Political Farewell, politiques adieu, politisch Abschied-kwa herini! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Political Farewell, politiques adieu, politisch Abschied-kwa herini!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Waberoya, Jul 4, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #1
  Jul 4, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,579
  Likes Received: 3,881
  Trophy Points: 280
  Tangu nimejiunga JF mwaka 2008 nimekuwa huru katika mawazo yangu, na nimekuwa huru kufuata msimamo mmoja ule ninaouona kuwa ni sahihi zaidi.

  Sijawahi kuipenda CCM hii, wala sijawahi ku-advocate ufisadi. Sijawahi kumdharau mtu yeyote hata nilipofanya makosa sikusita kuomba msamaha. Haikuwahi kuniingia akilini kuwa kumtukana mtu usiyemjua na anayetumia ID ya kificho ina tija yoyote.


  JF kama nilivyoikuta ni mahali nilipokuta mijadala ya hoja kwa hoja, sikuona matusi wala majibu ya kejeli. Ni JF ambayo ilikuwa familia hata kama mmetofautiana kimawazo bado ilikuwa familia. Familia kwa sababu wako wengi hata hawajui JF wanaishi, wako wasiokuwa wanachama wanaishi..kuwa na wanachama hapa ni bahati na encouragable. JF ni familia kubwa ya DEBATE, ni familia ambapo hoja yenye nguvu ndiyo inashinda. Nakumbuka kuna thread ulikuwa ukisoma inabidi ukasome kwanza kabla ya kujibu, maana inakutoa nje! mnashindana kwa hoja na baadae mnataniana. I inclined on that attitude and was posting teasing posts to see how someone may counteract them intelligently..my motives got stuck!


  Napenda mageuzi, napenda mabadiliko, lakini kila mtu ana theory za kufikia lengo. Napenda wanaojiita wanasiasa wawe kazini kama wanasiasa bila hadaa wala hila yeyote ile. Kwani kila mwanasiasa ni mwanasiasa. Kwangu mimi naweza kumpa sifa leo na kumkosoa kesho, naona ni sawa na haki yangu.

  Sikuzote nimetofautiana na Chadema jinsi inavyofanya mambo yake, sifichi ninaipenda , ila naona inahitaji msaada sana wa hapa na pale ili ifikie lengo. Ultimate ya CDM siyo topical na event issues , ni kushika dola ukiangalia hoja zangu siku zote ZIKICHUKULIWA kama changamoto basi zina nguvu pale ambapo nimeona pana udhaifu. Kwa bahati mbaya tuko JF ambayo CDM haipaswi kukosolewa, haipaswi kunolewa , haipaswi kupitishwa kwenye moto, ikajaribiwa na kujitayarisha kuishika dola. Kila thread humu ni malalamiko ya CCM ni mbaya-ila hakuna za kuipa mbinu CDM ya kushika dola! Nakubali, hakuna thread za kuipa CDM mbinu na changamoto za kuingia ikulu, kwani challenges ni nyingi. Napenda logic kama vile .."ikiwa CDM ambao ni smart walifanya makosa kumkaribisha Shibuda chamani, wangekuwa madarakani wangefanya maamuzi mangapi mabovu" asking these kind of questions build awareness among CDMs especially leaders; it is just thinking out of the box

  Siku zote nimetamani umoja wa chadema, pale nilipoona, au kusikia kuwa kuna migongano nilienda kinyume na anayetaka kuvunja umoja. Issue za madiwani kwa mfano ilitakiwa kuwa handled kwa uangalifu sana maana nyuma yake kuna issues za udini ambazo chadema mpaka sasa wanaandamwa kila kukicha. Nimejaribu kuwaamsha upande huo wa kuziona changamoto.

  Ndugu zangu wapendwa, napenda kuchukua fursa hii muhimu kuwaaga kuwa naondoka rasmi kwenye hili jukwaa.Najua mko ambao mtatukana, ambao mtakejeli, lakini utu wangu na uhuru wangu wa mawazo ni wa kuulinda sana kabla ya kuathiriwa kisaikolojia. Ombi moja , wakosoeni viongozi wanapokosea,wasifuni panapostahili, hata pale wanapoonyesha interest zao na si za taifa hili-waambinei tumegundua. Lindeni umoja, heshimu mawazo ya kila mtu, hata kama mabaya kwani inakupa picha ya safari yako ilivyo! JF was my home page and my friend. I though is a nice place to debate intelligently na si mahali pa kuandika tu post.

  Ni sehemu na mtandao pekee ambako wenye nguvu ya kutetea hoja wanapaswa wawepo kwani dunia yote ni ya hoja tu.

  Tulinde spirit hii ya kutaka mabadiliko kwa uangalifu mkubwa, tulinde umoja wa kitaifa, tukijua kuwa swala zima la failure ya CCM ni swala la kila mmoja wetu. Na kwa kugundua kosa hili , ni wajibu wa kila mmoja kufanya linalowezekana kuiondoa CCM madarakani. Kwa bahati mbaya sijaziona hizi jitihada upande wa CDM. Nimeona ad hoc plans.

  Nimetukanwa, nimedhalilishwa, nimevuliwa nguo, nimetafutwa na kuhackiwa na kusemwa akila aina ya ubaya. Sieleweki, sikubaliki.
  Sitaacha kuwakumbuka, lakini sitawachukia, you will always be beautiful in my eyes.

  ……………………………………………………………….
  in this proud land we grew up strong
  we were wanted all along
  I was taught to fight, taught to win
  I never thought I could fail

  no fight left or so it seems
  I am a man whose dreams have all deserted
  I've changed my face, I've changed my name
  but no one wants you when you lose

  Got to walk out of here
  I can't take anymore
  going to stand on that bridge
  keep my eyes down below
  whatever may come
  and whatever may go
  that river's flowing
  that river's flowing.

  Peter Gabriel


  Nawatakia forum njema, Ninaiombea JF will always be in my heart.


  Kwa niliowakosea I beg for your forgiveness , Nothing serious was just a NAUGHTY BOY to make our forums as live as possible!! sorry!


  Keep on smiling! but let me motivate you is possible CCM can be removed, but it is not easy..we need brainy to make this happens

  Love you all! and will miss you

  Only in the agony of parting do we look into the depths of love.
  George Eliot


  Wakatabahu

  Bukuku
   
 2. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #2
  Jul 4, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  I will miss you dude, especially with that radicalism, boasting, critical, true and sometimes mislead perception and understanding... I always remember when we were together again shibuda and when we differ on zitto

  Knowing JF, wewe utakua humu ila kwa jina jingine kama ambavyo wengi wamefanya

  all the best and surely you were someone special in your own way!!

  parting shot... Tanzania bila CCM inawezekana, and CHADEMA makini ni muhimu zaidi ya mageuzi ya kisiasa
   
 3. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #3
  Jul 4, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  potelea mbali weberoya
   
 4. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #4
  Jul 4, 2011
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,988
  Likes Received: 3,737
  Trophy Points: 280
  Bukuku, was this dramatic (or rather flamboyant) exit really necessary? For all what anybody on this forum would care, you could as well have gone quietly......

  One more thing........
  Am an engineer too. One thing I know about engineers is that they are not quitters....never ever! Even when they do quit, you will never ever find out that (let alone when/why/how) they did!

  Nina hamu sana ya kujua undani wa hiyo "Eng" tag ambayo umejivisha. I really do.....
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #5
  Jul 4, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,568
  Likes Received: 18,313
  Trophy Points: 280
  Bukuku, kwanza pole kwa yaliyokukuta jf kwa ikosoaji wa Chadema. I thought of you as a man of strength of character kutokana na kuandika kile unachoamini. Hili la kujitoa jf kwangu nalihesabu ni waekness. please think twice!. JF inahitaji watu wa type yako now more than any other time.

  Mbona mimi ninaikosoa sana CDM na niliposema haijajipanga, nilitukanwa sana. Nilishukiwa hadi na wakuu wao. Kwa vile nilisema hawajajipanga na kuanisha wajipange vipi, wanaendelea kutia pamba masikioni mwao wakijiaminisha 2015 ni mbali. Nimevumilia matukano na bado nasisitiza bado hawajajipanga na ni humu humu jf nawasubiria baada ya 2015 watakapokuwa wana lia lia tena kwa kuto amini kitakacho tokea.

  To me Tanzania kwanza. CCM imetufikisha hapa ilipotufikisha sasa imechokwa. Chadema ndio the only hope inayojichomoza lakini kwa mwendo huu wa kutojipanga, 2015 yatakuwa ni yale yale ya Watanzania kuendelea kufanywa dekio!.
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Jul 4, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,568
  Likes Received: 18,313
  Trophy Points: 280
  y
  M babe, naingana na wewe this kind of exit ni manifestation ya weakness ambayo kwayo ni aghlabu sana kwa ma Eng. wa ukweli.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...