Pongezi kwa diwani Gongo la Mboto Jerry Silaa

Kwa jiji la Dar es Salaam, kuendelea kuwekeza kwenye visima ni fedheha. Ni lini watu hawa watakuwa na maji ndani, na kuondoka na huu mfumo wa pre-industrial revolution?

Basi hamkosi cha kusema; kina mama wengi wa Chadema wameanza kunufaika na kisima!

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Una uhakika kama pesa zilizotelewa ni za halmashauri ya Ilala? jifunzeni kukubali ukweli sio kila kitu ni kupinga

Chama
Gongo la mboto DSM

chama mfikishie salamu huyo swahiba wako kwamba wananchi wa Ukonga Mzambarauni wanamkumbusha kwamba aliwachangisha fedha kwa ajili ya mradi wa maji mwaka 2007/2008 lakini hadi leo hii hawajapata maji na fedha yao hawajui aliipeleka wapi.
 
Last edited by a moderator:
Huyu kijana anajisikia sana na anadharau sana watu.Eti anajiandaa kugombea ubunge Ukonga.Hapa ameumia hapati kitu.

Kupata umeya tu amehama gongolamboto sasa akipata ubunge si atahama nchi!?
Jerry katufungulia dispensary pale mongolandege isiyokuwa na vifaa tiba wala daktari. Kuna waganga wawili ambao wanapima magonjwa kwa kupiga ramli, na jumapili dispensary inafungwa, sijui wameagana na magonjwa siku za jumapili!?
Ukonga hatuwezi kurudia kosa kwa kumchagua mbunge muuza sura kwakuwa huyu wa sasa baada ya kutangazwa mshindi alichofanya ni kumalizia nyumba yake mbezi beach na kuhamia huko.
 
Sipo hapa kupinga bali kukuelewesha kama uko mis informed, mimi ni mkazi wa Manispaa ya Ilala na ni mdau wa Maendeleo ya Manispaa yetu na kila mwaka ni lazima nipate kitabu chenye majedwali yote ya mapato na matumizi na miradi ya Maendeleo kwa kila kata.

Sina sababu ya kuwa na chuki yoyote kwa kijana mwenzangu ambaye amechanga karata zake vizuri na kupata wadhifa mzito akiwa na umri mdogo, Jerry Silaa ana nafasi ya kuwin mioyo ya watu wa Gongo la mboto kwa kutumia nafasi yake kama meya kukamilisha mradi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Mombasa mpaka Moshi Bar.

Kwa mfumo wetu wa local Government Jerry hatahukumiwa na sisi wakazi wote wa Manispaa ya Ilala bali na watu wake wa Gongo la mboto kwa sababu Meya hachaguliwi na Wananchi bali anachaguliwa na madiwani wenzake, akilijuwa hili vyema bado anauwezo wa kufanya kama alivyofanya Basil Mramba ambaye alipeleka maradi wa barabara ya Marangu Tarakea wakati haikupaswa kuwa hivyo. sina tatizo na Jerry.

Matola acha kujikanyaga; alichofanya Jerry Silaa ni kwa manufaa ya wakazi wake kata yake; mfumo wa utendaji wa halmashauri za jiji na miji unategemea mafungu kutoka serikali kuu; kama halmashauri zingekuwa na mamlaka kamili ya ukusanyaji na utumiaji wa mapato yake ni wazi miji mingi ingebadilika; kwa mfumo huu wa sasa bado kidogo hata Jerry angetamani kujenga barabara Gongo la mboto Kisarawe bado angepata matatizo kwani yote yanategemea fungu alilotengewa; kwa hili la kisima mpe pongezi!

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Mimi bila kumung'unya maneno, mwaka 2010 nilinunua 'kibanda' pale Gongo la mboto, ndio nikaanza kumjua huyu bw mdogo, nikafuatilia cv zake jamaa yuko vzr na hata UDSM alikuwa kiongozi. Nakumbuka kati ya ahadi alotimiza ni daraja la ulongoni. BIG UP.
 
Kupata umeya tu amehama gongolamboto sasa akipata ubunge si atahama nchi!?
Jerry katufungulia dispensary pale mongolandege isiyokuwa na vifaa tiba wala daktari. Kuna waganga wawili ambao wanapima magonjwa kwa kupiga ramli, na jumapili dispensary inafungwa, sijui wameagana na magonjwa siku za jumapili!?
Ukonga hatuwezi kurudia kosa kwa kumchagua mbunge muuza sura kwakuwa huyu wa sasa baada ya kutangazwa mshindi alichofanya ni kumalizia nyumba yake mbezi beach na kuhamia huko.

Ahaaa haa Mkuu Mwita ni yaleyale kugombea uraisi tu alilazimisha chama kimjengee nyumba mezi beach na kujipangia mshahara sasa akipata huo uraisi si atalazimisha tumjengee kisiwa!

Chama
Gongo la mboto DSM
 
chama mfikishie salamu huyo swahiba wako kwamba wananchi wa Ukonga Mzambarauni wanamkumbusha kwamba aliwachangisha fedha kwa ajili ya mradi wa maji mwaka 2007/2008 lakini hadi leo hii hawajapata maji na fedha yao hawajui aliipeleka wapi.

Mkuu Mwita mimi simjui Jerry Silaa wala kumuona in person namsoma kwenye magazeti tu; wakumpa salamu ni Matola yeye anaweza kumfikishia!

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Matola acha kujikanyaga; alichofanya Jerry Silaa ni kwa manufaa ya wakazi wake kata yake; mfumo wa utendaji wa halmashauri za jiji na miji unategemea mafungu kutoka serikali kuu; kama halmashauri zingekuwa na mamlaka kamili ya ukusanyaji na utumiaji wa mapato yake ni wazi miji mingi ingebadilika; kwa mfumo huu wa sasa bado kidogo hata Jerry angetamani kujenga barabara Gongo la mboto Kisarawe bado angepata matatizo kwani yote yanategemea fungu alilotengewa; kwa hili la kisima mpe pongezi!

Chama
Gongo la mboto DSM
chama nina uhakika haupo well Informed Manispaa ya Ilala ina mapato yake ya kugharamia miradi yake, achana na fungu la serikali kuu, inaonekana wewe mwenzetu hujui lolote linaloendelea ndani ya Manispaa hii, hivi unafahamu kwamba sasa hivi sehemu ambazo ni uswazi kama Buguruni na Vingunguti Barabara zote ni za kiwango cha changarawe na madimbwi yamebakia kuwa Historia?

Jerry Silaa yupo hapa JF ni Member mwenzetu kama ana uthubutu labda aje yeye akueleze ndio utamuelewa, kuna miradi inafadhiliwa na World bank inachohitajika ni kiongozi ambaye yuko Smart tu kuichangamkia na ukitaka ushahidi wa hili waulize wakazi Temeke kata ya Sandali na Diwani wao anaitwa Tarimo je aliwezaje kuichangamkia miradi hii mpka leo hii kata ya Sandari madimbwi ni historia, barabara ni za lami na Changarawe tu hakuna barabara ya vumbi.

Hicho kisima unachompa hongera Jerry mimi kwenye kata yetu tuliomba wenyewe mradi huo na tukafadhiliwa na world bank na mpaka sasa wana CCM ndio wamegeuza mtaji wa kupatia pesa za kula na mradi hauna pesa bank hata pump ikiharibika matengezo ni mgogoro.
 
Matola mfumo wa uendeshaji wa halmashauri za miji Tanzania ni matatizo matupu ziwe chini ya CCM au Chadema; siamini kama matatizo yanatokana na chama bali ni ubinafsi wa waliopewa dhamana ya kuendesha na wananchi wenyewe; mfano ni huu wa kisima cha kwenye kata yako utawalaumu viongozi kufuja pesa za mradi au wananchi wenyewe? inakuwaje wananchi mlio wengi mzidiwe na viongozi ambao hawazidi hata 5? Kuhusu miradi ya barabara bado yanahitaji ushiriki mkubwa wa serikali kuu; umesema unapatiwa vijarida vya mapato na matumizi ya Ilala inakuwaje hamhoji matumizi ya maendeleo?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Tumsifuni kwa mazuri anayoyafanya hakuna binadamu asiyejisikia

Chama
Gongo la mboto DSM
Ni yepi mazuri aliyoyafanya? Mimi ni mkazi wa Gongo la Mboto na namfahamu vizuri kijana huyu ambaye "amejikata" machoni kwa tuliomchagua tangu aingie madarakani. Nashangaa hiyo shida ya maji ndiyo ameiona leo baada ya kipindi cha ukimya na kujikata machoni kwa sisi wapiga kura wake! Halafu lilivyo kubwa eneo la Gongo la Mboto hana hata aibu kujitangaza kwa kisima kimoja, tena cha kuchota kwa kata! Hatujamsahau na hatutamsamehe alivyotutekeleza baada ya ajali ya kulipukiwa na mabomu ambapo serikali hii dhalimu ilitutapeli malipo kwa kutufanyia kiini macho cha baadhi yetu kulipwa cheki za Sh. elfu 18! Kijana huyu ni wale wale mafisadi na salamu zetu atazipata, yeye na mbunge wake yule mama kilaza ifikapo 2015.
 
Matola mfumo wa uendeshaji wa halmashauri za miji Tanzania ni matatizo matupu ziwe chini ya CCM au Chadema; siamini kama matatizo yanatokana na chama bali ni ubinafsi wa waliopewa dhamana ya kuendesha na wananchi wenyewe; mfano ni huu wa kisima cha kwenye kata yako utawalaumu viongozi kufuja pesa za mradi au wananchi wenyewe? inakuwaje wananchi mlio wengi mzidiwe na viongozi ambao hawazidi hata 5? Kuhusu miradi ya barabara bado yanahitaji ushiriki mkubwa wa serikali kuu; umesema unapatiwa vijarida vya mapato na matumizi ya Ilala inakuwaje hamhoji matumizi ya maendeleo? Chama Gongo la mboto DSM
Kwanza tu niseme online Politics ni nzuri sana na unaweza kujenga hoja zenye mashiko na ukaeleweka vyema, lakini unapokuja kwenye Battle Ground vitu ni tofauti sana na hili ndilo lililomkumba ndugu yetu Le Mutuz, alipoamuwa kupractise politics on the battle Ground.

Kwanza kabisa kwa kifupi sisi baada ya kufanikiwa kupata kisima tuliunda kamati ya wananchi watu 6 kama muongozo unavyoonesha na by that time CCM ilikuwa inaongoza DSM nzima kwa ngazi zote za kiongozi, tatizo likaja kuonekana baada ya wapinzani hasa CUF kupata viti vya uenyekiti wa mitaa CCM haikuridhika na mseto huu nakuonekana ni tishio kwa wale wala pesa za umma

Kasi ya mageuzi ilipopamba moto na mimi nikiwa kama mmoja wa tuliofanikisha kupata kisima kile niliwashauri kamati ya maji basi angalau wawe wanawasomea wananchi mapato na matumizi japo mara moja kwa kila miezi 6 lakini hili likashindikana na nilimuona Injinia wa Manispaa na niliongea na Abuu Jumaa akiwa meya wa Ilala na niliongea na Makongoro Mahanga akiwa kama Mbunge lakini ikaonekana kuivunja kamati ile ambayo kikanuni ilipaswa kukaa madarakani miaka 3 na kuitishwa uchaguzi mwingine ingekuwa na madhara makubwa kwa CCM kwani hakuna mtu wa kutoka upande wa CCM ambaye angeweza kuingia kwa kura kwenye kamati mpya.

Kwakuwa kuna watu wamejenga mpaka nyumba zao kwa kufuja mradi huu, wamefanikiwa kuwazunguka wananchi ambao kazi yao kubwa ni kunjwa pombe na hawajali mambo yanayohusu maendeleo yao, nimeambiwa sasa hivi ule mradi uko chini ya Dawasco na wale viongozi sasa watakuwa ni kama wakudumu na hata vikao kuhusu mradi wetu wamaji hautowahusu wananchi wote bali wadau wa maji, yaani wale ambao tumeunganishiwa maji majumbani kwetu ambao hatuzidi kaya 300. Je huu ndio utawala bora? hawa wengine wanaochota maji kwenye DP za mitaani yaani sasa hawaitwi kwamba ni wadau wa maji ya mtaa.

Ndio maana tunasema hii nchi inahitaji kufanyiwa overhaul, hatuwezi kuendelea kuishi kwa style na kinachokera zaidi wale watu wenye maisha duni ndio hawajui hata kuhoji wala kuelewa ni nini kinachoendelea juu ya maisha yao.
 
Matola maelezo mengi ukiyasoma na kuyachambua kwa kina wananchi husika ndio tatizo; hata mfumo ukibadilka yataendelea madudu haya haya hii kushindwa kuhoji mapato ya kisima ni sawa na wanachama wa kawaida wa Chadema wanavyoshindwa kuhoji mapato na matumizi ya Chadema; mfumo unawanufaisha watu wachache; naamini wapo wanachadema wengi maisha duni pamoja na kujitolea kwa hali mali sidhani leo hii kama wakiomba mkopo 30 watapewa; suala zima si kubadili mfumo bali kuwaelemisha wananchi wenye maisha duni wajue haki zao za msingi.

hapo sijaelewa kabisa je chama kinakopesha wananchi? meya wa ilala anazindua shimo la kuchotea maji ya chemchem za vyoo vilivyo tapakaa hapa goms urefu wa visima vya aina hii havizidi mita 40 vyoo na makalo ya wakazi wa mitaani kwetu ni mita 4 hadi 6 sioni usafi wa maji haya kwa matumizi ya binadamu , alipo kuwa anakabidhi shimo hili angewapa na cheti cha uthibitisho kuwa ni (salama kwa matumizi ya binadamu) hapo ningemsifu naona ameta maradhi mtaani
 
Jamaa anapendeza kweli, ingekuwa wale wnezake na yeye wangeongozana na mi-yunifomu ya kijani inachukiza kama ongea zao, gud boy, keep it up, ndio maendeleo ingawa tutakupiga chini tu bado
 
hapo sijaelewa kabisa je chama kinakopesha wananchi? meya wa ilala anazindua shimo la kuchotea maji ya chemchem za vyoo vilivyo tapakaa hapa goms urefu wa visima vya aina hii havizidi mita 40 vyoo na makalo ya wakazi wa mitaani kwetu ni mita 4 hadi 6 sioni usafi wa maji haya kwa matumizi ya binadamu , alipo kuwa anakabidhi shimo hili angewapa na cheti cha uthibitisho kuwa ni (salama kwa matumizi ya binadamu) hapo ningemsifu naona ameta maradhi mtaani

Mbona Dr. Slaa kapewa mkopo? wewe kaombe wakupe mkopo wa mabati 30 uone kama utapewa; kuhusu matumizi ya maji ya visima siku mnashauriwa mchemshe maji kabla ya kuyatumia.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Nenda you tube; I know where my faith stands; I am not gonna caught up with religious haters; the video never change my faith other than making me stronger! I don`t question what you believe or whether you truly understand what is written in bible; so don`t bring that mix to me; give your email I will send the link

Chama
Gongo la mboto DSM
hongera hapa umejibu kama GT kumbe wakati mwingine akili kubwa inatawala akili ndogo big up
 
chama mfikishie salamu huyo swahiba wako kwamba wananchi wa Ukonga Mzambarauni wanamkumbusha kwamba aliwachangisha fedha kwa ajili ya mradi wa maji mwaka 2007/2008 lakini hadi leo hii hawajapata maji na fedha yao hawajui aliipeleka wapi.

hii ndiyo jf bwana watu wana mafile kama tiss
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom