Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,172
- 7,428
Demokrasia ina kanuni na misingi yake. Kama tumeamua kuifuata, ni vyema tuifuate katika hatua, misingi na kanuni zake. Kama tukiamua kukwepa kanuni na misingi ya demokrasia tukakimbilia matokeo (ya demokrasia?); hatutapata matokeo ya kuridhisha na kinyume chake yatotokea mapovu ya kisiasa.
Tutakuwa na hatari ya kujikuta siku moja tuna viongozi wa kisiasa wasiokuwa na muunganiko wa kisiasa ‘Political legitimacy’ na wanaowaongoza. Matokeo yake sio tu kwamba ushirikiano kati ya waongozaji na waongozwaji hautakuwepo bali pia muongozaji atapoteza morali au kujikuta kwenye confusion kubwa. Katika hatua ya juu kabisa, waongozwaji na waongozaji wote watapoteza kisha jaribu kufikiria nini kitafuata?
Tunachoweza kushauri ni kwamba; kama tumeamua kufuata mfumo wa demokrasia, ni muhimu tuufuate pamoja na kanuni na misingi yake na kama tunaona demokrasia haifai tena kwa sababu zozote zile; ni muhimu wadau wakubaliane rasmi kuachana nayo na kutangaza mfumo mpya ambao utaonekana kama mbadala wa demokrasia.
Hata hivyo kabla ya kufikiria uamuzi wa pili hapo juu, ni muhimu kukumbuka kuwa hadi sasa bado hakuna mfumo mbadala wa kisiasa unaoaminika kuwa bora zaidi ya demokrasia duniani.