PONGEZI KWA RC MAKONDA

Mlanga

JF-Expert Member
Jun 7, 2014
1,023
467
PONGEZI KWA RC MAKONDA

Siku za karibuni tumeona jinsi kiongozi wa juu wa mkoa wa

Dar es salaam, RC Makonda akiwa katika ’’ vita ya kupambana na biashara ya madawa ya kulevya’’ngazi ya Taifa.

Rais wetu JPM ameliona hili na kumpongeza RC Makonda kwa kazi hiyo na kuenda mbele zaidi kutuambia kuwa vita hii sio ya Makonda pekee bali ni ya Taifa.
Sambamba na hilo amemteuwa Kamishna Sianga kuwa Kamishna mkuu wa kitengo cha kupambana na biashara hiyo kwa kutumia vyanzo ‘’circles’’ zake nyingine kwani wahusika hawakumsaidia kupendekeza mtu wa nafasi hiyo.

Pamoja na kazi nzuri ya RC Makonda na Rais JPM ningetegemea ikiwa kweli vita hivi ni kama tunavyoaminishwa kuwa ni vya kupambana na wafanya biashara ya madawa ya kulevya’’ na sio vinginevyo

Rais angewawajibisha wafutao:

1. Waziri wa mambo ya ndani

2. Waziri wa TAMISEMI

3. IGP

4. DCI

5. DPP

6. Huyo/hao ‘’walioficha ‘’ sheria hiyo hata Waziri mkuu asijue wajibu wake naye Rais asiweze kumteuwa Kamishna hadi hiyo jana.
 
Back
Top Bottom