Pombe yenye sumu yasababisha vifo vya watu 22 kaskazini mwa India

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Takribani watu 22 wamekufa baada ya kunywa pombe kali yenye sumu huko katika jimbo la kaskazini mwa India la Uttar Pradesh.

Afisa mwandamizi wa wilaya ya Aligharh, Chandra Bhushan Singh amesema vifo hivyo vimeripotiwa mapema Ijumaa na kwamba zaidi ya watu 28 wengine wanapatiwa matibabu katika hospitali za vijiji vya wilaya hiyo.

Waathirika ni wakazi wa vijiji vitatu tofauti na madereva wa malori, ambao walinunua kilevi hicho katika duka lenye leseni ya serikali. Na kwamba vifo vinaweza kuongezeka kutokana na baadhi ya watu kuwa katika hali mbaya.

Pamoja na takwimu za kila mwaka kuonesha idadi kubwa ya watu inapoteza maisha na hasa katika maeneo ya watu wenye kipato duni lakini biahara ya pombe haramu nchini India imekuwa ikiendelea kushamiri kutokana na kile kinachoelezwa kwamba bei yake ni nafuu kuliko pombe yenye kuzalishwa rasmi kibiashara.
 
Back
Top Bottom