Pongezi kwa kikosi cha kupambana na Dawa za Kulevya

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,076
7,647
Pongezi nyingi sana kwao kwa operesheni kabambe ya kuwanasa wauza Dawa za Kulevya almaarufu kama unga.

Tunaona sasa wamedhamiria kuwakamata,
Kamwe wasimuonee mtu yeyote aibu, awe na cheo au awe maarufu kamateni!!

Wapo wengi wanafahamika ambao sasa wamerudi kwa kasi ya ajabu kuuza madawa, hawa watu wanao taka utajiri kwa kuangamiza kizazi chetu nashauri Wapigwe risasi.

Bunge litunge sheria kuwa mtu yeyote akitiwa hatiani kwa madawa ya kulevya anyongwe hadi kufa.

Wauza madawa hawana tofauti na wauaji wengine.

Watanzania wenzangu tuendelee kuwafichua wauza madawa ya kulevya kweye maeneo yetu; Sinza, Kinondoni, Mbagala, K/Koo, Temeke, Boko, na maeneo mengine .
 
FB_IMG_16504464261866544.jpg
 
Bunge litunge sheria kuwa mtu yeyote akitiwa hatiani kwa madawa ya kulevya anyongwe hadi kufa
sikumbuki nimesoma wapi lakini imebainika kuwa sasa hv Drug lord wameenda extra mile kwa maana kuwa wanachofanya wanatengeneza baadhi ya vyakula hasa snacks kwa mchanganyiko wa bidhaa za kawaida na Drugs kidogo, i dont knw exactly wana lengo gn lkn naona vile taifa linavyoenda kuangamia maana kama pipi inakuwa mix na kitu kama Heroin, bangi au any kind of drugs kwenye biscuits, Bubble gums, Jam, kashata etc, ambazo ni kipenzi wa watoto basi ni dhahiri taifa lilo kwenye hatari kubwa!
 
sikumbuki nimesoma wapi lakini imebainika kuwa sasa hv Drug lord wameenda extra mile kwa maana kuwa wanachofanya wanatengeneza baadhi ya vyakula hasa snacks kwa mchanganyiko wa bidhaa za kawaida na Drugs kidogo, i dont knw exactly wana lengo lao lkn naona vile taifa linavyoenda kuangamia maana kama pipi inakuwa mix na kitu kama Heroin na biscuits, Bubble gums, Jam etc, ambazo ni kipenzi wa watoto basi ni dhahiri taifa lilo kwenye hatari sana.
Zipo kashata zinatengenezwa kwa kuchanganya bangi
Madem masista du wa mjini wanazipenda sana....
Ila kuna nmna ya kuzitengeneza wenyewe wanajuwa

Ova
 
ndio maana tatizo la afya ya akili linaongezeka kila kukicha katika jamii!! kumbe kuna wahuni wanazinogesha kashata na mmea wa bangi!!!
hatari sana!
tuwafichue hawa wahuni waanao haribu kizazi.
 
sikumbuki nimesoma wapi lakini imebainika kuwa sasa hv Drug lord wameenda extra mile kwa maana kuwa wanachofanya wanatengeneza baadhi ya vyakula hasa snacks kwa mchanganyiko wa bidhaa za kawaida na Drugs kidogo, i dont knw exactly wana lengo gn lkn naona vile taifa linavyoenda kuangamia maana kama pipi inakuwa mix na kitu kama Heroin, bangi au any kind of drugs kwenye biscuits, Bubble gums, Jam, kashata etc, ambazo ni kipenzi wa watoto basi ni dhahiri taifa lilo kwenye hatari kubwa!
Lengo lao ni kupanua wigo wa soko na ni concealment ya "mapunda".

Kwa mfano biskuti ama juisi ya bhangi waweza ishitukia namna gani wewe layman bila kuchomewa?

Halafu uelewe kwamba bidhaa hizo haziuzwi kiholela, zinawalenga wateja maalumu tu kuzitumia wao wenyewe ama kuleweshea wahanga wao.
 
naamini itaisha, jambo la msingi itungwe sheria ya kuwaua kabisa.
wauza madawa ni wauaji.

tuwafichuwe bila woga wale wote wanao husika na biashara hii haramu ya kuangamiza kizazi chetu, hakuna cha mkubwa wala mdogo.
China, Iran, Saudi Arabia, Malaysia, Singapore, nk! kote huko ukikamatwa na hayo madawa unauwawa kwa kunyongwa, au kukatwa kichwa haharani! Lakini watu hawaachi.

Hii biashara ya madawa ya kulvya, na ile ya ukahaba! Kwa mtazamo wangu bado zipo zipo sana tu. Ila naunga mkono juhudi za Serikali kwenye kupambama na hili janga la matumizi ya hayo madawa ya kulevya.
 
nadhani hata sisi Tanzania tunapaswa kuwa na sheria ya kuwauwa hawa watu, natamani wapigwe risasi wapotee kabisaa.
 
Tuesday, 20 December 2016​

KINARA DAWA ZA KULEVYA MBARONI​

KINARA wa mtandao wa biashara za dawa za kulevya, Kambi Zubeir Seif, maarufu kwa jina la Cambiasso, ametiwa mbaroni, kufuatia msako mkali uliofanywa na Polisi Kikosi Maalumu cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, katika nyumba yake ya kifahari aliyokuwa amejificha iliyoko Tuangoma, wilayani Kigamboni, Dar es Salaam.
Cambiasso, pia inadaiwa mwaka 2011, alikamatwa na kilo 179, za dawa za kulevya aina ya heroine, akiwa na wenzake watatu, Fredy Chonde, ambaye ni Mtanzania, Muhammad Shahbaz na Abdulghan Gulam, ambao ni raia wa Pakistan.
Mfanyabiashara huyo anayemiliki nyumba za kifahari pamoja na magari, anayedawa kuwa kinara muunganishaji wa mitandao ya dawa za kulevya, alikamatwa usiku wa kuamkia Desemba 10, mwaka huu, katika operesheni kali ya kuwasaka wafanyabiashara wa dawa za kulevya nchini.
Wengine waliokamatwa kwenye msako huo ni Marashi Zuberi Seif, ambaye ni dada wa mtuhumiwa namba moja na rafiki wa kike wa Cambiasso, Grace Aseasisye, ambaye alipangiwa nyumba eneo la Yombo Buza.
Imeelezwa kuwa polisi inaendelea na msako mkali baada ya watuhumiwa wengine kukimbia, ambapo kwa mujibu wa chanzo chetu, operesheni hiyo ni mwanzo wa operesheni kubwa zitakazoendeshwa na polisi kuumaliza mtandao huo unaohatarisha nguvu kazi ya vijana.
Akizungumzia kukamatwa kwa kinara huyo, Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Dawa ya Kulevya Tanzania, Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Polisi (SACP), Mihayo Msikhela, alisema Cambiasso alikamatwa Ijumaa, iliyopita na kufikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
“Huyu ni kiunganishi wa mitandao hiyo. Polisi walifanikiwa kumtia nguvuni baada ya kuweka mtego nyumbani kwake na Ijumaa alishafikishwa mahakamani kujibu moja ya kesi inayomkabili,” alisema Kamanda Msikhela.
Kwenye kesi hiyo, mtuhumiwa huyo aliunganishwa katika kesi namba PI 23/2016 ya raia wa Nigeria, Bede Eke, aliyekamatwa Juni, mwaka huu, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam, akiwa na kilo tano za dawa za kulevya.
Anakabiliwa na kosa la kula njama (conspiracy) na kusafirisha dawa za kulevya pamoja na raia huyo wa Nigeria.
Msako huo ni hatua za mapambano dhidi ya mtandao huo, ambao serikali ya awamu ya tano imeahidi kuutokomeza.
Katika mkesha wa kuliombea Taifa, Desemba 31, mwaka jana, Rais Dk. John Mafuguli, alisema Taifa kwa kipindi kirefu lilikabiliwa na vigogo wauza dawa za kulevya, watumishi na vigogo wakwepaji wa kodi pamoja na wizi wa dawa hospitalini, hivyo viongozi wa dini na Watanzania wote wanapaswa kumuombea ili aweze kutumbua majipu ya mafisadi hao.
Dk. Magufuli, ambaye aliwakilishwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, alisema viongozi wa dini wanapaswa kuendelea kuliombea Taifa na kuwaombea watu wabaya wasiopenda maendeleo waweze kubadilika ili nchi iweze kusonga mbele.
“Viongozi wa dini tunapaswa kuendelea kumuombea rais wetu (Dk.Magufuli), aendelee kutumbua majipu haya, ambayo yanasababisha maendeleo ya Taifa letu kurudi nyuma,” alisema Lukuvi.
 
Jamaa alianza muda mrefu!!
 
kama kuna mapapa wataje haraka sana halafu utona moto wake.

nakwambia safari hii hakuna jiwe litkalo baki juu ya jiwe, hii ni vita vitakatifu.
Ndoto za alinacha hizo. Kilichobaki utajikojolea huko ndotoni.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom