Pongezi kwa Rais Magufuli kusitisha Bomoa Bomoa kwa kuongeza kigezo cha "Human Face". He's so Human!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,467
113,567
Wanabodi,

Hili ni bandiko la matumizi ya kauli kuumba jambo jema kwa kutumia kitu kinachoitwa affirmation kwa kutumia the power of speech kuumba mema ya kila kinachozungumzwa na rais, hata kiwe kibaya vipi, unatumia nguvu ya kauli, kwa kuiundia wema kupitia kanuni ya affirmations kutumia affirmatives kupongeza kauli ya rais Magufuli kusimamisha bomoa bomoa ya nchi mzima, kabla bomoa bomoa yoyote haijatekelezwa, upembuzi yakinifu sasa pia utajumuisha kigezo kipya kiitwacho "a human face", lazima kitumike kwanza, ili zile nyumba zitakazo bomolewa ni zile tuu ambazo zina ulazima wa kubomolewa. (Hata kama rais alidhamiria ni Mwanza tuu, affirmations na affirmatives, zinaigeuza kauli hii kuwa ni kauli kwa nchi nzima, kauli huumba!)

Je, ni Kweli Kauli Huumba?
Wajameni ni kweli kabisa, kauli huumba, ukitoa kauli mbaya au ukitamka jambo baya, kauli ile inakuwa imeliumba hilo jambo baya na linakuja kutokea kiukweli. Ukitoa kauli njema, au ukitamka jambo jema, then kauli hiyo, inaliumba hilo jambo jema, hivyo jambo jema linakuja kutokea, hivyo kauli hii ya rais Magufuli kusitisha bomoa bomoa kwa kutumia human face, ni jambo jema, tuiumbie wema, kauli hii, ili itelelezwe kwa nchi nzima ya Tanzania.

Je, Kauli Hii ni Kwa Mwanza Tuu au Nchi Mzima
Japo kauli hii rais Magufuli ameitolea Mwanza ambako ni Usukumani, na yeye kujinasibu kuwa ni Msukuma na kusemekana kuwa ni kweli rais Magufuli ni Msukuma, hivyo kauli hiyo kuchukuliwa au kutafsiriwa wrongly na baadhi ya watu kuwa rais Magufuli ni mkabila na mbaguzi kwa kuzuia bomoa bomoa kwa Mwanza tuu kwa watu wa kabila lake tuu, mimi kwa vile naujua Usukuma wa Magufuli, napongeza uamuzi huu kwa hoja kuwa kauli hiyo ni applicable national wide and not necessarily Mwanza tuu, hivyo kwa kauli hiyo, rais Magufuli atakuwa amesitisha bomoa bomoa zote nchi nzima, hivyo naomba wasaidizi wake wajitokezeni, mlifafanue hili ili rais wetu kusitisha bomoa bomoa kama ni Mwanza tuu au nchi nzima, ili rais aeleweke vizuri na asitafsiriwe vibaya kuwa ni mkabili huku nyinyi mpo.

Je, Rais Anaweza Kulazimishwa Kufanya Jambo Lolote?
Kwa mujibu wa katiba yetu ya mwaka 1977, rais ndiye mkuu wa nchi, mkuu wa serikali na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, japo anakuwa na washauri, lakini katiba imempa rais mamlaka ya kufikia maamuzi yoyote yeye mwenyewe peke yake kwa kufanya jinsi ile anaona inafaa, bila kufuata ushauri wa mtu yoyote, ila kuna maeneo Fulani fulani, rais analazimika kufuata maelekezo ya katiba, sheria, taratibu na kanuni, na kuna maeneo rais analazimika kuchukua maamuzi Fulani fulani kutokana na trends za public opinions, hivyo kwa kutumia kanuni inayoitwa assertiveness, kwa kutumia kitu kinachoitwa precedence, tunaweza kabisa kumlazimisha rais, kutumia precedence ya kanuni hiyo ya human face katika bomoa bomoa ya Mwanza, pia itumike kusitisha bomoa boma nyingine zote zilizobakia, kwa hoja kuwa kama human face imeweza kutumika Mwanza, kwa nini isitumike maeneo mengine yote ya Tanzania nzima?.

Justification ya Pongezi
Naendelea kusisitiza kuwa kila jambo zuri linalofanywa na rais wetu, la kustahili pongezi, apongezwe, na kila baya, alaumiwe, akosolewe, ashauriwe au arekebishwe, hili la kuzuia bomoa bomoa kwa kutumia kigezo kipya cha human face, linastahili pongezi za dhati, kwa sababu linafanywa ina good faith, kwa nia njema kabisa ya kuwasaidia wananchi wake wasidhurike na bomoa bomoa zisizo na ulazima, au zinazoepukika.

Declaration of interest
Kumezuka mtindo humu jf, mtu akipongeza jambo lolote zuri linalofanywa na rais Magufuli anaambiwa anatafuta U-DC, naomba kushikilia msimamo wangu wa kuunga mkono katiba ya Warioba katika hili la ma DC kuwa ni posts za kikoloni tuu ambazo kwa sasa ni redundant ambazo ni only wastage of money and resources, saves for, kutumika ku maintain status quo ya serikali iliyopo madarakani kama mkoloni alivyowatumia ku maintain his status quo ya utawala wa kikoloni. Tanzania huru, haiwahiji ma DC, they are useless people, saves kwa kutumika kuhakikisha CCM inatawala milele.
Kauli za Rais Ni Sheria na Ombi la Raisi ni Amri.
Naomba tuanze kwa kumsikiliza kwa makini




Rais anapotoa kauli akiwa eneo fulani, katika mkutano unaotangazwa live nchi nzima, chochote anachokisema, anatuambia Watanzania wote, na maagizo yoyote anayoyatoa kwa watendaji, anayatoa kwa watendaji wa nchi nzima, tena hata akisema naomba, naomba ya rais sio ombi bali ni amri inayopaswa kufuatiwa na utekelezaji tuu. Hivyo kauli hiyo ya kutumia human face ni amri halali na sio kwa Mwanza tuu bali ni amri halali kwa nchi nzima, bomoa bomoa kutumia human face besides sheria, taratibu na kanuni.

Jee Kila Kauli ya Rais ni Amri Halali, Ni Sheria, ni Final na Conclusive?
Sio kila kauli ya rais ni sheria, au sio kila amri ya rais ni amri halali, baadhi ya kauli za rais, japo zinatekelezwa, lakini nyingine sio amri halali na nyingine sio sheria, mfano amri ya rais kupiga marufuku mikutano ya kisiasa, sio amri halali, ila kauli za rais ziwe ni sheria au amri halali, lazima kauli hizo ziwe ni amri halali, ili kauli hizo kuwa sharia au amri hizo, kuwa ni amri halali ni lazima ziendane na katiba, kauli yoyote ya rais, au amri yoyote ya rais inayokwenda kinyume cha katiba, sio amri halali, na sio sheria, lakini kufuatia heshima kwa rais wetu kama mkuu wa nchi, chochote atakachokisema, ama kukiamuru, kinatekelezwa tuu kwa heshima ya urais, regardless ni amri halali au laa. Sasa ili amri za rais ziwe halali, nimelieleza hapa, na pia kuna amri za rais zinaweza kupigwa chini na mahakama
AG, Mshauri Mh.Rais Atoe Maagizo kwa Presidential Decrees Kuyapa ...
Je, wajua amri za Rais sio final and conclusive?. Zinaweza kupingwa ...

Je, Magufuli ni Mkabila na Mbaguzi?
Kauli hii imetafsiriwa kama ni kauli ya kibaguzi wa kikabila kwa vile tuu imetolewa Mwanza. Hili la tuhuma za upendeleo wa Ukabila rais Magufuliwa kutuhumiwa kuwapendelea Wasukuma zimewahi kutolewa sana humu jf, kufuatia Wasukuma wachache wenye sifa kuteuliwa na rais kushika nafasi mbalimbali za uteuzi, au tuhuma kuwa rais Magufuli, anawachukia watu wa kabila fulani ambao zamani walizoea upendeleo wa ziada, kukapelekea rais Magufuli kuonekana ni mbaguzi, hili la tuhuma za ubaguzi, nimeishawahi kulizungumza hapa.
Tuhuma Za Ukabila: Wasukuma Sii Miongoni Mwa Makabila Yenye ...
Wito Kwa Bunge Letu Tukufu: Mkithibisha Hii Nepotism ya Ajabu na ...

Je, Kauli za Rais ni Territorial or National Wide?
Kuna kauli za rais ziko directed kwenye sehemu moja au eneo fulani specific lakini zikitolewa kupitia matangazo ya moja kwa moja ya redio na TV, kauli hizo zinakuwa ni kwa taifa zima na sio kwa lile eneo husika pekee unless wasaidizi wa rais waje watufafanulie kuwa rais alikuwa akimaanisha hiyo human face itumike Mwanza tuu kwa Wasukuma, lakini kwenye maeneo mingine yote, bomoa bomoa ieendelee tuu kama kawaida bila kutumia human face.

Hili liliwahi kufanyika wakati rais alipotoa kauli ya kufyatua watoto, atasomesha bure, ilitafsiriwa ni kwa Watanzania wote, hadi Waziri Ummy Mwalimu alipojitokeza na kufafanua kuwa kauli ile ilikuwa directional kwa watani zake Wazaramo tuu. Hivyo tunaichukulia kauli hii ni kwa Watanzania wote unless kama it was meant kwa Wasukuma tuu, tuelezwe.
Rais Magufuli: Fyatueni watoto wa kutosha, nitawasomesha bureee ...
Rais Kusitisha Uzazi wa Mpango Kwa"Fyatueni Watoto wa Kutosha",Ni ...
Waziri Ummy: Kauli ya Rais "Kufyatua watoto" ilikuwa ni utani ..

Nini Hatma ya Waliobomolewa Kabla Kigezo cha Human Face Hakijaanza Kutumika?
Hatuwezi kuacha kupongeza mazuri, kwa sababu tuu kuna mabaya yaishafanyika huko nyuma, kwa wale wote ambao wameisha bomolewa kabla ya kigezo hiki kipya cha human face hakijaanza kutumika, hakuna jinsi nyingine yoyote ya kuwasaidia, bali ni kuwapa pole tuu, haya ni maji yameishamwagika, hayazoleki, poleni sana,ila itafidiwa na karma, lakini kwa bomoa bomoa nyingine zote, sasa human face pia itatumika!.

Je, Hii Human Face Lengo Lake ni Kuzuia Bomoa Bomoa?
Hapana, hii human face haizuii bomoa bomoa, hivyo wale ambao mmeishabomolewa, msiingie chuki kwa kudhani hiyo human face ni kuzuia kabisa bomoa bomoa hadi kudhania kama ingeanza zamani, wote mngesalimika, hapana, human face ni kutumia tuu kitu kinachoitwa utu, kabla ya bomoa bomoa, ikikutikana watu wamejenga hifadhi ya barabara, au eneo lililotengwa kwa taasisi nyingine, then utu unatumika kutowabomolea kama barabara haijaanza kujengwa, au taasisi hiyo haina matumizi ya eneo lote hilo, hivyo wakazi hao, wananusurika kwa mipaka kurekebishwa, hivyo ndivyo ilivyofanyika kwa eneo la Jeshi, pale Mwenge, Mlalakuwa na Kawe Ukwamani, au maeneo kibao ya RTD, lakini kama eneo hilo barabara itapita, hiyo nyumba lazima tuu zitabomolewa, hiyo human face haiwezi kusaidia, labda kuwalipa kifuta machozi na kuwapatia maeneo mengine.

Wasaidizi wa Rais, Msaidiani Rais Wetu Kwa Kutafsiri Kauli Zake
Kufuatiwa lugha ya Kiswahili sio lugha yake ya kwanza, kuna mara kadhaa rais Magufuli huwa anajikwaa ulimi na kutoa kauli tata, hivyo wasaidizi wa rais wana jukumu na wajibu wa kumsaidia kuzifafanua baadhi ya kauli tata za rais ili zieleweke vizuri kwa Watanzania kuwa alimaanisha nini, kama nilivyo shauri hapa. Wasaidizi wa Rais, Please Msaidieni Rais Wetu Kwenye Public ...
Naamini Rais Magufuli ana washauri wazuri na anashauriwa vizuri ...

Kauli za Rais Zisitafsiriwe Literally Bali The Motive Behind.
Sio kila rais anachosema kutafsiriwe direct or literally bali baadhi ya kauli hizo, ziangaliwe kwa dhana ya rais alidhamiria kusema nini na sio kuangalia tuu rais ametamka nini, sometimes ni tatizo la matamshi, sometimes ni kuteleza tuu ulimi kama ile ya Saadam, hivyo kuangalia kauli hizi zimedhamiria nini. Mfano aliposema wasibomolewe kwa sababu wamenipa urais, hapa naamini ni kuteleza tuu ulimi, rais akiishatangazwa kuwa ndie ameshinda uchaguzi, then anakuwa amechaguliwa na wote waliomchagua, wote wasio mchagua, wote kura zao zilizoharibika, hata wale ambao hawakupiga kura, hivyo ni rais wa wote, ndie rais wa CCM, ndie rais wa Chadema, ndie rais wa CUF, ndie rais wa Watanzania wote, waliomchagua na wasiomchagua, hivyo huu upendeleo wa wazi wa kabila lake, au waliomchagua, au chuki ya wazi kwa kabila fulani, ni human weaknesses na human mistakes. tutumie affirmatives kulirekebisha hili, Magufuli nae ni binadamu tuu kama sisi na sio malaika, hivyo kuteleza ulimi, kukosea, au kutoa kauli tata sio jambo la ajabu!.

Hitimisho
Watanzania wazalendo wenzangu, tuungane nami katika matumizi ya kauli kuumba jambo jema kwa kutumia kitu kinachoitwa affirmation kwa kutumia the power of speech kuumba mema ya kila kinachozungumzwa na rais wetu, hata kiwe kibaya vipi, tutumie nguvu ya kaul zetu kukigeuza kuwa ni kitu kizuri, ni jambo jema kupitia kanuni ya affirmations kutumia affirmatives, hivyo kujenga Tanzania njema

Paskali
 
hahahaha

Mkuu hiyo inaitwa falacy of generalization..

Naona umewarahisishia watu kazi sasa
ila nilitarajia barua kama hiyo iwe imetoka mapema sana jana baada ya kauli ile "kutafsiriwa vibaya" hata hivyo bomo bomoa ilisha sitishwa kwa mkoa wa Dar na RC Makonda...

Lukuvi peke yake ndie sijawahi muelewa
 
Mkuu Pascal umemuelewa mh Rais? Niseme tu, ni vigumu kujiondoa akili. Kama ulizaliwa na akili, ukijikana na kutetea uwongo utaonekana waazi kabisa. Mwangalie J. Muro na Mpendazoe.Na wewe unataka kufafanua anayosema mh? Hutaweza bro! Tumeshamuelewa. Sisi ambao tulimpigia kura tunatamba kama Dogo aslay. Ole kwenu nyie mliojifanya vidume
 
Katamka wazi kuwa hawa Wa Mwanza ndio wamenipa kura kunipa Urais. Usimlishe maneno, Paskali we we ndio unamtungia uongo rais. Kimara kwani walimpa kura mpaka azuie wasibomolewe? Mahakama yenyewe imeshindwa kuzuia wasibomolewe kwa nini? Kuchagua diwani na mbunge nje ya ccm. Kasema hayo kwa maana ya kauli yake.
Kwa nini kila akisema ya moyoni mna usingizia ulimi kuteleza? Kwani yeye anakunywa oil kiasi kuwa mdomoni kumekuwa kunateleza?
 
Mkuu
Alisema wale ndio waliompa urais

Kigezo kikubwa nasababu kwake kutowabolea

DSM hususani kwa Mnyika nk hawakumchaguwa yeye ndo maana wamekiona chamtema kuni

Bomoabomoa zilizotangulia zilikuwa wahususi kuwatia adabu wapinzani

Kama ilivyo kwa teuzi za madc na marc watuhumiwa wa vyeti feki na wanunuwa madiwani kwa rushwa na hata wapayukaji kwapamoja wanapewa ulaji ilikuwatia adabu CHADEMA na wafuasi wengine wa upinzani wanaotuhum na kuorodhesha wenyesifa za hovyo...kwenye habari, dsm, Arumeru nk

Nidhahili kabisa, tena mubashara ubaguzi umafanyika wa aina tatu

1. Kisiasa......uteuzi wa wasiosifa na kibali cha kuendesha siasa kwa ccm pekee....wengina niharamu kufanya siasa

2. Kikanda......tumetembelea zaidi ya mara nne kanda moja na kuunemesha kule kwetu.....wakwetu wote wako juu ya sheria nakatiba.

3. Kikabila.... Maamuzi yakusaidia wakwetu, uteuzi wa wakwetu kwa % kubwa.....nk

Waleikumsalaam
?.................?...,,,,........?.............?..........?......!
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la kupongeza kauli ya rais Magufuli kusimamisha bomoa bomoa ya nchi mzima, kabla bomoa bomoa yoyote haijatekelezwa, upembuzi yakinifu kwa kutumia kigezo kipya kiitwacho a human face, lazima kitumike kwanza, ili zile nyumba zitakazo bomolewa ni zile tuu ambazo zina ulazima wa kubomolewa, japo kauli hii ameitolea Mwanza ambako ni Usukumani, na yeye kujinasibu ni Msukuma na kusemekana ni Msukuma, hivyo kauli hiyo kuchukuliwa au kutafsiriwa wrongly kuwa rais Magufuli ni mkabila na mbaguzi kwa kuzuia bomoa bomoa kwa kabila lake tuu, mimi napongeza uamuzi huu kwa hoja kuwa kauli hiyo ni applicable national wide and not necessarily Mwanza tuu, hivyo kwa kauli hiyo, rais Magufuli atakuwa amesitisha bomoa bomoa zote nchi nzima, hivyo naomba wasaidizi wake wa jitokezeni, mlifafanue hili ili rais watu aeleweke asitafsiriwe vibaya huku nyinyi mpo.

Declaration of interest. Kumezuka mtindo humu jf, mtu akipongeza jambo lolote zuri linalofanywa na rais Magufuli anaambiwa anatafuta U-DC, naomba kushikilia msimamo wangu wa kuunga mkono katiba ya Warioba katika hili la ma DC kuwa ni posts za kikoloni tuu ambazo kwa sasa ni redundant ambazo wastage of money and resources tuu saves kutumika ku maintain status quo ya serikali iliyopo madarakani kama mkoloni alivyowatumia ku maintain his status quo.

Kauli za Rais Ni Sheria na Ombi la Raisi ni Amri.
Naomba tuanze kwa kumsikiliza kwa makini


Rais anapotoa kauli akiwa eneo fulani, katika mkutano unaotangazwa live nchi nzima, chochote anachokisema, anatuambia Watanzania wote, na maagizo yoyote anayoyatoa kwa watendaji, anayatoa kwa watendaji wa nchi nzima, tena hata akisema naomba, naomba ya rais sio ombi bali ni amri inayopaswa kufuatiwa na utekelezaji tuu. Hivyo amri hiyo sio kwa Mwanza tuu bali ni amri halali kwa nchi nzima, bomoa bomoa kutumia human face besides sheria, taratibu na kanuni.

Jee Magufuli ni Mkabila na Mbaguzi?.
Kauli hii imetafsiriwa kama ni kauli ya kibaguzi wa kikabila kwa vile tuu imetolewa Mwanza. Hili la Ukabila wa Wasukuma nimeishawahi kulizungumza hapa.

Jee Kauli za Rais ni Territorial or National Wide?.
Kuna kauli za rais ziko directed kwenye sehemu moja au eneo fulani specific lakini zikitolewa kupitia matangazo ya moja kwa moja ya radio na TV, kauli hizo zinakuwa ni kwa taifa zima na sio kwa lile eneo husika pekee unless wasaidizi wa rais waje watufafanulie kuwa rais alikuwa akimaanisha hiyo human face itumike Mwanza tuu kwa Wasukuma, lakini kwenye maeneo mingine yote, bomoa bomoa ieendelee tuu bila human face.

Hili liliwahi kufanyika wakati rais alipotoa kauli ya kufyatua watoto, atasomesha bure, ilitafsiriwa ni kwa Watanzania wote, hadi Waziri Ummy Mwalimu alipojitokeza na kufafanua kuwa kauli ile ilikuwa directional kwa watani zake Wazaramo tuu. Hivyo tunaichukulia kauli hii ni kwa Watanzania wote unless kama it was meant kwa Wasukuma tuu, tuelezwe.

Kauli za Rais Zitafsiriwe.
Kufuatiwa lugha ya Kiswahili sio lugha yake ya kwanza, kuna mara kadhaa rais Magufuli huwa anajikwaa ulimi na kutoa kauli tata, hivyo wasaidizi
wa rais wana wajibu wa kumsaidia kuzifafanua kauli hizo zieleweke vizuri kwa Watanzania kama nilivyo shauri hapa.

Kauli za Rais Zisitafsiriwe Literally Bali The Motive Behind.
Sio kila rais anachosema kutafsiriwe direct or literally bali ziangaliwe zimedhamiria nini.

Paskali

MAGUFULI ni mkabila, mdini na mbaguzi asiyejua hata atamke nini mbele ya nani! Watu wanalala nje huko kimara na mbezi yeye anakuja kujua human face leo? Angejua watanzania wanavyomchukia huyu mtu angeacha kuongoza akafanya mambo mengine... jana alisikika akidai at watu wanapenda kumsikiliza hata mpaka asubuhi khaaà!yan kuliko kumsikiliza yy bora usikilize commed
 
Back
Top Bottom