Pongezi CCM kwa Kuushinda upinzani kwa sasa

Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Jul 5, 2007
5,185
56
Kwa mara nyingine tena inabidi niukubali ukweli na kumeza uchungu wa kupoteza nafasi ya kuleta mabadiliko nchini.

Ni kweli kuwa mimi nimeweka wazi hapa kuwa ni mpinzani wa CCM na sitangojea kwa siku ambayo kutakuwa na serikali nyingine ambayo inajali raia wake tofauti na hii ya ccm ambayo inauza nchi kwa wazungu.

Kwa mara nyingine, nakubali kushindwa na mbinu za ushindi wa ccm na hivyo nameza tena kidonge cha uchungu kama nilichomeza mwaka 1995 waliposhindwa Mrema na Seif Shariff kwenye uchaguzi, mwaka 2000 alivyoshindwa Lipumba, na mwaka 2005 wapinzani wengi walivyoshindwa vibaya sana kwenye uchaguzi.

Katika siasa, mafanikio hujengwa na kisha kuendelezwa kwa kushikilia momentum iliyopo. Mwanasiasa au chama cha siasa akipoteza momentum maisha yake kisiasa yanakuwa matatani.

Upinzani Tanzania ulikuwa umepata momentum nzuri sana ya kuleta mabadiliko kwenye sekta ya madini. Zitto aliomba iundwe kamati huru ya bunge ambayo ingekuwa na nguvu zaidi za kupata ukweli na kuleta mabadiliko ya kweli.

Wananchi wengi walikuwa wameanza kukumbwa na momentum hii na wakafanya ambacho kilikuwa hakijafanyika nchini kwa muda mrefu sana - kuzomea viongozi wa ccm.

Kwa uwezo mkubwa sana wa kisiasa, CCM wamechukua hiyo momentum kwa kuunda kamati ambazo hazitafanya chochote katika kile watu wengi Tanzania walitaka kifanyike. Hebu soma haya maneno toka katika tamko la ccm kuhusu kamati ya Kikwete iliyoundwa:

"Ni vema ikaeleweka kuwa tume huundwa pale ambapo imethibitika kuwa kuna kosa lililotendeka au athari za wazi zimeonekana kwenye utendaji wa chombo cha serikali, lakini kamati huundwa pale ambapo mwelekeo mpya unahitajika katika utendaji wa chombo cha serikali,

"Tunapenda wananchi waelewe kuwa, alichounda rais ni kamati ya kuangalia upya sera, sheria na mikataba ya uchimbaji madini na si tume ya kuchunguza mikataba ya uchimbaji madini,"

Haya ni maneno ya Chiligati. Kilichoundwa na Kikwete, sio cha kuchunguza yaliyotokea, bali ni kufanya kile ambacho kimefanywa na kamati ya mboma, masha, na zingine nyingi tu--- kupendekeza maoni ambayo rais anaweza kuamua kuyapuuzia kama alivyofanya kwenye kamati zilizopita bila kujali mamilioni yanatumika katika kamati hizo.

Uteuzi wa Zitto kwenye hii kamati, umetoa momentum toka kwa upinzani na mimi nakiri kuwa hapa ccm wameshinda kwa sasa. Ushindi wao wa kwanza ulifikiwa juzi baada ya tarehe 25/11 ambayo iliwekwa kuwa siku ya mwisho (deadline) kwa ccm kushughulikia ufisadi, wizi na yote la sivyo hatua zitachukuliwa kupita bila chochote kutokea.

Kinachoonekana sasa ni mgongano tu ndani ya upinzani na haionyeshi kama kuna chochote kitatokea kwa sasa. Sijui kama Zitto alitegemea hili alivyokubali na kusisitiza kuwa kwenye kamati ambayo haina nguvu yoyote kisheria.

Kwa sasa, nameza kidonge cha maumivu na kukaa chini kujipanga upya kwa ajili ya next strategy. CCM wameshinda kwa sasa na mimi binafsi nawapongeza kwa strategy nzuri. Kwa vile kulialia sio sehemu ya maisha yangu, nitaendelea kusaka kwa nguvu zote hii mikataba ya serikali na kuitunza mpaka siku nitakapohakikisha fisadi wa mwisho akiwekwa Keko.

Hongera ccm kwa ushindi. Endeleeni kuuza nchi tu mwaya kwa vile mnaweza. Kama vile makocha wa timu wanavyopongezana baada ya mechi, na mimi nawapa pongezi kwa hili. Kwa kweli hapa mmecheza.

Tutakutana tena next time tukiwa tumejiandaa vyema.
 
You can loose the battle but win the war! Cha muhimu ni kuwa na uwezo wa kureflect na kujua makosa uliyoyafanya na kutoyarudia I think that you are on the right path.
Fool me once shame on you, fool me twice, shame on me!
Let's hope Chadema hawatakuwa tayari tena kukubali mialiko ya kukaa kwenye kamati kabla ya kujua kamati inafanya kazi gani,maani hiyo itakuwa sasa SHAME ON THEM!:(
 
Zitto siyo aliyeleta haya bali ni wananchi wenye njaa. wakina zitto walikuwa ni wapelekaji habari tu .Njaa haiwezi kuzimwa na ujanja ujanja kama huu. Hivyo mpiganaji usikate tamaa kabisa soon watatokea wakina zito 100 na watashindwa kuunda kamati kumi kuwadilute. hapo ndipo moto utawaka
 
Kweli Shalom,

Kukiwa na Zitto wengi itakuwa vigumu kuunda kamati nyingi za kuwamaliza. Ni kweli Zitto amefanya kazi nzuri na ngumu na nchi ikafanikiwa kupata mkataba wa Buzwagi, Richmonduli, na mingine mingi iliyopita hapa au ambayo tumeitunza tunasubiria kuiweka mambo yote yakiwa tayari. Kwa hili na mengine mengi anastahili pongezi - yaani yale mambo ya timu ikifungwa, ah wametufunga ila uliona ile free kick ya Gaga?

Hata hivyo kwa hili la kamati, ccm wameshinda maana wamechukua momentum toka kwa wapinzani kwa kuunda kamati ambayo haina nguvu yoyote ya kisiasa zaidi ya kufanya kazi kwa ridhaa ya raisi ambaye amepuuzia kamati nyingine mamia zilizotoa mapendekezo anayotaka sasa hivi.

Kulingana na taarifa ya ccm, watanzania hawatajua kile walitaka kujua kuhusu Buzwagi and the like. Na baada ya kupita tar 25. Hii issue ni kama vile imefia kwenye hiyo kamati.

Kwa hili, nawapongeza ccm kwa ushindi maana hapa wamepiga bonge la bao na wanastahili pongezi kwa kushinda kisiasa.
 
Binafsi naamini kabisa kuwa goli ambalo CCM wanaamini wamefunga na linesman wao kapepea kibendera kuelekeza mpira kati litajulikana baada ya muda kuwa ni goli la kuotea. Ni vizuri washangalie sasa lakini mwamuzi wa kweli (wananchi) watakapoona vizuri watafuta bao hilo!

Jambo moja ambalo wapinzani bado halijawaingia akilini kuwa CCM inaangalia kila kitu kwa mwanga wa "manufaa kwa CCM". Hivyo watafanya lolote, watasema lolote ilimradi tu wananchi wasiichukie CCM. Wapinzani wao wamekaa na hii dhana ya "maslahi ya Taifa" kiasi kwamba hawataki kuingiza siasa au mikakati ya kisiasa (kama wafanyavyo CCM) na hapa ndipo kosa kubwa la upinzani linapotokea.

a. Zitto alipofungiwa walikuwa na uchaguzi wa kuvuta watu kujiunga na upinzani hawakufanya hivyo kwa sababu "hatutaki kulifanya suala hili liwe la kisiasa". Matokeo yake ni kugaragazwa kwenye sanduku la kura kwani CCM walipoenda vijijini pamoja na kuzomewa waliendelea kupepea bendera zao za kijani na njano zenye alama za jembe na nyundo! Waliendelea kuwavutia wananchi kuwa CCM ndiyo chama bora n.k Wapinzani wakabakia na kibwagizo cha "maslahi ya Taifa" wakati CCM wanaimba na kucheza "maslahi ya Taifa kupitia Maslahi ya CCM".

b. Suala la kamati zilipoundwa wapinzani wakakurupuka kushabakia walioshabikia na wale waliopinga wakatoa sababu za kitoto. Kudai ni kamati ya mafisadi na kwanini "tushirikiane nao" zilikuwa ni hoja dhaifu ambazo ziliwapa mwanya CCM kuonesha udhaifu wa upinzani. Kama MwK alivyosema hapo juu CCM wakaunda hizi Kamati siyo kwa ajili ya madai yaliyoenea juu ya Richmond na Madini bali kupangua hoja kwa kujenga hoja isemayo "Rais anajali madini na matatizo yaliyoko kwenye madini ndio maana ameunda kamati yake". CCM wakajitokeza kufurahia na kushangilia, wakamsifia Rais na kumwimbia nyimbo. Wapinzani hawakua wamepigwa na nini lakini waliposhtuka walijikuta wanalazimika kukaa kwenye kikao cha dharura! CCM wakakunja nne kuchekelea.

c. Zitto ikaamuriwa aendelee kukaa kwenye Kamati akitarajia kutetea "maslahi ya Taifa"... tatizo ni kuwa atagundua kuwa "maslahi ya Taifa" hayamo kwenye jina la "Kamati ya Rais" bali yamo kwenye uwezo na nguvu za Kamati hiyo. HIyo kamati kimsingi imekuwa kama picha ya simba aungurumaye ambaye ametoa meno na manyoya yamemsimama, simba huyo anapitishwa kwa watoto kuwatishia... wao wanabaki wanacheeeeka!

So, CCM wamewashinda wapinzani kama mchezo wa draft au chess; kama ingekuwa draft basi hapa ndipo mtu kaliwa "double" au hata triple" na kilichobaki ni mtu kuvishwa king! Na kama ingekuwa chess one more move wapinzani watakuwa kwenye check mate!

Wapinzani lazima wabadilike na kuanza kuangalia kila wakifanyacho kwa mtazamo wa kisiasa pia na watumie mbinu gani ili wanapotetea maslahi ya Taifa, na maslahi ya upinzani (kujiimarisha na kujijenga, kukubalika na kupendekea) yanaongezeka. Vinginevyo, wao watapiga kelele lakini kinachopendwa na kuzidi kujengwa ni CCM. Kama hamuamini subirini ripoti ya BoT mtashangaa jinsi gani ambavyo haitawapa credit wapinzani! I can see the spins from Daily News, Majira na wadogo zao.. wapinzani itabidi waitishie mkutano wa waandishi wa habari kudai credit!!!
 
Lakini mwanakijiji,

hata kama bao ni la kuotea, nani ana uwezo wa kulibadili? Katika hili mimi nakubali kushindwa na nawapongeza washindi kwa hili.

Political Strategy yao hapa ni nzuri na wanastahili pongezi. Nina hakika kabisa kuwa hili ni wazo la wanaccm wenye akili kina FMES and the like na wala sio Kingunge na Makamba.

Yatakuwa yale yale ya goli la Maradona lakini watu weeeeeeeee ishatoka hiyo.

Hakuna cha deadline ya November 25th wala nini!
 
Y'all are whining too much...
And didn't one of you start a thread about whining or stop whining and do some' bout or some' like that...geeeez...y'all are cry babies...i mean big babies
 
Y'all are whining too much...
And didn't one of you start a thread about whining or stop whining and do some' bout or some' like that...geeeez...y'all are cry babies...i mean big babies

Ngabu,

Giving shout aint whining!

CCM played this game well and we give shout to 'em all winners here.

That's all!
 
Y'all are whining too much...
And didn't one of you start a thread about whining or stop whining and do some' bout or some' like that...geeeez...y'all are cry babies...i mean big babies

mzee sasa na wewe una whine about whiners... so you accuse us that which you are doing.. hata hivyo wengine tunakubali ukweli kuwa CCM kwenye hili la madini wamewapiga bao wapinzani tena la kisigino!
 
He he Mkjj inanikumbusha post yako ya tukubali yaishe.
Mechi haijaisha bado lakini ndio watu wanaenda half time.
 
Unajua, goli la half time unaweza kulishangilia na unaweza kulilinda hadi mwisho... CCM tunawapongeza kwa kuongoza hadi halftime..swali ni je wapinzani wataamka ngwe ya pili au wanasubiri bado la dakika za "lala salama"..
 
Wanasubiri kusaidiwa na pepo zinazovuma kutoka kaskazini mwa uwanja kusukuma mashambulizi.
 
Wanasubiri kusaidiwa na pepo zinazovuma kutoka kaskazini mwa uwanja kusukuma mashambulizi.

Icadon,

I pray unachosema kitokee kuwa kweli. Tatizo ni kuwa muda si mrefu mvua itaanza kunyesha na hiyo ritraktabo ruuf itabidi iwekwe kwa hiyo pepo za kaskazi zitaisha right away!
 
mzee sasa na wewe una whine about whiners... so you accuse us that which you are doing.. hata hivyo wengine tunakubali ukweli kuwa CCM kwenye hili la madini wamewapiga bao wapinzani tena la kisigino!

Duh! unajua wahenga walisema mimi (Nyani) sioni kundule....kwikwikwiiiiii...hawakukosea!!!
 
Kwa sasa, nameza kidonge cha maumivu na kukaa chini kujipanga upya kwa ajili ya next strategy. CCM wameshinda kwa sasa na mimi binafsi nawapongeza kwa strategy nzuri. Kwa vile kulialia sio sehemu ya maisha yangu, nitaendelea kusaka kwa nguvu zote hii mikataba ya serikali na kuitunza mpaka siku nitakapohakikisha fisadi wa mwisho akiwekwa Keko.

Very interesting, tena indeed!
 
Maslahi ya Taifa vs Maslahi ya Chama!

Niliwahi kusema kwamba swala la muungano wa wapinzani lilikuwa na matatizo tangu mwanzo. Mwanakijiji aliwahi kusema na bado amekuwa akirudia kwamba wakati wa mikutano ya Zitto baada ya kufungiwa, wapinzani walitakiwa watumie mikutano hiyo kupata wanachama wapya. Swali ni kwamba: Je, wananchi wangeambiwa wajiunge na chama kipi? Maana kwenye hiyo mikutano kulikuwa na viongozi wa vyama vinne (Chadema, TLP, NCCR Mageuzi na CUF). Hapo kulikuwa na kosa la kiufundi kubwa na hivyo ingekuwa ni ngumu sana kupata wanachama, utawaambia wajiunge na chama kipi?

Kauli ya Zitto kuendelea kutetea maslahi ya Taifa inazidi kumaliza upinzani na itazidi kuubomoa kwa nguvu zote. Nimesoma mahojiano yake na gazeti la Raia Mwema, amerudia kauli yake aliyoitoa Shinyanga wakati akiwa kwenye tume ya Wangwe, alimwambia mwandishi wa habari kwamba hana mpango wa kugombea tena Ubunge jimboni kwake Kigoma Kaskazini hapo itakapofika 2010. Lakini swala hilo lilipoletwa hapa kuna baadhi ya watu walikanusha kwa nguvu zote na ndipo baadhi ya members walipokuja na ushahidi kwamba Mh Zitto alisema. Zitto alikuja akatoa ufafanuzi, kwamba kilichoandikwa gazetini haikuwa official statement bali aliongea na huyo mwandishi pembeni na mwandishi huyo akapeleka kwenye gazeti lake na ikawa ni big news.

Nina swali moja kwa Mh. Zitto, hivi ni kwanini anapokuwa kwenye hizi kamati teule za Rais huwa anatoa kauli zenye utata? Juzi amerudia tena same statement na akasema kazi atakayofanya ni kuongeza idadi ya wabunge kutoka upinzani. Kwanini aseme kutoka upinzani wakati yeye ana chama chake na tena ni kiongozi wa ngazi ya juu kabisa. Sijawahi kuwasikia viongozi wengine wa upinzani wakiongelea hayo mambo si mwenyekiti wake Mbowe ama Maalim au Profesa. Hapa kwa kweli ninapata mashaka sana, si kwamba sina imani nae bali nadhani anaelekea kupoteza mwelekeo. Mimi ningekuwa Zitto ningefanya kazi ya kuamsha watu wengi wagombee ubunge kupitia chama changu na kuwasaka wanachama wapya wengi wa chama changu. Kwa umaarufu alio nao na ujasiri alio uonyesha Bungeni ni tiketi tosha kabisa ya kumrudisha bungeni na tena si kwa 51%, may be hata zaidi ya hizo.

Kwa kifupi, msimamo wa Mh Zitto unaelekea kupunguza viti vya wabunge wa upinzani na si kuongeza kama yeye anavyodai. Naogopa asije akawa kama akina Dr. Masumbuko Lamwai, Ngawaiya, Kaborou, na wengineo. Unajua ni rahisi sana kurudi bungeni kama umefanya kazi yako vyema na ni ngumu sana kuingia Bungeni kama wewe ni mpya kabisa unless uwe na mshindani ambaye alivurunda sana wakati akiwa Mbunge.

Ninaungana na Mwanakijiji kwamba hili swala la maslahi ya Taifa halina manufaa kwa wapinzani na kila kukicha watakuwa wanazungukwa na CCM, na wapinzani wataendelea kupoteza viti kila mwaka wa uchaguzi. Upinzani utabaki na viti vyote vya Pemba na huku bara inawezekana wakaendelea kupoteza kiti kimoja baada ya kingine. Maana hata wale walio mjini ambao wanaelewa upinzani ni nini na ubaya wa CCM unaosemwa na wapinzani, wakiona kauli kama za Mh. Zitto wanakata tamaa na kuamua kutoenda kupiga kupiga kura na uchaguzi ukija hatuangalii ni watu wangapi walijitokeza kupiga kura bali ni mshindi kapata asilimia ngapi ya kura zilizopigwa. Unadhani watu wengine wanapoona mtu maarufu kama Zitto anasema hagombei ubunge tena, kuna atakayefikiria kugombea kupitia upinzani? Huo ndiyo mwanzo wa watu wengi wanaotaka kugombea ubunge kuamua kupitia CCM badala ya upinzani. Mwelekeo wa upinzani uko mashakani na CCM sasa hivi wanaangalia namna wapinzani wanavyocheza karata zao, na majibu yao yanakuja kwa mahesabu. Hii ni mojawapo ya sababu ya kwanini Makamba mpaka sasa hatoi tena matamko ya kujibu mapigo ya wapinzani. Akina Tambwe tutaanza tena kukutana nao kwenye makala za Tanzania Daima na siyo kwenye majukwaa ya Makamba. Nadhani CCM sasa wanafanya mambo kitaalam kwa kuangalia move za wapinzani na ndipo wanapokuja na mbinu za kufunga magoli ambayo ni ngumu kujua kama wameotea ama hawakuotea, tunasubiri mshika kibendera na refa waseme kama ni goli au la.
 
Kwa mara nyingine tena inabidi niukubali ukweli na kumeza uchungu wa kupoteza nafasi ya kuleta mabadiliko nchini.

Ni kweli kuwa mimi nimeweka wazi hapa kuwa ni mpinzani wa CCM na sitangojea kwa siku ambayo kutakuwa na serikali nyingine ambayo inajali raia wake tofauti na hii ya ccm ambayo inauza nchi kwa wazungu.

Kwa mara nyingine, nakubali kushindwa na mbinu za ushindi wa ccm na hivyo nameza tena kidonge cha uchungu kama nilichomeza mwaka 1995 waliposhindwa Mrema na Seif Shariff kwenye uchaguzi, mwaka 2000 alivyoshindwa Lipumba, na mwaka 2005 wapinzani wengi walivyoshindwa vibaya sana kwenye uchaguzi.

Katika siasa, mafanikio hujengwa na kisha kuendelezwa kwa kushikilia momentum iliyopo. Mwanasiasa au chama cha siasa akipoteza momentum maisha yake kisiasa yanakuwa matatani.

Upinzani Tanzania ulikuwa umepata momentum nzuri sana ya kuleta mabadiliko kwenye sekta ya madini. Zitto aliomba iundwe kamati huru ya bunge ambayo ingekuwa na nguvu zaidi za kupata ukweli na kuleta mabadiliko ya kweli.

Wananchi wengi walikuwa wameanza kukumbwa na momentum hii na wakafanya ambacho kilikuwa hakijafanyika nchini kwa muda mrefu sana - kuzomea viongozi wa ccm.

Kwa uwezo mkubwa sana wa kisiasa, CCM wamechukua hiyo momentum kwa kuunda kamati ambazo hazitafanya chochote katika kile watu wengi Tanzania walitaka kifanyike. Hebu soma haya maneno toka katika tamko la ccm kuhusu kamati ya Kikwete iliyoundwa:

Haya ni maneno ya Chiligati. Kilichoundwa na Kikwete, sio cha kuchunguza yaliyotokea, bali ni kufanya kile ambacho kimefanywa na kamati ya mboma, masha, na zingine nyingi tu--- kupendekeza maoni ambayo rais anaweza kuamua kuyapuuzia kama alivyofanya kwenye kamati zilizopita bila kujali mamilioni yanatumika katika kamati hizo.

Uteuzi wa Zitto kwenye hii kamati, umetoa momentum toka kwa upinzani na mimi nakiri kuwa hapa ccm wameshinda kwa sasa. Ushindi wao wa kwanza ulifikiwa juzi baada ya tarehe 25/11 ambayo iliwekwa kuwa siku ya mwisho (deadline) kwa ccm kushughulikia ufisadi, wizi na yote la sivyo hatua zitachukuliwa kupita bila chochote kutokea.

Kinachoonekana sasa ni mgongano tu ndani ya upinzani na haionyeshi kama kuna chochote kitatokea kwa sasa. Sijui kama Zitto alitegemea hili alivyokubali na kusisitiza kuwa kwenye kamati ambayo haina nguvu yoyote kisheria.

Kwa sasa, nameza kidonge cha maumivu na kukaa chini kujipanga upya kwa ajili ya next strategy. CCM wameshinda kwa sasa na mimi binafsi nawapongeza kwa strategy nzuri. Kwa vile kulialia sio sehemu ya maisha yangu, nitaendelea kusaka kwa nguvu zote hii mikataba ya serikali na kuitunza mpaka siku nitakapohakikisha fisadi wa mwisho akiwekwa Keko.

Hongera ccm kwa ushindi. Endeleeni kuuza nchi tu mwaya kwa vile mnaweza. Kama vile makocha wa timu wanavyopongezana baada ya mechi, na mimi nawapa pongezi kwa hili. Kwa kweli hapa mmecheza.

Tutakutana tena next time tukiwa tumejiandaa vyema.

Mie kwa maoni yangu shughuli ndio kwanza zimeanza, tusibwage manyanga mapema kiasi hicho. Tusubiri tusikie na kuona hii kamati iliyoteuliwa itakuja na mapendekezo gani na kama siri kali itakuwa tayari kuyafanyia kazi mapendekezo hayo na speed gani. Kama tukiona usanii unaendelea basi mapambano yataendela. Hakuna kukaa kimya kuona rasilmali zetu zinawanufaisha wajanja wachache na wageni wakati asilimia kubwa ya Watanzania wanaishi maisha ya dhiki kubwa.

Tukibwaga manyaga mapema tutawapa mwanya jamaa kwamba hatuna ubavu wa mapambano dhidi ya ufisadi, mikataba mibovu, wala rushwa na viongozi uroho wa utajiri wa haraka haraka kupitia nyadhifa zao, na watapata kichwa na kuanza kujipongeza.

Tumeshapata mafanikio mengi tu katika kelele zetu hapa JF. Kamati ya madini imeundwa kufuatia kelele za Watanzania kila kona ya Tanzania na hapa JF. Kamati imeundwa kufuatilia mkataba wa Richmonduli. Wakaguzi waliteuliwa ili kuchunguza upotevu mkubwa wa forex pale BOT, mabadiliko ya mawaziri yako njiani baada ya mawaziri wengi kulalamikiwa kuhusu utendaji wao na hata Daily news gazeti lenye miaka mingi limeanzisha forum yao kuiga mafanikio makubwa ya JF, haya si mafanikio madogo. Inaonyesha kwamba maamuzi ya CCM ambao wenyewe wanajiita nambari one hayatapokelewa kama ilivyokuwa mwaka 47 bila pingamizi lolote toka kwa wananchi, kama maamuzi hayo hayakubaliki kwa kuwa hayana maslahi na Tanzania basi tutapiga kelele kwa nguvu zetu zote ili kuhoji maamuzi hayo.

Tanzania ni yetu sote, na wote tunataka kuona maendeleo ya kweli. MWK, shughuli bado mama, kaza kibwebwe Watanzania wote wamechoka na usanii na viongozi wanaojali matumbo yao. Tunamuhitaji kila Mtanzania mpenda maendeleo ya kweli kwa Watanzania na Tanzania katika vita hii, hivyo nakuomba usikate tamaa mapema maana mapambano ndio kwanza yameanza na yataendelea mpaka viongozi wabadilishe mwenendo wao.

Mungu ibariki Tanzania.

Alutta Continua.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom