufuatia uzoefu wangu ni kuwa mwajiri anajaza fomu kuonyesha michango uliyochangia na unaipeleka kwenye mfuko husika,Pesa iliyokuwa kwenye fomu ya mwajiri na niliyolipwa tofauti yake ni kidogo nikimaanisha kuongezeka,na nilipouliza jibu ni kwamba pesa yako inapata liba kidogo.

Kuhusu kikokotoo cha kustaafu kwamba unapewa fedha nyingi kidogo kuliko michango yako,sijui ila nina wasiwasi kama inafanyika hivyo.Kuna watu nawafahamu,fedha waliyopewa ya kustaafu kwa kuzingatia hicho kikokotoo inatia aibu. Binafsi naona mambo haya huko mbele tuendako yatachochea rushwa na wizi kazini,maana sheria ya kazi ilifuta kiinua mgongo kwa misingi ya kwamba mwajiri anachangia kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii,ukienda kwenye hiyo mifuko unakutana na rungu la kikokotoo ambacho na hicho kidogo kinapatikana baada ya mwaka na kitu.

Kama huna imani unaweza kuchukua maamuzi magumu,ili usiadhirike huko mbeleni.
Na hata wewe ukijikaza,mwanao anayeshuhudia unayoyapitia,nadhani haihitaji kuwa na digrii ndo
ujue ni nini atafanya endapo ataajiliwa siku za usoni.

Nadhani serikali ichukue hatua stahiki kunusuru,hii hali.
 
Trimmer

JF-Expert Member
Apr 25, 2014
1,677
2,000
Kwani inashindikana nini kumlipa mchangiaji pesa yake yote aliyochangia akafie mbele,, kwanini watunzi wa hizi kanuni wanakua na roho za kihayawani kiasi hiki,,
 
uchumi2018

JF-Expert Member
Mar 4, 2018
906
1,000
Kwani inashindikana nini kumlipa mchangiaji pesa yake yote aliyochangia akafie mbele,, kwanini watunzi wa hizi kanuni wanakua na roho za kihayawani kiasi hiki,,
Na huu ndo mshangao tunaoupata,kama ni suala la kumsaidia muhusika asile pesa yote kwa mpigo,mbona kuna watu wengine hawapo kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii na maisha yanasonga?
 
CHIEF WINGIA

JF-Expert Member
Jul 12, 2013
1,290
2,000
Ukweli ni kwamba mwendazake a.k.a mtetezi wa wanyonge pamoja na gege lake ndio walio ushadadia na kuutia sahihi huo muswada na kufanya kuwa sheria kisha wakazikomba pesa zote kwenye mifuko ya jamii.
 
uchumi2018

JF-Expert Member
Mar 4, 2018
906
1,000
Lumpsum anayopewa anapostaafu, jumlisha na anayoendelea kupewa kila mwezi mpaka mwisho wa maisha yake, kulingana na alichokuwa anachangia.
Na hapo ndo penye changa la macho,hivi life expectance ya mtanzania ni miaka mingapi? kama ni chini ya miaka sitini ina maana unategemewa kufa wakati wowote,kama ndivyo ni kwa nini basi usipewe angalau asilimia 75%?
 
uchumi2018

JF-Expert Member
Mar 4, 2018
906
1,000
Ukweli ni kwamba mwendazake a.k.a mtetezi wa wanyonge pamoja na gege lake ndio walio ushadadia na kuutia sahihi huo muswada na kufanya kuwa sheria kisha wakazikomba pesa zote kwenye mifuko ya jamii.
Jamani nadhani mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Mimi nakumbuka yule mdada aliyekuwa kiongozi wa mamlaka inayosimamia mifuko ya hifadhi ya jamii,rais alimtumbua kwa kauli yake ya kejeli kwa wafanyakazi kwamba wanalilia fedha za mifuko hii wakati inachangiwa na waajiri,nakumbuka na mimi nilikuwa miongoni mwa waliopiga kelele na yule mdada akatumbuliwa.

Kama sikosei,hii sheria ikiwa ni pamoja na ile iliyofuta fao la kujitoa alitungwa na serikali takatifu zisizokuwa na mawaa zilizopita,
kabla haijaji hiyo ya wanyonge,nakumbuka TUCTA ilipeleka mapendekezo yake kwa rais,na ndo akatoa maamuzi ya vigezo na masharti yaliyopo yaendelee kutumika hadi 2023 ambapo taratibu hizo zingeangaliwa upya,mimi nilikuwa miongoni mwa walioshangilia usemi huo.
Lakini nilipokuja kujua kwamba sheria ya NSSF ndo mbaya kuliko zote ,na ndo inalipa asilimia 25 ambayo iko chini kuliko mifuko mingine,nikasikitika na kujutia kile kilichonifanya nishangilie kama chizi,nikajicheka mwenyewe.
 
Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
1,709
2,000
Habari zenu wadau.

Nimeona mimi kama mfanyakazi ninayeguswa na sheria na taratibu za mifuko ya hifadhi ya jamii nitoe pongezi kwa wabunge hawa Halima Mdee na Ester Bulaya kwa hoja zao bungeni kutetea wastaafu ambao ndio wachangiaji na wanufaika wa mifuko hii.
Ni mara nyingi tumesikia wabunge wengi wakitetea wakulima,wafanyabiashara wafugaji n.k lakini si mara nyingi kusikia mfanyakazi akitajwa pamoja na kwamba naye anahusika kuwachagua.

Ni ukweli usiopingika kwamba mfanyakazi ndo mtu pekee anayelipa kodi kwa uaminifu bila hata kuhusishwa kujadili namna gani akatwe kodi,Cha ajabu na kusikitisha ni pale ambapo hata baada ya kulipa kodi kwa uaminifu,bado fedha aliyokatwa ili imsaidie akistaafu inapangiwa mipango mingine tofauti na malengo yake na wakati wa kustaafu anakutana na danadana.Jambo hili limeleta usumbufu mkubwa kwa wastaafu na hata kupelekea vifo vya mapema kwa wahusika.

Pamoja na utetezi huo uliotolewa na wabunge hawa,naomba pia tuongelee mafao yanayotolewa, iwe kwa kuwahi au kwa kuchelewa.

Nichukulie mfano mfuko wa NSSF ambao unahudumia sekta binafsi, mstaafu hupewa asilimia ishirini na tano (25%) ya fedha yake yote aliyokusanya muda wake wote wa utumishi.

Kiasi hiki ni kidogo sana ukilinganisha na kiwango kinachotolewa na mifuko mingine. Pia mantiki ya kutoa kiasi hiki kwa mstaafu mwenye miaka 60 ukilinganisha na matarajio umri wa kuishi wa mtanzania(life expectance).

Ni muhimu mifuko yote ikawa na kiwango kimoja maana wote tunaishi taifa moja lenye matumizi/mahitaji yanayofanana,

Nawapongeza waheshimiwa wabunge hawa kwa kuliona hili na naomba wabunge wengine waige mfano huo.

Pamoja na kwamba wao mafao yao wanapata moja kwa moja lakini ni vyema kujua kuwa wapo watanzania wenzenu mnao wawakilisha,ndugu zenu na hata watoto wenu ambao au wameajiriwa au wataajiriwa baadaye.

Asanteni saaana.
Hakuna Jipya ktk hilo Sheria ilikwisha sainia hawana uwezo wa kuibadilisha
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom