Poll: Muammar Gaddafi Vs Nelson Mandela? Nani Shujaa/mwamba Wa Afrika?

Muammar Gaddafi vs Nelson Mandela? Nani shujaa/mwamba wa Afrika?


  • Total voters
    237
Muamar gadafi....huyo Mandela "ushujaa" wake ni kukaa jela mengine aliyoyafanya ni ya kawaida sana, tena yalifanywa na wapigania Uhuru wenzie
Hata nashindwa kuelewa kwa nini huwa wanamshusha Nyerere mbele yake
 
Dictator Gaddafi sijui kwanini anafananishwa na Papa Madiba, alikuwa msambaza dini mzuri na si vinginevyo.

Stupid Gaddafi, better gone to hell.
 
Dictator Gaddafi sijui kwanini anafananishwa na Papa Madiba, alikuwa msambaza dini mzuri na si vinginevyo.

Stupid Gaddafi, better gone to hell.
kesho tumia ubongo kufikiri na sio kwapa kama leo. Mandela kafanya nini kama sio kusaidiwa tu na OAU.
 
Mandela alikuwa mtu wa kusaidiwa na viongozi wenzie wa Afrika kama Mwl Kambarage na Gaddafi, in short Mandela hajatoa mchango wowote wenye manufaa barani Africa wa kumfananisha na Gaddafi, Julius au Kwame. tatizo la Waafrika wana akili fupi hivyo kucheza ngoma ya Wazungu wanaotuaminisha kuwa Mandela ndo kila kitu, ila hawajuwi why Mzungu anampromote Mandela, ni kwa sababu kawa samehe madhira na mateso yote waliyompa yeye aliamua kuwasamehe yote, na alilazimishwa kusamehe ili atolewe gerezani(masharti). hivyo Fadhira za mzungu kwa msamaha wa Mandela ni kumpromote dunia zima.
 
Maarufu zaidi ni Mandela
Kuisaidia zaidi Afrika ni Ghadafi

kaka umaarufu wa wasanii na wa mwanaharakati bora wa mwana harakati yalio fanya gadfi yalifinikwa na watu wabaya kwa kumchokonoa gadafi kupandisha mori-ila gadafi c wakufananisha afrika hii yule alikua mtu mwengine
 
1: Muammar Gaddafi ni bora zaidi kwa maana yakutetea Africa kuwa nguzo moja. Ukiaachana na nguvu aliojitolea kwa waafrika tuangalie alikoitoa Libya. Libya kabla ya Gaddafi ilikuwa duni sana lakini baada ya mapinduzi yaliomuondoa madarakani mfalme Idris, Gaddafi aliijenga Libya kiuchumi na kijamii nathubutu kusema hapajawahi kutokea kiongozi ukanda wa kusini mwa jangwa la Sahara aliyeiijenga nchi yake kwa maslahi mapana ya watu wote kama Muammar Mohammed Abu Minyar Gaddafi. Kitu ambacho huwa kinanishangaza ni kwamba Gaddafi alithitisha masomo yake ya elimu ya juu na kujiunga na JESHI na akawa kiongozi mkuu wakitaifa akiwa na umri wa miaka 28. Naamini wengi wetu tunafahamu huduma zilizokuwa zinatolewa na serikali ya Libya kipindi cha utawala wa Gaddafi. Sijui ni kitu gani kiliwakuta hawa ndugu zetu kiasi cha kumchukia na kumkataa kiongozi nguli kama Gaddafi.

2: Nelson Mandela ni maarufu sana tena kwa mataaifa ya Magharibi kwasababu ya kukubali/kuruhusu Makaburu mabingwa wa apartheid kuendelea kuishi na kufanya shughuli zao za kiuchumi na kijamii. Ila kwa maana ya harakati ngumu kumeza Nelson Mandela aende tuition kwanza afu arudi kukimbizana na kisiki Muammar Mohammed Abu Minyar Gaddafi.

3: Wazee wangu (Mandela na Gaddafi ) napenda kuchukua fursa hii kuwafahamisha kwamba babu yetu kipenzi R. G. Mugabe amekuwa muhenga na sasa tuna MNANGAGWA NA POMBE MAGUFULI mtuombee.

WAZEE WETU PUMZIKENI KWA AMANI HUKO MLIKO.
 
Sisi ni wepesi sana wa kusahau. Kweli Gaddafi kwetu ni shujaa au msaliti. Mwaka 1978 majeshi yake na rafiki ya Idd Amini Dada yaliua ndugu zetu wasio na hatia mkoani Kagera, bado ni shujaa kwenu. Kwangu Gaddaf alipata haki yake.
1: Mkuu kwa hicho unachozungumzia upo sawa na mimi nakuunga mkono. Lakini katika hizi harakati huwezi kupatia kila jambo na ndio maana kunatetesi Gaddafi aliomba msamaha kwa hicho alichokifanya dhidi ya Tanzania kipindi cha vita ya kagera. Kwa Mandela kitu ambacho sitamuelewa ni jambo la kuwaruhusu Makaburu kuendelea kuwepo hapo Afrika ya kusini.

2: Afrika ya kusini ni nchi ya ahadi ya watu weusi wa kusini kabisa mwa bara la Afrika kama ilivyo Israel kwa vizazi vya Jakobo., na ndio maana hata hivi sasa tunavyoongea Israel anatetea eneo lake la ahadi katikati ya nchi nyingi adui. Sasa kitendo cha Mandela kuruhusu Makaburu kuwepo kwenye ardhi ya ahadi ya mtu mweusi nathubutu kusema alitusaliti wa Afrika.

3: Nelson Mandela ningemkubali sana kama angeamsha harakati za kutuonganisha wa Afrika wote Duniani na kuwa na nguvu moja na sauti moja afu tukashusha ghalika ya moto dhidi ya Makaburu.
 
Sisi ni wepesi sana wa kusahau. Kweli Gaddafi kwetu ni shujaa au msaliti. Mwaka 1978 majeshi yake na rafiki ya Idd Amini Dada yaliua ndugu zetu wasio na hatia mkoani Kagera, bado ni shujaa kwenu. Kwangu Gaddaf alipata haki yake.

Hata wewe ungemuomba aje akusaidie kwenye ardhi yako asingekataa,,, so na waganda pia wangeanza kulalama kama wewe. Ni makubaliano kati ya nchi mbili......hapo hakuna kulaumiana mzee. Jamaa alikuwa alikuwa kazini
 
Gadaf alikosa credit tu alipomsaidia Idd Amin Dada kutushughulikia
Alikosa credit nyingi sana kama kuzika watu hasa wapinzani hai na kuwafukia na makatapila, alikuwa na dharau zilizokubuhu kwa kuona ikulu za wenzake zina najisi hivyo kusafiri na mahema na chakula chake, mtu mwenye credit hawezi kuzikwa kama mbwa na watu watano na kuzikwa porini kusikojulikana, alivunja katiba ya nchi na kung'ang'ania madaraka kama kwamba Walibya wengine wote ni wajinga, aluchukiwa na mataifa mengi ndo maana kifo chake hakikushitua mtu yeyote.Wewe kama unamfagilia una matatizo ya fikra.
 
Alikosa credit nyingi sana kama kuzika watu hasa wapinzani hai na kuwafukia na makatapila, alikuwa na dharau zilizokubuhu kwa kuona ikulu za wenzake zina najisi hivyo kusafiri na mahema na chakula chake, mtu mwenye credit hawezi kuzikwa kama mbwa na watu watano na kuzikwa porini kusikojulikana, alivunja katiba ya nchi na kung'ang'ania madaraka kama kwamba Walibya wengine wote ni wajinga, aluchukiwa na mataifa mengi ndo maana kifo chake hakikushitua mtu yeyote.Wewe kama unamfagilia una matatizo ya fikra.
We ni mlibya mbona unaumia Sana ila wenyewe wanamkumbuka Now days
 
Back
Top Bottom