Pongezi kwa wizara ya Elimu-Rushwa ya ngono SAUT.

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
515
2,874
Inakumbukwa kuwa tarehe 20/Nov/2018 ,Niliibua suala la rushwa ya ngono katika chuo cha SAUT Mwanza hii ilikuwa kabla ya Dr.Shule kuibua zile tuhuma za rushwa ya ngono UDSM tar.27/Nov/2017 siku saba baada ya mimi kusemea swala la Rushwa ya ngono chuo cha SAUT Mwanza.

Mwalimu aliyekuwa anasumbua wanafunzi kwa Rushwa ya ngono na hata kufanya wanafunzi wawili waliomkataa ku- carry somo lake kwa miaka 2 mfululizo ,na yeye akijinadi kuwa atawakomesha (Ushahidi upo).

Tar 20/Nov/2018 baada ya kupata taarifa, niliwasiliana na waziri wa Elimu Prof.Joyce Ndalichako na alionesha kukasirishwa na tabia hiyo na kuahidi kulifuatilia ili mwalimu huyo achukuliwe hatua .

Siku ya kadhaa TAKUKURU walifika na kumuhoji huyo mwalimu (Lecturer) na kumnyanganya simu yake.

Wanafunzi hao wahanga walionipa taarifa waliendelea kutishiwa na hata kulazimishwa kusema kuwa wanaongopea ,baadaye ikaandikwa email ya ku-forge kuonesha hao Dada wahanga wamekiri eti ni uongo na wanaomba radhi utawala !

Wizara ya elimu iliendelea kufuatilia na Kiongozi mmoja muhimu wa serikali anaitwa Adamu ,ila Chuo kiliendelea kuficha ficha .

Hadi wizara ya Elimu ilipotoa agizo kutenguliwa kwa Vice Chancellor aitwaye prof. mbassa.Na akateuliwa Prof.Costarica Mahalu tar.28 February 2019.

Haikuishia hapo ,tar 04/March 2019 Naibu waziri ole Nash alifika chuoni SAUT - Mwanza na kuongea na uongozi wa chuo ,pia Naibu waziri aliomba Mhanga wa Rushwa ya ngono aongee aliongea binti huyo aliyewahi nitumia malalamiko yake .

Na Mh.Naibu waziri akaagiza Tume kuanza kuchunguza wiki ijayo na huyo mwalimu anayetuhumiwa kumbe aliondoka kwenda kenya kusoma ameagiza ,arudi haraka na taarifa zake zifike ofisini kwake.

Kuhusu mikopo ,tuliwahi semea sana Mikopo SAUT maamuzi ni Loans officer alitenguliwa ,na chuo kuagizwa kuwe na mfumo mzuri.

Napenda kupongeza wizara ya Elimu, kuanzia Mh.Waziri Ndalichako, Naibu waziri ,makatibu na Manaibu katibu wanafanya kazi nzuri ,mara nyingi ukiwapa malalamiko wanayafanyia kazi.

Pia napenda kumpongeza huyu Msichana mhanga wa Rushwa ya ngono aliyekataa kurubuniwa ,aliyekubali vitisho ,na akasimama kutetea wenzake na yeye mwenyewe hata kuthubutu kutoa ushuhuda mbele ya Naibu waziri bila kuogopa ; taasisi za kijinsia muoneni huyu Dada ni shupavu hakika.

Shukran sana.

Abdul Nondo.

abdulnondo10@gmail.com

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom