Pongezi Kwa Dr D. Kamala Kwa Kutetea Maslahi Ya Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pongezi Kwa Dr D. Kamala Kwa Kutetea Maslahi Ya Tanzania

Discussion in 'International Forum' started by Ngongo, Nov 14, 2008.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  Nov 14, 2008
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Mazungumzo ya kuanzishwa kwa Soko la Pamoja la Afrika Mashariki yamekwama baada ya Tanzania kugomea baadhi ya vipengele ambavyo imeona vina maslahi kwa taifa. Mazungumzo hayo ambayo yanafanyika chini ya Jumuiya ya Afrika Mashiriki (EAC) ilibidi yakamilike mwezi ujao, lakini kutokana na kushindwa kufikiwa kwa mwafaka, yamesogezwa hadi Aprili mwakani.

  Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Diodorus Kamala alisema Dar es Salaam kuwa Tanzania haijakubaliana na mawazo ya nchi nyingine kuhusu uhuru wa kusafiri, mgawanyo wa ardhi, uraia wa kudumu na masuala ya huduma. Dk. Kamala alisema baadhi ya nchi zinataka soko la pamoja likianzishwa, kuwe na uhuru na haki ya kupata ardhi, kitu ambacho Tanzania inakataa kwa sababu nchi nyingine haina ardhi ambayo Watanzania wataweza kupata.

  Alisema pia sheria za ardhi za nchi hizo zinatofautiana, kitu kitakacholeta mtafaruku ambao mwisho wa siku, Tanzania ndiyo itaathirika kwa nchi nyingine kuchukua ardhi kwa kuwa ina ardhi kubwa. “Tumeona suala la ardhi tusiliingize kabisa kwenye suala la soko la pamoja…ukitaka kuleta machafuko basi ingiza suala la ardhi kwenye soko la pamoja,” alisema Dk. Kamala ambaye pamoja na Kamati ya kisekta ya Mawaziri wa EAC walikutana Zanzibar wiki hii.

  Kuhusu uraia wa kudumu, Dk. Kamala alisema Tanzania inapinga kuwapo kwa haki ya kupata uraia kwa wananchi waliokaa ndani ya nchi moja kwa miaka mitano, kwa sababu itailazimisha Tanzania kuwapa uraia hata wageni ambao wamekaa nchini isivyo halali. Alisema Tanzania itaendelea na utaratibu wake uleule wa kuwapa uraia wageni wenye sifa ili kuziba mianya ya wachache ambao wanaweza kutumia mgongo wa soko la pamoja kukaa nchini.

  Kamala alisema Tanzania pia inapinga mawazo ya baadhi ya nchi kutaka vitambulisho vya uraia vitumike mipakani badala ya pasipoti ili kurahisisha wasafiri kuingia nchi nyingine kwa urahisi. Alisema mazungumzo hayo yataendelea tena Machi mwakani na kama hadi Aprili mwafaka hautafikiwa, basi wataongeza muda zaidi, lakini Tanzania haitakubali kwenda haraka kama itaona hakuna manufaa.

  Chanzo"Habari leo"
  Napenda kutoa pongezi nyingi kwa mh Dr D Kamala kwa msimamo mzuri wa kuendelea bila kuchoka kupinga mkakati wa nchi za EAC kuingiza masuala ya Ardhi,uhuru wa kusafiri na uraia.
  Mimi sipingi uanzishwaji wa soko la pamoja lakini watanzania tunatakiwa kuwa makini sana na hii jumuiya ya Afrika mashariki kwasababu nchi nyingine zinataka kutuingiza mgenge.Nchi zote za Afrika mashariki ukiondoa Tanzania hazina ardhi ya kutosha suluhu pekee waliyonayo ni kunyakua ardhi ya Tanzania.Kenya sehemu kubwa ya ardhi yake inamilikiwa na wanasiasa wachache [Kenyatta,Moi,Mwaikibaki & other].
  Tanzania bado inawakimbizi kutoka nchi za Rwanda na Burundi kama kipengele cha uraia wa kudumu na uhuru wa kusafiri kitaridhiwa na Tanzania wakimbizi wote watakuwa ni raia wa Tanzania.Pia raia wengi wa Burundi,Rwanda,Kenya na Uganda waliokosa ardhi watakimbilia Tanzania.
  Tanzania katika suala hili iko pekee yake hakuna nchi ya EAC inayopinga kwasababu nilizozitaja hapo.
  Wakuu wakati mwingine nawafagilia sana ndugu zetu wazanzibar walivyotayari kutetea maslahi ya Zanzibar hata kwa jambo la kijinga lakini sisi watanzaia {Tanzania bara} tunaliacha jukumu hili muhimu mikononi mwa serekali pekee.
  Natoa rai kwa watanzania wote tuungane kutetea maslahi ya Tanzania kwa hali na mali.
   
 2. K

  Kabonde JF-Expert Member

  #2
  Nov 14, 2008
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ngongo kwani kuna tatizo gani tukiwapa uraia wakimbizi wa Rwanda na Burundi.
  Binafsi naona watakuwa wamepata fursa kishiriki katika shughuli za ujenzi wa taifa.
   
 3. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #3
  Nov 14, 2008
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280

  Kunatatizo mkuu Kabonde.
  Wakimbizi wanaotoka katika nchi za Rwanda na Burundi wamekuwa mzigo mkubwa kwa serekali na kwa sehemu walizofikia.Uharibifu wa mazingira,wanatumia hudumu chache zilizopo kwaajili ya watanzania(hospital,shule na nk).
  Hawa wakimbizi pia wanakuja na silaha ambazo zinatumika katika uhalifu.
  Ardhi ya Tanzania haiongezeki lakini watanzania wanaongezeka,ni muhimu kuilinda kwaajili ya vizazi vijavyo.Nchi za Uganda,Kenya,Rwanda na Burundi zinapaswa kutafuta njia nyingine badala ya kuleta mbinu zao za kisungura.
   
 4. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #4
  Nov 14, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,422
  Likes Received: 393
  Trophy Points: 180
  Niliangalia TV wakati waziri Kamala akiongea nilijisikia vizuri kweli kweli. Kumbe kuna watu wanaweza simamia maslahi ya nchi vizuri namna hii kwenye serikali ya awamu ya nne!!! Swala la ardhi lisiletewe mzaha hata kidogo...hapo ndipo machafuko hutokea. Kenya ardhi yao waliipoteza kwa walowezi na mafisadi wa serikali yao...wabaki tu huko huko.Najisikia vizuri kuwa Mtanzania..mmmh TzPride.
  Waziri Kamala sisi tuko nyuma yako, weka maslahi ya nchi mbele na Mungu atakubariki.

  Mungu ibariki Tanzania.
   
 5. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #5
  Nov 15, 2008
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Hongera Dr. Kamala.Nilitarajia hilo kutoka kwa kiongozi mwenye uzalendo usio na mashaka
   
 6. K

  Kabonde JF-Expert Member

  #6
  Nov 15, 2008
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mpango wa kutaka kuingiza kipengele cha ardhi utashindika kwasababu nchi zote zinaikodelea macho ardhi ya Tanzania na fursa nyingi za kiuchumi.Suluhisho pekee ni kujaribu kuishawishi DRC ijiunge na EAC labda itaweza kusaidia kiu ya ardhi kwasababu DRC ina ardhi ya kutosha.
   
 7. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #7
  Nov 15, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Tanzania pia tuna ardhi ya kutosha. Kichekesho ni kwamba akija Sinclair anaomba ardhi Watanzania wanahamishwa haraka haraka na mzungu kupewa ardhi, lakini jirani zetu ambao tunazungumza nao lugha moja tunaanza kuwatilia mashaka kuwa wanataka ardhi yetu. Hata kama so what? Sijaona lolote la kupongeza hapa, ni narrow minded mentality tu.
   
 8. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #8
  Nov 15, 2008
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Mkuu jasusi,
  Waziri Kamala kaliweka suala la ardhi wazi kwa wana EAC,wawekezaji kutoka nchi za EAC wanaweza kupata ardhi kama akina Sinclair.Wanachi wa EAC {Kenya,Uganda,Rwanda na Burundi}wanatakiwa kufuata sheria na taratibu za ardhi kama wageni wengine.Tanzania ikiridhia vipengele vilivyokataliwa na mheshimiwa waziri Dr Kamala maana yake wakenya,waganda,wanyaruanda na warundi watakuwa na haki ya kupata ardhi kama ilivyo kwa raia wa Tanzania.
  Naomba kuwasilisha.
   
 9. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #9
  Nov 15, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135


  Duh!


  .
   
 10. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #10
  Nov 15, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Sijasema kuwa watu wapewe ardhi carte blanche, au Wakenya, Waganda, Wanyarwanda na Warundi waingie kiholela tu. Hizo sheria na taratibu za ardhi tayari zipo lakini tusifanye iwe vigumu kwa majirani zetu na ndugu zetu kiutamaduni kuwa na ardhi Tanzania. Kinachonipa shida mimi ni kwamba anapoingia mzungu tuko radhi kumhamisha Mtanzania ili mzungu apate hiyo ardhi kwa kisingizio cha uwekezaji lakini Mnyarwanda akitaka ardhi ya kilimo tutatumia kigezo cha kwamba si raia kumnyima ardhi. Kama wawekezaji wanaweza kupata ardhi why not raia wa kawaida tu ambaye anataka kulima? Kwani huyu si mwekezaji? Mwaka 1995 alipokuwa anaaga rais Mwinyi alienda Afrika kusini na kuwataka wakulima wa Kikaburu waje Tanzania wapewe ardhi. Lakini sijasikia kiongozi yeyote anakwenda Rwanda kuwaomba jirani zetu waje walime Tanzania. Inaingia akilini? That is my point. Waache waje. Walime, wajenge shule, wafanye biashara, walete utaalamu na uzoefu wao, tuishi nao.l Hayo ndiyo maendeleo. Hata EU wameshaliona hilo.
   
 11. O

  Ogah JF-Expert Member

  #11
  Nov 15, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  .....Jasusi kula tano Mkuu...........

  Trust me...hapo ungekuwa ni mjadala wa type ya IPTLs or BUZWAGIs........story ingekuwa tofauti.............tunataka kusikia Kamala et al wapinga MKATABA WA let say BUZWAGI Contract au IPTL then.......na sio hizi cheap shots ambazo hata kipofu anaona........damn
   
 12. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #12
  Nov 15, 2008
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Waziri Kamala umeonyesha msimamo halisi wa waTanzania katika hili suala la jumuia ya Afrika Mashariki.Sharti twende pole pole na kila kipengele lazima kieleweke ili yasije tokea matatizo kama ya mikataba ambayo haina maslahi kwa Taifa na watu wake.
   
 13. J

  Janejo Member

  #13
  Nov 15, 2008
  Joined: May 26, 2008
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kwa vile hajapinga IPTL au Buzwagi unataka asitetee suala la ardhi ya Tanzania? I don't buy your argument...it cuts no eyes to me!
   
 14. J

  JokaKuu Platinum Member

  #14
  Nov 15, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,751
  Likes Received: 4,968
  Trophy Points: 280
  Jasusi,

  ..Wakenya na Wanyarwanda wanajaribu kututia ujinga Watanzania.

  ..Kagame alijaribu kulazimisha Tanzania iwape uraia wakimbizi wa Kinyarwanda. hoja yake ilikuwa Rwanda kwa sasa hivi kumejaa. ilibidi Mkapa ampige dongo kwamba hoja ya Kagame inafanana na ile ya Habyarimana wakati RPF walipokuwa wakidai kurudi Rwanda.

  ..taratibu zetu[tanzania] za uwekezaji zinaruhusu wawekezaji wa Kenya,Rwanda,Uganda...kuwekeza Tanzania bila vipingamizi vyovyote vile. majuzi Kikwete ameweka jiwe la msingi kwenye kiwanda kikubwa cha sementi cha mwekezaji toka Kenya.

  ..hawa wenzetu wanataka kuhamishia machinga,mama ntilie,chokoraa,ma-day waka,...huku Tanzania. ukweli ndiyo huo. wa-Tanzania tujiulize kama tunahitaji wahamiaji wa aina hiyo toka Kenya,Rwanda,Burundi,na Uganda.

  ..kuna kipindi hata walijaribu hata kutushawishi kwamba ziwa victoria litumiwe na wavuvi toka nchi zote bila kuheshimu na kuzingatia mipaka. walifanya hivyo baada ya kuona kwamba wao wana eneo dogo, na zaidi samaki wamepungua ktk eneo lao.

  ..halafu kitu cha ajabu kabisa, kama hivi wa-Tanzania tumekataa hizi hoja zao, Uganda,Burundi,Uganda, na Kenya, hawasongi mbele na hii ajenda ya muungano wa Afrika Mashariki.

  ..why cant they[ky,ug,rw,br] form the EA federation in exclusion of Tanzania?
   
 15. SaidSabke

  SaidSabke JF-Expert Member

  #15
  Nov 15, 2008
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 1,968
  Likes Received: 222
  Trophy Points: 160
  kaka mimi naona hapo umechanganyikiwa labda huelewi tofauti ya masuala haya mawili
   
 16. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #16
  Nov 15, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Nielimishe kaka yangu, nielimishe. Ndio faida hiyo ya JF.
   
 17. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #17
  Nov 15, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  jokaKuu,
  Tanzania is a vital link in the EA federation. For Kenya we are a common market and for Rwanda and Burundi we are a link to the sea. Unajua nini, had it not been for colonialism and the world war Rwanda and Burundi would still be part of Tanganyika.
   
 18. Ladslaus Modest

  Ladslaus Modest JF-Expert Member

  #18
  Nov 15, 2008
  Joined: Jun 27, 2008
  Messages: 638
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mie pia ninampongeza kwa Moyo wa dhati Mh. Dr. D. Kamala kwa kulitetea Taifa letu.

  Mie ningependa Tanzania ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki tuwe kama Waingereza ndani ya Jumuiya ya Ulaya.

  Nawasilisha

  (Mimi Mchungaji)
   
 19. J

  JokaKuu Platinum Member

  #19
  Nov 15, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,751
  Likes Received: 4,968
  Trophy Points: 280
  Jasusi,

  ..lakini bila hata ya hiyo federation na kuruhusu Wakenya kuhamia Tanzania bado Kenya inauza bidhaa zake nyingi tu Tanzania.

  ..zaidi Warundi na Wanyarwanda wanatumia bandari za Mombasa na Dsm. hakuna aliyewazuia ktk hilo.

  ..ninachokataa mimi ni wanapojaribu kutulazimisha tubadili sheria zetu za kazi na uajiri, uhamiaji, pamoja na umiliki wa ardhi.

  Jasusi,

  ..hapo juu umechanganya kidogo.

  ..Rwanda,Burundi,Tanganyika, zilikuwa "nchi" moja kwa mipango ya wakoloni. baadaye wakoloni hao hao walipogombana zikatenganishwa.

  ..mimi nadhani kama ni kuungana tuzingatie maslahi ya kiuchumi na kijamii ya sasa hivi--karne ya 21. hakuna haja ya kulalamikia wakoloni hapa.

  NB:

  ..Tanzania tuna matatizo yetu mengi tu ya ndani. we need our space in dealing with them.
   
 20. F2S

  F2S JF-Expert Member

  #20
  Nov 15, 2008
  Joined: Feb 16, 2008
  Messages: 216
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwanza nampongeza Dr. Kamala kwa kufanikiwa kutetea kile ambacho waTZ wamemuagiza atetee yap si ndio mtu anayetuwakilisha. Tujaribu kutafakari kwa makini ni nini kilisababisha kuvunjika kwa iliyokuwa jumuia ya afrika mashariki na kujaribu kukwepa hayo yasitokee tusiburuzwe. Then tufanye utafiti ktk nchi zingine na kuona wanafanya nini hasa likifikia swala la aldhi na makazi, natoa mfano kidogo Singapore ni nchi iliyojirani na Malaysia na inasemekana ilikuwa ni part ya Malaysia. Sheria walizojiwekea zote zinamlinda mzawa ni kiama. Mzawa ndio mwenye priority ya kwanza kupewa makazi na hata mgeni akikaa miaka kumi na zaidi ataendelea kupanga kwenye nyumba ya mzawa. Kama kuna divident yoyote kutoka serikalini ni mzawa pekee anapata mgeni ulie tu. Hata kufungua bank account ni ngumu kama wewe sio mzawa. Makampuni mengi yapo chini ya CEO wazawa labda kuwe hakuna mzawa mwenye vigezo kitu ambacho ni kigumu. Kazi za kawaida sana ndio wapewa wageni. Japo ni ngumu kumeza huo utaratibu lakini ndio wamefanikiwa kupiga hatua na sasa wana ni number tano duniani as far as GDP per capital is concerned.

  Nachotaka kusema ni kwamba tusipokuwa makini ktk policy tutasababisha waTZ kuwa watumwa ktk nchi yetu. We still have time tusikimbilie kuuza nchi yetu eti kwa kisingizio cha EAC. Niliwahi kupata habari kutoka kwa jamaa yangu mmoja anafanya kazi ya trafic control pale JNIA kwamba baada ya kuvunjika kwa africa mashariki waTZ walipata shida ktk aviation Industry kwa sababu kulikuwa hakuna wataalam wakutosha wakiTZ. Hii inaonesha no one was interested kusomesha hawa waTZ ila waKNY na jamaa zao WAGND may be. Tunakimbilia wapi,tuandae wataalam wakutosha na tuhakikishe tuko tayari kushika nafasi za CEOs and other managerial posts then tuingie ktk jumuia lakini tukiwa makini kulinda Wazawa. Ni nchi yetu hatutaki kuburuzwa na kulazimishwa na kina Mu7.

  Aldhi ni kitu nyeti mmsahau Amini alitaka kumega nchi yetu, mmesahau Kenya watangaza mnt Kilimanjaro iko Kwao, mmesahau kuwa Mu7 anatakakutawala EAC anataka nini? later waganda watatawala wabongo yap wataajiri ndugu zao hata kama wapo wabongo walio na vigezo.

  NB no country is 100% race blind tutaleteana chokochoko na vita kama sheria nzito hazitawekwa. Kila nchi itumie aldhi yake na yeyote anayetaka aldhi ktk nchi nyingine afate utaratibu atakaopangiwa na nchi husika.
   
Loading...