digba sowey
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 7,893
- 14,347
Wakuu habari za wakati huu,
Napenda kutumia fursa hii kumpongeza Waziri wa elimu Profesa J.Ndalichako pamoja na Wizara ya Elimu kwa ujumla kwa kutoa waraka unao husu ufundishaji na ujifunzaji.
Naomba nikiri kuwa huu waraka umefika kwa wakati muafaka kwani ukiiusoma utabaini kuwa wakuu wa mikoa na maafisa elimu walitumia mamlaka yao kudhulumu haki za wanafunzi na walimu kwa kigezo cha kuinua ufaulu huku wakiwalazimisha walimu na wanafunzi kubaki kusoma wakati wa likizo na pia masomo kwa darasa la mitihani ililazimishwa kuanza saa kumi na mbili na nusu eti lengo kuu ni kuinua ufaulu wa wanafunzi.
Hivyo kwa waraka huu wa elimu kwa mwaka 2020 wizara ya elimu imepiga marufuku upuuzi huo, maana wahanga wakubwa walikuwa ni wanafunzi na walimu wa chini na ilifikia hatua walimu walinyumwa likizo kwa kigezo cha kufundisha wakati wa likizo,Mimi mwenyewe ni mhanga wa hili, niliwahi kugombana na bwana Godfrey Zambi mkuu wa mkoa wa Lindi juu ya ukiritimba huu alipotembelea shuleni kwangu mwaka 2017 na kuzuia walimu kwenda likizo ili wafundishe
Ukisikia serikali ya wanyonge basi tambua kuwa ni ile ile serikali ya awamu ya tano,
Soma waraka hapa>>>>>>View attachment WARAKA WA ELIMU 2020.pdf
Sent using Jamii Forums mobile app