Pongezi kwa Serikali ya awamu ya tano kudhibiti siasa za harakati zilizokuwa zinachelewesha maendeleo

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,708
5,711
Jamani wana JF palipo na ukweli lazima usemwe.

Huko nyuma kuna mambo yaliachwa lakini hayakuwa na tija kwa umma wa watanzania.

Hasa haya mambo yalishamiri sana awamu ya nne ya Jakaya Kikwete.

Yaani miaka kumi ya utawala wa Jakaya ilikuwa ni siasa zisizo na tija kwa taifa na raia wake.

Operation Sangara, maandamano na mikutano ya siasa isiyo na tija bali kuhamasisha umma kupinga maendeleo.

Baada ya kupigwa marufuku,tumeshuhudia mambo makubwa yakifanyika hapa Tanzani. Mfano ni ujenzi wa Hospital zaidi ya 70 za wilaya ndani ya miaka minne,vituo vya afya 450+ n.k

Maoni yangu ni kuwa hii ni hatua nzuri na sasa ni wasaa serikali ya awamu ya tano kuhakikisha inawaletea maendeleo makubwa watanzania, maana hakuna tena obstacle to progress.
 
Acha unafiki shida yako unaangalia maslahi yako zaidi ya uhalisia.
 
Jamani wana Jf palipo na ukweli lazima usemwe.

Huko nyuma kuna mambo yaliachwa lakini hayakuwa na tija kwa umma wa watanzania....

First they came for the socialists, and I did not speak out—because I was not a socialist.

Then they came for the trade unionists, and I did not speak out— because I was not a trade unionist.

Then they came for the Jews, and I did not speak out—because I was not a Jew.

Then they came for me—and there was no one left to speak for me.

Martin Niemoller


 
First they came for the socialists, and I did not speak out—because I was not a socialist.

Then they came for the trade unionists, and I did not speak out— because I was not a trade unionist...
Inahusika vipi?
 
Walizoea kuishi kwa udanganyifu sasa wanaumbuka
chato chato chato kila kona kwa hiyo ni zamu yenu siyo sisi yetu macho ngoja mmalize awamu yenu. mjisifu mmesaidie kanda yenu aibu sana nyie
 
Inahusika vipi?
Siasa za harakati ni haki ya kikatiba ya kila Mtanzania. Haya mambo yamewekwa kwenye katiba, ukitaka tujadili vifungu vya katiba nitaviweka hapa.

Kwa hiyo, kimsingi kabisa, ni vibaya kushabikia watu kunyimwa haki zao za kikatiba. Unaelekea kutoka kwenye utawala wa sheria na kuleta habari za watu kuuana kwa vita bila kuheshimu sheria.

Katiba ya nchi inatoa uhuru wa siasa za harakati kama ulikuwa hujui, kama hupendi hilo, badilisha katiba.

Hilo shairi ni la mtu ambaye awali alikuwa kama wewe hajali wengine wanapominyiwa haki zao za msingi.

Chini ya utawala wa Adolf Hitler na Nazi Ujerumani, walikamatwa wasoshalisti, watu wa vyama vya wafanyakazi na Wayahudi. Huyu kasisi wa Kilutheri aliona yeye hayo hayamhusu, kwa sababu yeye si msoshalisti, si mtu wa vyama vya siasa, wala si Myahudi.

Ilipofika zamu yake kukamatwa na askari za Nazi, chama cha Hitler, anasema hakukuwapo na mtu wa kumtetea, kwa sababu wale wote ambao kawaida wangemtetea walikuwa wamekwishakamatwa.

Unapofurahia watu kunyimwa haki zao za kikatiba leo, matokeo yake ni kwamba, kesho haki zako wewe zitakapominywa, hao hao unaofurahia leo kuminywa kwa haki zao, ambao ndio wangekuwa watetezi wako, watakuwa hawapo kukutetea.
 
Nilijua tu hauta muelewa ulivyo na kichwa kibovu, siku hao unaowaimbia mapambio wakikugeukia ndio utaelewa inahusiana nini.
Wanigeukie kwa lipi? Kwani kuna mauaji ya kimbari. Kwani wewe huoni maendeleo yanayofanyika hapa Tz?
 
Well said mkuu
Siasa za harakati ni haki ya kikatiba ya kila Mtanzania. Haya mambo yamewekwa kwenye katiba, ukitaka tujadili vifungu vya katiba nitaviweka hapa.

Kwa hiyo, kimsingi kabisa, ni vibaya kushabikia watu kunyimwa haki zao za kikatiba. Unaelekea kutoka kwenye utawala wa sheria na kuleta habari za watu kuuana kwa vita bila kuheshimu sheria....
 
Ccm miaka 60 mmeshindwa kuleta maendeleo, kila siku ni hadith zile zile.

Ccm hata mkipewa miaka 300 hakuna kitu mtafanya.
 
Siasa za harakati ni haki ya kikatiba ya kila Mtanzania. Haya mambo yamewekwa kwenye katiba, ukitaka tujadili vifungu vya katiba nitaviweka hapa..
Haki za kikatiba sio kueneza propaganda mfu za kupinga maendeleo,sio kufanya siasa mpaka mnasahau shughuli za maendeleo.
 
Haki za kikatiba sio kueneza propaganda mfu za kupinga maendeleo,sio kufanya siasa mpaka mnasahau shughuli za maendeleo.
Kwanza kabisa maendeleo ni nini?

Pili, elezea kwa mfano, propaganda mfu moja ya kupinga maendeleo ni ipi tuijadili kwa kina.

Ili tuthibitishe kwamba, wewe kuongelea "propaganda mfu" ambayo hata hujaitaja kwa detail, nako si hiyo "propaganda mfu" unayoisema.

Weka mfano specific na maneno verbatim yaliyotumika tujadili hapa.

Halafu jiridhishe upande wa chama tawala nako hakuna hizo propaganda mfu unazozisema, ili tujue kwamba, usichotaka ni propaganda mfu kweli, na kuwa huna lengo la kushambulia upinzani kwa "double standard" tu.
 
Elezea kwa mfano, propaganda mfu moja ya kupinga maendeleo ni ipi tuijadili kwa kina.

Ili tuthibitishe kwamba, wewe kuongelea "propaganda mfu" ambayo hata hujaitaja kwa detail, nako si hiyo "propaganda mfu" unayoisema...
Unajitoa ufahamu? Umesahau mlivyopinga ujenzi wa bwawa la JNHP kwa kisingizo cha kulinda mazingira,huku mkijifanya kueneza uongo kuwa mazingira ya Selous game reserve ni muhimu kuliko umeme!
 
Wamepoteana,wengine wakimbizi,wengine wamesusa,wengine wameamua kuwekeza biashara za hoteli.
JPM kawavuruga mpaka wamevurugika kabisa wamepotea.
 
Back
Top Bottom