Pongezi kwa wanaharakati na wanamapinduzi wote kwa kazi nzuri ya jana, | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pongezi kwa wanaharakati na wanamapinduzi wote kwa kazi nzuri ya jana,

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by WJN, Feb 5, 2011.

 1. W

  WJN Member

  #1
  Feb 5, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pongezi ziwaendee wanamapinduzi na wanaharakati wote wa UDSM, kwa kazi nzuri mliyoifanya jana. Nnaamini siku zote haki hailetwi ulipo bali unaifwata huko huko iliko, mifano hai ni harakati za kimapinduzi zinazoendelea huko tunisia, egypt na sasa yemeni pamoja na jordan. Japo safari ni ndefu lakini naamini terminal tutafika. Aluta continua haijalishi kama punda atafia njiani lakini mzigo lazima ufike, Solidarity......
   
 2. The Only Kilo

  The Only Kilo JF-Expert Member

  #2
  Feb 6, 2011
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 355
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  tumekustudy mkereketwa!!!
   
 3. Deodat

  Deodat JF-Expert Member

  #3
  Feb 6, 2011
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 1,279
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Tunisia na Egypt wanadai maslai ya nchi, nyie mnadai maslai ya matumbo yenu (10000 kwa siku), hamuwezi kufanikiwa, badilisheni ajenda.
   
 4. Click_and_go

  Click_and_go JF-Expert Member

  #4
  Feb 6, 2011
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 451
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33

  ....ha ha haaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!
  kati ya vilaza wa Tanzania na wewe umo!!!! hivi unapozungumzia "maslahi ya nchi" unamaanisha nini??? Bila ELIMU BORA nchi itafika wapi?? na hiyo ELIMU itapatikanaje kama mazingira ya kuipata hayajaandaliwa?? Hao wasomi wa kuongoza nchi watapatikanaje???

  Mkuu,,,am sorry to say this but VIKIRIA ANGALAU KIDOGO,,,ANGALAU KAMA MWANAFUNZI WA CHEKECHEA!!
  DUH!!!
   
 5. Jitihada

  Jitihada Senior Member

  #5
  Feb 6, 2011
  Joined: Feb 6, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nawiwa kuamini kwamba uzalendo wako ni wa kugushi, mandamano ya UDSM, yalikuwa na ajenda kama tatu hivi, zikiwemo kupinga kuilipa DOWANS na suala la KATIBA MPYA, lakini we bado huoni kama hizi ni ajenda za maslai ya nchi? na ukae ukitambua 5000/= ya 2005 sio sawa na 5000/= ya 2011. thamani ya pesa inashuka kila dakika hata BOT wanalitambua hilo ndo maana wakaamua kutoa noti mpya ili kupambana na inflation rate.
   
 6. Deodat

  Deodat JF-Expert Member

  #6
  Feb 6, 2011
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 1,279
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Hivi unafikiri kuna mmachinga atakae unga mkono kwa huo upupu wenu wa kutaka elf 10000? unafikiri kuna mkulima aliyeko kule mbinga atasikiliza ujinga wenu? kwanza watashangaa kwamba hata kuna watu wanapata 5000 kwa siku. Ninachowashauri ni kwamba ili mgomo wenu uwe na mashiko lazima muwe na ajenda kuu zenye misingi ya kudai mabadiliko ya mfumo ambayo eventually yataleta sustainable changes.

  Nikuulize, hivi leo mkipewa 10000, halafu inflation ikaendelea kama ilivyo mpaka kufikia 30% unafikiri hiyo elfu 10 itatosha? Nasikitika kwamba hata nyie tunaowaita wasomi ni bure kabisa, bora serikali ingetumia nguvu kuwapeleka wote veta na vyuo vingine vya ufundi ili baadae tupate watu wanaoweza kuzalisha tangible products kuliko kuwa na maelfu ya watu wanaosomea ualimu wa historia, civics na geography huku wakitaka waongezewe boom mpaka elf 10000.

  Hivi wewe unajua kuwa kuna watu wengi tu wasiopata hiyo 150,000 (5000*30) kwa mwezi? Hoja zenu nyepesi na ni kero kwa watu wenye akili timamu wanaodai mabadiliko ya kweli. Kwa nini msiandamane kupinga malipo ya dowans? kwa nini msiandamane kudai katiba mpya? kwanini msiandamane kupinga kutochukuliwa hatua za maana kwa mafisadi papa? kwa nini msiandamane kupinga mfumuko wa bei (ambao hautaisha kwa nyinyi kupewa 10000/day), kwa nini msiandamane kuwa kwenye vyuo vikuu visivyokuwa na facilities za kutosha kama vitabu na computers?.

  Tatizo lenu wengi mmesoma elimu za kwenye majarida ya msabila na nyambari nyangwine na hapo chuo kikuu mkishasoma slides za walimu basi huna habari na vitabu (hata vikiwepo). Kwa kifupi taifa hili halina tena vyuo vyenye kuzalisha wasomi ila tuna taasisi za kusaidia vijana wakue huku wakijidanganya wanasoma.

  Serikali embu pelekeni veta hawa wahuni wanaofikiria matumbo yao (eti 10000/day) bila kuangalia hali halisi.


  NB: Pale kwenye bluu nadhani ulitaka kuandika FIKIRIA lakini kwasababu ya elimu za kudesa hata spelling check ni tatizo kwako.
   
 7. Deodat

  Deodat JF-Expert Member

  #7
  Feb 6, 2011
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 1,279
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145

  Si kweli, huo ulikuwa unafiki, makelele yao yote yapo hapo kwenye elf 10000. nilipita hapo UDSM siku wanayojadiliana kuanzisha huo mgomo na nilisimama pale kusikiliza, wanachotaka ni hiyo elfu na wakipewa hutosikia habari za katiba mpya wala dowans, kwa kifupi hao ni wasomi HEWA.

  Kuhusu thamani ya pesa, nimesoma TIME VALUE OF MONEY hivyo huna haja ya kunielimisha.

  Piganeni serikali ipambane na mfumuko wa bei siyo nyinyi kupewa pesa nyingi. Ingekuwa kiwango cha pesa kinasaidia wenzenu Zimbabwe wananunua biscuit kwa laki mbili sasa. Embu jitahidini kudai vitu vitakavyoleta mabadiliko ya kudumu.
   
 8. nziriye

  nziriye JF-Expert Member

  #8
  Feb 8, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 960
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  bwana mkubwa angalia hatua zako hatusemi vikiria ila ni fikiria.otherwise mshikamane ipasavyo kwani umoja ni nguvu ,utengano ni udhaifu.,it can be done,bravoo
   
 9. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #9
  Feb 8, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  u sound to be right somehow
   
 10. f

  furahi JF-Expert Member

  #10
  Feb 9, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 947
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Nikijaribu kuigawa hii 5000 kwa siku mahesabu hayakubali kabisa, sijui wanasurvive vipi hawa wanafunzi mpaka sasa.
  Asubuhi Chai -1000
  Maji ya kunywa siku nzima minimum-1500
  Lunch (ya kujibana pamoja na kipande cha tunda)-2000
  Balance-500
  Supper-????????
   
 11. X

  XOXOQY JF-Expert Member

  #11
  Feb 9, 2011
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 220
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Kama haya mwaweza kuyazungumza nyumbani kwenu hapa "educhat.wapka.mobi" fungua adress hii kwa pc au mobile phone
   
Loading...