Pongezi Kwa Mh Rais Jakaya Mrisho Kikwete

Mtaalam

JF-Expert Member
Oct 1, 2007
1,371
237
katika pita pita yangu katika blog mbali za watanzania nimekutana na barua hii ya mdau mmojawapo aliyeko india akimpongeza raisi wake..

sasa ninachojiulizaga mie ni watu huwa vipofu wa kufikiri ama viziwi wa kutafakari???ama ukiwa mwana ccm basi hata kufeel ukweli na uchungu juu ya nchi yetu haupo tena??

kweli mtu ambaye ana uchungu wa nchi yetu Tz anaweza dhubutu sifia hilo wakati tukikaa na kutafakari lipi jema serikali hii ililofanya kwa Tz tutabakia kuhesabu moja if not mawili tuu?
 
hii niliikuta kwa Haki Ngowi

PONGEZI KWA MH RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki -Moon(kushoto) akimpongeza Rais
wa Tanzania Jakaya Kikwete kwa kuteuliwa kwake juzi kuwa Mwenyekiti mpya wa africa Union walipokutana kwenye Mkutano huo wa 1oth uliyofanyika Addis Abba,Ethiopia.


Napenda kuchukua nafasi hii kumpongeza rais wetu Mh Kikwete kuchaguliwa kwake na umoja wa Afrika kuwa mwenyeketi kwa kipindi cha mwaka mmoja,mh rais nakupongeza sana na ninakutakia kila la kheri katika kazi hii nyeti .pili nakupongeza kwa hotuba yako nzuri ya mwisho wa mwezi wa kwanza(january) mh ,hotuba yako ni ndefu na nzuri sana na ziara yako ya mkoa wa kageraNikianza na hili la umoja wa afrika ,hili litasaidia katika kuitangaza nchi yetu ya Tanzania kisiasa ,kiuchumi na kijamii,kwani naamini kabisa katika safari zote za kikazi mh rais atakuwa akitumia kofia zote mbili katika kuitangaza afrika na Tanzania kiujumla.Afrika imefika mahali ambapo inahitaji kuwa na misingi mizuri ambayo itasaidia nchi zake kujikwamua kiuchumi,kisiasana kijamii ,misingi hiyo ndio imesaidia jumuiya kama za asia(India,Srilanka,maldives,pakistan),asia ya kati kama Thailand,Singapore,Malyasia,Indonesaia nk ,jumuiya hizi zimefikia mahali ambapo nchi za kibepari zimekuwa hazi lali usingizi kutokana na maendeleo yake yanayopatikana kila kukicha.Leo, London stock exchange inajiuliza what happen at Mumbai stock exchange to day?,zamani ikiitwa Bombay,(India) shangai,hongkong,tunahitaji nasi tufike mahali wajiuleze what happen at D'salaam,Cairo,Lagos,Johanesburg, ?na nk,tukiweza kufika hapo basi yale yote wanayofikiri kuhusu Afrika yatakuwa yakiwasuta wao wenyewe kama yanavyowasuta yale yanayotokea Mumbai,Hongkong,,Bangkok na nkPili nakupongeza Mh rais ktk hotuba yako ya mwisho wa mwezi wa kwanza(january),ktk hotuba yako jambo la mwisho ndilo ambalo naamini limewavutia wengi na mimi binafsi,kuhusu maadili ya viongozi na uongozi ,hili ni jambo kubwa sana katika kuhakikisha nchi inasonga mbele, ni lazima wala si hiari kwa wale wote wanaopenda kutumikia uma wa nchi zao kuachana na biashara ya aina yeyote kama wanazo ,hili litasaidia kupunguza rushwa ,umimi,usisi,uwao katika maslahi ya Taifa.Mh rais naamini hii ni ishara kwamba what next after that………………….,na kwa kuwa limejadiliwa na kamati kuu ya CCM,litafika serikalini muda si mrefu na kupelekwa bungeni kama muswada,ili lipitishwe kuwa sheria,mh rais nakuombea kwa mwenyezi mungu maisha marefu,afya njema ili uweze kulisimamia hili kwa uadilifu,nchi kama India zaidi ya hili haihitaji raisi,waziri mkuu,mbunge,waziri kiongozi,katibu mkuu na nk kuwa na nyadhifa mbili zaidi ya ile moja aliyokuwa nayo(hili lipo katika katiba yao)tunafaham katiba ya India ndio kubwa kuliko zote duniani,nchi za kibepari katiba zao zinaingia kwa India ..kama ifuatavyo….marekani mara saba,France mara tano,Australia mara sita na nk
Katika hili la maadili ya viongozi na uongozi, ndio linalotokea leo hii kwa mfanyabiashara maarufu na mmliki wa manchester city ya uingereza(football club) Dr Thaksin shinawatra alipokuwa waziri mkuu wa Thailand siku za nyuma ,leo hii ana kesi ya kuhusiana na rushwa alipokuwa waziri mkuu,japo alikuwa ni mfanyabiashara hata kabla hajawa waziri mkuu wa Thailand.

Nampongeza Mh raisi pia katika ziara yake ile ya mkoa ule wa kagera ,pale alipozungumza na wananchi wa muleba/Biharamuro na kusisitiza katika suala lile la ujambazi ,kwa kuwataka wanaowafaham majambazi hayo wayataje ,ama yajisalimishe yenyewe,ni kweli wananchi wanawafaham,kwani ni wajomba,mtoto wa kaka,dada,binamu,nakuunga mkono 100% kuweka mikakati mipya ambayo itasidia kulikomesha hili,ambalo limekuwa sugu sana kwa sasa,wenzetu wanasheria inayosema "shoot order to kill" hii ikiwa na maana ukihisiwa tu kuwa wewe ni jambazi basi unauwawa.Hakuna mahakamani wala gerezani nchi kama Brazil,Nigeria,Amerika ,Afrika ya kusini hili linafanyika na nchi nyingine nyingi tu duniani , hata jirani zetu Kenya ilikuwepo wakati wa utawala wa Moi miaka fulani fulani, sijui kama bado iko au la...,lakini mm nasema iliwasaidia jirani zetu naamini kwa Tanzania tunahitaji mbadala wa hili ,ambalo litawezesha kumaliza suala la ujambazi nchini.Napenda kumtakia Mh Rais Jakaya Mrisho Kikwete afya njema,maisha marefu na vilevile naitaki a nchi yangu ya Jamuhuri ya muungano waTanzaia amani na upendo na afrika kwa ujumla.Ni mtanzaia mwenzenu Baraka Abdallah kange,Bangalore,India.nikiwanafanya shahada ya kwanza ya uongozi wa biashara na fedha.
 
naombeni mnisaidie ndugu zangu labda ni mie tuu nina feel in a negative way abt this..na mnipe ushauri as mie maana....nakereka kweli kweli na mambo haya...na nimesikia amepokelewa kwa maandamano aliporudi TZ
 
inasemaje hiyo ibara ba ndugu maana wengine tumepigwa kikumbo na sheria zetu wenyewe


Inasema hivi

18.Kila mtu

a)anao uhuru wa kuwa na maoni na kueleza fikra zake
b)anayo haki ya kutafuta, kupokeana kutoa habari bila ya kujali mipaka ya Nchi
c)anao uhuru wa kufanya mawasilianona haki ya kuto ingiliwa katika mawasiliano yake na
d)anayo haki ya kupewa taarifa wakati wowote kuhusu matukio mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na pia kuhusu masuala muhimu kwa jamii.
 
http://issamichuzi.blogspot.com/2008/02/pongezi-toka-india.html#comments

PONGEZI KWA MH RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE


Napenda kuchukua nafasi hii kumpongeza rais wetu Mh Kikwete kuchaguliwa kwake na umoja wa Afrika kuwa mwenyeketi kwa kipindi cha mwaka mmoja,mh rais nakupongeza sana na ninakutakia kila la kheri katika kazi hii nyeti .pili nakupongeza kwa hotuba yako nzuri ya mwisho wa mwezi wa kwanza(january) mh ,hotuba yako ni ndefu na nzuri sana na ziara yako ya mkoa wa kagera.
Nikianza na hili la umoja wa afrika ,hili litasaidia katika kuitangaza nchi yetu ya Tanzania kisiasa ,kiuchumi na kijamii,kwani naamini kabisa katika safari zote za kikazi mh rais atakuwa akitumia kofia zote mbili katika kuitangaza afrika na Tanzania kiujumla. Afrika imefika mahali ambapo inahitaji kuwa na misingi mizuri ambayo itasaidia nchi zake kujikwamua kiuchumi,kisiasana kijamii ,misingi hiyo ndio imesaidia jumuiya kama za asia(India,Srilanka,maldives,pakistan),asia ya kati kama Thailand,Singapore,Malyasia,Indonesaia nk ,jumuiya hizi zimefikia mahali ambapo nchi za kibepari zimekuwa hazi lali usingizi kutokana na maendeleo yake yanayopatikana kila kukicha,
Leo, London stock exchange inajiuliza what happen at Mumbai stock exchange to day?,zamani ikiitwa Bombay,(India) shangai,hongkong,tunahitaji nasi tufike mahali wajiuleze what happen at D’salaam,Cairo,Lagos,Johanesburg, ?na nk,tukiweza kufika hapo basi yale yote wanayofikiri kuhusu Afrika yatakuwa yakiwasuta wao wenyewe kama yanavyowasuta yale yanayotokea Mumbai,Hongkong,,Bangkok na nk
Pili nakupongeza Mh rais ktk hotuba yako ya mwisho wa mwezi wa kwanza(january),ktk hotuba yako jambo la mwisho ndilo ambalo naamini limewavutia wengi na mimi binafsi,kuhusu maadili ya viongozi na uongozi ,hili ni jambo kubwa sana katika kuhakikisha nchi inasonga mbele, ni lazima ;wala si hiari kwa wale wote wanaopenda kutumikia uma wa nchi zao kuachana na biashara ya aina yeyote kama wanazo ,hili litasaidia kupunguza rushwa ,umimi,usisi,uwao katika maslahi ya Taifa,Mh rais naamini hii ni ishara kwamba what next after that………………….,na kwa kuwa limejadiliwa na kamati kuu ya CCM,litafika serikalini muda si mrefu na kupelekwa bungeni kama muswada,ili lipitishwe kuwa sheria,mh rais nakuombea kwa mwenyezi mungu maisha marefu,afya njema ili uweze kulisimamia hili kwa uadilifu,nchi kama India zaidi ya hili haihitaji raisi,waziri mkuu,mbunge,waziri kiongozi,katibu mkuu na nk kuwa na nyadhifa mbili zaidi ya ile moja aliyokuwa nayo(hili lipo katika katiba yao)tunafaham katiba ya India ndio kubwa kuliko zote duniani,nchi za kibepari katiba zao zinaingia kwa India ..,kama ifuatavyo….marekani mara saba,France mara tano,Australia mara sita na nk
Katika hili la maadili ya viongozi na uongozi, ndio linalotokea leo hii kwa mfanyabiashara maarufu na mmliki wa manchester city ya uingereza(football club) Dr Thaksin shinawatra alipokuwa waziri mkuu wa Thailand siku za nyuma ,leo hii ana kesi ya kuhusiana na rushwa alipokuwa waziri mkuu,japo alikuwa ni mfanyabiashara hata kabla hajawa waziri mkuu wa Thailand.

Nampongeza Mh raisi pia katika ziara yake ile ya mkoa ule wa kagera ,pale alipozungumza na wananchi wa muleba/Biharamuro na kusisitiza katika suala lile la ujambazi ,kwa kuwataka wanaowafaham majambazi hayo wayataje ,ama yajisalimishe yenyewe,ni kweli wananchi wanawafaham,kwani ni wajomba,mtoto wa kaka,dada,binamu,nakuunga mkono 100% kuweka mikakati mipya ambayo itasidia kulikomesha hili,ambalo limekuwa sugu sana kwa sasa,wenzetu wanasheria inayosema “shoot order to kill” hii ikiwa na maana ukihisiwa tu kuwa wewe ni jambazi basi unauwawa,hakuna mahakamani wala gerezani nchi kama Brazil,Nigeria,Amerika ,Afrika ya kusini hili linafanyika na nchi nyingine nyingi tu duniani , hata jirani zetu Kenya ilikuwepo wakati wa utawala wa Moi miaka fulani fulani, sijui kama bado iko au la...,lakini mm nasema iliwasaidia jirani zetu naamini kwa Tanzania tunahitaji mbadala wa hili ,ambalo litawezesha kumaliza suala la ujambazi nchini.
Napenda kumtakia Mh Rais Jakaya Mrisho Kikwete afya njema,maisha marefu na vilevile naitaki a nchi yangu ya Jamuhuri ya muungano waTanzaia amani na upendo na afrika kwa ujumla.
 
Nani alisema kuwa Kikwete hasifiwi hapa JF?

Hii thread na jina la muanzisha hii thread ni uthibitisho kuwa kuna wanaomsifia JK hapa.
 
Mwanzisha mada- hilo jina lako limekaa kimatusi- sii la heshima!

Huwezi kutumia jina kama hilo kumsifu Raisi wa nchi!
 
Kumbuka pia kuwa hii mada ilishaanzishwa hapa


Uthibitisho kuwa Kikwete amesifiwa tayari ingawa muanzisha mada ameamua kuileta tena na tena
 
Ndiyo. Siyo mimi nileyandika hiyo barua bali ni Mtanzania mwenzetu Ndugu BARAKA ABDALLAH KANGE anayesoma huko Bangalore, India. Hakika bamdogo Baraka ameonyesha uzalendo, mapendo, heshima na unyenyekevu kwa rais wetu, kitu amabacho kinafaa kuigwa. Rais wetu anafaa kuungwa mkono kwa makubwa na madogo yote anayofanya kwa manufaa ya taifa, siyo kushutumiwa na kukejeliwa!
 
Ndiyo. Siyo mimi nileyandika hiyo barua bali ni Mtanzania mwenzetu Ndugu BARAKA ABDALLAH KANGE anayesoma huko Bangalore, India. Hakika bamdogo Baraka ameonyesha uzalendo, mapendo, heshima na unyenyekevu kwa rais wetu, kitu amabacho kinafaa kuigwa. Rais wetu anafaa kuungwa mkono kwa makubwa na madogo yote anayofanya kwa manufaa ya taifa, siyo kushutumiwa na kukejeliwa!

Mhhh...

Naona karibuni Kikwete ataitwa Mfalme Kikwete ambaye atataka watu wote wainamishe vichwa vyao kila anapopita ili kuonyesha unyenyekevu, mapendo......... what a crap!
 
Ndiyo. Siyo mimi nileyandika hiyo barua bali ni Mtanzania mwenzetu Ndugu BARAKA ABDALLAH KANGE anayesoma huko Bangalore, India. Hakika bamdogo Baraka ameonyesha uzalendo, mapendo, heshima na unyenyekevu kwa rais wetu, kitu amabacho kinafaa kuigwa. Rais wetu anafaa kuungwa mkono kwa makubwa na madogo yote anayofanya kwa manufaa ya taifa, siyo kushutumiwa na kukejeliwa!

Admin na mods
inabidi kuangalia tena maadili ya forum kama yanafuatwa. Nadhani hilo jina kwenye quote ni extreme na linashusha heshima hapa.

Maoni yangu abadili au apigwe stop! Period
 
Admin na mods
inabidi kuangalia tena maadili ya forum kama yanafuatwa. Nadhani hilo jina kwenye quote ni extreme na linashusha heshima hapa.

Maoni yangu abadili au apigwe stop! Period

Naunga mkono hoja Mods pls taratibu na kanuni zetu zinasemaje kuhusu matumizi ya majina ya aina hii.

Tunaomba muongozo wa Invisible pls....
 
Back
Top Bottom