Political tolerance. Bidhaa adimu kwa sasa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Political tolerance. Bidhaa adimu kwa sasa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtumishi Mkuu, Jul 16, 2012.

 1. Mtumishi Mkuu

  Mtumishi Mkuu JF-Expert Member

  #1
  Jul 16, 2012
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 260
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ninayaandika haya kutokana na tukio la karibuni la mwenyekiti wa UVCCM kupoteza maisha kutokana na vurugu zilizoibuka kwenye mkutano uliokuwa ukiendeshwa na CHADEMA. Hadi sasa kumekuwa na kutupiana lawama kati ya vyama hivi viwili kila kimoja kikikituhumu kingnine kwa kuhusika na mauaji haya.

  Kwa maelezo ya kamanda wa polisi ni kwamba Viongozi wa chadema walianza kwa kutoa lugha za kukishafu chama tawala pamoja na mbunge wa eneo hilo (Nchemba) na hivyo wale wanaosadikika kuwa wafuasi wa ccm wakakosa subira na kuanza kurusha mawe ahli iliyoleta vurugu na kupelekea m/kiti wa uvccm kuuawa kwa mawe na silaha nyingne za jadi.

  Hadi hapa nadhani chanzo cha vurugu kishafahamika. Katika siasa ni lazima mtu uwe tayari kuyasikika yale ambayo hupendi kuyasikia. Kikubwa kinachotakiwa ni tolerance. Nakumbuka kuna wkt kiongozi wa CCM wkt wa uchaguzi mdogo wa arumeru alisema kama mtu unaona huna uvumilivu wa kusikika chama chako kikikosolewa na chama kingine basi usiende kwenye mikutano ya vyama hivyo. Maana yake ni kwamba huwez kwenda kwnye mikutano ya ccm ukakuta wanawasifia cdm, vivyo hivyo kwa vyama vingine. Hivyo uvumilivu ni jambo la muhimu hapa.

  Sasa najiuliza hawa vijana walioshindwa kuvumilia wkt mbunge wa iramba akitajiwa tuhuma zake na kuanza vurugu wanataka nan alaumiwe kwa matokeo ya vurugu hizo???
   
Loading...