Pombe si chai jamani!

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,896
21,983
Wanawake siku zote (si wote) wakinywa pombe kidogo tu hulewa na kuonekana wameutwika ile mbaya kuliko wanaume.
Wengine huenda mbali zaidi hata kujikojolea na kujisahau kabisa mahali walipo hubaki hapo hadi kilevi kitoke na wengine hata wakiutwika hukaa muda mrefu sana ili fahamu ziwarudie na fahamu zikirudi wengine huwa tayari mambo kadhaa mabaya wameshafanya au wamefanyiwa.


Why?
Timu ya wanasayansi ikiongozwa na Profesa Charles Lieber kutoka Mount Sinai School of Medicine New York Marekani, wamegundua kwamba wanawake wanakosa au wana upungufu mkubwa wa Enzyme ijulikanayo kwa jina la Gastric alcohol dehydrogenase (ADH), hii Enzyme huvunjavunja kilevi (alcohol) kabla ya kuingia kwenye damu.
Hii ina maana kwamba mwanamke akinjwa pombe kilevi huenda moja kwa moja kwenye damu bila kuchunjwa wala kuvunjwavunjwa kwanza kupunguza nguvu na sumu ambazo zinaweza kuwa kwenye pombe.

Pia wanatoa tahadhari kwamba wanawake wanaweza kuathirika zaidi na magonjwa yanayohusiana na ulevi haraka kuliko wanaume kama vile Cirrhosis ya Ini na Dementia

Pia wapo wanaume hutumia kilevi kama chambo kuwapata wanawake kwani wanafahamu kiwango sawa mwanamke hulewa zaidi.

Kumbuka ulevi ni mbaya kwa wanawake na wanaume husababisha familia mambo kwenda ndivyo sivyo.

Hutahukumiwa kwa kuwa ulikuwa mlevi bali kwa sababu ulikataa yule anayeweza kuondoa kiu ya kilevi yaani Kristo.

Source: http://www.independent.co.uk/news/science/scientists-discover-why-women-get-drunk-easily-681483.html

Dada kautwika hadi anajihisi yupo kwenye Queen bed yake home.
Pombe si chai au soda
 
Inasikitisha sana hasa mwanamke kushindwa kujizuia hasa pale unapoona pombe zimekuzidiaa, kuna mkasa mmoja umempata mama mmoja anapenda sana kulewa kupita kiasi, na akilewa huwa anamwita kijana wake ambaye anasema ni binamu yake anamfata , kuna siku kale kakijana kakapaki gari pembeni kakajisave bila hiyana yule mama inasemekana alikuwa hawezi kumzuia amelewa chakari na mimba ikaingia siku hiyohiyo, kuna mambo mengine ya kujitakia tu
 
kwa hiyo unataka kutuambia,tuwazuie kupiga maji kama mamba?

Bro, ni aibu iliyopitiliza kwa mwanamke kulewa mpaka kutokujitambua, ni vyema kumshauri kutokunywa kama hawezi kucontroll kabla hajaanza kufakamia pombe, wewe uliyekaa nae pia utajisikia aibu kama ni mwandani wako.
 
Yaani kuna watu wanachanganya? Badala yakunywa chai wanapiga biya?
 
nawaleetea picha ya mamammoja nilimpiga kimara saa tatu nakunywa supu ana kunywa castle akiwa na moto began ndugu achen sijui maisha ndio magumu ama??
 
Pombe inafundisha mpaka kizungu kwa asiyekijua.Anaongea kizungu akiwa amelewa ile mbaya.Kesho yake muulize kile kizungu ni balaa tu ajui kitu kabisa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom