Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 15,551
- 19,419
Vilaza wa seminari ni shidah!, hapa anaweza kumkosoa Dr.Kitima.
P
Huyu "Cannon Lawyer" mwenzetu anayejua kila kitu asichojua na asiyekuwa mvivu wa kusoma asiyojua kusoma, ndugu yetu Paschal sijui alipitiwa na mapepo gani yanayomzuia kuwa humble wakati anajadiliana na watu asiowajua. Hata hivyo tusipersonalize mjadala huu kutokana na uwehu wa watu wachache, tukumbuke tu kuwa JF ni jamvi lenye ngedere na mchwa; tukishajua hivyo basi tuwe tunachambua facts tu.
Polycarp Cardinal Pengo amestaafu kutoka kuwa Archbishop wa Dar es Salaam ambapo sasa atakuwa ni Archbishop emeritus wa Dar-es-Salaam, ila atabaki kuwa Cardinal Priest kwenye College of Cardinals ya Vatican, na kwa nafasi hiyo ikitokea uchaguzi wa papa mwingine kabla hajafikisha miaka 80 bado atapiga kura. Akishafika au kuvuka miaka 80 ndipo hataruhusiwa tena kupiga kura ya kumchagua papa, lakini ataendelea kuwa Cardinal hadi anafariki. Akishafarki ndipo nafasi yake itabaki wazi na papa atachagua mtu mwingine kujaza nafasi hiyo. Binafsi, ningependa kuwa ikifika muda huo, basi wa kuchaguliwa kujaza nafasi hiyo atoke Tanzania tena. Tanzania tumebeba nafasi ya Cardinal miaka yote ya uhuru wetu; tulipata Cardinal wa kwanza nchini mwaka 1960 hata kabla hatujapata uhuru na hatuijawahi kuikosa nafasi hiyo.