Poll: Mikataba ya hovyo ya madini na hasara taifa limepata, je nani alaumiwe?

Poll: Mikataba ya hovyo ya madini na hasara taifa limepata, je nani alaumiwe?

  • Total voters
    166
  • Poll closed .

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,265
23,198
Katika mikataba ya madini tuliyoingia kama taifa kuna pande mbili ambapo jukumu la kila upande ni kulinda maslahi yake. Serikali huingia katika mikataba hii kwa niaba ya wananchi wake baada ya kujiridhisha kwamba maslahi ya wananchi wake yamelindwa. Wawekezaji ni wafanya biashara na katika biashara yoyote lengo kubwa ni kupata faida kwa kutumia gharama ndogo.

Kwa hali iliyopo hivi sasa nchini, kuna maswali yamezuka ambayo yanawaacha wananchi wengi njia panda. Hapa nchini wananchi wanakitegemea chombo chao cha uwakilishi, Bunge, kuisimamia serikali katika utekelezaji wake wa kila siku. Kutokana na ukweli huu wanashindwa kuelewa kama kwenye mikataba inayoingiwa na serikali, je Bunge limehusushwa?

Hii sintofahamu inakuja baada ya taarifa kusikika kwamba mingi ya hii mikataba, ni siri na hiivyo jamii kutaharuki. Swali linaloumiza kichwa ni je yakitokea matatizo kama tunayoyashuhudia hivi sasa wa kulaumiwa ni nani? Je ni serikali kwa kutojua, kuzidiwa akili, kutokuwa makini, au viongozi kwa ulafi kutanguliza maslahi yao badala ya maslahi ya taifa?

Hebu wana JF tupige kura kulingana na kila moja wetu anavyoamini na bila shaka matokeo ya hii kura yatatoa mwanga wa kiini cha matatizo. Unaruhusiwa kuchagua zaidi ya mara moja kama unadhani vipengele zaidi ya moja vinahusika.
 
Selikali ya awamu ya tatu ndio ya kulaumiwa! Nashangaa Lisu anakula sahani moja na Sumaye mmoja ya waliotufikisha hapa alafu eti anajifanya kupiga kelele!
 
Bila kutafuta jibu mbali,wa kulaumiwa ni wabunge vilaza wa CCM walioishabikia hii mikataba ya kijinga,elimu kwa wabunge ni muhimu sana,afu issue kama hii haikutakiwa kuamliwa kwa wingi wa NDIYOOO,ilitakiwa wajiulize kwa nini kuna vijisauti vya hapanaaa,
 
Mkuu wanaangalia maslahi yao kwanza,Wananchi baadaye,Mikataba mingi inapitishwa gizan,mfano hai ni ule wa Gesi Serikali haikutaka ujadiliwe,hivyo ndivyo wafanyavyo na wao ni wamoja,kumtimua Muhongo siyo suruhisho
 
Katika mikataba ya madini tuliyoingia kama taifa kuna pande mbili ambapo jukumu la kila upande ni kulinda maslahi yake. Serikali huingia katika mikataba hii kwa niaba ya wananchi wake baada ya kujiridhisha kwamba maslahi ya wananchi wake yamelindwa. Wawekezaji ni wafanya biashara na katika biashara yoyote lengo kubwa ni kupata faida kwa kutumia gharama ndogo.

Kwa hali iliyopo hivi sasa nchini, kuna maswali yamezuka ambayo yanawaacha wananchi wengi njia panda. Hapa nchini wananchi wanakitegemea chombo chao cha uwakilishi, Bunge, kuisimamia serikali katika utekelezaji wake wa kila siku. Kutokana na ukweli huu wanashindwa kuelewa kama kwenye mikataba inayoingiwa na serikali, je Bunge limehusushwa?

Hii sintofahamu inakuja baada ya taarifa kusikika kwamba mingi ya hii mikataba, ni siri na hiivyo jamii kutaharuki. Swali linaloumiza kichwa ni je yakitokea matatizo kama tunayoyashuhudia hivi sasa wa kulaumiwa ni nani? Je ni serikali kwa kutojua, kuzidiwa akili, kutokuwa makini, au viongozi kwa ulafi kutanguliza maslahi yao badala ya maslahi ya taifa?

Hebu wana JF tupige kura kulingana na kila moja wetu anavyoamini na bila shaka matokeo ya hii kura yatatoa mwanga wa kiini cha matatizo. Unaruhusiwa kuchagua zaidi ya mara moja kama unadhani vipengele zaidi ya moja vinahusika.
Ccm.
 
Mkuu nichangie

Mikataba mibovu ya madini si suala la Acacia. Tuna historia mbovu sana

Utaratibu nchini ni Bunge kusimamia serikali. Na serikali inaundwa na chama tawala
Kwa mantiki hiyo, serikali ni ya CCM na Bunge ni la CCM kwasababu ya majority

Mikataba inaandikwaje na inatakelezwaje, kamati kuu ya CCM inajua kuliko upinzani
Ubovu wote ni kutokana na CCM ambayo kwa miaka zaidi ya 20 imeuza nchi

Kipi kigeni leo hii? Mikataba yote ikitiwa saini hawa waliopo leo walikuwepo. Walisema nini?
Hawakusema kwasababu walitaka kuwa 'wenzetu' na kuogopa CCM kuliko nchi

Huko bungeni miswada inapitishwa kwa 'ndiyoo' ya CCM. Akiuliza mwingine utaona uongozi wa bunge utakavyomjia juu. Bunge limegeuka kuwa ''halmashauri kuu ya CCM'' kwa mhuri wa ndiyoo

Acacia hakuja kufanya charity work hapa. Aliingia mktaba na wanasheria kutoka serikali ya CCM
Mkataba ukaridhiwa na Cabinet inayotokana na CCM. Ukatekelezwa na serikali ya CCM

Walioteuliwa kusimamia wanatoka katika uongozi wa CCM.

Leo tunaambiwa eti tusimame pamoja kwa uzalendo wa nchi.
Wakati wakitajwa wahujumu ambao hadi leo wengine wapo CCM hakukuwa na uzalendo.

Eti uzalendo kwavile mfanyabiashara Acacia anachuma kutokana na mikataba tuliyosainii

Anayedhani Acacia wana makosa atuonyeshe mkataba, kama hakuna tukae kimya tuwaache Acacia

Tunachotakiwa kufanya si kulaumu Acacia, ni CCM ambao si mara ya kwanza au ya piliau tatu
Tazama mikataba yote halafu mtu aonyeshe mkataba upi ulisainiwa na chama kingine

Nimeuliza Acacia kafanya kosa gani katika mkataba tusioujua? Jibu tuwe wazalendo
Yaani tuwe wazalendo kwa uzembe wa CCM.
 
  1. Wabunge wamjia juu Waziri Karamagi mkataba mpya London
    *Washangaa uzembe wa serikali kuruhusu mchanga
    *Wataka Stamico kurejeshewa meno

    Na Daniel Mjema, Dodoma

    WABUNGE wamedai kuwa suala la kupanda kwa mafuta na migodi mikubwa kumilikiwa na wageni kuwa ni ushauri mbovu na uzembe wa watendaji serikalini.

    Masuala ya madini, kupanda holela kwa bei ya mafuta na kutopelekwa kwa umeme vijijini ndio mambo makuu yaliyozua mjadala mzito bungeni mjini hapa jana wakati wabunge wakichangia bajeti ya Wizara ya Madini na Nishati.

    Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA) alihoji hatua ya Waziri wa Madini na Nishati, Nazir Karamagi, kusaini mkataba mpya wa madini na Kampuni ya Barrick wakati serikali haijamaliza kupitia mikataba ya zamani.

    Zitto alisema inashangaza kwamba wakati agizo la Rais Jakaya Kikwete la kupitiwa upya kwamikataba halijafikia tamati, Waziri Karamagi ametia saini mkataba na kampuni hiyo kufungua mgodi mpya wa Buzwagi.

    "Kinachosikitisha ni kuwa mkataba huo umetiwa saini kwa niaba ya Serikali na Waziri wa sasa wa Madini na Nishati tena utiaji saini mkataba huo umefanyika London (Uingereza) na sio Tanzania," alisema Kabwe.

    Kabwe aliongeza kuhoji: "Ni kwa nini mkataba mpya umesainiwa wakati taifa linapitia mikataba. Vitu kama hivi ndio mwanzo warushwa&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];tunataka kufahamu vipengele vya mkataba huu."

    Pia, alitaka serikali itoe maelezo ni kwa nini iliuza hisa ilizokuwa ikimiliki katika migodi nchini na sasa inataka kumiliki tena hisa na akatahadharisha kuwa dhahabu inayochimbwa na kampuni ya Barrick itamalizika baada ya miaka 18.

    Kwa upande wake, Mbunge wa Nzega, Lucas Selelii (CCM), alisema kukamatwa kwa mchanga wa dhahabu uliosombwa Kahama na baadaye kukamatwa jijini Dar es Salaam ni uzembe wa serikali.

    "Wizara imejiondoa mno katika usimamizi wa uchimbaji madini kwa makampuni makubwa kiasi kwamba wanachimba wenyewe, kufunga madini wenyewe na kusafirisha wenyewe halafu watuletee taarifa, hii haifai," alisema Selelii.

    Selelii alisema, makampuni hayo yanachukua mchanga wenye dhahabu kutoka kwenye mashimo na kuupakia moja kwa moja kwenye malori na kupeleka nje ya nchi bila kupitia kwenye mitambo ya uchekechaji.

    Mbunge wa Rufiji (CCM), Profesa Idriss Mtulia, alitaka Shirika la Madini (Stamico) lirudishiwe jukumu lake la kusimamia uchimbaji wa madini nchini na akataka linunue mitambo ya uchimbaji na kuikodisha kwa wachimbaji wadogo.

    Kuhusu suala la kupanda kwa bei ya mafuta nchini, Mbunge wa Viti maalumu, Mhonga Ruhwanya (Chadema), alitaka wabunge wa CCM kutosikitikia hali hiyo wakati wao ndio waliounga mkono kupitishwa kwa bajeti hiyo kwa mbwembwe nyingi.

    "Nimeletewa ujumbe na wananchi wa Kigoma wananiambia niwaulize wabunge wa CCM walikuwa wapi mafuta yakipanda na wao ndio walioshabikia bajeti&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];wananiambia niwaulize wanasikitika nini sasa," alisema Ruhwanya.

    Mbunge huyo alipendekeza serikali iliwezeshe Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), kiwe chombo pekee cha kuingiza na kusambaza mafuta nchini kwani, kwa kufanya hivyo inaweza kudhibiti biashara ya mafuta nchini.

    Kwa upande wake, Mbunge wa Bukene, TeddyKasella-Bantu (CCM) alitaka serikali iyabadili magari ya kifahari aina ya Toyota Land Cruiser, maarufu kama mashangingi ili yatumie gesi asilia kama njia ya kubana matumzi.

    "Kuwepo na utashi wa kisiasa ili serikali iyabadilishe magari yote ya serikali na mabasi ya abiria ili yatumie gesi asilia kwa kuwa matumizi ya nishati hiyo ni nafuu mara dufu kulinganisha na mafuta ya petroli," alisema Kasell-Bantu.

    Alitoa mfano kuwa, Land Cruiser likitoka Dar es Salaam kwenda Dodoma litatumia gesi asilia yenye thamani ya Sh18,000 tu wakati kwa hali ilivyo sasa magari hayo hutumia zaidi yaSh100,000 kwa umbali huo huo. Umbali wa kutoka Dar es Salaam mpaka Dodoma ni kilomita 453.

    Kuhusu hoja ya kupanda kwa bei ya mafuta, Selelii alisema matatizo yanayolikumba taifa hivi sasa yanatokana na ushauri mbaya ambao serikali ilipewa na watendaji wake na kufikia uamuzi wa kuitelekeza TPDC.

    Mbunge wa Viti maalum, Josephine Genzabuke(CCM), alisema kutokana na tamaa ya utajiri wa haraka, baadhi ya makampuni ya mafuta yamekuwa yakichanganya mafuta ya ndege na dizeli na kuyauza kama mafuta ya taa.

    Genzabuke alisema matumizi ya mafuta hayo yamekuwa na madhara makubwa hasa kwa wananchi wa eneo analotoka la Kigoma ambako watu watano wameshapoteza maisha kwa kulipukiwa na mafuta hayo.

    Wabunge karibu wote waliochangia bajeti hiyo, kilio chao kikubwa kilikuwa ni umeme vijijini, huku Ruhwanya akisema maendeleo ya Kigoma yanachelewa kusonga mbele kutokana na kukosekana kwa umeme.

    Baadhi ya Wabunge ambao maeneo yao hayajafikiwa na gridi ya taifa, waliiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kupeleka jenereta ili wananchi wa maeneo hayo waweze kushiriki katika kukuza uchumi.

    Report
    Like+ QuoteReply
  2. K
    Katibu TarafaJF-Expert Member
    #11
    Jul 17, 2007

    hawa vibogoyo,ni bora wakatafuta meno ya bandia

    Report
    Like+ QuoteReply

  3. Mtu wa PwaniJF-Expert Member
    #12
    Jul 17, 2007

    mie nnaona tuwaite mbwa koko, kazi kubweka tu, kutafuna hawawezi

    Report
    Like+ QuoteReply
  4. D
    DAR si LAMUJF-Expert Member
    #13
    Jul 17, 2007

    ...ni ya msingi.

    ...ila baadhi ya issues wanazichukulia juujuu bila kupata details ambazo zingewafanya wasizishikilie bango kiasi hicho!

    ...kama ni chakula kina chimvi nyingi!ila kinalika hivyo hivyo!

    Report
    Like+ QuoteReply

  5. BAKJF-Expert Member
    #14
    Jul 22, 2007

    na Schola Athanas

    WAZIRI wa Nishati na Madini, Nazir Mustafa Karamagi, jana alidai kwamba aliokolewa na Spika wa Bunge, Samuel Sitta kutoka katika kibano cha wabunge wakati wa kuchangia hotuba ya bajeti ya makadirio ya wizara yake.
    Akizungumza katika kipindi cha Bunge Wiki Hii, kinachorushwa na Televisheni ya Taifa (TvT) na kuongozwa na Tido Mhando ambaye ni mkurugenzi wa kituo hicho, Karamagi alisema Sitta alimuokoa baada ya kuvunja baadhi ya vipengele katika kanuni za Bunge, vinavyowawezesha wabunge wengi kuchangia.

    “Mjadala ulikuwa mkali kidogo, si kwa nia mbaya, ni kwa nia ya kuboresha, ni kweli, vyombo vya habari viliandika kuwa niliokolewa na Spika, hii ni kutokana na Spika kuvunja baadhi ya vipengele katika kanuni za Bunge, vinavyowawezesha wabunge wengi kuchangia,” alisema Karamagi.

    Alisema wabunge wengi walikuwa na hamasa ya kuchangia ili wapate umeme katika maeneo yao, hivyo kulikuwa na maswali mengi.

    Akizungumzia baadhi ya hoja za wabunge zilizotolewa katika mjadala wa wizara yake, alisema suala la wageni pekee kufanya utafiti wa awali wa madini si la kweli kwa kuwa kuna Watanzania 5,800 wanaofanya utafiti huo na wamekwishapewa leseni za kazi ya kuchimba madini.

    “Bado wizara inaendelea kutoa leseni kwa Watanzania ambao waliingia katika maeneo ya wachimbaji wenye leseni kubwa, hawa tunawaondoa katika maeneo hayo na kuwatafutia maeneo mengine ilimradi wafuate sheria,” alisema Karamagi.

    Kuhusu mikataba kuharakishwa na kubadilishwa, alisema huwa inabadilishwa na inatofautiana kati ya mikataba ya zamani na ya sasa.

    Akizungumzia agizo la rais la kupitia upya mikataba ya madini, alisema si jambo rahisi kuiondoa haraka kwa sababu mikataba ina taratibu zake, hivyo inapaswa kuwasiliana na wenye kampuni ili kuwaomba wakubali kuibadili kwa hiari yao.

    “Mikataba ya mwanzo ilikuwa kwa ajili ya kuwavutia wawekezaji, hivyo kwa kuwa soko la madini la Tanzania limeishajulikana, tutabadilisha vipengele kwenye mikataba ambavyo tuliviweka kwa ajili ya kuwavutia.

    “Na hata mafuta na gesi, kuna kampuni 19 ambazo zinafuatilia, nishati hizi zimeshagundulika katika maeneo ya Songosongo, Mnazi Bay, Mkuranga na Kigoma Bay,” alisema Karamagi.

    Akizungumza katika kipindi hicho, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), alisema serikali iliahidi kuwa mikataba ya madini itabadilishwa na kamati itaundwa, cha kushangaza bado mikataba inaendelea kusainiwa kinyume cha azma ya serikali na rais mwenyewe.

    “Mikataba inatakiwa kubadilishwa haraka kwani kuchelewa kunasababisha kampuni kushindwa kulipa kodi haraka ambayo ni asilimia 30, kutokana na kuondolewa kwa vipengele katika sheria ya mwaka 2001-2002, kuna kampuni ambazo zilitakiwa kuanza kulipa kodi ikiwemo Barrick, lakini inashangaza kuona wakisaini mkataba mwingine,” alisema Kabwe.

    Gema Akilimali kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), alisema wawekezaji wanaokuja kuchimba madini wanakuja kunyang’anya maeneo kwa sababu wanawakuta wananchi wanachimba madini katika sehemu hizo, hivyo hawafanyi utafiti kama inavyodaiwa katika mikataba hiyo.

    “Nashauri wavune madini, lakini badala ya kuyauza nje kama madini, vitengenezwe vito vya thamani na viuzwe ili taifa lipate faida zaidi,” alisitiza Akilimali.

    Katika mjadala wa makadirio ya wizara yake, Waziri Karamagi ambaye ni Mbunge wa Bukoba Vijijini, alibanwa kwa kiasi kikubwa na wabunge, wengi wakitaka maelezo ya kina juu ya kero ya umeme, mikataba ya madini na mambo mengine kadha wa kadha.

    Hata hivyo, kutokana na idadi kubwa ya wachangiaji ambao kila mmoja alionekana kuwa na hoja nzito, Spika alilazimika kuingilia kati mara kwa mara na hatimaye kufanikisha kupita kwa mbinde kwa bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini.

    Report
    Like+ QuoteReply

  6. Mpaka KielewekeJF-Expert Member
    #15
    Jul 23, 2007

    Bravo Karamagi kwa kuweka ukweli hadharani kuwa spika alikuokoa

    Hatuwezi kujenga taifa kwa mawaziri wetu kusema uongo
By BAK

SWISSME
 
Katika mikataba ya madini tuliyoingia kama taifa kuna pande mbili ambapo jukumu la kila upande ni kulinda maslahi yake. Serikali huingia katika mikataba hii kwa niaba ya wananchi wake baada ya kujiridhisha kwamba maslahi ya wananchi wake yamelindwa. Wawekezaji ni wafanya biashara na katika biashara yoyote lengo kubwa ni kupata faida kwa kutumia gharama ndogo.

Kwa hali iliyopo hivi sasa nchini, kuna maswali yamezuka ambayo yanawaacha wananchi wengi njia panda. Hapa nchini wananchi wanakitegemea chombo chao cha uwakilishi, Bunge, kuisimamia serikali katika utekelezaji wake wa kila siku. Kutokana na ukweli huu wanashindwa kuelewa kama kwenye mikataba inayoingiwa na serikali, je Bunge limehusushwa?

Hii sintofahamu inakuja baada ya taarifa kusikika kwamba mingi ya hii mikataba, ni siri na hiivyo jamii kutaharuki. Swali linaloumiza kichwa ni je yakitokea matatizo kama tunayoyashuhudia hivi sasa wa kulaumiwa ni nani? Je ni serikali kwa kutojua, kuzidiwa akili, kutokuwa makini, au viongozi kwa ulafi kutanguliza maslahi yao badala ya maslahi ya taifa?

Hebu wana JF tupige kura kulingana na kila moja wetu anavyoamini na bila shaka matokeo ya hii kura yatatoa mwanga wa kiini cha matatizo. Unaruhusiwa kuchagua zaidi ya mara moja kama unadhani vipengele zaidi ya moja vinahusika.
ni mbumbavu tu ndie asiye juwa kuwa janga la nchi hii ni CCM
 
Back
Top Bottom