IKULU: Rais Magufuli amteua Dkt. Bashiru Ally Kakurwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi

Kwema Mkuu?

Kwa mujibu wa Kanuni za Utumishi wa Umma, Rais ni mamlaka ya nidhamu ya Katibu Mkuu Kiongozi.

Kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma, Katibu Mkuu Kiongozi ndiye Mkuu wa Utumishi wa Umma.

Kwa mujibu wa sheria hiyo pamoja na Kanuni za Utumishi wa Umma, Katibu Mkuu Kiongozi ni mamlaka ya nidhamu kwa makatibu wakuu wa wizara, manaibu katibu wakuu, wakuu wa idara zinazojitegemea, katibu wa bunge, makatibu tawala wa mikoa, mkurugenzi wa uhamiaji, mabalozi, n.k.

Kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma, Katibu Mkuu Kiongozi anaweza kumchukulia hatua za kinidhamu mtumishi yeyote niliyemtaja hapo juu kwa kadri atakavyoona inafaa. Mtumishi au mamlaka yoyote isiyoridhika na uamumzi wa Katibu Mkuu Kiongozi inaweza kukata rufaa kwa Rais.

Naona kama Rais kamteua Dkt Bashiru kuwa Balozi ili kuepusha insubordination. Labda bila kuwa balozi, Bashiru asingeweza kumchukulia hatua balozi yoyote kwa kadri anavyoona inafaa. Other than this sioni sababu nyingine ya msingi. Historia inaonyesha kuwa waliowahi kushikilia nafasi hiyo walikuwa mabalozi pia possibly for the very same reason.

Swali linakuja: kati ya Katibu Mkuu Kiongozi (ambaye pia ni Cabinet Secretary) na Balozi who is the most powerful? Mie nilidhani Katibu Mkuu Kiongozi ndiye kinara wao lakini kwa appointment ya leo inaonyesha wazi kuwa hana lolote kwa balozi unless nae awe balozi. Hii inachanganya ukiangalia jinsi appointments za mabalozi zinavyofanyika siku hizi.

Mkuu umepotea kichizi. Mpaka tukafikiri ushaukwaa uteuzi na wewe.

Kama Katibu Mkuu Kiongozi ndiye head of civil service, regardless ya ubalozi, then it doesn't matter kama Katibu Mkuu Kiongozi ni balozi au si balozi.

Yeye kama head of civil service, yuko juu ya mabalozi, by virtue of being head of civil servive.

Mbona Katibu Mkuu kiongozi si Jaji, lakini ni mkubwa wa majaji kwa sababu yeye ni head of civil service.

Je, Bashiru apewe ujaji pia? Atapewa vyeo vingapi?

Hapa kuna mawili.

Ama kuna mkakati maalum wa kumpa diplomatic immunity, ama ni mbwembwe tu za kuzawadiana vyeo.

Suala la insurbodination silioni, kwa sababu, sawa, tulikuwa na mabalozi Sefue, Lumbanga na Rupia.

Lakini pia tumekuwa na kina Timothy Apiyo, Philip Luhanjo walikuwa Makatibu Wakuu Viongozi bila kuwa mabalozi.
 
..unamaanisha mahakimu na majaji ni civil servants au watumishi wa serikali?
Civil servants ambayo msemaji wa kwanza anakataa kuwa siyo; yeye kwake civil servants ni wafanyakazi wa serikali...Get ypur facts right guys...Pamoja na hayo yote concept ya institution siyo kwamba moja jumlisha moja ni mbili...Wakati mwingine kuweka utendaji vizuri unarekebisha tu sheria ambapo kwa sasa sheria yetu haitutofautishi sisi sote ni watumishi wa umma na unaweza pelekwa kokote kama sifa zina ruhusu
 
Wakuu someni comments kwenye huu uzi kwa makini ndipo mtajua hii nchi walio wengi hawajui wanataka nini na uelewa mdogo kuhusu mifumo ya kiutawala.

Aidha wengine wanafahamu ila tu wameathiriwa na harakati za kisiasa hivyo wamekuwa watu wa negativity wakiweka kando ufahamu na taaluma zao.

Kuna elimu kubwa sana kwenye mada kama hizi ikiwa hutokuwa mvivu.
 
Ubalozi angepewa mwingine eroo,unashindilia watu dabo vyeo yanini?? Polepole naye ktb mwenezi ubunge wann tena ??
 
Civil servants ambayo msemaji wa kwanza anakataa kuwa siyo yeye kwake civil servants ni wafanyakazi wa serikali...Get ypur facts right guys...Pamoja na hayo yote concept ya institution siyo kwamba moja jumlisha moja ni mbili...Wakati mwingine kuweka utendaji vizuri unarekebisha tu sheria ambapo kwa sasa sheria yetu haitutofautishi sisi sote ni watumishi wa umma na unaweza pelekwa kokote kama sifa zina ruhusu
..swali langu ni dogo sana.

..Je, mahakimu na majaji ni civil servants kwa maana watumishi wa serikali?
 
Dr Bashiru is not qualified for that post, at least on how succession planning goes in unitary government system na uwezi kupewa hiyo nafasi if you are not a qualified top spy nor having held other senior civil services post.

At the same time naona logic ya Magufuli kumteua Dr Bashiru, civil services ya Tanzania ni ovyo sana in administering party manifesto. Kwa fikra za raisi kwa kumteua Dr Bashiru he will push more other senior civil servant.

But then that role is bigger than that maana kuna aspects za international relations and national security issues.

The bottom line TISS inapwaya kwenye kuandaa viongozi, safu ya juu nchi kama UK tulipo-copy mfumo wa serikali yetu makatibu wakuu wote + senior civil servant ni watu ambao wanaelewa strategic operation zao kuanzia juu mpaka chini na control measures.

Na kwenye kupanda kwao ukifikia level za kuitwa senior civil servant unakuwa afisa usalama maana unajukumu la kutunza siri za nchi.

Sisi tunaokoteza tu watu at senior post, most lack the skills to implement a strategy fit for the party manifesto, can’t execute a mission efficiently nor pay attention to the manifesto. Nadhani Magufuli kaona mapungufu hayo and he thinks Bashiru might get things moving fast.
Mfumo ulivurugwa pale chama na serikali vilipotengenishwa na kuleta vyama vingi chuo cha kivukoni na Mzumbe vilikuwa vinafanya kazi yake vizuri....Siyo mbaya we learn through mistakes...Leadership imekuwa shida sana kwa watu wetu kwakua wengi hawana necessary skills only because hakuna system rasmi ya kuandaa viongozi...Nadhani hili ni muhimu kuangaliwa upya.
 
..swali langu ni dogo sana.

..Je, mahakimu na majaji ni civil servants kwa maana watumishi wa serikali?
Jamani unataka nikujibu unachotaka kusikia? Have said a third time now ni civil servant and that doesnt mean watumishi wa serikali ni watumishi wa umma
 
Jamani unataka nikujibu unachotaka kusikia? Have said a third time now ni civil servant and that doesnt mean watumishi wa serikali ni watumishi wa umma
..Je, Katibu Mkuu Kiongozi anaweza kumuadhibu Hakimu au Jaji?
 
EMT,

..kuna mabalozi ambao huteuliwa toka nje ya serikali, kama Balozi Masilingi, Balozi Paul Bomani, Balozi Omar Mapuri, ... je hao nao mamlaka yao ya nidhamu ni Chief Secretary, au wanaweza kuchukuliwa hatua za kinidhamu na Chief Secretary?
Labda hii makala iliyoandikwa na Ndg Abbas Mwalimi mwaka 2019 itasaida kuelewa zaidi juu ya uteuzi na aina za mabalozi.

ULIVYO UTARATIBU WA KUTEUA MABALOZI

Katika muktadha wa uteuzi wa mabalozi kuna mabalozi wa aina mbili, mosi mabalozi wanaoteuliwa kutokana na utashi wa kisiasa na pili, wanaoteuliwa kutokana na weledi wao. Mabalozi wanaoteuliwa kutokana na utashi wa kisiasa huwa ni pendekezo la Rais moja kwa moja kutokana na kuwa na sifa za kuteuliwa wakati wale wanaotokana na weledi, ni waliotokea Wizara ya Mambo ya Nje na hupatikana kutokana na kufikia ngazi ya mwisho katika vyeo vya utumishi wa maofisa wa wizara hiyo.

Vyeo hivi huanzia katibu wa tatu (kwa sasa nadhani haipo), hupanda na kuwa katibu wa pili, katibu wa kwanza, mshauri, mshauri mwandamizi na mwisho kuwa afisa mkuu wa juu. Afisa mkuu wa juu (MPP) ni ngazi ya mwisho ya utumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje ambapo baada ya hapo inatarajiwa mtumishi huyo kuweza kuteuliwa kuwa balozi kama hajafika umri wa kustaafu. Mabalozi wanaotokana na weledi, uteuzi wao hutokana zaidi na mapendekezo ya Wizara ya Mambo ya Nje.

Uteuzi hufanyika ifuatavyo; kwanza mawasiliano hufanyika kwa siri baina ya wakuu wa nchi au serikali juu ya nia ya kumteua mtu fulani kuwa balozi. Kama ni balozi aliyetokana na utashi wa kisiasa, jina hupendekezwa kwa siri kutoka Ofisi ya Rais na kama ni kutoka wizara ya mambo ya nje jina hupelekwa kwa rais kwa siri. Kama Balozi mtarajiwa ametokana na kundi la kwanza la wanaotokana na utashi wa kisiasa kwa maana ya Rais kuona huenda mtu huyo atamfaa na baada ya kushauriana na timu yake ya ushauri, jina hupelekwa idara ya usalama wa taifa ili kumfanyia uchunguzi mtajwa huyo. Wakati huo huo jina hilo huwa limefika katika idara za upelelezi za nchi ambayo balozi mtarajiwa hutazamiwa kutumwa huko ili wao pia wamfanyie uchunguzi.

Endapo usalama watajiridhisha kwamba mtu huyo anafaa kuwa balozi, jina litarudishwa kwa Rais tayari kwa hatua zinazofuata. Kwa upande wa nchi ambayo jina hilo limepelekwa, nao watakapokuwa wameridhika na mtajwa huyo baada ya kufanya uchunguzi wao wa kina, wataridhia kwa njia za kidiplomasia. Kitendo hiki huitwa kwa lugha ya kilatini agrema kwa mujibu wa Ibara ya nne ya Mkataba wa Vienna wa Mwaka 1961.

Endapo nchi inayotarajiwa kumpokea balozi mtarajiwa itaona mtajwa huyo haifai, itafanya mawili kati ya yafuatayo: Mosi nchi hiyo itatoa taarifa juu ya kutomkubali mtajwa huyo kuwa balozi katika nchi yao kwa njia ya kidiplomasia. Kwa mfano, iliwahi kutokea katika nchi fulani mteule wa ubalozi alikuwa mwandishi wa makala na aliwahi kuandika makala iliyoielezea vibaya nchi aliyotarajiwa kupelekwa. Ile nchi iliyotarajiwa kumpokea balozi ilituma makala aliyowahi kuandika mteule huyo kuisema nchi hiyo, hapo nchi iliyomteua balozi ilijua kuwa jibu ni kuwa mtu huyo ‘hakubaliki.’

Lakini pili, nchi hiyo itakaa kimya bila ya kutoa taarifa yoyote. Zamani baadhi ya nchi zilikuwa zikitoa taarifa, lakini siku hizi hilo halifanyiki na badala yake nchi huamua kukaa kimya. Kitendo hiki cha kukaa kimya moja kwa moja huifanya nchi ambayo imepanga kumtuma balozi huyo katika nchi hiyo kutambua kuwa mtajwa huyo amekataliwa au persona non grata kwa Kilatini.

Kimsingi nchi inayotarajiwa kumpokea balozi haipaswi kueleza sababu za kumkataa balozi mtarajiwa kama ilivyoelezwa kwenye Ibara ya Nne ya Mkataba wa Vienna. Hilo hubaki kuwa kazi ya nchi iliyopendekeza jina kutafuta sababu za balozi mteule kukataliwa ama kumtafutia nchi nyingine au kumbakiza nchini mwao.

Ifahamike vema kuwa, wakati huo huwa hakuna anayejua zaidi ya Idara ya Usalama wa Taifa, Ofisi ya Rais na Waziri wa Mambo ya Nje. Maana yake ni kuwa hata huyo mtarajiwa anakuwa hajui kuwa yeye amependekezwa kuwa balozi na anafanyiwa uchunguzi. Ingawa hutokea kwa baadhi ya watumishi ambao siyo waaminifu wanapobahatika kujua huanza kumdhihaki aliyetarajiwa kuwa amekataliwa, lakini pia hali huwa mbaya pale muhusika aliyekuwa akijua kuwa alikuwa akichunguzwa ili ateuliwe kuwa balozi anapotajwa kuwa amekataliwa. Ndiyo sababu kazi hizo huwa za siri mno.

NAMNA NCHI INAVYOJUA KAMA MTAJWA AMEKATALIWA

Kuna kipindi ambacho nchi ikiona kimya kimetawala hujua kabisa mtajwa amekataliwa. Ikipita zaidi ya miezi mitatu na nchi inayotarajiwa balozi atumwe kwao haijasema kitu nchi iliyoteua jina hutambua kabisa kuwa mteule amekataliwa, hivyo hujipanga upya. Inapotokea nchi hizo kwa pamoja zimeridhishwa na balozi huyo mtarajiwa hatua nyingine hufuata.

Hapa ndipo jina la mteule huyo hutajwa kwa tangazo toka Ofisi ya Rais kupitia Katibu Mkuu Kiongozi. Kwa wale wanaotokana na weledi, majina hupendekezwa na wizara na baadae kupelekwa kwa Rais kwa ajili ya utaratibu zilizoelezwa awali.

Swali la msingi la kujiuliza ni kwamba, kwa nini baadhi yao wateuliwe kuwa mabalozi na wabaki nchini? Tufahamu kuwa muundo wa wizara za mambo ya nje duniani hufanana isipokuwa huweza kuwa na tofauti ndogo sana kutokana na mfumo wa utawala wa nchi husika.

Hivyo sababu ya kuwateua mabalozi na kuwabakisha wakifanya kazi nchini ni kutokana na kwamba mabalozi mbalimbali waliopo nchini hufanya kazi zao kupitia idara za kikanda zilizopo wizara ya mambo ya nje na pia, kikanuni mabalozi hawafanyi kazi na watu wengine moja kwa moja isipokuwa mabalozi wenzao ama watu wenye hadhi ya ubalozi. Hapo ndipo inapokuja sababu ya kuwateua mabalozi kufanya kazi nchini kwa lengo la kuongoza idara za kikanda kama vile Afrika, Mashariki ya Kati, Ulaya, Amerika, Asia na Australasia zilizopo katika wizara ya mambo ya nje ya Tanzania.

Hivyo Stephen Patrick Mbundi aliyekuwa Mkurugenzi Idara ya Ulinzi, Siasa na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na wengine Ali Sakila Bujiku na Musa Lulandala waliokuwa Wasaidizi wa Rais, wameteuliwa kuwa mabalozi na watabaki nchini kama alivyosema Katibu Mkuu Kiongozi ili wafanye kazi na mabalozi wanaowakilisha nchi zao Tanzania. Lakini watu wanaweza kujiuliza kwa nini maelezo yaliyotolewa na katibu mkuu kiongozi yalieleza kuwa waheshimiwa Mbundi, Bujiku na Lulanda wamepandishwa vyeo kuwa mabalozi?

Hii inatokana na utaratibu wa vyeo vya utumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje kwamba, hawa watatu walipanda mpaka kufika ngazi ya ofisa wa juu kabisa wa wizara (MPP) na kwa vyeo vya utumishi wa wizara hiyo, MPP ni cheo cha mwisho hivyo baada ya hapo hutarajiwa wahusika kuteuliwa na Rais kuwa mabalozi ndiyo maana taarifa ile ilieleza kuwa wamepandishwa vyeo kuwa mabalozi kwa sababu hawa ni mabalozi wanaotokana na weledi.

Chanzo: Usiyoyajua kuhusu uteuzi wa mabalozi wa nchi
 
..Je, Katibu Mkuu Kiongozi anaweza kumuadhibu Hakimu au Jaji?
Kiranga kaandika hapo juu....Na hapo juu kidogo soma notes za institution nilizoweka...Flow of power and information ipo structured but that does not alter the rules and regulations in place ambazo pia zina flow kwakufuata structure...hapo sasa ni kama unaniuliza Judge mkuu anayemwapisha raisi anaweza kumwajibisha?

I said, I repeat; institutions are note operating in the manner of one plus one equals two...It depends on the rules and regulations in relation to the organization structures therewith these rules and regulations flow...Ukirudi kwenye establishment Act ya utumishi wa umma utakuta mamlaka ya uwajibishaji ni ipi...Mimi pia siyo mwanasheria lakini nina knowledge in institutions from economic perspectives na hasa New Institutional Economics...Inapokuja issues za legality na legitimacy nina limitations
 
Binafsi mm nipende kumpongeza Mhe Doctor JPM kwa alichokifanya kwa uteuzi wake aliofanya siku ya leo tarehe 26th February 2021
IMG-20210226-WA0285.jpg
 
Mkuu umepotea kichizi. Mpaka tukafikiri ushaukwaa uteuzi na wewe.

Kama Katibu Mkuu Kiongozi ndiye head of civil service, regardless ya ubalozi, then it doesn't matter kama Katibu Mkuu Kiongozi ni balozi au si balozi.

Yeye kama head of civil service, yuko juu ya mabalozi, by virtue of being head of civil servive.

Mbona Katibu Mkuu kiongozi si Jaji, lakini ni mkubwa wa majaji kwa sababu yeye ni head of civil service.

Je, Bashiru apewe ujaji pia? Atapewa vyeo vingapi?

Hapa kuna mawili.

Ama kuna mkakati maalum wa kumpa diplomatic immunity, ama ni mbwembwe tu za kuzawadiana vyeo.

Suala la insurbodination silioni, kwa sababu, sawa, tulikuwa na mabalozi Sefue, Lumbanga na Rupia.

Lakini pia tumekuwa na kina Timothy Apiyo, Philip Luhanjo walikuwa Makatibu Wakuu Viongozi bila kuwa mabalozi.
Nipo Mkuu,

It could be any reason. Ingekuwa poa kama mteuaji angewaleza wapiga kura wake sababu za kumteua balozi.

Sina uhakika na Timothy Apiyo ila kwa mujibu wa tovuti ya Katibu Kiongozi Philip Luhanjo alikuwa balozi. Unless kama aliteuliwa baada ya kustaafu.
 
Kwa hiyo anakuwa Katibu Mkuu wa Chama na Katibu Mkuu Kiongozi kwa wakati mmoja au anaacha kuwa katibu mkuu wa CCM?

Vipi kuhusu muongozo wa utumishi serikalini unaotenganisha mambo ya chama na utumishi wa umma serikalini?

Hata kama atajiuzulu Ukatibu Mkuu CCM, huu uteuzi unaonesha kwamba utumishi serikalini unaenda kupelekwa kichama chama zaidi.

Kinachodhihirika sasa ni mpango maalum wa kuua nguvu ya sheria, kanuni, miongozo na taratibu NA kuimarisha mamlaka ya mkuu katika masuala yote ya kiutendaji.

Yeye ndiye mwenye kauli ya mwisho kwenye uteuzi wa yeyote serikalini, kwenye chama na, sasa, hata bungeni akitaka. Teuzi zake hazihojiwi na yeyote yule. Na anaweza kumtimua yeyote, wakati wowote na kwa sababu yoyote kadiri busara yake itakavyomuongoza.

Yeye ndiye anayeamua miradi na vipaumbele vya kutekelezwa. Yeye ndiye anayetoa fedha za maendeleo na matumizi ya kawaida kwa kadiri anavyotaka na kwa wakati anaotaka.

Ana absolute power.
 
Back
Top Bottom