Pongezi kwa Waarabu/ Wahindi waislamu wanaoishi hapa Tanzania. Mnyonge mnyongeni, haki yake.....!

Countrywide

JF-Expert Member
Mar 2, 2015
18,173
27,223
Leo Kuna Jambo ambalo nimeona ni wazi napaswa kulizungumza kwa kuwa limenigusa sana.

Waarabu na wahindi ambao ni waislamu, Wana utaratibu ambao nimetokea kuupenda sana na ikitupendeza wakristo naomba tuuige.
Najua Kuna mabaya mengi yanayofanywa na Hawa watu wa race hii ila kwenye mazuri tuwape sifa zao.

Wana utaratibu wa kujitolea kutoa huduma ya maji bure kabisa. Kuna sehemu wapo karibu na shule, huwezi amini wanafunzi maji yao ya kunywa wanaenda kuchota kwa hao watu kwenye mabomba yao ambayo wameyaweka nje, tena kuna bango kubwa "MAJI BURE"
sio kwa wanafunzi tu, hata raia anaruhusiwa kuchota hapo maji bure.

Huu ni zaidi ya uungwana na kwa hili nawapongeza sana na iigwe na watu wengine(sijawahi kuona mswahili kafanya hivi).
Pengine ni maelekezo ya dini yao, hivyo kwa dini zingine jambo Kama hili tunapaswa kuliiga.
 
Hebu kwanza hayo mabaya yao ambayo umesema yapo mengi tu
Wengine hatuyajui
Kwa muktadha wa mzee wangu hayupo duniani kwa sasa aliwahi kusema maneno haya; "Ukiwa unatenda maovu na unataka jamii iwe mtetezi wako ikija kubumburuka, fanya hivi; wafanyie mambo mazuri ambayo kila siku waonapo wawe wanakusema kwa wema wako, mfano kusaidia, ibada, kutoa nk."

NB: Vaa barakoa, kaa mbali na mkusanyiko na osha mikono kwa sabuni.
 
Kuna mmoja hapa mwanza shafi melari(Sasa kazi petrol station)jamaa no tajiri kweli Tena kweli kweli jamaa Ana roho ya kipekee Sana kwenye nyumba zake Kuna Mambo nje maji kwa wananchi bure 24 hrs.

Pale Pepsi pia walizi wake wa magodauni take ni wazee na hawafukuzi kazi na kuwapa mahali pakuishi na ukiwa na shida anakusaidia na ukatwi mshahara
 
Umefanya uungwana kukubali na kupongeza wanachofanya wengine..
Kabisa, kwa hili tuwapongeze.

Mimi ni mkristo Ila ni mnufaika mkubwa sana wa haya maji ya bure. Tena Wala hawana hata time na Mtu. Na Wala hakuna haja ya kwenda kuomba. Wewe ukifika fungua maji, Kinga alafu nenda zako
 
Wewe akili huna
Wahindi na waarabu wa Tanzania Wana mahusiano na Isis?
Au unahukumu watu Kwa rangi?
We Una ushahidi?
Hapo si ndio umeonyesha kuwa wewe huna akili?
Hujui Kuna watanzania wapo Hadi Al-Quaeda?? Au unafikiri ukiishi Tanzania huruhusiwi kwenda kujiunga nao?
 
Kunaa mmoja hapa mwanza shafi melari(Sasa kazi petrol station)jamaa no tajiri kweli Tena kweli kweli jamaa Ana roho ya kipekee Sanaa kwenye nyumba zake Kuna Mambo njeee maji kwa wananchi bure 24 hrs,pale Pepsi pia walizi wake wa magodauni take Ni wazee na hawafukuzi kazi na kuwapa mahali pakuishi na ukiwa na shida anakusaidia na ukatwi mshahara
Hivi ni vitu ambavyo tunapaswa kuvipongeza na kuviongelea Sana.

Hawa watu wanafanya Jambo kubwa Sana.

Hata nchi iwe tajiri vipi Maskini hawawezi kuisha, hivyo anayejitoa kuwasadia basi apongezwe
 
Hii ni moja katika thawabu ambazo zimeainishwa katika vitabu.

Kutoa sadaka kama maji ni nzuri na ndio msingi huo.

Unaweka kisima na bomba la maji kwa faida yako na wengine.

Ni jambo la kawaida kufanya hivyo
 
Mbona yule jamaa mwenye Yale Maji ya chupa toka chemchem iliyopo buguruni huwa anatuuzia? Nakumbuka wakati anaanza hii Biashara ya Maji miaka ya mwanzo ya 2000 alikuwa anajinadi kuwa anauza dumu tu hayo Maji ni nyongeza kwani dini yake hairuhusu kuuza maji
 
Back
Top Bottom