PONGEZI: Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam yamshukuru Mkuu wa Wilaya ya Temeke kwa Jitihada za upatikanaji wa Vitendea Kazi

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
PONGEZI: Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam yamshukuru Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Jokate kwa Jitihada za upatikanaji wa Vitendea Kazi kwa Jeshi la Polisi

Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Jumanne Mulilo amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Jokate Mwegelo baada ya kujitoa na kupigania upatikanaji wa vitendea Kazi katika Jeshi la Polisi Wilayani Temeke, ambapo leo kupitia Kampuni ya Hero moto Tanzania wamekabidhi Pikipiki za kisasa 5 kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke. Pikipiki hizo ni mahususi kwa Kazi za kipolisi ili kuwarahisishia utendaji Kazi wao katika Jamii.

"Nampongeza sana Jokate, kwa kweli ni Mkuu wa Wilaya anayejitahidi sana na ameibadilisha sana Temeke, na uhalifu umepungua kwa asilimia kubwa lakini kingine ni kwamba amewarahisishia Polisi wangu kea kupata vifaa kwa ajili ya Kazi zao" - Jumanne Mulilo Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam



#TemekeSalama
 
Back
Top Bottom