Poll: Muammar Gaddafi Vs Nelson Mandela? Nani Shujaa/mwamba Wa Afrika?

Muammar Gaddafi vs Nelson Mandela? Nani shujaa/mwamba wa Afrika?


  • Total voters
    237
We ni mlibya mbona unaumia Sana ila wenyewe wanamkumbuka Now days
Kwa nini wanamkumbuka !! Wafuasi wa Gaddafi bado wapo na wanataka kuendelea kutawala na wapinzani nao wapo wanataka pia watawale.Moto wa vita uliowaka wa kuuzima hakuna, kwa jinsi wazungu wanavyowachukia Waarabu tayari wameshafanikiwa kuwafitinisha, wafuasi wa Gaddafi wanapewa silaha nzito na wapinzani nao kwa upande mwingine wanapata silaha nzito ndo maana mapigano ni makali na wanaumia ni raia na ndo wanaomkumbuka Gaddafi.Lakini shida hii yote ni Gaddafi mwenyewe baada ya kuvunja katiba ya nchi.Angalia mauaji DRC Kongo,machafuko hayaishi kwa sababu Kabila amevunja katiba ya nchi kwa kurefusha muhula wa uongozi.Mimi siumii bali nawapa ukweli juu ya Gaddafi anaepewa credit wakati dunia nzima alikuwa ananuka uovu.Naona wewe alikuonjesha tende na halua maana hapa kwetu alikuwa anajenga misikitiki na kuleta tende na halua kujiosha baada ya kuleta silaha za maangamizi kumsaidia Iddi Amin kwenye vita ya Kagera.Wewe ni mojawapo ulifaidi matunda ya Gaddafi ya kula tende na halua.
 
:)
 

Attachments

  • Capture.PNG
    Capture.PNG
    7.4 KB · Views: 58
Baba wa Taifa kawafunika wote hawa wawili kwa kusimamia ukombozi wa nchi nyingi za Afrika pia kumpa kipigo Ghadafi cha mbwa mwizi pale alipopeleka majeshi yake Uganda ili kumsaidia nduli Idi Amin Dada (kama ilivyoandikwa na kwenye vitabu kuhusu vita vya Kagera)

Mandela kafanya lipi kwa Waafrika au hata huyo Ghadafi kawanyia lipi Waafrika?

Kwa uonavyo wewe kati ya colonel Muammar Gaddafi au Nelson Mandela (Tata Madiba) nani shujaa/mwamba wa Afrika?

View attachment 534066
 
Sio hakikumshtua mtu yeyote sema hivi kifo chake wewe ndiyo hakijakushtua wenye nchi yao wenyewe wanajuta acha kua na chuki binafsi mkuu
Alizikwa na watu wangapi??? Hawazidi watano na haijulikani ni wapi alikozikwa.Hakuna raisi yeyote duniani alieenda kuhudhuria msiba wake hii ina dhihirisha hawakushituka na madhira yake.
 
Gaddafi achomwe na kuungulia vizuri huko aliko maana alihusika kusambaza dini ya magaidi duniani ikiwemo kujenga majengo Mengi ya ibada zao za kishetani
 
Gaddafi alisaidia sana afrika.

Umaarufu wa Mandela unakuzwa na wazungu kisa hakuwafanyia kisasi alipotoka jela. Nasisi tulivyo mazuzu tunamkweza hivyo hivyo. Huwez linganisha Gaddafi na Mandela

Mandela alitoa msaada gan nje ya afrika kusini?
 
Muamar gadafi....huyo Mandela "ushujaa" wake ni kukaa jela mengine aliyoyafanya ni ya kawaida sana, tena yalifanywa na wapigania Uhuru wenzie
Mandela kapaishwa sana na haohao wazungu mpaka kupewa Nobel sababu ya ile reconciliation iliyofanya wazungu waachie madaraka ya kisiasa lakini waendelee kuhodhi uchumi mpaka leo hii.
 
..waTz hatupaswi kumsifia mtu aliyetoa roho za askari wetu ktk vita vya Uganda...Ndiyo maana vijana wa kiTz mnadharaulika kwasababu mnakurupuka kujadili mambo mazito lakini hamsomi.

Exactly!! Imagine midege yenye vifaa na askari kutoka kwa Gadaffi wangefanikiwa kumsaidia Amini akashinda hiyo vita unadhani waTZ wangapi wangeuawa na huyo mnaomwona shujaa wenu. Mambo mengine ya ajabu sana. Mtu mwenyewe alikuwa vey undemocratic. Wewe tangu 1959 yuko madarakani mpaka kaja kuondolewa kwa maandamano baada ya watu kuchoka. lakini ndo shujaa wa watu hapa ndani. hapo mnalalamika eti TZ hakuna demokrasia. mambo ya ajabu sana haya.
 
Gadaf alikosa credit tu alipomsaidia Idd Amin Dada kutushughulikia
Huyu jamaa alikuwa ni mbaguzi wa kidini wa kiwango cha juu, na alikuwa anatumia mali zake kushawishi na kuwahonga baadhi ya viongozi ili kuibadilisha Afrika kuwa ya dini moja. Huo umoja wa Afrika aliokuwa anazungumzia ni Tofauti na ile ya NKURUMAH na NYERERE yeye alikuwa kwenye mrengo wa kidini , ndio sababu kuu ya kumpa sapoti NDULI wakati wa vita ya kagera akiamini kuwa bongo ndio ilikuwa kikwazo kwa baadhi ya sera zake mbovu
 
Muamar gadafi....huyo Mandela "ushujaa" wake ni kukaa jela mengine aliyoyafanya ni ya kawaida sana, tena yalifanywa na wapigania Uhuru wenzie

Kuna vitu vingine ni vigumu sana kuvipima! Ila ninavyoamini mimi sacrifice ya Tata Madiba ilisaidia sana kuuangamiza utawala wa makaburu, its because of Tata Madiba the world rallied together to fight apartheid, na wakati huo huo Gadafi was busy looting his country, killing fellow citizens and pretending to do a favour to his people by starting some development projects to cover his looting spree on the nations treasury! Or how else could he own more than usd 500.billion in his personal accounts overseas?! One of his sons had a cruise ship!
When all is said and done, if he was a good leader why did his subjects and fellow citizens take up arms to throw him out? Why didnt they fight foreign powers instead to protect Gadafi?!
 
Madiba yuko juu..
Gaddafi aliifanyia nn Afrika zaidi ya kujilimbikizia mali,utawala,madaraka mpaka kufa kifo cha aibu
 
Back
Top Bottom