Pompeo to make 1st trip to Africa in a bid to reassert US as a leading partner The secretary of state will visit Senegal, Angola and Ethiopia

Hujaeleweka, umeandika Kama bata anaehakisha!! Eti china imejenge reli kutoka Pakistan hahahahaaaaah!

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe kuandika tu kwa kiswahili fasaha ni majanga, utaweza kuchanganua maoni yanayohitaji akili na fikra kubwa?

Kajifunze kwanza kuandika kiswahili fasaha kabla ya kuanza kuhangaika na masuala ambayo yako juu ya uwezo wako kiakili na kifikra!

Samahanai kama nitakukwaza!
 
Shida hua inakuja pale tunapokwenda huko then inakuja session ya Rais wa nchi husika kuhojiwa na waandishi wa habari,hapo hua ni majaribu bora tupotezee tu.

Ulishawahi kupata picha mkuu mwenyewe Vs The hard talk(BBC) au Mkuu vs amanpour(CNN)?
Labda kuna siku tutazinduka na kutambua jinsi tunavyopoteza fursa kwa upuuzi wetu wa kuchagua hovyo. Tanzania ni kama taifa lililojaaliwa mali asili lakini likanyimwa akili ya kuzitumia. PhD za Tanzania ni sehemu ya wingu la ujinga lililolifunika taifa na hadi hapo tutakapokiri hatujui kwamba hatujui tutaendelea kusifu wingu hilo bila kujua tunapapasa gizani. Kibaya zaidi tunalilea hilo wingu na kufanya juhudi za kuzima kila mwanga unaochomeza na hivyo kuzidi kutumbukia kwenye giza totoro.
 
Hakuna cha ku-promote demokrasia au uongozi bora bali ni kupigania maslahi ya Marekani kiuchumi.

Marekani anajaribu kupambana na China ambayo kwa sasa imejenga Addis-Djibouti railway ili kusafirisha bidhaa mpaka bandari ya Djibouti ambapo iko karibu na Pakistani kwenye Arabian Sea ambapo pia China inajenga reli (Silk Road) kutoka bandari ya Gwandar-Pakistani mpaka China(China-Pakistan Economic Corridor-CPEC)

Senegal anaenda kwa sababu ya kambi za kijeshi za Marekani "zinayopambana na Islamic terrorist" katika nchi za Magharibi mwa Afrika.

Angola anaenda kwa sababu ya malighafi kama mafuta na almasi ambazo makampuni ya Marekani kama ExxonMobil na Chevron yanapambana kuhakikisha nchi ya Ufaransa na Ureno hainufaiki nazo.

Rais wao, Abraham Lincoln aliwahi kusema, "You can fool all the people some of the time and some of the people all the time, but you cannot fool all the people all the time".

Hiyo nchi ya Ethiopia juzi tu imepitisha sheria kali ya mitandao ambayo kifungo chake ni miaka 5. Sasa huyu Pompeo tunayeambiwa anaenda ''ku-promote demokrasia na utawala bora'' upi kwenye nchi kama Ethiopia?

View attachment 1357877
Majangili FISIEM Mkisikia Polisi wa Dunia wamekuja Africa mnajawa hofu Kwa Sababu mnajua hakawii kulikamata lile Jambazi linaloua watu pamoja na Baabake

Sent from my Nokia 6.1 using Tapatalk
 
pompeo anareport kwa trump chief
Mimi sijaongelea ukubwa wa vyeo Wala Nini Bali nimeongelea uwezo wa Akili (intelligence).

Intelligence ya Trump kwa Mambo ya kitaifa/kimataifa Ni nyepesi Sana ukilinganisha na huyo pompeo.
 
Hakuna cha ku-promote demokrasia au uongozi bora bali ni kupigania maslahi ya Marekani kiuchumi.

Marekani anajaribu kupambana na China ambayo kwa sasa imejenga Addis-Djibouti railway ili kusafirisha bidhaa mpaka bandari ya Djibouti ambapo iko karibu na Pakistani kwenye Arabian Sea ambapo pia China inajenga reli (Silk Road) kutoka bandari ya Gwandar-Pakistani mpaka China(China-Pakistan Economic Corridor-CPEC)

Senegal anaenda kwa sababu ya kambi za kijeshi za Marekani "zinayopambana na Islamic terrorist" katika nchi za Magharibi mwa Afrika.

Angola anaenda kwa sababu ya malighafi kama mafuta na almasi ambazo makampuni ya Marekani kama ExxonMobil na Chevron yanapambana kuhakikisha nchi ya Ufaransa na Ureno hainufaiki nazo.

Rais wao, Abraham Lincoln aliwahi kusema, "You can fool all the people some of the time and some of the people all the time, but you cannot fool all the people all the time".

Hiyo nchi ya Ethiopia juzi tu imepitisha sheria kali ya mitandao ambayo kifungo chake ni miaka 5. Sasa huyu Pompeo tunayeambiwa anaenda ''ku-promote demokrasia na utawala bora'' upi kwenye nchi kama Ethiopia?

View attachment 1357877
Kwenye demokrasia Ethiopia wanaelejea kuzuri ,
 
Tanzania naona kama vile inasahaulika kidogo kidogo kwenye ramani ya dunia kwa nchi zinazopiga hatua kidemokrasia na utawala wa sheria.. Mara ya kwanza Commerce Secretary Wilbur Ross alizitembelea Ethiopia, Kenya, Cote d'Ivoire na Ghana mwezi wa July 2018. Mara ya pili Secretary of State wa US, Rex Tillerson alizitembelea nchi za Kenya, Ethiopia, Chad, Djibouti na Nigeria.
Walituzidi nini baada ya hao Mawaziri kuwatembelea? Sisi walipokuja Rais Clinton, Rais Bush na Rais Obama tuliwazidiGI nini?
 
Back
Top Bottom