Pongezi kwa serikali kwa kuimarisha demokrasia

MPIGA ZEZE

JF-Expert Member
May 16, 2011
2,539
2,296
WanaJF nimevutiwa sana na hiki kipande kutoka katika taarifa ya Wizara ya Mambo ya nje kuhusu Sherry Party iliyofanyika Ikulu 10-2-2017.
“Mhe. Rais Magufuli ametoa shukrani hizo leo wakati wa hafla ya kuukaribisha mwaka mpya (Diplomatic Sherry Party) iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam kati yake, Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa yaliyopo nchini.

Katika hotuba yake, Mhe. Rais Magufuli alisema kuwa mwaka 2016 ambao ulikuwa mwaka wake wa kwanza tangu achaguliwe kuwa Rais wa Awamu ya Tano umekuwa wa mafanikio makubwa ambapo nchi imendelea kudumisha amani, mshikamano, umoja na Muungano umeimarika. Aidha katika mwaka huo, Serikali imeongeza jitihada za kuimarisha demokrasia, kupiga vita rushwa, ujangili na ufisadi.”


-Mwisho-

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,


Dar es Salaam, 10 Februari, 2017


VIJIMAMBO: Rais Magufuli akutana na Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa

My take:
Kazi ya diplomasia inahitaji hali ya juu sana ya unafiki! We fikiria ni balozi unayeiwakilisha nchi yako hapa Dar na umekuwepo mwaka mzima wa 2016 na kushuhudia (sio kusimuliwa) jinsi ambavyo utawala mpya umekazana kuikanyaga demokrasia (mfano kuzuia vyama vya upinzani kufanya mikutano). Mtawala huyo huyo anakukaribisha katika Sherry Party na kukuhutubia jinsi ambavyo serikali yake imefanikiwa kuimarisha demokrasia. Unapenda usipende ni lazima upige makofi!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Wazungu Siyo wajinga.Labda kuomarisha Demokrasia ni kuwafunga Wapinzani wa CCM.
 
Back
Top Bottom