Pongezi kwa mlioandaa Kongamano Maalum katika kumbukizi ya mwaka mmoja tangu Hayati Benjamin Mkapa afariki dunia

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,542
108,858
Jumatano ijayo tarehe 14 katika Siku ya Kumbukizi ya mwaka Mmoja wa Kifo cha Rais wangu bora wa Pili Tanzania Benjamin Mkapa kutakuwa na Kongamano la Kujadili yale mema yote ambayo Hayati Mkapa ameifanyia Tanzania yetu hii.

Kongamano hilo litafanyika katika Ukumbi wa Mlimani City na Mgeni rasmi atakuwa ni Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na japo utarushwa hewani na vyombo mbalimbali vya Habari nchini lakini pia utahudhuriwa na Viongozi wengine wengi Wastaafu na Wageni wa Kimataifa ambao walimwelewa vyema 'Lupaso Genius' Hayati Rais Mkapa.

Naomba GENTAMYCINE niwe wa kwanza kuwapongeza kaandaaji wa hili Tukio zuri na kubwa la Kongamano la Kumbukizi ya mwaka Mmoja ya Kifo cha Rais Benjamin William Mkapa kwani Kwangu Mimi ukimuondoa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere Rais mwingine Bora alikuwa ni Hayati Mkapa na mwingine aliyekuwa akifuatia Nyendo zao kwa ukaribu ni Hayati Rais Dkt. Magufuli kutokana na aina ya Uongozi wao makini, madhubuti na ulioiletea Heshima sana Tanzania.

RIP Nyerere, Mkapa na Dkt. Magufuli.
 
Back
Top Bottom