Pongezi kwa diwani Gongo la Mboto Jerry Silaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pongezi kwa diwani Gongo la Mboto Jerry Silaa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by chama, Sep 23, 2012.

 1. c

  chama JF-Expert Member

  #1
  Sep 23, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
  Wanabodi,
  Kwanza nachukua nafasi kumpongeza diwani wangu mh. Jerry Slaa kwa kutekeleza moja ya ahadi zake za kuwapunguzia shida ya maji wakazi wa Gong la mboto; hii itasaidia kuwapunguzia adha akina mama bila kujali itikadi zao za kisiasa; wanabodi ni kawaida ndani JF kuongelewa mabaya ya mtu, nawakumbusha tu tuliteeni na yale mazuri anayofanya kwenye jamii inayomzunguka; BIG UP JERRY!

  Chama
  Gongo la mboto DSM
   
 2. PMNBuko

  PMNBuko JF-Expert Member

  #2
  Sep 23, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 971
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hongereni. Lakini naomba kufahamu, Jerry Slaa ni ndugu wa Dr Slaa au ni majina tu kufanana??
   
 3. c

  chama JF-Expert Member

  #3
  Sep 23, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Jaribu kuwasiliana na molemo atakupa majibu muafaka!

  Chama
  Gongo la mboto DSM
   
 4. Don Mangi

  Don Mangi JF-Expert Member

  #4
  Sep 23, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,206
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Anaitwa Jerry Silaa. . .na Rais wangu anaitwa Wilbroad Peter Slaa.
   
 5. M

  Molemo JF-Expert Member

  #5
  Sep 23, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Anaitwa Jerry Silaa na sio Slaa
   
 6. M

  Molemo JF-Expert Member

  #6
  Sep 23, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Huyu kijana anajisikia sana na anadharau sana watu.Eti anajiandaa kugombea ubunge Ukonga.Hapa ameumia hapati kitu.
   
 7. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #7
  Sep 23, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Kisima chenyewe ni cha kutumia kata?
  Kitawatosha wana Gongo la Mboto wote?
   
 8. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #8
  Sep 23, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,195
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  chama jaribu kutofautisha Shimo la choo na kisima anawatafutia watu kipindupindu
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. a

  ambagae JF-Expert Member

  #9
  Sep 23, 2012
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 1,655
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Eh yaani urais aw Nyumbani kwako unampa mwingine wewe unakuwa nani hapo kwako Makamu aw Rais Au Waziri mkuu
   
 10. c

  chama JF-Expert Member

  #10
  Sep 24, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Tumsifuni kwa mazuri anayoyafanya hakuna binadamu asiyejisikia

  Chama
  Gongo la mboto DSM
   
 11. c

  chama JF-Expert Member

  #11
  Sep 24, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Chadema mnafurahisha sana hivi visima anavyochimba kada wenu Sobodo vina tofauti gani na cha Jerry Silaa?

  Chama
  Gongo la mboto DSM
   
 12. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #12
  Sep 24, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 160
  Pongezi kwake!
   
 13. c

  chama JF-Expert Member

  #13
  Sep 24, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mimi mwananchi wa kawaida mkazi wa Gongo la mboto

  Chama
  Gongo la mboto DSM
   
 14. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #14
  Sep 24, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,195
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Tuna drill na machine. Halafu mkuu wenzako wamesusia bidhaa za USA wewe vipi utaweza kweli? Naomba unitumie ile filamu niicheck mkuu wangu
   
 15. F

  FJM JF-Expert Member

  #15
  Sep 24, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kwa jiji la Dar es Salaam, kuendelea kuwekeza kwenye visima ni fedheha. Ni lini watu hawa watakuwa na maji ndani, na kuondoka na huu mfumo wa pre-industrial revolution?
   
 16. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #16
  Sep 24, 2012
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Haya ni matusi kwa wananchi wa Gongo la Mboto kupewa kisima badala ya kuwekewa bomba la maji,hivi hiki kisima kinaweza hudumia watu wote wa eneo husika?Leo hii mkazi wa Gongo la Mboto anapewa kisima je walioko mbali na hapo watapewa nini kama sio kukejeli watu??
   
 17. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #17
  Sep 24, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,046
  Likes Received: 13,259
  Trophy Points: 280
  Tofauti ni kwamba Sabodo anatumia pesa yake ya mfukoni anatowa msaada kwa sababu Serikali ya CCM imeshindwa kutimiza wajibu wake, na ni haki kuviita visima vya Sabodo, lakini hiki cha Gongolamboto siyo msaada bali ni pesa za walipa kodi hasa wa Manispaa ya Ilala na kamwe huwezi kuita eti ni kisima cha Jerry Silaa. upo hapo?
   
 18. c

  chama JF-Expert Member

  #18
  Sep 24, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Una uhakika kama pesa zilizotelewa ni za halmashauri ya Ilala? jifunzeni kukubali ukweli sio kila kitu ni kupinga

  Chama
  Gongo la mboto DSM
   
 19. c

  chama JF-Expert Member

  #19
  Sep 24, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nenda you tube; I know where my faith stands; I am not gonna caught up with religious haters; the video never change my faith other than making me stronger! I don`t question what you believe or whether you truly understand what is written in bible; so don`t bring that mix to me; give your email I will send the link

  Chama
  Gongo la mboto DSM
   
 20. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #20
  Sep 24, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,046
  Likes Received: 13,259
  Trophy Points: 280
  Sipo hapa kupinga bali kukuelewesha kama uko mis informed, mimi ni mkazi wa Manispaa ya Ilala na ni mdau wa Maendeleo ya Manispaa yetu na kila mwaka ni lazima nipate kitabu chenye majedwali yote ya mapato na matumizi na miradi ya Maendeleo kwa kila kata.

  Sina sababu ya kuwa na chuki yoyote kwa kijana mwenzangu ambaye amechanga karata zake vizuri na kupata wadhifa mzito akiwa na umri mdogo, Jerry Silaa ana nafasi ya kuwin mioyo ya watu wa Gongo la mboto kwa kutumia nafasi yake kama meya kukamilisha mradi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Mombasa mpaka Moshi Bar.

  Kwa mfumo wetu wa local Government Jerry hatahukumiwa na sisi wakazi wote wa Manispaa ya Ilala bali na watu wake wa Gongo la mboto kwa sababu Meya hachaguliwi na Wananchi bali anachaguliwa na madiwani wenzake, akilijuwa hili vyema bado anauwezo wa kufanya kama alivyofanya Basil Mramba ambaye alipeleka maradi wa barabara ya Marangu Tarakea wakati haikupaswa kuwa hivyo. sina tatizo na Jerry.
   
Loading...