Pongezi kwa ndugu Adama Barow kuchaguliwa kuwa rais wa Gambia


ACT Wazalendo

ACT Wazalendo

Verified Member
Joined
May 5, 2014
Messages
365
Likes
494
Points
80
Age
4
ACT Wazalendo

ACT Wazalendo

Verified Member
Joined May 5, 2014
365 494 80
TAARIFA KWA UMMA.

Chama Cha ACT Wazalendo kinatoa pongezi za dhati kwa Ndugu Adama Barrow kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Gambia katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliofanyika tarehe 01/12/2016.

Katika uchaguzi huo Ndugu Barrow anayetokana na Chama cha UDP (United Democratic Party) lakini katika uchaguzi huu aligombea akiungwa mkono na vyama vingine sita vya upinzani alishinda kwa kura 263,515 dhidi ya kura 212,099 za Ndugu Yahya Jammeh wa Chama Cha APRC (Alliance For Patriotic Reorientation and Construction) ambaye alikuwa ni Rais wa Gambia aliyeiongoza nchi hiyo kwa miaka 22 tangu mwaka 1994 alipongia madarakani kwa njia ya mapinduzi.

Ushindi wa Ndugu Barrow si ushindi wake na watu wa Gambia pekee bali ni ushindi wa kila mwanademokrasia na mpenda mabadiliko ya kweli popote pale alipo.

Pia kwa namna ya pekee ACT Wazalendo inampongeza Ndugu Yahya Jammeh kwa kukubali kushindwa uchaguzi huo na kumpigia simu mshindi na kumpongeza. Kitendo hiki ni darasa tosha kwa viongozi wengine wa Afrika ambao wamekuwa wakishindwa kuheshimu matokeo ya uchaguzi. Ndugu Jammeh angeweza kukataa matokeo hayo na kutumia vyombo vya dola vilivyo chini yake kuendelea kutawala.

Ni vyema viongozi wengine wa Afrika kujifunza kwa tendo hili la kiungwana kabisa lililofanywa na Ndugu Jammeh kwa kuheshimu matakwa ya Wananchi wa Gambia japo aliwahi kutangaza kuitawala nchi hiyo kwa miaka bilioni.

John Patrick Mbozu.
Katibu wa Kamati ya Mambo ya Nje, ACT Wazalendo.
04/12/2016.
 

Forum statistics

Threads 1,275,100
Members 490,908
Posts 30,532,670