Mtego wa Noti
JF-Expert Member
- Nov 27, 2010
- 2,591
- 1,599
Napenda kutoa pongezi za dhati kwa jeshi la polisi Mkoa maalumu wa Kinondoni chini ya RPC Kingai kwa kuwa na utendaji wa haraka wa kufika kwenye matukio mara wanapopokea taarifa za uhalifu hata ikiwa usiku wa manane.
Mimi ni shuhuda maana majambazi waliingia mtaani na mara baada ya Polisi kupewa taarifa walifika haraka sana eneo la tukio tena magari mawili kutokea maeneo tofauti lakini wakielekea kwenye kupambana. Hii ni tofauti na ilivyotegemewa hasa siku za nyuma. Majambazi walihisi wako hatarini wakaondoka vinginevyo pangetifuka maana makamanda walifika wengi wakiwa wamejipanga kimapigano.
Na kwa muda wote mara baada ya taarifa kufika Polisi RPC Kingai mwenyewe alikuwa anaratibu vikosi mbalimbali kutokea Wazo, Goba na Madale kuvielekeza vifike eneo la tukio huku akiwapigia simu wahanga ili waelekeze vikosi vifike eneo la tukio.
Hongereni sana makamanda na sisi wakazi wa Goba tumefurahi mno na kujivunia uwepo na utendaji wenu wa haraka sana kwa kufika kwenye matukio. Endeleeni na spirit hiyo.