Political Espionage: Jifunze kuhusu jasusi mchochezi (Agents Provocateur)

  • Thread starter Beautiful Nkosazana
  • Start date

Beautiful Nkosazana

Beautiful Nkosazana

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2016
Messages
791
Points
1,000
Beautiful Nkosazana

Beautiful Nkosazana

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2016
791 1,000
Intelijensia: Pandikizi Chochezi

Source: Agent provocateur - Wikipedia

Suala la Intelijensia, ujasusi na ushushushu ni kitu adhimu sana kukifahamu si tu kwa manufaa ya usalama wa nchi bali pia yaweza kukufaa hata katika maisha ya kawaida. Mbinu za kijasusi na intelijesia kwa sasa zinatumika katika kila sekta na nyanja ya maisha. Iwe wewe ni mwanaharakati, mwanasiasa, mfanyabiashara, mwanazuoni, mwajiriwa au mjasiriamali… uelewa walau mdogo tu wa masuala ya intelijensia unaweza kukufanya kuwa hatua kadhaa mbele ya wenzako na hata pia kuweza kujikinga dhidi ya mashambulio dhidi yako pale yanapotokea.

Kwa ufupi sana siku ya leo nitaongea kuhusu moja ya mbinu adhimu ya intelijensia yenye kutumika sana ulimwenguni kote na ambayo pia nimeiona imeshika hatamu mno. Lugha yetu ya kiswahili ni changa hivyo inakosa baadhi ya misamiati kueleza kitu kwa ufasaha unaoulenga. Kwa ukosefu wa msamiati maridhawa nitaiita mbinu hii "Pandikizi Chochezi" ambayo kwa umombo inajulikana kama "Agent Provocateur".

Katika masuala ya ujasusi, pandikizi chochezi ni mtu ambaye anafanya au anashawishi mtu mwingine kufanya kitu kilicho kinyume na sheria au tendo la hila au kumuhusisha mwingine kuhusika kwenye tendo hilo.
Pandikizi Chochezi anaweza kuwa ni afisa wa chombo cha usalama, au afisa wa kiserikali au Idara na hata wakala wa chama cha siasa na kwenye ulimwengu wa biashara anaweza kuwa hata mwajiriwa wa kampuni shindani.

Pandikizi chochezi anatumiwa na Idara iliyomtuma, kujipenyeza kwenye kundi lengwa (mfano chama cha siasa au kampuni au vugu vugu ka harakati) na akiisha kujipenyeza na kukubalika kwenye kundi hilo anakuwa mstari wa mbele kabisa kindakindaki kiasi kwamba anakuwa moja ya watu wenye kutazamwa kwa mwongozo kwenye kundi hilo. Baada ya hapo Pandikizi chochezi anatumia mwanya huo kushawishi wengine kufanya tendo la hila ambalo ni kinyume cha sheria. Lengo kuu hapa linakuwa ni mfano kuvuruga harakati/vuguvugu au kujaribu kupaka matope kundi hilo husika au kulichafua kwenye jamii ama kuifanya serikali kuchukua hatua dhidi ya kundi hilo.

Mbinu hii inatumiwa mfano na serikali nyingi au vyombo vya usalama pale ambapo wanahitaji kupiga marufuku kundi fulani (chama cha siasa, vuguvugu au kampuni) hivyo pandikizi chochezi anatumiwa ili kuipa serikali au idara ya usalama sababu ya kuwachukulia kundi hilo hatua.

Si hivyo tu, lakini pia Pandikizi chochezi anaweza kutumia kushawishi mtu mwingine kufanya tukio la kudhuru kama vile mauaji bila anayetumiwa kujua. Yaani kwamba pale ambapo Idara husika au serikali husika ikihitaji 'kumu-eliminate' mtu fulani lakini haitaki yabakie maswali na sintofahamu, wanaweza kutumia Pandikizi Chochezi kushawishi mtu wa kawaida kufanya tukio hilo la mauaji pasipo mtu anayetumiwa kujua kuwa anatumika.

Nitatoa mifano michache…

Inawezekana wengi hawafahamu kwamba Kim Jong-Un hakuwa chaguo la kwanza la baba yake Kim Jong-il kumrithi kuongoza taifa la Korea Kaskazini.
Chaguo la kwanza la Kim Jong-il lilikuwa ni mtoto wake wa nje aliyeitwa Kim Jong-nam ambaye alizaliwa mwaka 1971 na mwanamke aitwaye Song-Hye-rim. Kutokana na baba yake (yaani babu yao akina Kim Jong-nam na Kim Jong-un) kutokukubali mahusiano ya kimapenzi kati ya mwanaye Kim Jong-il na yule mwanamke Song Hye-rim ilibidi alipozaliwa Kim Jong-nam afichwe kwa kupelekwa kuishi na shangazi yake na baadae alipelekwa nje ya nchi ambako alikaa huko utoto wake wote na kusoma huko kwenye nchi za Urusi na Uswisi na kurejea Korea Kaskazini mwaka 1988.

Kama maandalizi ya kumrithi baba yake, mwaka 1998 Kim Jong-nam aliteuliwa kuongoza Wizara ya Masuala ya Usalama wa Taifa. Pia Kim Jong-nam alipewa jukumu na baba yake kuongoza kamati ya Taifa ya kuunda sekta ya Tehama nchini humo.
Pia ni Kim Jong-nam ambaye aliambatana na baba yake kwenye ziara ya nchini China mwaka 2001 ili kujadili namna ambavyo wachina wanaweza kuwasaidia kuinua sekta ya Tehama nchini Korea Kaskazini.

Kila aina ya maandalizi yalikuwa yanafanyika kumuandaa Kim Jong-nam kuwa mrithi wa Kim Jong-il kuongoza taifa la Korea Kaskazini.

Japokuwa Kim Jong-nam alikuwa anafanana sana kihaiba na baba yake kutokana na hasira zake, hisia za haraka na ujuzi wa masuala ya sanaa kama vile uandishi wa miswada ya filamu lakini Kim Jong-nam alikuwa na kasoro moja mbaya… alikuwa ni mtu mwenye kupenda anasa na wanawake hovyo. Kulikuwa na uvumi kwamba Kim Jong-nam mara kadhaa amekuwa akitoka nje ya Korea Kaskazini kwa pasipoti za kughushi zenye majina ya uongo ili kwenda kufanya starehe Macau, China na hata Japan. Uvumi huu ulikuwa ukikanushwa mara nyingi na serikali ya Korea Kaskazini.

Za mwizi ni arobaini, mwezi May mwaka 2001 Kim Jong-nam alikamatwa na mamlaka ya uhamiaji nchini Japan akijaribu kuingia nchini humo kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Narita akitumia hati ya kughushi ya kusafiria ya taifa ya Dominican Republic na jina bandia la asili ta kichina la Pang Xiong. Alikamatwa akiwa ameongozaba na wanawake wawili na baada ya kuhojiwa alieleza kuwa alikuwa amelenga kwenda sehemu ya starehe ya Tokyo Disneyland.
Ilikuwa ni aibu kubwa kuwahi kutokea kwa taifa Korea Kaskazini… ati mrithi wa kiti cha kuongoza taifa hilo anatoroka nje ya nchi na hati bandia za kusafiria ili akale starehe na wanawake.
Sitaeleza sana lakini hii ndio ilikuwa sababu ya Kim Jong-nam kuondolewa kwenye mpango wa kumrithi baba yake Kim Jong-il.

Ndipo hapa ikaanzishwa kampeni nchini Korea Kaskazini yente kauli mbiu isemayo "Mama tunayemuheshimu ndiye mtiifu zaidi kwa Kiongozi wetu Mtukufu" (wakimaanisha mama yake Kim Jong-un kiongozi wa sasa wa Korea).

Kwa hiyo taratibu Kim Jong-un akaanza kupigiwa ndogondogo aanze kuiteka mioyo ya wananchi wa Korea Kaskazini na wananchi wamsahau Kim Jong-nam.The rest is history, Kim Jong-un alitawazwa kuwa kiongozi wa taifa la Korea Kaskazi tarehe 24 Desemba mwaka 2011baada ya kifo cha baba yake Kim Jong-il.

Inaelezwa kuwa Kim Jong-nam na Kim Jong-un hawajawahi kuonana tangu wazaliwe kutokana na tamaduni ya Kikorea ya kuwalea mbali mbali watoto ambao mmoja katu yao anatarajiwa kuwa kiongozi.
Kwa mujibu wa vyombo vya intelejensia vya Korea kusini, kwa mara ya kwanza walionana baada ya baba yao kufariki ambapo Kim Jong-nam aliruhusiwa kuingia Korea kaskazini kutoa heshima zake za mwisho kwa baba yake lakini hakuruhusiwa kuonekana kwa umma.

Baada ya hapo maisha yakaendelea mdogo mtu (Kim Jong-un) akiongoza taifa la Korea Kaskazini huku kaka mtu Kim Jong-nam akiishi kwa kutanga tanga kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine.
Lakini pia kihoro cha kuikosa nafasi ya kuongoza taifa hakikumuisha kaka mtu Kim Jong-nam… alifanya mahojiano kadhaa na vyombo vya habari vya kimataifa akimshutumu mdogo wake kuwa hana uzoefu wa utumishi na lazima uingozi wake utafeli. Alienda mbali zaidi na kuanza kutoa shutuma mara kadhaa kuwa taifa hilo linahitaji kufanya mageuzi ya namna ya uendeshwaji wake kuendana na ulimwengu ulivyo sasa.

Kelele hizi za kaka mtu zilianza kumkera Kim Jong-un. Ndipo hapa aliagiza maafisa wake wa vyombo vya ujasusi kuhakikisha kaka yake anauwawa mara moja.
Kazi hiyo haikuwa rahisi kutokana na kaka mtu naye kuwa na uelewa juu ya masuala ya ujasusi. Alinusurika kuuwawa mara kadhaa nchini Singapore, Macau, na hata uswisi. Majaribio haya yalifanya mataifa hayo husika kuwawashia moto Korea Kaskazini kwamba hawataruhusu mauaji hayo yafanyike nchini mwao.

Ndipo hapa majasusi wa Korea Kaskazini wakaamua kutumia mbinu adhimu… Agent Provocateur… Pandikizi Chochezi ili kuficha uhusika wao na tukio hilo kuonekana halina uhusiano na wao serikaki ya Korea Kaskazini.

Ilikuwa hivi…

Siku ya tarehe 13 February mwaka jana 2017, majira ya saa tatu asubuhi Kim Jong-nam alikuwa amewasili katika uwanja wa ndege wa wa Kimataifa wa Kuala Lumpar kwa kutumia hati bandia ya kusafiria yenye jina Kim Chol… akiwa katika sehemu ya kujihudumia mwenyewe ya check-in, walijitokeza wanawake wawili ambao walimpulizia kitu fulani usoni. Baada ya kupuliziwa tu Kim Jong-nam alidondoka chini na hali yake kubadilika ghafla. Alianza kutoka jasho lingi mfululizo huku akipaparika kama anakifafa.
Mara moja aliwahishwa hospitali na licha ya juhudi za madaktari kuokoa uhai wake, Kim Jong-nam alipoteza maisha.

Kutokana na kutumia jina bandia mwanzoni hakuna aliyemtambua ni nani. Lakini baadae vyombo vya usalama vya Malaysia wakang'amua kuwa alikuwa ni Kim Jong-nam.
Haraka akafanyiwa autopsy ili kujua ni nini hasa kilichosababisha kifo chake… daktari akarudisha majibu kuwa ameuwawa kwa 'nerve gas' hatari aina ya VX.
Hii ilikuwa ni taarifa ya kushtua mno. Gesi hii hairuhusiwi hata kutumika kwenye uwanja wa vita na ilishapigwa marufuku tangu mwaka 1993 na tamko la Kongamano la Kudhibiti silaha za kemikali.

Wanawake wale… wadada wa mjini wasio na mbele wala nyuma wametoa wapi silaha hatari kama hii?

Walipoenda kutazama mikanda ya video ya kamera za ulinzi za Uwanja wa ndege waligundua viroja zaidi. Wakati wale wanawake wanafanya tukio hilo walionekana walikuwa wameongozana na wanaume wanne waliojifunga nyuso zao… lakini kipindi wao wanampulizia Kim ile gesi wale wanaume walitimua mbio.

Polisi wakaanza msako wa kuwapata hao akina dada wawili. Ajabu ni kwamba kesho yake moja ya wale wadada akarejea tena pale uwanja wa ndege. Akakamatwa. Na huyu akasaidia kukamatwa kwa mwenzake.

Walipohijiwa walieleza kuwa walikuwa wamelipwa hela kushiriki kwenye kipindi cha TV kinachohusu Pranks (michezo ya utani kumshitukiza mtu kwa tukio ambalo hakulitegemea) na kwamba tukio la hapo uwanja wa ndege ndio ilikuwa 'prank' yao ya kwanza ambayo walitakiwa kuifanya. Wanadai walishangaa baada ya kumpulizia Kim kitu ambacho waliambiwa ni rangi walipogeuka nyuma hawakuwaona wale wenzao wanaume wanne.

Ukitazama mikanda ya video ya ulinzi pale uwanja wa ndege unathibitisha maelezo ya hawa akina dada… moja, hawakuwa wamejiziba pua na mdogo tofauti na wale wanaume wanne wengine ambao walijifunika nyuso… maana yake ni kwamba hawakuwa wanajua hatari ya ile gesi ambayo walikuwa wanapuliza na hivyo walikuwa wanahatarisha pia maisha yao.
Lakini pili, baada ya Kim kupuliziwa gesi na kudondoka na kuanza kupaparika chini, hawakukimbia bali walibakia na wameduwaa na wameshikwa na bumbuwazi ikionesha dhahiri kabisa hawakutegemea hilo. Na hata kitendo cha yule dada kurejea tena pale uwanja wa ndege kesho yake kujaribu kuwatafuta wale wenzao wanne waliowakimbia pia ilikuwa inatoa pichwa kwamba hawakuelewa uhatari wa tukio walilolifanya.
Kwa hiyo maelezo yao kuwa walikuwa wanadhani wanashiriki kipindi cha televisheni cha 'Pranks' yanakuwa na mashiko kwa kiasi kikubwa.

Nchi zote wamewanyooshea kidole Korea Kaskazini kutokana na tukio hili. Lakini hakuna ushaidi wa moja kwa moja kuthibitisha Korea Kaskazini wamehusika kumuua Kim Jong-nam japo wote tunajua wamehusika. Korea kaskazini wenyewe wanadai kuwa Kim Jong-nam amedhuliwa na 'vimada' wake… wakisisitiza juu ya historia ya Kim Jong-nam kupenda starehe, pombe, wanawake na michezo ya kamali.

Zigo hili wamebebeshwa wadada wale wawili na wanashtakiwa kwa kesi ya mauaji nchini Malaysia. Hivi ninavyoandika ni wiki iliyopita tu upande wa mashtaka umemaliza kuwasilisha ushahidi wao na sasa tubasubiri Jaji aseme kama wale akina dada wana kesi ya kujibu au la.

Hivyo ndivyo ambavyo mbinu ya kutumia 'Agent Provocatuer'… Pandikizi Chochezi inavyofanya kazi.

img_20180420_211859-jpg.751361
 
H

havanna

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2016
Messages
1,436
Points
2,000
Age
49
H

havanna

JF-Expert Member
Joined Sep 17, 2016
1,436 2,000
Dah inavutia sana na inaakisi mambo flani
 
kwabwina

kwabwina

Senior Member
Joined
May 29, 2016
Messages
129
Points
250
kwabwina

kwabwina

Senior Member
Joined May 29, 2016
129 250
Nikupe hongera sana Dada kwa mada maridhawa imekaa vema sana na umenifungua masikio Leo katka ulimwengu wa intelejensia nitarud baadae kwa maswali
 
Mnabuduhe

Mnabuduhe

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2015
Messages
304
Points
500
Mnabuduhe

Mnabuduhe

JF-Expert Member
Joined May 8, 2015
304 500
Agent Provocateur ni chambo anayejipenyenza katika kundi flani la jamii kuwasabibisha wale waliokusudiwa kuvunja sheria au Kutambua nani Kinara wa harakati fulani zisizoruhusiwa au zinazowakera Watawala au Serikali.

Tanzania iliwahi kutokea mara nyingi! Inasemekana kwa mara ya kwanza ni Ule mgomo wa miaka ya 1960's Chuo Kikuu cha DSM! Ulikuwa hauna impact na Rais alikuwa ameshapewa taarifa ya kuwa vijana wamejiandaa kugoma alitaka kuzungumza nao na kumaliza mgomo huo kwa amani! ila kundi flani ndani ya serikali lilipania wasomi wale waione hasira ya Nyerere! Wakapandikiza vijana wa idara ya usalama wa Taifa kujiingiza kwenye Mgomo na ndio waliobeba ujumbe ambao walijua ungeiamsha gadhabu ya Julius "Afadhali ya Mkoloni"Maneno hayo inasemekana yalimchefua sana Mwl. Nyerere akawatimua wote warudi nyumbani haraka.

Augustine Lyatonga Mrema - Mwaka 1990s akiwa Waziri wa mambo ya ndani akatembelea baadhi ya Vyuo vikuu akawaonya wanafunzi kuwa wajihadhari na Ujio Mageuzi nchini kwani lengo lake ni kuleta machafuko na taharuki! Yeye punde akaja kuwa Mwanamageuzi wa Kwanza Tz ndiye aliyewabaini wapinzani wote na Kuvuruga vyama vyote vilivyoonesha upinzani halisi nchini dhidi ya chama Tawala -NCCR,TLP - Kati ya real agent provocateur ni huyu Mzee.

Na wengine ambao wanajamvi mnawajua sana!
Kazi yao kubwa ni Kuprovoku! Kuleta uchochezi ili wenye Hisia kali wajulikane na watu hatari washughulikiwe haraka by any means necessary!
KGB ilitumia watu na namna hii kupima uzalendo fake na halisi ndani ya Urusi.

Asante.
 
kichakaa man

kichakaa man

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2011
Messages
3,027
Points
2,000
kichakaa man

kichakaa man

JF-Expert Member
Joined Oct 20, 2011
3,027 2,000
Asante kwa mada murua hiii
 
mkulungu mkuyengo

mkulungu mkuyengo

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2015
Messages
764
Points
1,000
mkulungu mkuyengo

mkulungu mkuyengo

JF-Expert Member
Joined Feb 5, 2015
764 1,000
Good,ila Beautiful Nkosazana naona hii dhana ya agent provocateur inashabihiana na story katika post no.14 au unasemaje?
 
Bujibuji

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Messages
43,887
Points
2,000
Bujibuji

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined Feb 4, 2009
43,887 2,000
Hii post imekuja purposely tukiikaribia siku ya unabii. Hawa wakutabiri mabadiliko makubwa ya kumtusi, huku Hawa wengine wakutabiri kuwakomesha Na kuwashughulikia wenzao. [HASHTAG]#26042018[/HASHTAG]
 
Ciprofloxacin.

Ciprofloxacin.

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2015
Messages
1,498
Points
2,000
Ciprofloxacin.

Ciprofloxacin.

JF-Expert Member
Joined Apr 15, 2015
1,498 2,000
Intelijensia: Pandikizi Chochezi

Suala la Intelijensia, ujasusi na ushushushu ni kitu adhimu sana kukifahamu si tu kwa manufaa ya usalama wa nchi bali pia yaweza kukufaa hata katika maisha ya kawaida. Mbinu za kijasusi na intelijesia kwa sasa zinatumika katika kila sekta na nyanja ya maisha. Iwe wewe ni mwanaharakati, mwanasiasa, mfanyabiashara, mwanazuoni, mwajiriwa au mjasiriamali… uelewa walau mdogo tu wa masuala ya intelijensia unaweza kukufanya kuwa hatua kadhaa mbele ya wenzako na hata pia kuweza kujikinga dhidi ya mashambulio dhidi yako pale yanapotokea.

Kwa ufupi sana siku ya leo nitaongea kuhusu moja ya mbinu adhimu ya intelijensia yenye kutumika sana ulimwenguni kote na ambayo pia nimeiona imeshika hatamu mno kwa sasa hapa nchini afrika mashariki. Lugha yetu ya kiswahili ni changa hivyo inakosa baadhi ya misamiati kueleza kitu kwa ufasaha unaoulenga. Kwa ukosefu wa msamiati maridhawa nitaiita mbinu hii "Pandikizi Chochezi" ambayo kwa umombo inajulikana kama "Agent Provocateur".

Katika masuala ya ujasusi, pandikizi chochezi ni mtu ambaye anafanya au anashawishi mtu mwingine kufanya kitu kilicho kinyume na sheria au tendo la hila au kumuhusisha mwingine kuhusika kwenye tendo hilo.
Pandikizi Chochezi anaweza kuwa ni afisa wa chombo cha usalama, au afisa wa kiserikali au Idara na hata wakala wa chama cha siasa na kwenye ulimwengu wa biashara anaweza kuwa hata mwajiriwa wa kampuni shindani.

Pandikizi chochezi anatumiwa na Idara iliyomtuma, kujipenyeza kwenye kundi lengwa (mfano chama cha siasa au kampuni au vugu vugu ka harakati) na akiisha kujipenyeza na kukubalika kwenye kundi hilo anakuwa mstari wa mbele kabisa kindakindaki kiasi kwamba anakuwa moja ya watu wenye kutazamwa kwa mwongozo kwenye kundi hilo. Baada ya hapo Pandikizi chochezi anatumia mwanya huo kushawishi wengine kufanya tendo la hila ambalo ni kinyume cha sheria. Lengo kuu hapa linakuwa ni mfano kuvuruga harakati/vuguvugu au kujaribu kupaka matope kundi hilo husika au kulichafua kwenye jamii ama kuifanya serikali kuchukua hatua dhidi ya kundi hilo.

Mbinu hii inatumiwa mfano na serikali nyingi au vyombo vya usalama pale ambapo wanahitaji kupiga marufuku kundi fulani (chama cha siasa, vuguvugu au kampuni) hivyo pandikizi chochezi anatumiwa ili kuipa serikali au idara ya usalama sababu ya kuwachukulia kundi hilo hatua.

Si hivyo tu, lakini pia Pandikizi chochezi anaweza kutumia kushawishi mtu mwingine kufanya tukio la kudhuru kama vile mauaji bila anayetumiwa kujua. Yaani kwamba pale ambapo Idara husika au serikali husika ikihitaji 'kumu-eliminate' mtu fulani lakini haitaki yabakie maswali na sintofahamu, wanaweza kutumia Pandikizi Chochezi kushawishi mtu wa kawaida kufanya tukio hilo la mauaji pasipo mtu anayetumiwa kujua kuwa anatumika.

Nitatoa mifano michache…

Inawezekana wengi hawafahamu kwamba Kim Jong-Un hakuwa chaguo la kwanza la baba yake Kim Jong-il kumrithi kuongoza taifa la Korea Kaskazini.
Chaguo la kwanza la Kim Jong-il lilikuwa ni mtoto wake wa nje aliyeitwa Kim Jong-nam ambaye alizaliwa mwaka 1971 na mwanamke aitwaye Song-Hye-rim. Kutokana na baba yake (yaani babu yao akina Kim Jong-nam na Kim Jong-un) kutokukubali mahusiano ya kimapenzi kati ya mwanaye Kim Jong-il na yule mwanamke Song Hye-rim ilibidi alipozaliwa Kim Jong-nam afichwe kwa kupelekwa kuishi na shangazi yake na baadae alipelekwa nje ya nchi ambako alikaa huko utoto wake wote na kusoma huko kwenye nchi za Urusi na Uswisi na kurejea Korea Kaskazini mwaka 1988.

Kama maandalizi ya kumrithi baba yake, mwaka 1998 Kim Jong-nam aliteuliwa kuongoza Wizara ya Masuala ya Usalama wa Taifa. Pia Kim Jong-nam alipewa jukumu na baba yake kuongoza kamati ya Taifa ya kuunda sekta ya Tehama nchini humo.
Pia ni Kim Jong-nam ambaye aliambatana na baba yake kwenye ziara ya nchini China mwaka 2001 ili kujadili namna ambavyo wachina wanaweza kuwasaidia kuinua sekta ya Tehama nchini Korea Kaskazini.

Kila aina ya maandalizi yalikuwa yanafanyika kumuandaa Kim Jong-nam kuwa mrithi wa Kim Jong-il kuongoza taifa la Korea Kaskazini.

Japokuwa Kim Jong-nam alikuwa anafanana sana kihaiba na baba yake kutokana na hasira zake, hisia za haraka na ujuzi wa masuala ya sanaa kama vile uandishi wa miswada ya filamu lakini Kim Jong-nam alikuwa na kasoro moja mbaya… alikuwa ni mtu mwenye kupenda anasa na wanawake hovyo. Kulikuwa na uvumi kwamba Kim Jong-nam mara kadhaa amekuwa akitoka nje ya Korea Kaskazini kwa pasipoti za kughushi zenye majina ya uongo ili kwenda kufanya starehe Macau, China na hata Japan. Uvumi huu ulikuwa ukikanushwa mara nyingi na serikali ya Korea Kaskazini.

Za mwizi ni arobaini, mwezi May mwaka 2001 Kim Jong-nam alikamatwa na mamlaka ya uhamiaji nchini Japan akijaribu kuingia nchini humo kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Narita akitumia hati ya kughushi ya kusafiria ya taifa ya Dominican Republic na jina bandia la asili ta kichina la Pang Xiong. Alikamatwa akiwa ameongozaba na wanawake wawili na baada ya kuhojiwa alieleza kuwa alikuwa amelenga kwenda sehemu ya starehe ya Tokyo Disneyland.
Ilikuwa ni aibu kubwa kuwahi kutokea kwa taifa Korea Kaskazini… ati mrithi wa kiti cha kuongoza taifa hilo anatoroka nje ya nchi na hati bandia za kusafiria ili akale starehe na wanawake.
Sitaeleza sana lakini hii ndio ilikuwa sababu ya Kim Jong-nam kuondolewa kwenye mpango wa kumrithi baba yake Kim Jong-il.

Ndipo hapa ikaanzishwa kampeni nchini Korea Kaskazini yente kauli mbiu isemayo "Mama tunayemuheshimu ndiye mtiifu zaidi kwa Kiongozi wetu Mtukufu" (wakimaanisha mama yake Kim Jong-un kiongozi wa sasa wa Korea).

Kwa hiyo taratibu Kim Jong-un akaanza kupigiwa ndogondogo aanze kuiteka mioyo ya wananchi wa Korea Kaskazini na wananchi wamsahau Kim Jong-nam.The rest is history, Kim Jong-un alitawazwa kuwa kiongozi wa taifa la Korea Kaskazi tarehe 24 Desemba mwaka 2011baada ya kifo cha baba yake Kim Jong-il.

Inaelezwa kuwa Kim Jong-nam na Kim Jong-un hawajawahi kuonana tangu wazaliwe kutokana na tamaduni ya Kikorea ya kuwalea mbali mbali watoto ambao mmoja katu yao anatarajiwa kuwa kiongozi.
Kwa mujibu wa vyombo vya intelejensia vya Korea kusini, kwa mara ya kwanza walionana baada ya baba yao kufariki ambapo Kim Jong-nam aliruhusiwa kuingia Korea kaskazini kutoa heshima zake za mwisho kwa baba yake lakini hakuruhusiwa kuonekana kwa umma.

Baada ya hapo maisha yakaendelea mdogo mtu (Kim Jong-un) akiongoza taifa la Korea Kaskazini huku kaka mtu Kim Jong-nam akiishi kwa kutanga tanga kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine.
Lakini pia kihoro cha kuikosa nafasi ya kuongoza taifa hakikumuisha kaka mtu Kim Jong-nam… alifanya mahojiano kadhaa na vyombo vya habari vya kimataifa akimshutumu mdogo wake kuwa hana uzoefu wa utumishi na lazima uingozi wake utafeli. Alienda mbali zaidi na kuanza kutoa shutuma mara kadhaa kuwa taifa hilo linahitaji kufanya mageuzi ya namna ya uendeshwaji wake kuendana na ulimwengu ulivyo sasa.

Kelele hizi za kaka mtu zilianza kumkera Kim Jong-un. Ndipo hapa aliagiza maafisa wake wa vyombo vya ujasusi kuhakikisha kaka yake anauwawa mara moja.
Kazi hiyo haikuwa rahisi kutokana na kaka mtu naye kuwa na uelewa juu ya masuala ya ujasusi. Alinusurika kuuwawa mara kadhaa nchini Singapore, Macau, na hata uswisi. Majaribio haya yalifanya mataifa hayo husika kuwawashia moto Korea Kaskazini kwamba hawataruhusu mauaji hayo yafanyike nchini mwao.

Ndipo hapa majasusi wa Korea Kaskazini wakaamua kutumia mbinu adhimu… Agent Provocateur… Pandikizi Chochezi ili kuficha uhusika wao na tukio hilo kuonekana halina uhusiano na wao serikaki ya Korea Kaskazini.

Ilikuwa hivi…

Siku ya tarehe 13 February mwaka jana 2017, majira ya saa tatu asubuhi Kim Jong-nam alikuwa amewasili katika uwanja wa ndege wa wa Kimataifa wa Kuala Lumpar kwa kutumia hati bandia ya kusafiria yenye jina Kim Chol… akiwa katika sehemu ya kujihudumia mwenyewe ya check-in, walijitokeza wanawake wawili ambao walimpulizia kitu fulani usoni. Baada ya kupuliziwa tu Kim Jong-nam alidondoka chini na hali yake kubadilika ghafla. Alianza kutoka jasho lingi mfululizo huku akipaparika kama anakifafa.
Mara moja aliwahishwa hospitali na licha ya juhudi za madaktari kuokoa uhai wake, Kim Jong-nam alipoteza maisha.

Kutokana na kutumia jina bandia mwanzoni hakuna aliyemtambua ni nani. Lakini baadae vyombo vya usalama vya Malaysia wakang'amua kuwa alikuwa ni Kim Jong-nam.
Haraka akafanyiwa autopsy ili kujua ni nini hasa kilichosababisha kifo chake… daktari akarudisha majibu kuwa ameuwawa kwa 'nerve gas' hatari aina ya VX.
Hii ilikuwa ni taarifa ya kushtua mno. Gesi hii hairuhusiwi hata kutumika kwenye uwanja wa vita na ilishapigwa marufuku tangu mwaka 1993 na tamko la Kongamano la Kudhibiti silaha za kemikali.

Wanawake wale… wadada wa mjini wasio na mbele wala nyuma wametoa wapi silaha hatari kama hii?

Walipoenda kutazama mikanda ya video ya kamera za ulinzi za Uwanja wa ndege waligundua viroja zaidi. Wakati wale wanawake wanafanya tukio hilo walionekana walikuwa wameongozana na wanaume wanne waliojifunga nyuso zao… lakini kipindi wao wanampulizia Kim ile gesi wale wanaume walitimua mbio.

Polisi wakaanza msako wa kuwapata hao akina dada wawili. Ajabu ni kwamba kesho yake moja ya wale wadada akarejea tena pale uwanja wa ndege. Akakamatwa. Na huyu akasaidia kukamatwa kwa mwenzake.

Walipohijiwa walieleza kuwa walikuwa wamelipwa hela kushiriki kwenye kipindi cha TV kinachohusu Pranks (michezo ya utani kumshitukiza mtu kwa tukio ambalo hakulitegemea) na kwamba tukio la hapo uwanja wa ndege ndio ilikuwa 'prank' yao ya kwanza ambayo walitakiwa kuifanya. Wanadai walishangaa baada ya kumpulizia Kim kitu ambacho waliambiwa ni rangi walipogeuka nyuma hawakuwaona wale wenzao wanaume wanne.

Ukitazama mikanda ya video ya ulinzi pale uwanja wa ndege unathibitisha maelezo ya hawa akina dada… moja, hawakuwa wamejiziba pua na mdogo tofauti na wale wanaume wanne wengine ambao walijifunika nyuso… maana yake ni kwamba hawakuwa wanajua hatari ya ile gesi ambayo walikuwa wanapuliza na hivyo walikuwa wanahatarisha pia maisha yao.
Lakini pili, baada ya Kim kupuliziwa gesi na kudondoka na kuanza kupaparika chini, hawakukimbia bali walibakia na wameduwaa na wameshikwa na bumbuwazi ikionesha dhahiri kabisa hawakutegemea hilo. Na hata kitendo cha yule dada kurejea tena pale uwanja wa ndege kesho yake kujaribu kuwatafuta wale wenzao wanne waliowakimbia pia ilikuwa inatoa pichwa kwamba hawakuelewa uhatari wa tukio walilolifanya.
Kwa hiyo maelezo yao kuwa walikuwa wanadhani wanashiriki kipindi cha televisheni cha 'Pranks' yanakuwa na mashiko kwa kiasi kikubwa.

Nchi zote wamewanyooshea kidole Korea Kaskazini kutokana na tukio hili. Lakini hakuna ushaidi wa moja kwa moja kuthibitisha Korea Kaskazini wamehusika kumuua Kim Jong-nam japo wote tunajua wamehusika. Korea kaskazini wenyewe wanadai kuwa Kim Jong-nam amedhuliwa na 'vimada' wake… wakisisitiza juu ya historia ya Kim Jong-nam kupenda starehe, pombe, wanawake na michezo ya kamali.

Zigo hili wamebebeshwa wadada wale wawili na wanashtakiwa kwa kesi ya mauaji nchini Malaysia. Hivi ninavyoandika ni wiki iliyopita tu upande wa mashtaka umemaliza kuwasilisha ushahidi wao na sasa tubasubiri Jaji aseme kama wale akina dada wana kesi ya kujibu au la.

Hivyo ndivyo ambavyo mbinu ya kutumia 'Agent Provocatuer'… Pandikizi Chochezi inavyofanya kazi. Keep your eyes open…

View attachment 751361
Nimekuelewa vizuri sana mkuu,sasa hivi wanamtumia Msiba,ili wapate Sababu ya kuifuta CHADEMA,magufuli in rais wa hovyo kuwahi kutokea
 
Forum statistics

Threads 1,295,407
Members 498,303
Posts 31,211,066
Top