Pongezi kwa mahakama za Tanzania mnatenda haki, na haki imeonekana kutendeka pale Kisutu

Masinki

JF-Expert Member
Dec 18, 2014
694
451
Penye ukweli watanzania lazima tuseme.
Pongezi nyingi Sana kwa Mahakama za Tanzania na watumishi wake haswa Mahakimu,waendesha mashtaka,karani na wengineo.Hakika mnastahili kuwa hapo.

Pongezi kubwa zaidi na za kipekee ziende kwa Jaji Mkuu wa Tanzania unafanya kazi kubwa sana,sote tunajua kazi ya kuwapatia wananchi Haki huwa ni ngumu na inahitaji weledi wa kutosha.

Kesi ya Viongozi wa upinzani licha ya kuchukua muda mrefu lakini ilitolewa hukumu inayostahiki Tena yenye huruma kubwa ndani yake ya kifungo Cha muda mfupi Sana ama faini ambayo pia kwa mtu mmoja na makosa waliyotenda Ni ndogo.

Hakimu aliyesimamia kesi ile ya kihistoria anastahili nishani ama kupandishwa Cheo alitafasiri sheria vizuri akatumia na Hekima na Busara za ki Hakimu kuhukumu,vingenevyo Leo hii tungekuwa tunaongea mengine.

Mhimili wa makahama siku zote hapa Nchini Ni Huru na unajitegemea haungiliwi na Mtu yeyote ama kupokea maagizo yoyote kutoka mhimili Mwingine.

Kinachofurahisha Ni Mahakama kujitanua kwa kujenga Mahakama za Kanda ambazo Zina majaji kwa mikoa mingi mfano Pale Musoma,Mara nilipita juzi nikitokea zangu Kahama nilishangazwa na jitihada zinaendelea kwa hayo tunawapongeza msife moyo Bali endeleeni kutoa haki kwa watanzania na msikubaliane na propaganda Uchwara za wanasheria ama wanasiasa wasiotakia Mema Nchi yetu.

Wakati nikitaka kuhitimisha nawakumbuka makarani nasema wengi wao Ni wazalendo pigeni kazi Tupo kwa ajili yenu, lakini nitakuwa mchoyo wa Fadhili nisipo washukuru mihimili mingine inayosababisha Mahakama sheria zinasimamiwa ipasavyo nayo Ni Bunge wao hutunga sheria pongezi Sana kwao, Serikali ya awamu ya Tano chini ya Jemedari Dr John Pombe Magufuli nyie vizazi na vizazi vitawakumbuka endeleeni kuwalipa vizuri mishahara watumishi wote wa Mahakama.

Nahitimisha kwa kusema Kama Shughuli za Mahakama zingekuwa zinaingiliwa na mhimili Mwingine basi Mbowe angehukumiwa kifungo Cha mbwa mwizi, Naipenda Tanzania.
Masinki -Nipo Katavi kwa Sasa.
 
Ulikwishawahi kusikia watu wengine wanasemaje juu yako? Kuna magonjwa mengine, siyo rahisi wewe mhusika kujua kuwa unaumwa.

Lakini ujue kuwa walio wazimu wote, Watanzania na wasio watanzania, wote wamesema kesi yenyewe ilikuwa ya hovyo, na hukumu ikawa ya hovyo zaidi.
 
Hakimu kajitahidi sana kubalance mambo. Hon. Simba ni mzoefu wa makesi kama hayo, i appeared before him several times.
 
Hakika mahakama imetenda haki sana na hakimu ametumia huruma iliyo pitiliza maana ni wazi wabunge wa chadema na Mbowe walisababisha kifo cha yule binti kwa maandamano yasiyo na tija!

Kama hakimu angeliweka huruma pembeni hakika Wabunge wa chadema na Mbowe walistahili kifungo cha maisha jela au kunyongwa!

Hakika mahakama zetu ni huru sana na zina tenda haki
 
Hivi kangi lugola anasubiri nini mtaani hadi muda huu? Au kwa kuwa yupo chama dola
 
Hakika mahakama imetenda haki sana na hakimu ametumia huruma iliyo pitiliza maana ni wazi wabunge wa chadema na Mbowe walisababisha kifo cha yule binti kwa maandamano yasiyo na tija!

Kama hakimu angeliweka huruma pembeni hakika Wabunge wa chadema na Mbowe walistahili kifungo cha maisha jela au kunyongwa!

Hakika mahakama zetu ni huru sana na zina tenda haki
Kumbe mahakimu wetu hawahukumu tena kwa mujibu wa Sheria Bali kwa huruma waliyo nayo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakika mahakama imetenda haki sana na hakimu ametumia huruma iliyo pitiliza maana ni wazi wabunge wa chadema na Mbowe walisababisha kifo cha yule binti kwa maandamano yasiyo na tija!

Kama hakimu angeliweka huruma pembeni hakika Wabunge wa chadema na Mbowe walistahili kifungo cha maisha jela au kunyongwa!

Hakika mahakama zetu ni huru sana na zina tenda haki
Kama hakimu alizingatia huruma kuamua kesi, haki iliyotendeka iko wapi? Kuzingatia huruma maana yake hakimu aliangalia sura. Kosa ambalo lilipelekea umauti kwa mtu halafu adhabu yake iwe ndogo kuliko adhabu anayopata mwizi wa kuku, hapo kuna haki kweli? Basi hukumu za wafungwa wengine ziwe reviewed kwa kuzingatia huruma pia.
 
Nahitimisha kwa kusema Kama Shughuli za Mahakama zingekuwa zinaingiliwa na mhimili Mwingine basi Mbowe angehukumiwa kifungo Cha mbwa mwizi, Naipenda Tanzania.
Masinki -Nipo Katavi kwa Sasa.
Hivi mwendawazimu huwa anajuaga kuwa yeye ni mgonjwa?
 
Back
Top Bottom