simplemind
JF-Expert Member
- Apr 10, 2009
- 16,418
- 9,205
Written by Abdul Zakinthos // 26/02/2016 // Habari // Maoni 1
Utangulizi:
Kuna ile hadithi ya zamani maarufu Zanzibar ambayo Simba alipokuwa akiogopewa Bara na Mikoani na alipomaliza kula watu wa kutosha akaamua sasa apande jahazi aje Visiwani Zanzibar, labda ataogopewa kama alivokuwa Bara,lakini badala yake alipotoka tu Bandari ya Malindi akakaribishwa kikombe cha chai ya Karafuu na tangawizi,Chai ambayo hadi hii leo hajaimaliza kwa ule utamu wake,na mate yanamtoka hadi hii leo,basi ule ukali wake ukamalizia hapo hapo Malindi tu.
Haya ndio yanayompata sasa Rais Pombe John Magufuli, Juu ya ukali wake wote na nguvu zake zote alizonazo na majeshi yake huko bara, lakini lilipokuja suala la Zanzibar ,ameliogopa kama vile alivokuwa simba Chai. Endelea kumsikiliza Nassor Moyo zaidi.
Mwanasiasa mkongwe, Hassan Nassor Moyo, amesema Rais Dk. John Magufuli, ana haki na nguvu za Kikatiba kuingilia kati ili kutatua mgogoro wa uchaguzi mkuu unaofukuta Zanzibar.
Alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na Nipashe mjini hapa jana kuhusu hatma ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa na mkwamo wa kisiasa baada ya Chama cha Wananchi (CUF) kususia uchaguzi mkuu wa marudio uliopangwa kufanyika Machi 20, mwaka huu.
Mzee Moyo alisema Rais Dk Magufuli anapaswa kushughulikia mgogoro wa Zanzibar kama Rais wa Jamhuri ya Muungano na haikuwa kwake muafaka kujiweka kando ya mkwamo huo wakati Zanzibar ni sehemu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Nashangaa kumsikia Rais Magufuli akisema hana mamlaka ya kuingilia mgogoro wa uchaguzi wa Zanzibar…Yeye ndiye baba na watoto wanagombana, mzazi hutakiwi kukaa kimya na kuacha familia yako ikigawanyika,” alisema Moyo.
Alisema Zanzibar inapita katika mazingira magumu ya hali ya kisiasa na juhudi za haraka zinahitajika kutafuta muafaka kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa marudio.
Alisema yeye binafsi ameamua kukutana na baadhi ya wazee Tanzania Bara na Zanzibar akiwataka wachukue hatua za kuingilia mgogoro wa mkwamo wa uchaguzi mkuu wa Zanzibar.
Moyo ambaye ni Waziri wa zamani wa Katiba na Sheria mara baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964, pia amewahi kuwa Waziri wa Kilimo katika Serikai ya Mapinduzi Zanzibar.
Alisema tangu kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu Zanzibar Oktoba 28, hali ya kisiasa sio nzuri kutokana na mgawanyiko mkubwa wa wananchi uliojitokeza na kuzorotesha umoja wa kitaifa.
Alieleza kuwa iwapo wazee watakuwa huru na kuweka kando maslahi ya vyama vyao, mgogoro wa uchaguzi unaweza kupatiwa ufumbuzi kwa muda mfupi kwa maslahi ya Zanzibar na wananchi wake.
Hata hivyo alisema juhudi za kutafuta njia ya kutatua mgogoro wa Zanzibar, amekuwa akizifanya kwa tahadhari kubwa kutokana na kuwapo kwa wahafidhina wanaopinga kupatikana maelewano.
“Hakuna lisilowezekana katika utatuzi wa migogoro kama watu wanakuwa na nia njema hata Mwalimu Nyerere alifanikiwa mambo mengi kwa kuwashirikisha wazee katika nchi.
Nipashe