Poll: Je Utakubali Matokeo ya Urais Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Poll: Je Utakubali Matokeo ya Urais Tanzania

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Chapakazi, Nov 3, 2010.

 1. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #1
  Nov 3, 2010
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hii ni poll ya upesi upesi kujua mwelekeo wa fikra za watu.

  Je Utakubali matokeo ya Urais pale NEC itakapoamua kuyatangaza?

  a) Hapana - Sitakubali matokeo yoyote
  b) Hapana - Kama CCM itatangazwa mshindi
  c) Hapana - Kama Chadema itatangazwa mshindi
  d) Ndio - yeyote akiwa mshindi
   
 2. Digna37

  Digna37 JF-Expert Member

  #2
  Nov 3, 2010
  Joined: May 17, 2010
  Messages: 835
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 60
  a) Hapana!!! Wamechakachua ni matokeo gani hayo????
   
 3. k

  kitatange Member

  #3
  Nov 3, 2010
  Joined: Aug 1, 2008
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  a) Sitakubali matokeo yote, yarudiwe na uhesabuji uwe outsourced to a professional body
   
 4. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #4
  Nov 3, 2010
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  D:smile-big:
   
 5. Mnene 1

  Mnene 1 Senior Member

  #5
  Nov 3, 2010
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 125
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hapana..........
   
 6. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #6
  Nov 3, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  hapa nafikiri tunazungumzia kitu tusichokijua. Kwa mujibu wa sheria yetu ya uchaguzi mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ndiye mwenye mamalaka ya kutangaza matokeo ya kura za urais, hoja ya kukubali au kukataa haikuwa taken into consideration katka sheria hiyo.

  Hivyo ni kupoteza muda kujadili kukubali au kukataa matokeo chini ya sheria mbovu kama hiyo. Lakiniu kwa kuwa wachezaji waliingia uwanjani wakijua sheria za mchezo zilivyo, basi mchezo huo ni halali
  .
   
 7. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #7
  Nov 3, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,626
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Hayo ni matokeo ya NEC sio matakwa ya wananchi ndio maana yanachelewa.!!
   
 8. L

  Ligoboka Member

  #8
  Nov 3, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jatropha nimeona comments zako,labda unielimishe tu-inakuwaje kwa wabunge?nani anayewatangaza?si NEC hiyohiyo?na mbona wengine wamekwenda mahakamani na kushinda kesi?..sheria gani huwa inatumika?
   
 9. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #9
  Nov 3, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,945
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Nope.
   
 10. m

  majuva Senior Member

  #10
  Nov 3, 2010
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ndio na kwa muelekeo JK rais halali wa tanzania kwa kura za trh 31.october 2010,
  hivi mlitegemea slaa awe rais kwa hizo kura za wasomi wachache! wenye uroho na uchu wa madaraka wa kutaka nao kupewa nafasi pindi atakaposhinda kwa kisingizio cha maslahi ya taifa! tena wengine wanapigia kura mtandaoni, wakidhani kura za mtandaoni zitampa urais slaa nao warudi kushika nafasi za uongozi...
   
 11. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #11
  Nov 3, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Hapana
   
 12. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #12
  Nov 3, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
 13. k

  kilimajoy Senior Member

  #13
  Nov 3, 2010
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 132
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wala hatukushangai...watanzania wa kweli wana uchungu na nchi yao, hawawezi kukubali nchi yao ishikwe na mafisadi na kutawaliwa bila kujali maslahi ya wananchi wote! Hakuna mtanzania wa kweli anaweza kukubali nchi yake iwe kichwa cha mwendawazimu kama ilivyo sasa..kila mmoja anapata uchungu..ila kwa nyie mnaojivunia matokeo haya kwa maneno yangu binafsi sio watanzania halisi..na hamjui mnalolifanya...na sijui kwa nini mpo kwanza Tanzania.
   
 14. Kishongo

  Kishongo JF-Expert Member

  #14
  Nov 3, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  WAANGALIZI wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu uliofanyika Oktoba 31,kutoka Jumuiya ya Ulaya ( EU EOM) na Umoja wa Afrika wamesema kuwa uchaguzi huo ulikuwa wa huru na haki, utulivu na amani.

  Waangalizi hao walitoa kauli hizo kwa nyakati tofauti wakati walipofanya mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana(leo) kuhusu taarifa ya awali ya uchaguzi huo.

  Akizungumza na waandishi wa habari Mwangalizi Mkuu wa EU EOM, David Martin alisema uchaguzi huo ambao ni wa nne kufanyika nchini tangu mfumo wa vyama vingi kuanzishwa Tanzania, hadi sasa kwa ujumla umefanyika kwa amani na mpangilio mzuri.

  " Siku ya Uchaguzi Mkuu ilijitokeza kwa utulivu mkubwa na kwa ujuml a waangalizi wa uchaguzi wa Ujumbe Maaalumu wa Jumuiya ya Ulaya(EU EOM) ulikadria mchakato mzima wa uchaguzi huo kuwa ama ulikuwa ‘mzuri' au ' kuridhisha' katika asilimia 95 ya vituo vyote vya kupigia kura walivyovitembelea upande wa Tanzania Bara na upande wa Zanzibar," alisema Martin.

  Aliongeza kuwa kwa ujumla taratibu muhimu katika vituo vya kupigia kura zilitumwa kwa ulinganifu kwa kila kituo cha kupigia kura nchini kote, licha kuwepo mapungufu machache.

  Martin alisema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) zilisimamia chaguzi kwa namna ya kitaalamu, hivyo kwa sehemu kubwa ziliwapatia watu watu wote haki ya kupiga kura.

  Aliongeza kuwa ujumbe huo utabakia nchini kuzidi kufuatilia kwa karibu zaidi zoezi la kuhesabu matokeo ya uchaguzi, utangazaji wa matokeo na matukio yoyote yatakayojitokeza baada ya uchaguzi.

  "Taarifa hii ni ya awali .Taarifa ya kina ya mwisho itatolewa baina ya miezi miwili na miezi mitatu baada ya mchakato mzima wa uchaguzi kukamilika," alisema.

  Kwa upande wake Kiongozi wa waangalizi hao, kutoka AU, Rais wa zamani wa Jamhuri ya Sierra Leone, Dk. Ahmad Tejan Kabbah alisema uchaguzi huo umefanyika wa amani na umefanyika kwa mujibu wa sheria za uchaguzi wa Tanzania .

  Aliongeza kuwa umefanyika kwa kuzingatia Azimia la Durban Demorasia katika Chaguzi za Afrika la Julai mwaka 2002.

  " Waangalizi wa Umoja wa Afrika wamesema uchaguzi umefanyika kwa huru, haki , uwazi na uadilifu(Credible) .  Naye Katibu Mtendaji wa International Conference of the Great Lakes Region (ICGLR) Balozi Liberata Mulamula amesema wiki hii kwamba wameridhishwa na mchakato mzima wa uchaguzi mkuu Tanzania na kwamba ukiondoa matatizo madogo madogo yaliyojitokeza sehemu mbili tatu, ulikuwa huru na wa haki.
  Balozi Mulamula amesema uchaguzi wa Tanzania ni mfano wa kuigwa kwa nchi wanachama wa ICGLR ambao wengi watakuwa na uchaguzi katika kipindi hiki. Ameisifu serikali ya Tanzania kwa juhudi zake za kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa na kuruhusu kila mwananchi aliejiandikisha kupiga kura bila wasiwasi.

  Waangalizi hao ,waliwapongeza wananchi wa Tanzania, Vyama vya Siasa, wagombea , NEC, ZEC na vyombo vya usalama kwa kuwezesha uchaguzi huo ufanyike kwa amani na kuwashauri wagombea kukubali matokeo yanayotangazwa na NEC.
   
 15. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #15
  Nov 3, 2010
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu soma angalizo nililoweka mwanzo:
  'hii ni poll ya upesi upesi kujua mwelekeo wa fikra za watu"
  mimi siangalii sheria, bali naangalia watu binafsi kama kweli watakubali haya matokeo!
   
 16. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #16
  Nov 3, 2010
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  mods...naomba msaada kuweka hii kuwa a poll!
   
Loading...