Pongezi John Mnyika kutumbua jipu la Salma Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pongezi John Mnyika kutumbua jipu la Salma Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mpayukaji, Apr 19, 2012.

 1. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #1
  Apr 19, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  [h=3]Source: mpayukaji blog[/h]

  [​IMG][​IMG][​IMG]


  Blogu hii imekuwa ikifichua uoza mbali mbali unaofanywa na wake wa wakubwa. Ilifikia kipindi nikaonekana kama nina chuki binafsi na mama Salma Kikwete. Hii ilitokana na kushupalia uchafu anaofanya kwa kutumia NGO yake ya WAMA ambayo mimi huiita MAWAWA yaani Maulaji ya Wake za Wakubwa. Kimsingi, uanzishwaji wa NGO za wake wa wakubwa hasa marais wanapoingia madarakani ni aina mpya ya ufisadi unaopaswa kupigwa vita kwa nguvu zote. Alianza Anna Mkapa (Mama Tamaa) na sasa anaendeleza Salma Kikwete. Kinachofanyika ni kujitafutia utajiri kwa njia haramu kwa kutumia ikulu.
  Mnyika akiaririwa na vyombo vya habari akisema, “Mheshimiwa Spika naitaka serikali itoe tamko hapa kuwa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) inayoongozwa na mke wa rais itakuwa ya kwanza kuchunguzwa na kuwajibishwa kutokana na kuwa ilihusika katika kipindi cha uchaguzi mwaka 2010 kwa kufanya kampeni.”
  Sambamba na kumpongeza Mnyika, nawapongeza wabunge wote hasa Deo Filikunjombe (CCM), Ludewa, Tundu Lissu (CHADEMA) Singida Mashariki na Zitto Kabwe (CHADEMA) Kigoma Kaskazini na wengine wote walioshupalia upanya na umchwa unaoendeshwa na mawaziri wetu. Kimsingi, kwa shinikizo na azimio lao tutajua mbivu na mbichi za Jakaya Kikwete na Mizengo Pinda. Haya shime msikate tamaa wala kulegeza kamba tunaweza kulichinja joka lililowashinda CCM kulichuna ngozi.
  kuna haja ya kuwapa shime wabunge wa CCM kuachana na kutumika kama mihuri ya ufisadi. Kama rais atawapuuzia waachane na CCM. Maana wanavyo vyama mbadala kuhamia na kufanya kile kilichofanywa na Wakenya, Wamalawi na Wazambia walipovipiga buti vyama vyao tawala.

  [​IMG]
   
 2. u

  umsolopagaz Member

  #2
  Apr 20, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ....mbunge wa ccm anaongea dhidi ya madudu ya serikali ya chama chake bungeni...dhidi ya viongozi wenzake wa chama chake...dhidi ya mwenyekiti wake...je...wa upinzani mwaliweza hilo? au somo la hamad rasheed limeeleweka?
   
 3. M

  MAPIKU New Member

  #3
  Apr 21, 2012
  Joined: May 5, 2010
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hongereni wabunge kwa kuondoa u mimi wa muda mrefu,msiogope sisi wana nchi tupo nyuma yenu
   
 4. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #4
  Apr 21, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mpinzani mnafiki na kibaraka wa magamba Kamwe hatoweza kusema ulichokomenti lakini mpinzani kwa ukweli siku zote hawezi kuhofia nafasi yake kisa madudu ya viongozi wake. Viva Hamad Rashid, Viva Zito, Lissu etal.
   
Loading...