Poll: Muammar Gaddafi Vs Nelson Mandela? Nani Shujaa/mwamba Wa Afrika?

Muammar Gaddafi vs Nelson Mandela? Nani shujaa/mwamba wa Afrika?


  • Total voters
    237
katika hili kila mtu ataweza kumchambua hawa wawili kivyake.Ukienda kwa wapinzani wa Nelson Mandela watasema alikuwa ni mtu mbaya ukienda kwa walionufaika na Mandela watasema kwao ni mtu shujaa vivohivyo kwa Muhamar
 
Nyerere ndio above all, the greatest unsung hero, mchango wake kwa liberation struggle during colonialism ktk subsahara hakuna anayemfikia hata robo
 
mandela pale hamna kitu bora tena na mwl.nyerere alifanya kazi nzito na kubwa mpaka kumhifadhi nelson mandela
 
Hehehe, kumbe kulikuwa na thread kama hii, my foot, Mleta mada, Ukome kumfananisha Madiba na mambo ya kijinga...

Kama kuna kuna mtu hamjui Madiba vizuri, akasome biographs, ziko nyinhi, mimi nimesoma Mbili, yake mwenyewe ya Long walk to freedom na moja imeandikwa na dada anaitwa Zelda la Grange..
 
Sijui watu wanalichukuliaje hili suala la Mandela lakini personally namuona kama binadamu wa ajabu alieishi ktk dunia hii niliyoijua...naamini hata hao wanaojiita viongozi wa dini kuna wakati wanakiri ktk mioyo yao kwamba kwa alilowafanyia makaburu hata wao wasingeweza kufanya.my point is,Ghadaf kwa Mandela haingii hata theluthi kiongozi ukiishakuwa kiongozi kisha ukawa na wapinzani wanaokutuhumu kuwatesa hii inakuondolea sifa ya uadilifu.ushujaa hutokana na siha nzuri ya uongozi sio tofauti na hivyo.
 
..Gadaffi huyu aliyeua askari wetu wakati wa vita vya Uganda?!

..vijana wa siku hizi hebu someni kidogo.

..manaake mnaaibisha kwa kuanzisha thread kama hizi.
Hapa hatuja uliza aliua nani bro, gadaffi n shujaa wa Africa tulihitaj watu 5 km hawa kuikomboa Africa,
 
Nahis kilichomnyanyua mandela ni ile hali ya kuteswa na wazungu halafu akawasamehe, ila kiushujaa wa ukombozi naona hata mwalimu nyerere yuko juu.. mandela did nothing to africa, baada ya kumaliza harakat zake nchini kwake akatulia.

Kwangu ni gaddafi
Nakuunga mkono mkuu.mandela ameinuliwa na wazungu na kutajwa kuwa ni shujaa wa afrika baada ya kuwasamehe kila kitu.yaani mandela hakuna hata alichokuwa anapigania mpk leo. Wala hana ushujaa wowote.labda ni kile kibuli tu cha kukaa jela mda mrefu.hebu njoo A.kusini mpk leo watu weusi ni watumwa wa makabulu.Ardhi wana miliki makabulu nguvu za kiuchumi makabulu.yeye alikuwa anapigania uhuru wa bendera tu.shujaa wa kwanza wa afrika ni julius nyerere.2. Ni mohamad ghadaff.mandela hayumo hata kwenye kumi bora.winnie mandela yupo juu ya mandela.
 
Apo kweli ndo maana hadi leo wazungu wanampromote sana madiba ila watu kama Nyerere, samora, nkurumah, lumumba na sankara siwasikiagi kwenye media za mbele ila gadaf wanamchafua tuu wa watu.
Goood.mandela alibadilika na kuwa kibaraka wa wa makabulu.hebu niambie ni kitu gn alichobadilisha south afrika mandela??!!
 
..Gadaffi huyu aliyeua askari wetu wakati wa vita vya Uganda?!

..vijana wa siku hizi hebu someni kidogo.

..manaake mnaaibisha kwa kuanzisha thread kama hizi.
umesoma documents za marekani???

gaddafi kasaidiana sana na nyerere kutetea uhuru wa nchi nying za africa

yy na nkurumah walikua na dream ya kuifanya africa united unajua nan aliua hio dream?? kama sio hao walokupa hzo documents usome wanachotaka wao uamini
 
umesoma documents za marekani???

gaddafi kasaidiana sana na nyerere kutetea uhuru wa nchi nying za africa

yy na nkurumah walikua na dream ya kuifanya africa united unajua nan aliua hio dream?? kama sio hao walokupa hzo documents usome wanachotaka wao uamini

..Gaddafi alitupa ultimatum tuondoe majeshi yetu Uganda la sivyo chamoto tungekiona.

..Na kweli kuna kipindi askari wa Gaddafi waliwachachafya vijana wetu waliokuwa mstari wa mbele Uganda.

..Vijana wetu waliweka ambush eneo linaitwa LUKAYA. Askari wa Gaddafi walitandikwa na kusambaratishwa kabisa. Wengi waliuawa na waliosalimika walichukuliwa mateka.

..Tangu hapo Gaddafi alifyata mkia na hakutusumbua tena.

..Kwangu mimi Gaddafi alikuwa mshenzi.

Cc Echolima
 
..SOURCE:

How Mbarara, Kampala fell to Tanzanian army

The battle for Lukaya
It was at Lukaya that the Tanzanians first encountered the Libyans, according to the history of the TPDF operations as documented in TPDF: An Operation History

Lukaya was Amin’s primary axis while the secondary axis was through Kalungu-Villa Maria, in his bid to retake Masaka. The area between Buganga and Lukaya was his concentration and assembly point.
Unfortunately for him, this place was in TPDF artillery range. TPDF deployed a brigade of reserve force to defend the town with other brigades taking position at different points in the outskirts as a backup depending on which direction the attack comes from.

A convoy of Libyan soldiers equipped with T-55 tanks, 12 APC’s, plus BM-21 multiple rocket launchers were part of Amin’s team to recapture Masaka. On March 10, the Libyans clashed with the TPDF sending 201 Brigade retreating to Masaka.

The 201st brigade regrouped and fought the Libyans for two consecutive nights with 208 Brigade in support bombing from northwest of Masaka. About 200 Libyans and another 200 Ugandan soldiers were killed. Tanzania took a few causalities.

cc dedon, Echolima
 
..Gaddafi alitupa ultimatum tuondoe majeshi yetu Uganda la sivyo chamoto tungekiona.

..Na kweli kuna kipindi askari wa Gaddafi waliwachachafya vijana wetu waliokuwa mstari wa mbele Uganda.

..Vijana wetu waliweka ambush eneo linaitwa LUKAYA. Askari wa Gaddafi walitandikwa na kusambaratishwa kabisa. Wengi waliuawa na waliosalimika walichukuliwa mateka.

..Tangu hapo Gaddafi alifyata mkia na hakutusumbua tena.

..Kwangu mimi Gaddafi alikuwa mshenzi.

Cc Echolima
Ni kweli kabisa Gaddafi aliwachachafya vijana wetu kwa upande wa MEDIA maana redio nyingi zilikuwa zikitangaza na kuwatangaza askari wake kuwa ni wazuri katika Medani za vita,cha ajabu walipofika eneo la vita wengi waliuwawa na wengine kushikwa kama kuku hivyo walishindwa kuonyesha umahiri wao katika nyanja za kivita pamoja na kuwa na vifaa vizuri wakati huo!!!.Operation iliyofanyika pale LUKAYA lilikuwa ni jibu tosha kwa Gaddafi na askari wake.
 
madiba na gaddafi???

madiba amekaa sana gerezani unajua gaddafi amesaidia uhuru nchi ngap africa??
Acha kuhadaa watu Gaddafi hajawahi kusaidia(For good will)nchi yeyote afrika,kama wewe unaijua hiyo nchi tuambie!!!
 
Back
Top Bottom